Wednesday, December 31, 2014

SSRA EMERGED AN OVERALL – ATE WINNER UNDER THE CATEGORY OF WORKFORCE FOCUS

In a jovial mood the Director General of SSRA,Irene Isaka receiving a certificate of participation from the Prime Minister Hon. Mizengo Peter Pinda during the Employer of the year Award, where SSRA emerged an overall winner under the category of Workforce Focus. From left is Ms. Zuhura Muro Vice Chairperson of Association of Tanzania Employers (ATE); Hon. Gaudentia Kabaka Minister for Labour and Employment; on right is Mr. Almasi Maige ATE Chairperson.
Very proud with her team the Director General Mrs. Irene Isaka holding a trophy as an overall winner of the Employer of the year Award under the category of Workforce Focus. On left is Ms. Lightness Mauki Director of Compliance and Registration.
SSRA members of Staff celebrate by holding the trophy from left; Ms. Beatrice Ngong’ho, Ms.Husna Lukosi, Mr. Simon Aikambe and Mr. Innocent Kyara.
Director General of SSRA Mrs. Irene Isaka with her team posing for a group photo after emerging the overall winners of the Employer of the year Award under the category of Workforce Focus 2014. Holding the Trophy is Mr. Ansgar Mushi Director of Research, Actuarial and Policy analysis.
Posing with his team holding trophy is Human Resource and Administration Manager Mr. Teophory Mbilinyi.

TAARIFA YA UFAFANUZI WIZARA YA NISHATI NA MADINI


Katika gazeti la NIPASHE la Jumatatu tarehe 08 Desemba, 2014 ziliandikwa habari kuhusu Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) chini ya kichwa cha habari “Wanaomtetea Muhongo Wajibu haya”. Hoja zilizotolewa katika gazeti hilo zililenga kupotosha ukweli. Wizara inapenda kutoa maelezo kuhusu hoja zilizotolewa kama ifuatavyo:
Utendaji wa Wizara chini ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb)
Taarifa za gazeti hilo zilieleza kuwa utendaji wa Wizara ya Nishati na Madini hasa katika uongozi wa Waziri Muhongo umekuwa ni wa kukatisha tamaa. Moja ya mifano iliyotolewa ni kuendelea kuwepo kwa wachimbaji madini wanaozidi kutorosha madini kwa nia ya kukwepa kodi. Hoja hii haina ukweli wowote kwani chini ya uongozi wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) utendaji wa Wizara umeimarika kwa kiasi kikubwa. Chini ya Uongozi wake kumekuwepo na uwajibikaji mkubwa kwa watumishi wa wizara ili kuhakikisha kuwa wanawatumikia wananchi ipasavyo. Ni katika kipindi chake kumekuwepo na uanzishwaji wa madawati ya ukaguzi wa madini katika viwanja vikubwa vya ndege vya JNIA, KIA na Mwanza chini ya Wakala wa Ukaguzi wa madini (TMAA) ili kudhiditi wachimbaji madini na watu wengine wenye nia ya kutorosha madini nje ya nchi bila kuzingatia sheria. Kutokana na hatua hiyo madini mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 15 yameweza kukamatwa. Madini yaliyokatwa bila kuwa na vibali halali yametaifishwa na Serikali. Serikali ilianza kuuza baadhi ya madini yaliyokamatwa kwa njia ya mnada kwenye Maonyesho ya Vito yaliyofanyika Mjini Arusha kuanzia tarehe 18 - 20 Novemba, 2014. Katika mnada huo jumla ya zaidi ya shilingi milioni 70 zilipatikana na kuingia Serikalini. Serikali itaendelea kupiga mnada madini mengine yaliyokamatwa kwa manufaa ya taifa. Wizara inaendelea kuimarisha udhibiti ili kuhakikisha kuwa mtu yeyote anayekusudia kutorosha madini anakamatwa na kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na madini yake kutaifishwa na Serikali. Katika kusimamia sheria na taratibu, chini ya Uongozi wa Prof.Muhongo, Wizara imedhibiti tabia ya kuchukua vitalu vya madini na kuhodhi ili wale tu wanaozingatia masharti ya leseni ndio waendelee kuvifanyia kazi vitalu. Hili limewaumiza waliokuwa na tabia hiyo ambao kimsingi walikuwa wanavunja sheria. Baadhi ya vitalu vilivyopokonywa vimekuwa vikigawiwa kwa wachimbaji wadogo.Hivyo, si kweli kwamba utendaji wa Wizara ya Nishati na Madini chini ya Prof. Sospeter Muhongo (Mb) ni wa kukatisha tamaa katika kudhibiti utoroshaji wa madini nje ya nchi na katika ukiukwaji wa masharti ya leseni mbalimbali za madini kama ilivyodaiwa.
Upitiaji Mikataba ya Madini
Taarifa za gazeti hilo la NIPASHE la Jumatatu tarehe 08 Desemba, 2014 zilieleza kuwa chini ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) Serikali imeshindwa kupitia mikataba ya madini ili taifa linufaike zaidi. Taarifa hizo si za kweli zinalenga kupotosha umma.
Ukweli ni kuwa chini ya Uongozi wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb), Wizara imepitia mikataba ya madini kwa kufanya majadiliano na Kampuni za uchimbaji madini zenye mikataba ili kurekebisha vipengele vya mikataba ambavyo vinalenga kuleta manufaa zaidi kwa Taifa. Kazi hiyo imefanyika kwa Kampuni zote zenye mikataba na tarehe 9 Oktoba, 2014 Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM) imetiliana saini mkataba wa kurekebisha vipengele katika mkataba uliosainiwa huko nyuma baada ya majadiliano kukamilika. Aidha, majadiliano na Kampuni ya ACACIA (zamani Kampuni ya African Barrick Gold –ABG) yamekamilika na kilichobaki ni pande mbili (Serikali na Kampuni) kusaini marekebisho yaliyofanyika kwa ajili ya mikataba ya migodi yake ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara.
  1. KUKATIKA KWA UMEME

Kukatika kwa umeme kunasababishwa na kuzeeka kwa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji umeme. Ikumbukwe kuwa, kwa kipindi cha karibu miaka kumi TANESCO iliwekwa chini ya PSRC kwa nia ya kubinafsishwa mwaka 1997 – 2007. Katika kipindi hiki TANESCO haikuruhusiwa kuwekeza wala kufanya ukarabati wa miundombinu yake hivyo hali hiyo ilipelekea kuchakaa kwa miundombinu hiyo ikiwemo mfumo wa usafirishaji na usambazaji wa umeme. Hata hivyo baada ya Serikali kubadili mtazamo wake wa kulibinafsisha Shirika, TANESCO mipango kabambe ya kufanya ukarabati wa miundombinu hiyo na kujenga mipya ili kuwa na mfumo wa usafirishaji na usambazaji umeme ulio wa uhakika. Kazi hiyo inaendelea katika sehemu mbalimbali nchini ikiwemo jiji la Dar es Salaam ambako kazi ya kukarabati na kupanua miundombinu ya usambazaji umeme inaendelea. Aidha, TANESCO ilishaelekezwa kutoa taarifa kwa umma kuhusu katizo lolote la umeme lililopangwa kwa ajili ya matengenezo ya miundombinu ya umeme. TANESCO imekuwa ikifanya hivyo kwa kutumia vyombo vya habari vikiwemo televisheni, radio na magazeti na pia kwa kutumia magari ya TANESCO kufikisha taarifa kwa maeneo yanayoathirika. Kwa upande wa katizo la umeme usiotarajiwa, TANESCO inacho kikosi cha dharura ambacho watumishi wake wanafanya kazi masaa ishirini na nne kwa zamu ili kuhakikisha kuwa hitilafu ndogondogo zinatatuliwa mara moja zinapojitokeza. Jamii ya Watanzania wanalishuhudia hilo.


  1. DENI LA TANESCO LAPAA.

Mpaka kufikia mwanzoni mwa mwaka 2014, deni la TANESCO lilikuwa limefikia takribani Shilingi bilioni 695.30. TANESCO kwa kutumia vyanzo vyake vya fedha kutokana na ukusunyaji wa maduhuli ndani ya kipindi cha miezi 11 imepunguza deni hilo mpaka kufika takribani Shilingi bilioni 355.11. Kukua kwa deni la TANESCO kulisababishwa na hali ya ukame uliolikumba taifa kuanzia miaka ya 2011 ambapo TANESCO ililazimika kununua umeme aghali kutoka kwa wazalishaji wa umeme binafsi ikiwemo mitambo ya kukodi ya dharura. Deni hilo lilikua kama ifuatavyo:

Mwaka Deni (Bilioni Sh.)
2011           538.47
2012            563.02
2013           695.30
2014 (9 Disemba) 355,11

TANESCO imeongeza ufanisi wake katika kukusanya maduhuri na kufikia kiwango cha asilimia 97 na fedha inayopatikana inatumika kupanua huduma ya umeme nchini, kuendesha Shirika na kulipa madeni inayodaiwa.

Ukweli ni kwamba deni la TANESCO limeshuka kwa kiasi kikubwa na kwa sasa TANESCO imeweka mkakati maalumu wa kuwalipa wadeni wake wakubwa kiasi cha Shilingi bilioni tatu kwa wiki kwa kila mdai, hivyo ni matarajio ya Shirika kumaliza deni hilo mwaka kesho (2015).

  1. NCHI ITASONGA MBELE

Wazo la kuanzishwa kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) lilibuniwa na watumishi na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini mwaka 2005/6 chini ya uongozi wa Nazir Karamagi akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Taratibu za kuanzishwa kwa REA zilikamilika mwaka 2007 ambapo REA ilianza kutekeleza majukumu yake.

Mheshimiwa Sospeter Muhongo baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini ameisaidia REA kupata fedha kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo na hivyo amesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kwa kasi ya kupeleka huduma ya umeme vijijini.

Aidha, Ili kufikia lengo la kuwaunganishia umeme asilimia 30 ya watanzania ifikapo mwaka 2015, Chini ya uongozi wa Waziri Muhongo Serikali kupitia TANESCO, ilipunguza gharama za kuunganisha umeme wa njia moja (single phase) kwa wateja wadogo kwa wastani wa kati ya asilimia 30 na 77 kama ifuatavyo:

  1. Kwa wateja watakaojengewa njia moja (single phase) kwenye umbali usiozidi mita 30 bila kuhitaji nguzo, katika maeneo ya vijijini watalipa Shilingi 177,000na wa mijini watalipa Shilingi 320,960 badala ya Shilingi 455,108 zinazolipwa na wateja hao kwa sasa.


  1. Kwa wateja watakaojengewa njia moja (single phase) na kuwekewa nguzo moja, katika maeneo ya vijijini ni Shilingi 337,740 na wa mijini ni Shilingi 515,618badala ya Shilingi 1,351,884 zinazolipwa na wateja hao kwa sasa.


  1. Kwa wateja watakaojengewa njia moja na kuwekewa nguzo mbili katika maeneo ya vijijini ni Shilingi454,654 na wa mijini ni Shilingi 696,670 badala ya Shilingi 2,001,422 zinazolipwa na wateja hao kwa sasa.


Kwa ujumla katika kipindi hiki huduma ya umeme nchini imepanuka na kuwa bora zaidi kuliko siku za nyuma. Ni matarajio ya Serikali kuwa huduma hii itazidi kuwa bora zaidi katika siku chache zijazo kutokana na juhudi kubwa zinazoendelea katika sekta ndogo ya umeme.

  1. DALALI WA FEDHA ZA ESCROW

Waziri wa Nishati na Madini ndiye msimamizi mkuu wa masuala yanayohusu sekta za Nishati na Madini nchini. Mtambo wa IPTL ulijengwa kwa ajili ya kufua umeme unaotumiwa na jamii ya watanzania. Kuwepo kwa mgogoro kungeweza kuondoa azma ya uwepo wa mtambo huo ya kufua umeme ili kuliepusha Taifa kuingia katika mgawo wa umeme kutokana na upungufu wa upatikanaji wa nishati hiyo, hivyo lilikuwa ni jukumu lake kuona kuwa mgogoro wa wawekezaji wa mitambo ya IPTL unakwisha ili mitambo iendelee kutoa huduma ya umeme kwa Taifa. Jukumu la Waziri ni kusimamia Sera, Sheria na taratibu katika sekta anazozisimamia. Katika kufanya hivyo, Waziri hukutana na wadau na kujadili masuala kwa uwazi bila kificho kwa nia ya kujenga nchi na kuhakikisha kuwa maslahi ya Taifa ndiyo kipaumbele. Kwa hiyo mikutano na Wadau ikiwa ni pamoja na wawekezaji hufanyika si kwa udalali. Suala la fedha za akaunti ya Escrow lilihusu uamuzi wa mahakama iliyojiridhisha kuwa mnunuzi wa hisa zote za VIP na MECHMAR ni halali na alitakiwa kukabidhiwa mali na madeni ya IPTL. Mali ni pamoja na kiasi cha fedha stahiki kwenye Akaunti ya Escrow ambazo hata hivyo ilidhihirika kuwa hazitoshi kukidhi deni halali.

Akaunti hiyo ilikuwa na Sh. 182 bilioni wakati malipo yaliyokubalika kwa pande zote (IPTL na TANESCO) kwa mujibu wa maamuzi ya ICSID I yalikuwa Sh. 306 bilioni. Kumwita Waziri wa Nishati na Madini kuwa ni dalali ni kupotosha ukweli.

Tuesday, December 30, 2014

Miss Tanzania 2014 asaidia kituo cha New Life Orphans Home,Boko jijini Dar

Miss Tanzania Lilian Kamazima (kulia) akimkabidhi zawadi ya mwaka mpya Msimamizi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life kilichopo Boko, Mwanaisha Magambo kwa ajili ya watoto 102 waliopo kituoni hapo, tukio hilo lilifanyika juzi.
Miss Tanzania Lilian Kamazima (kulia) akiwa na Miss Kinondoni Maria Shila wakiwa wamembeba mtoto aliekuwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life cha Boko, mtoto huyo alifikishwa hapo akiwa na siku nne tu tangia kuzaliwa kwake.
Sehemu ya Watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life kilichopo Boko,wakimsikiliza Miss Tanzania Lilian Kamazima.
Miss Tanzania Lilian Kamazima (kulia) akiwa na watoto katika kituo cha New Life cha Boko.

Redds Miss Tanzania 2014 Lilian Deus Kamazima jumapili iliyopita alitoa misaada ya vyakula vya aina mbalimbali kwa kituo cha New Life Orphans Home kilichopo eneo la Boko nje kidogo ya jiji la D’salaam. 

Kituo hicho ambacho kilianzishwa mwaka 2005 awali kilikuwa maeneo ya magomeni makuti kilianza na watoto yatima 17 na baadae kuongezeka hadi kufikia 70. Na kulazimika kuhama eneo hilo na kuhamia kigogo ambapo waliishi eneo hilo hadi hivi karibuni walipopata mfadhili mmoja kutoka nchini Qatar ambaye amewajengea jumba moja kubwa na la kisasa eneo la Boko Dawasa, alisema bi Mwanaidi Magambo ambaye ni Mlezi wa Kituo hicho. 

Kituo hicho kina watoto wapatao 105 ambapo  60 kati yao ni wasichana na 45 wavulana. Kituo hicho kinalea watoto wadogo kabisa wa umri wa mwezi mmoja hadi miaka 18. Hivi karibuni tulimpokea mtoto mwenye umri wa siku 5 kutoka hospitali ya wilaya ya Temeke ambaye mama yake alifariki mara tu baada ya kujifungua, alisema bi. Magambo. 

Kituo hicho kwa sasa kina matatizo ya vyakula, vitanda, magodoro, madaftari pamoja na sare za shule kwa ajili ya watoto hao yatima. Bi Magambo alimshukuru sana Mfadhili huyo kutoka nchi ya Qatar kwa kuwajengea jengo hilo, lakini alisema kwa sasa watahitaji mfadhili wa kuwalipia bili za umeme na maji pamoja na mahitaji mengine kituoni hapo. 

Kituo hicho kina bahati ya kutembelea na warembo wa Miss Tanzania ambapo mwaka 2007,  Miss Tanzania 2000 Jacqueline Ntuyabariwe alitembelea kituo hicho wakati bado wapo eneo la Magomeni Makuti na kuwapatia misaada mbalimbali. 

Miss Tanzania 2014 Lilian Kamazima alikabidhi vyakula vya aina mbalimbali ikiwemo mchele, unga wa ngano, sembe, sukari, maharage, mafuta ya kupikia, sabuni, soda, juisi, maji ya kunywa, na biskut vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni mbili. 

Miss Tanzania 2014 Lilian aliishukuru kampuni ya Swissport Tanzania ambao ndio waliofadhili ziara yake hiyo, na kuwaomba watanzania wengine kujitokeza kwa wingi kusaidia watoto yatima na wengine wanaoishi katika mazingira magumu. 

Ziara hiyo ya mrembo wa Taifa Lilian ilikuwa ni zawadi ya sikukuu za mwisho wa mwaka ambao ililenga kuwafariji watoto waliopoteza wazazi wao kwa namna moja au nyingine, na pia kutimiza Kauli mbiu ya mashindano ya urembo ya Miss Tanzania isemayo [Beauty with Purpose] Urembo na Malengo. 

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AAGANA NA MABALOZI WA URUSI, CANADA NA ALGERIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Mhe. Djelloul Tabel, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 30, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Zoka, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 30, 2014 kwa ajili ya kumuaga akienda kuanza kazi rasmi nchini Canada.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Alexander Rannkikh, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 30, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Mhe. Djelloul Tabel, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 30, 2014 alipofika kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Zoka, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 30, 2014 alipofika kumuaga akienda kuanza kazi rasmi nchini Canada.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Alexander Rannkikh, baada ya mazungumzo yao alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 30, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Zoka, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Desemba 30, 2014 kwa ajili ya kumuaga akienda kuanza kazi rasmi nchini Canada. Picha na OMR

mwanafunzi wa MUCE alamba Mil. 3 za BayPort

Ruth Bura, Mratibu wa Bima ya Elimu Bayport Tanzania kulia akimkabidhi hundi bwana Kennedy Kaupenda kwa ajili ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu baada ya kufariki mzazi wake. 
Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania, Ruth Bura kulia, akizungumza jambo katika makabidhiano ya hundi kwa bwana  Kennedy Kaupenda kushoto kwake, Makao Makuu ya Bayport, mapema wiki hii. 

TAASISI ya kifedha ya inayojihusisha na mambo ya mikopo ya Bayport Tanzania, imempatia Sh Milioni tatu (3,000,000) mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa (MUCE), Kennedy Kaupenda, kufuatia huduma mpya ya Bima ya Elimu inayoendeshwa na taasisi hiyo nchini.

Huduma hiyo mpya ya Bima ya Elimu ya Bayport Tanzania ilianza mapema mwaka huu kwa ajili ya kuwapatia fursa wanafunzi kuendelea na masomo baada ya mzazi aliyejiunga na huduma hiyo kufariki Dunia.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Bima ya Elimu inayotolewa na Bayport Tanzania, Ruth Bura, alisema Kaupenda alitajwa kama mnufaika kwa mzazi wake aliyefariki Dunia, hivyo waliamua kumtafuta kwa ajili ya kumpatia mafao yake kwa ajili ya kuendelea kupata elimu bila vipingamizi vyovyote.

Alisema huduma hiyo ina vipengele vine ambavyo ni Bronze, Gold, Silver na Exucutive, huku akisema kuwa makato ya kila mwezi ya Bronze ni Sh 2,500, ambapo fao lake ni Sh Milioni 3, wakati makato ya Gold ni Sh 6,250, huku fao lake likiwa ni Sh 7,500,000.

