Saturday, November 10, 2018

PUMA ENERGY TANZANIA YAZINDUA MRADI WA SKY IS THE LIMID PROJECT KWA LENGO LA KUAMSHA MOYO WA UJASIRI NA KUJIWEKEA MALENGO KATIKA KUFANIKIWA

????????????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (wa pili kulia) na Meneja Masoko wa mafuta ya Ndege Puma Tanzania, Illuminata Yateri (katikati) wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Josephat Kagirwa (kulia) alipokuwa akizungumza na wanafunzi kutoka Shule za Msingi wilayani Kisarawe walipofanya ziara ya mafunzo uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni adhimisho la mradi ujulikanao kama Sky is the limit.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (wa pili kulia) akizungumza na wanafunzi wa shule za msingi kutoka wilaya yake wakati wa ziara ya kimafunzo kutembelea karakana ya ndege jijini Dar es Salaam jana kwa kushirikiana na Kampuni ya Puma Energy Tanzania katika kuhudumia utoaji wa mafuta ya ndege chini ya mradi ujulikanao kama Sky is the limit.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, Meneja Masoko wa mafuta ya Ndege Puma Tanzania, Illuminata Yateri na wanafunzi wa Shule za Msingi wilayani Kisarawe, wakiingia kwenye Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), walipofanya ziara ya kimafunzo katika mradi wa Sky is the limit kwenye uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam (JNIA) jana.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akimfunga vifungo mmoja wa wanafunzi wakati walipofanya ziara katika uwanja wa ndege wa JNIA katika mradi mradi ujulikanao kama Sky is The Timit
????????????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, Meneja Masoko wa mafuta ya Ndege Puma Tanzania, Illuminata Yateri na wanafunzi wa Shule za Msingi wilayani Kisarawe, wakimsikiliza Injinia wa Ndege kutoka Shirika la Ndege Tanzania (ATC), Nkhambi Salanga walipofanya ziara ya kimafunzo katika mradi wa Sky is the limit katika uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam jana.
????????????????????????????????????

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Energy (T) LTD kwa kushirikiana na Kampuni ya Air Tanzania Limited imezindua mradi unaojulikana kama “Sky is the Limit Project”wenye lengo la kuwatambulisha na kuwapa uelewa wanafunzi wa shule za msingi wasio na fursa au uwezo wa kuufikia kwa urahisi ulimwengu wa anga ili kuwapa uelewa kuhusu sekta hiyo yenye kuvutia.

Imeelezwa lengo la mradi huo ni kuwahamasisha watoto wanaotoka mazingira ya kawaida sana ya vijijini kwa kuwatia moyo katika masomo yao ili wajue na kuvutiwa na sekta ya anga na maeneo mengine ya fursa za kazi za nje ya maeneo wanaoishi.

Katika kufanikisha mradi huo zaidi ya wanafunzi 40 kutoka Shule za msingi za wilayani Kisarawe wamepata fursa ya kutembelea Shirika la Ndege la Air Tanzania pamoja na kushuhudia namna Kampuni ya mafuta ya Puma inavyohifadhi mafuta ya ndege katika Uwanja wa Ndege Terminal One jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko wa Mafuta ya Ndege Tanzania kutoka kampuni ya Mafuta ya Puma Illuminata Yateri amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa kama neon linavyojieleza la Sky is the Limit , mradi huo unataka kuamsha moyo wa ujasiri na kujiwekea malengo ya juu katika kufanikiwa.

Amefafanua mradi huo wa Sky is the limit utawapa wototo kutoka shule za msingi waliochaguliwa kutoka kwa jumuiya zisizo na fursa na uzoefu wa sekta ya anga kwa ukaribu zaidi, kwa kufanya ziara ya elimu inayofanywa katika miundombinu ya uwanja wa ndege kama ugavi wa mafuta ya ndege,huduma zinazotolewa kwenye ndege ,udhibiti wa safari za ndege, kupata habari mbalimbali za ndege kupitia watalaam wa sekta ya ana wanaohusika.

“Watoto watajua shughuli za kampuni ya mafuta ya Puma kuhusu biashara ya mafuta ya ndege jinsi yanavyouzwa kwenye ndege za ndani na za kimataifa.Kampuni ya Puma Tanzania ambayo ndio inayoongoza katika soko la kuuza mafuta ya ndege nchini imekuwa mshirika wa muda mrefu katika sekta ya anga katika kuunga mkono maendeleo ya kiuchumi ya Serikali ya Awamu ya Tano.

“Pia watoto watapata fursa ya kujua biashara ya kampuni ya ndege Tanzania –Air Tanzania “The wings of Kilimanjaro” kwa kutembelea kituo cha matengenezo ,kupata habari na kufahamu vizuri kuhusu juhudi zake za kuchangia uchumi wan chi kwa njia ya usafiri wa anga,”amesema Yateri na kuongeza kuwa idadi ndogo ya wanafunzi watapata fursa ya kupanda ndege kwa safari fupi ambayo inajumuisha majadiliano kutoka kwa rubani na wafanyakazi wa ndege katika siku za mbele.

”Tunashukuru mamlaka ya Kisarawe chini ya uongozi wa Mkuu wa Wilaya hiyo Jokate Mwegelo,Ofisa elimu Wilaya ya Kisarawe pamoja na walimu husika kwa msaada wa kupata wanafunzi hawa ambao leo hii wamejifunza kwa vitendo.Puma tutaendelea kushirikiana na walimu wa shule mbalimbali nchini katika kuhakikisha tunashiriki kuwahamsisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi na mwisho wa siku kuongeza wataalam wa mafuta ya ndege na mambo ya anga,”amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema kuwa anaishukuru Kampuni ya Puma kwa kushirikiana na Air Tanzania kwa kandaa mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya wanafunzi hao na kwamba hatua hiyo inaonesha namna ambavyo wamedhamiria kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Magufuli katika kubooresha sekta ya anga nchini.

“Tumeona juhudi za Rais wetu mpendwa katika kuboresha sekta ya anga.Kitendo cha kuleta wanafunzi kujifunza kwa vitendo kuhusu masuala ya anga na mafuta ya ndege maana yake ni moja tu tunakwenda kuhamasisha vijana wa Tanzania kupenda masomo yanayohusu mafuta na anga.Tumepata taarifa kutoka Puma kwa mhandisi wa mafuta ya ndege nchini Tanzania yupo mmoja tu na anakaribia kustaafu, hivyo ujio wanafunzi hawa ni fursa nyingine ya kuwahamasisha na hatimaye kuwa na wahandisi wengi wa mafuta ya ndege,”amesema Jokate Mwegelo.

No comments: