Monday, January 23, 2012

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MKOA WA LINDI,AWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA AFYA CHA KITOMANGA, LINDI VIJIJINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mkewe Mama Zakhia Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Lindi, wakati akikagua Daraja la Mingumbi baada ya kuzindua daraja hilo lililopo Kilwa, akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya mkoa wa Lindi jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi, alipozindua Daraja la Mingumbi lililopo Kilwa, wakati akiwa kwenye ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo jipya la Bwalo la Shule ya Sekondari ya wasichana Ilulu, iliyopo Kilwa, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya mkoa wa Lindi jana Januari 22, 2012. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Ilulu, baada ya kuzindua rasmi Jengo la Bwalo la shule hiyo, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Mkoa wa Lindi jana Januari 22, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Chumo Namkamba, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana Januari 22, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka jilwe la msingi katika Ofisi mpya ya Chama cha Mapinduzi CCM, iliyopo Chumo Namkamba Kilwa jana januari 22, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya mkoa wa Lindi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua ujenzi wa jengo la Zahanati ya Kilanjelanje iliyopo Jimbo la Kilwa Kusini, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya Mkoa wa lindi jana Januari 22, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwasalimia wananchi baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika jengo la Kituo cha Afya cha Kitomanga lililopo Lindi Vijijini wakati akiwa katika zaiara yake mkoa wa Lindi jana, januari 22, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Moahammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi wa Kitomanga, baada ya kuzindua rasmi jengo la Kituo cha afya cha Kitomanga, Lindi Vijijini, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana Januari 22, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

No comments: