Friday, June 15, 2012

MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA KAMPENI YA MATIBABU YA FISTULA JIJINI DAR LEO

Mke wa Rais NaMwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete akizungumza kwa kusisitiza jambo wakati wa Ufunguzi wa Kampeni ya Matibabu ya ugojwa wa Fistula uliofanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT,Dkt, Wilbroud Slaa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA,akiwa amemshika mtoto mchanga baada ya kukabidhiwa na wazazi wake baada ya ushuhuda walioutoa wakati nwa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya Fistula- Tanzania ,katika viwanja vya Mnazi mmoja leo.kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT Dk, Wilbroud Slaa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT Erwin Telemans akitoa maelezo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya FISTULA Tanzania ,leo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar eSalaam , Uzinduzi rasmi umefanywa na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (alievaa kilemba cheupe) akisikiliza maelezo ya ugojwa wa Fistula kutoka kwa Muelimishaji katika kitengo cha Mama na Mtoto (CCBRT) Seraphina Faya (kushoto) kabla ya Kuzindua Kampeni ya Uhamasishaji wa matibabu ya Fistula Tanzania leo jijini Dar es salaam,Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT Dkt, Wilbroud Slaa.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete (alievaa miwani) akipata maelezo ya matibabu ya Fistula kutoka kwa Daktari Bigwa wa upasuaji Fistula kutoka hospitali ya CCBRT Dkt, Robert Murenga (wapili kulia),kabla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa matibabu ya Fistula Tanzania leo jijini Dar es salaam.Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT,Dr. Wilbroud Slaa(mwenye kadeti).
Shuhuda wa ugonjwa wa FISTULA Beatrice Mlunga (kulia) akitoa ushuhuda wa matatizo alliyoyapata ya ugojwa Fistula wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya Fistula Tanzania katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo. Mradi wa Fistula kwa mwaka inakadiriwa wastani wanawake wapya 2,500 hadi 3000 hupatwa na ugojwa huo wakati wanapojifungua. Kwa sasa wanawake zaidi ya 31,000 inasemekana wanalo tatizo la Fistula hapa nchini, Hivyo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoa wito wakina mama wenye matatizo ya Fistula kumuacha kujificha kwani unatibika .hivyo waende katika matibabu ambayo hupatikana bure ktk hosp. ya CCBRT jijini DSM na hosp, ya Kilutheli ya Selian. (kushoto ni mume wake shuhuda) Hosea Sanga.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete (mwenye miwani ) akibonyeza kitufe wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Matibabu ya Fistula Tanzania leo jijini Dar es Salaam, (Pichani alevaa vazi la kadeti) ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT Dk. Wilbroud Slaa,(kulia) ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa DSM ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema.
Mjomba Mpoto akiwatumbuiza waalikwa wakati wa Uzinduzi.
Baadhi ya wagojwa waliopna FISTULA wakiimba katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam.
WASANII KUTOKA KATKA KIKUNDI CHA SANAA CHA MJOMBA MRISHO MPOTO WAKITOA IGIZO KUHUSU UNYAAPAA KWA MKE MWENYE UGOJWA WA FISTUL
Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa matibabu ya Fistula Tanzania leo katika viwanja vya Mnazimmoja ambapo mgeni rasmi alikuwa Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisis ya WAMA Mama Salma Kikwete,(hayupo pichani), Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.

No comments: