Monday, February 29, 2016

Uwekezaji mkubwa zaidi kwenye kunyonyesha maziwa ya mama kunaweza kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kuokoa maisha ya watoto wa Tanzania

Mfululizo mpya wa makala zilizochapishwa na The Lancet unatoa ushahidi kuwa kuboresha unyonyeshaji wa maziwa ya mama kunaweza kuokoa maisha ya zaidi ya watoto 820,000 kila mwaka duniani na Dola za Kimarekani bilioni 300 kila mwaka. 

“Katika kipindi cha miaka iliyopita kumekuwa na maendeleo katika kupunguza vifo vya watoto na utapiamlo nchini Tanzania. Hata hivyo, watoto 270 chini ya miaka mitano wanakufa kila siku na karibu asilimia 40 ya watoto hao wanakufa ndani ya mwezi mmoja wa kuishi. Kati ya watoto wanaonusurika, mtoto mmoja kati ya watatu wanadumaa kwa sababu ya utapiamlo sugu. 

Watoto hawa wanakosa fursa zao katika maisha. Hali duni ya lishe inaathiri uwezo wa mtoto kujifunza na pia uwezekano wa mtoto huyo kutengeneza kipato akiwa mtu mzima. Lakini kuna afua zinazojulikana zinazoweza kusababisha mabadiliko makubwa na kuhamasisha kunyonyesha maziwa ya mama. ” amesema Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania, Bibi Maniza Zaman, wakati akiongea na vyombo vya habari Dar es Salaam. “Mfululizo wa makala ya “The Lancet” unatoa ushahidi wenye ushawishi kuhusu faida mbalimbali za kunyonyesha. Uwekezaji kwenye kulinda, kukuza, na kusaidia unyonyeshaji maziwa ya mama kunaweza kuokoa maisha ya watoto wa Tanzania, na hatimaye, kusaidia kukuza uchumi.” 

Makala za “The Lancet” zinaonyesha kuwa kuna faida nyingi za kiafya za kunyonyesha maziwa ya mama. Unyonyeshaji maziwa ya mama kwa kiasi kikubwa sana kunaweza kuzuia karibu nusu ya matukio ya kuhara na theluthi moja ya maambukizo ya njia ya hewa– zikiwa ni sababu mbili zinazoongoza kupelekea vifo kwa watoto walio chini ya miaka mitano. Watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama kwa kawaida wanahitaji kupelekwa hospitali mara chache zaidi na kuwa na uwezekano mdogo wa kupata maambukizo na magonjwa, pia wana uwezekano mdogo zaidi wa kuwa na uzito mkubwa na kupata kisukari baadaye maishani mwao.

Kuna faida za kiafya kwa mama pia. Kwa kila mwaka ambao mama ananyonyesha, uwezekano wa  kupata saratani ya matiti ya hatua ya pili unapungua kwa asilimia 6. Viwango vya sasa vya kunyonyesha maziwa ya mama tayari vinazuia vifo karibu 20,000 vinavyotokana na saratani ya matiti kila mwaka duniani – idadi hii inaweza kuwa kubwa zaidi kwa kuboresha mbinu za  unyonyeshaji wa maziwa ya mama. Pia kunyonyesha kwa muda mrefu zaidi kumehusishwa na kupungua kwa saratani ya mfuko wa mayai. 

Kuongeza viwango vya unyonyeshaji maziwa ya mama katika jamii kuna faida za kiuchumi. Watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama wanapata matokeo mazuri zaidi kwenye vipimo vya upeo wa kiakili. Kimataifa, imekadiriwa kuwa gharama zinazotokana na kuwepo na watoto wenye  upeo mdogo zaidi wa kikakili  unaohusishwa na kutonyonyeshwa maziwa ya mama ni jumla ya takriban dola za kimarekani bilioni 300 kwa mwaka. Nchi zenye kipato cha chini na kipato cha wastani zinapoteza zaidi ya dola za kimarekani bilioni 70 kila mwaka. Nchi zenye kipato cha juu zinapoteza zaidi ya dola za kimarekani bilioni 230 kila mwaka. 

Hata hivyo, hapa Tanzania kuna mikoa  inayooyesha mwelekeo unaotia moyo. Kwa mfano, mkoa wa Kilimanjaro, Tanga na Iringa ina asilimia 75 ya watoto wananyonyeshwa maziwa ya mama ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa. Zaidi ya nusu ya watoto wenye umri wa miezi 0-5 wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee katika miezi 6 ya mwanzo wako katika mikoa ya Iringa, Kigoma, Morogoro, Singida, Katavi na Geita, huku Kagera ikiwa na kiwango kikubwa zaidi cha asilimia 70.  

Ili kuimarisha jitihada za kitaifa za kuboresha unyonyeshaji maziwa ya mama, vikwazo vinavyowakabili wanawake wengi duniani kote pia vinapaswa kushughulikiwa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na:  
Mapungufu  kwenye uelewa wa watoa huduma ya afya ambayo yanawaacha wanawake bila taarifa au msaada sahihi; 
Kukosekana kwa mifumo imara ya msaada kwenye familia na jamii, pamoja na mila na tamaduni zisizounga mkono kunyonyesha maziwa ya mama; na 
Likizo ya uzazi ya muda mfupi au kutokuwepo kabisa kwa likizo hiyo. Likizo ya uzazi ya muda mfupi inaweza kuongeza uwezekano wa kutonyonyesha maziwa ya mama au kuacha kunyonyesha maziwa ya mama mapema kwa asilimia 400; 

Jambo lingine ni uuzaji usiofaa wa vyakula mbadala vya maziwa ya mama (ikiwa na pamoja na maziwa ya kopo kwa ajili ya watoto wachanga) na watengenezaji na wasambazaji ambao hutoa matangazo yanayohusiana na ulishaji wa watoto wachanga hali inayodhoofisha unyonyeshaji maziwa ya mama kama njia yenye ufanisi ya kuboresha afya  katika siku za kwanza za maisha ya mtoto. Hapa Tanzania, Kanuni ya Uuzaji wa Chakula (Udhibiti wa Ubora) cha Mbadala wa maziwa ya Mama na Bidhaa Teule ya mwaka 2013, inalinda unyonyeshaji. – ufuatiliaji na utekelezaji imara zaidi wa Kanuni hiyo unahitajika. 

Wanawake wanaofanya kazi wanahitaji kusaidiwa kupitia sheria zinazolinda uzazi zinazotosheleza. Kwa wanawake waliopo kwenye sekta isiyo rasmi, kuna haja ya kuboresha mifumo ya misaada ya kifamilia na kijamii, na kuandaa mazingira bora zaidi ya kufanyia kazi, ili kuokoa muda na nguvu za wanawake waweze kufanikisha unyonyeshaji maziwa ya mama.

“Kunyonyesha maziwa ya mama ni njia ya asili zaidi, yenye ufanisi zaidi wa gharama, iliyo rafiki zaidi kwa mazingira na rahisi zaidi tunayoijua ya kuwapa watoto wote, tajiri au maskini, mwanzo mzuri zaidi kiafya wa maisha,” alimalizia kusema Bibi Zaman. “Kuweka vipaumbele kwenye kuwekeza katika kukuza unyonyeshaji maziwa ya mama ni pendekezo bora.” 

WAKENYA WAENDELEA KUTAMBA KATIKA MBIO ZA KILIMANJARO MARATHONI 2016

Washiriki wa Mbio za Kilometa 42 katika mashindano ya kimataifa ya Kilimanjaro Marathoni 2016 wakianza mbio zao katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU) .
Mshindi wa kwanza katika Mbio za Kilimanjaro  Marathoni Km 42 upande wa wanaume ,Kiprotich Kirui raia wa Kenya akihitimisha mbio katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika baada ya kutumia muda wa saa 2:16:43.
Mshiriki wa pili katika Mbio za Kilimanjaro Marathoni Km 42 upande wa wanaume ,Kenneth Ronoh raia wa Kenya akihitimisha mbio katika uwanja wa Chuo kikuu Cha Ushirika Moshi baada ya kutumia muda wa saa 2:16:48.
Mshindi wa kwanza katika Mbio za Kilimanjaro  Marathoni Km 42 upande wa wanawake Alice Kibor raia wa Kenya akihitimisha mbio huku akipiga ishara ya msalaba katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika baada ya kutumia muda wa saa 2:38:03.
 
Mshindi wa pili katika Mbio za Kilimanjaro  Marathoni Km 42 upande wa wanawake E Chemweno r raia wa Kenya akihitimisha mbio huku akipiga ishara ya msalaba katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika baada ya kutumia muda wa saa 2:44:20.

Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Kushila Thomas akikabidhi bahasha ya zawadi kwa washindi wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni 2016 upande wa wanawake.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Nape Nnauye akisalimiana na mshindi wa pili katika mbio za Km 42 E,Chemweno kabla ya kumviha medali.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Nape Nnauyeakikabidhi mfano wa hundi kwa washindi wa kwanza hadi wa tatu kwa wanawake katika mbio za Km 42.
Washindi wa kwanza hadi wa 10 wakiwa katika picha ya pamoja na  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Nape Nnauye.
 
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Kushila Thomas akikabidhi bahasha ya zawadi kwa washindi wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni 2016  km 42 upande wa wanaume.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Nape Nnauyeakikabidhi mfano wa hundi kwa washindi wa kwanza hadi wa tatu kwa wanawake katika mbio za Km 42.
.Washindi wa kwanza hadi wa 10 wakiwa katika picha ya pamoja na  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Nape Nnauye. 
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group Kushila Thomas akitoa hotuba yake wakiwa ndio wadhamini wakuu wa Mbio za Kilimanjaro Marathoni 2016  
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania ,Anthony Mtaka akizungumza katika hitimisho la mashindano ya kimataifa ya mbio za Kilimanjaro Marathoni 2016.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUFUNGWA KWA DUKA LA DAWA LA SHINE CARE PHARMACY LA TEMEKE KWA KUKIUKA UENDESHAKI WAKE.

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa kwa Duka la dawa za binadamu la Shine Care Pharmacy lililopo Temeke, baada ya kubainika kuendeshwa kinyume cha sharia ikiwemo kutokuwa na kibali cha uendeshaji na mfamasia husika.

Dk. Kigwangalla ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Mfamasia Mkuu wa Serikali pamoja na msajili wa Baraza la famasia nchini na maafisa wengine, ambapo katika tukio hilo mapema leo Februari 29.2016, walikuta madawa mbalimbali yaliyokwisha muda wake na yale ambayo hayatakiwi kuuzwa katika duka kama hilo.

Aidha, Dk. Kigwangalla akitoa agizo la kufungwa kwa duka hilo, ameagiza kuchukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa Mahakamani mara moja il iwe fundishi na kwa maduka mengine yenye kufanya hivyo.

Kwa upande wake, Mfamasia wa Serikali, Bw. Henry Irunde amebainisha kuwa, dawa hiza za binadamu zilizokutwa hazifai kuuzwa katika maduka hayo na pia duka ambalo linaendeshwa bila kuwa na Mfamasia ni kinyume na sharia kwani watumiaji wakitumia dawa bila kuwa na maelezo ya kutosha kutoka kwa mtaalam wa dawa zinaweza kusababisha usugu kwa mwili wa binadamu n ahata kumsababishia matatizo.

Duka hilo la dawa ambalo lipo hatua chacche kutoka Hospitali ya Temeke, ni miongoni mwa maduka makubwa ya dawa za binadamu ambapo pia wachunguzi ha wa madawa ya binadamu walibaini kuwa milango mingi zaidi kinyume na ile inayotakiwa kuwa kwa maduka ya dawa hali ambayo walitilia mashaka huenda vitendo vingine vya kutoa huduma vinatumika licha ya kuwa milango hiyo ilifungwa kwa kile kilichoelezwa kuwa wahusika hawakuwapo.

Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, zoezi hilo la kukagua maduka ya dawa ni la nchi nzima na watazunguka nchi nzima kufanya ukaguzi huo bila kutoa taarifa hivyo kwa yeyote atakaekutwa anaendesha kinyume cha sharia atachukuliwa hatua stahiki.



Tazama  tv, Kuona video hiyo hapa: 
Imeandaliwa na Andrew Chal.
Mmoja wa maafisa wa TFDA, akikagua dawa katika duka hilo
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akiwaonyesha waandishi wa habari cheti cha Famasia kilichoisha muda wake huku akiendelea na biashara yake hiyo kinyume na sheria.
Baadhi ya maafisa walioambatana na Naibu Waziri wa Afya. Dk Kigwangalla wakimsikiliza kwa makini, Dk. Kigwangalla (hayupo pichani) wakati wa tukio hilo.
Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akiongea kwa njia ya simu na mmiliki wa duka hilo la Shine Pharmacy , Abraham Mathayo...ambaye alieleza kuwa yupo Mkuranga, hivyo waliamua kuongea naye kwa njia ya simu kwa nini anaendesha duka bila ya kutokuwa na vibali.
Mfamasia Mkuu wa Serikali Henri Irunde, akitoa taarifa yake ya ukaguzi katika duka hilo kwa wanahabari na Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani).
Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo ya kufungwa kwa duka hilo.
Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla akitoka katika duka hilo la dawa baada ya kuagiza kulifunga.
(Picha zote na Andrew Chale.)

Mke wa Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa WAMA asisitiza umuhimu wa Chama cha Girl Guide Tanzania Kuongeza Wanachama

 Mke wa Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa WAMA akisalimiana na Mama Othman Chande alipowasili katika Shule ya Sekondari Tambaza kuhudhuriaWorld Thinking Day iliyoandaliwa na Tanzania Girl Guide Association.
 Wanachama wa Girl Guide wakiwasili katika Shule ya Sekondari Tambaza  katika kusherekea World Thinking Day  ambao walipokelewa na Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete.
 Mama Salma Kikwete akiingia katika ukumbi wa Tambaza Sekondari akiwa na viongozi wa Girl Guide kushoto ni Mama Symphorosa Hangi, Kamishna Mkuu  na kulia ni Mama Matilda Balama na Mkuu wa Shule ya Tambaza.
 Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi  na baadhi ya wanafunzi Wanachama na viongozi wa  Girl Guide
 Mama Salma Kikwete akiangalia kazi za wakinamama wajasiriamali ambao walifanya maonyesho katika sherehe hizo.

PICHA NA YUSUPH BADI.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA WARSHA YA PILI YA KIMATAIFA YA UNESCO MKOANI TANGA LEO.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
\Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO kanda ya Afrika Firmin Matoko katikati na mwakilishi Mkaazi wa UNESCO Tanzania Zulmira Rodrigues kabla ya kufungua rasmi Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Balozi wa Korea kusini Nchini Geum-Young Song kabla ya kufungua rasmi Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Cheti kiongozi wa Spice kutoka Zanzibar ambae ni mmoja kati ya washiriki Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Cheti Judith Mwambela mmoja kati ya washiriki Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
(Picha na OMR)

WADAU WAAANZA KUJENGA UELEWA KUHUSU SIKU YA MAGONJWA YANAYOTOKEA KWA KUNDI DOGO LA JAMII

Wadau hao wakinyoosha mikono juu kuonesha umuhimu wa kuadhimishwa kwa siku hiyo ya Magonjwa Yanayotokea kwa kundi dogo la jamii ndani ya jamii.
Mratibu wa tukio hilo Bibi Sharifa Mbaraka akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye moja ya ukumbi wa hoteli ya Serena leo jijini Dar,Bi.Sharifa alisema kuwa tukio hilo limedhamiria kujumuisha  vyombo vya habari na wadau wengine ili kujenga uelewa kuhusu magonjwa hayo. 

“Yapo magonjwa tofauti yanayowasibu watu wachache takribani 7000 ambayo yameshabainishwa duniani hadi leo na Tanzania haiwezi kujitoa kwenye  hili. Hata hivyo watu wengi hapa Tanzania hawana uelewa  kuhusu magonjwa hayo”,alisema Bi Sharifa ambaye watoto wake wawili Ali Mohammed Kimara 5, na Nasreem Mohammed 3, wanasumbuliwa na magonjwa hayo.

Alifafanua kuwa kutokana na uzoefu wake, amepata msukumo  na kuamua kuwaunganisha wazazi, wagonjwa walio na magonjwa hayo na raia wenye mapenzi mema ili kujenga uelewa muhimu na kutoa wito kwa jamii kuchukua hatua.

Pichani wa pili kulia ni Mdau mkubwa wa sekta ya afya Monica Joseph kutoka Philips Medical Systems , akifafanua zaidi kuhusiana na huadhimishwa kwa Siku ya 'Rare Disease' Duniani ambayo inaadhimishwa leo.Monica amesema kuwa ni wakati mwafaka kwa Watanzania kuwa na tahadhari ya kuelewa kuhusu magonjwa hayo ili wanajamii waweze kufahamu mbinu za kuyadhibiti iwapo watayakuta ndani ya jamii. pichani kulia ni Dkt.Mariam Nooram kutoka hospital ya Aghakhan.
 
Kauli mbiu ya Siku ya Magonjwa Yanayotokea kwa kundi dogo la jamii Mwaka 2016 ni ‘Sauti za Wagonjwa’ na inamaanisha kutambua mchango muhimu unatolewa na wagonjwa katika kutaka mahitaji yao na kuchochea mabadiliko ambayo yataboresha maisha yao na masiha ya familia zao na maisha ya wale wanaowahudumia.

Kauli mbiu ya Siku ya Magonjwa yanayotokea kwa kundi dogo la wanajamii ambayo ni, “Ungana nasi kuzifanya sauti za waathirika zisikike” ikitaka jamii kwa jumla, wale wanaishi bila magonjwa hayo au wanaothirika nayo moja kwa moja kuungana na jamii ya waathirika katika kuelewa athari za magonjwa hayo. Watu wanaoishi na magonjwa hayo na familia zao mara kadhaa hutengwa. Jamii inaweza kuwaunganisha kutoka kwenye kutengwa huko. 


Lengo la jumla la Siku ya Magonjwa yanayotokea kwa kundi dogo la jamii ni kuhamasisha uelewa miongoni wa umma kwa jumla kuhusu magonwa hayo na athari zake kwa maisha ya wagonjwa ili kuyapa kipaumbele kwenye afya ya jamii ya Tanzania na kwenye bajeti ya serikali kupitia Wizara husika.

Professor Kareem Manji kutoka Muhimbili akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa Habari namna magonjwa hayo yanavyoisumbua jamii kwa kiasi kikubwa na pia uzoefu wake katika suala zima la kutoa matibabu,kushoto kwake ni Dkt Nurudin Lakhan ambaye pia alielezea namna ya magonjwa hayo  Yanayotokea kwa kundi dogo la jamii yanapaswa kuangaliwa upya ili kuitaka jamii kutambua kuwa magonjwa hayo yapo na yamekuwa yakiisumbua jamii kwa muda mrefu.

Bi.Monica Joseph kutoka Philips Medical Systems  alieleza mambo kadhaaa katika kupambana na magonjwa hayo,ameeleza kuwa ipo haja ya wadau wa sekta ya Afya na jamii kwa ujumla kuyafahamu magonjwa yasiyotambulika yapo katika jamii yetu na lazima tuchukue hatua za kushughulika nayo. Miongoni mwa hatua zinazopaswa kuchukuliwa ni pamoja na:
 
( a) Zifanyike juhudi za makusudi kuwapatia wataalam wa afya mafunzo maalum ya kutambua na kutibia magonjwa hayo,( b) Kuanzisha vitengo maalum vya kushughulikia magonjwa hayo hususan kwenye Hospitali za Rufaa. Vitengo hivyo havinabudi kuwa na vifaa mbalimbali vya kusaidia matibabu ya ugonjwa huo,(c) Uanzishwe mpango maalum wa kuwafanyia uchunguzi watoto wanaozaliwa ili kubaini kama wanao ugonjwa huo toka awali ili hatua zichukuliwe bila kuchelewa,(d) Serikali na wadau wengine wa Sekta ya Afya waangalie uwezekano wa kuwa na kampeni za kuelimisha umma juu ya ugonjwa huu kama inavyofanyika kwa magonjwa mengine kama cancer,malaria,kipindupindu,(e) Uangaliwe uwezekano wa kuanzisha shule maalum kwa ajili ya watoto wenye magonjwa yasiyotambulika.

Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.

Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
PICHA NA MICHUZI JR-MMG