“Pia tunacho kipengele cha Silver ambapo makato yake kwa mwezi ni Sh 3,800, huku mteja akilipwa fao la Sh Milioni 4,500,000 na kipengele cha Executive kikihusisha makato ya Sh 9,000 na kumpatia mteja fao la Sh 10,800,000, huku tukiamini kuwa huduma hii ni sehemu ya kuhakikisha kuwa Watanzania wanawawekea ulinzi wa elimu watoto wao na yoyote wanayemchagua wao,” alisema Ruth.

Akizungumzia fao hilo, Kaupenda alisema hakuwa na imani kuwa angesoma vizuri baada ya baba yake kufariki, ila baada ya kutafutwa na Bayport na kutaarifiwa juu ya mafao hayo, amepata nguvu mpya.

“Nasikitika sana baba kwa kunificha juu ya kujiunga na huduma hii sambamba na kuwa mkopaji wa Bayport, hata hivyo namshukuru kwasababu fedha hizi zimekuja kunipa mwanga mpya wa kuhakikisha kuwa nasoma kwa bidii, nikiamini kiasi cha Sh Milioni tatu kitaniweka katika wakati mzuri mno,” alisema Kaupenda, huku akiwasisitiza wazazi kujiunga kwenye huduma hiyo kwa manufaa ya familia zao.

Mbali na huduma hiyo ya Bima ya Elimu kwa uwapendao, pia Bayport inajihusisha na mikopo kwa watumishi wa umma na kampuni zilizoidhinishwa, ambapo mwishoni mwa mwaka 2014 walizindua huduma ya Mikopo ya Bidhaa, ambapo bidhaa za bodaboda aina ya Lifan, Toyo na Boxer zinakopeshwa kwa wateja wa Bayport Tanzania.

Matukio ya kutishia amani ya nchi na usalama wa raia yatapungua kama mabalozi wa nyumba kumi watafanya kazi zao kwa uaminifu - Vuai Ally Vuai

Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi

Matukio ya kutishia amani ya nchi na usalama wa raia yatapungua kama mabalozi wa nyumba kumi watafanya kazi zao kwa uaminifu kwani wao ni viongozi wa kwanza walio karibu na wananchi hivyo basi wanatakiwa kuwafahamu wakazi wa maeneo yao.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Vuai Ally Vuai wakati akifungua semina ya siku moja ya  uwezeshaji wa chama hicho kwa  mabalozi (viongozi wa mashina) wa wilaya ya Lindi mjini.

Vuai alisema Balozi ni kiongozi wa kwanza anayetakiwa kujua idadi ya wakazi wake, kazi wanazozifanya na majina yao kitendo ambacho kitasaidia kuimarisha usalama wa eneo husika lakini miaka ya hivi karibuni wameacha kufanya kazi hiyo kwa uadilifu na kuviachia vyombo vya dola pekee.

“Jukumu la kulinda amani ya nchi na usalama wa taifa letu ni la kila mtu, lakini hivi sasa kazi hiyo vimeachiwa vyombo vya dola pekee, mabalozi fanyeni kazi ya kuwatambua wakazi wa maeneo mnayoishi hii itasaidia kumtambua mualifu pale atakapofika katika eneo lenu”, alisema Vuai.

Alisema kikao cha kwanza cha CCM ni kikao cha shina hivyo basi mabalozi ni viongozi wa muhimu ndani ya shina wanatakiwa kutetea ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010 na kutowaachia viongozi wakuu wa chama pekee kufanya kazi hiyo.

Vuai alisisitiza, “Muwe na uthubutu wa kujibu hoja potofu za wapinzani na kutokubali wawapotoshe wananchi juu ya mafanikio yaliyofanywa na Serikali. Kipindi cha uchaguzi kikifika endeleeni kuwahimiza na kuwasimamia wananchi wakapige kura ili wasipoteze haki yao ya msingi ya kupiga kura”.

Aliwataka mabalozi hao kuhakikisha wakati wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika hapo mwakani wawahimize  wananchi ili waweze kujitokeza kwa wingi kujiandikisha majina yao.

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete alisema mabalozi ni msingi na nguzo ya chama bila ya mabalozi chama hakiwezi kwenda vizuri ni kama vile binadamu anaweza kuwa na kila kitu lakini kama hana miguu hawezi kutembea.

Aliwapongeza kwa ushindi walioupata wakati wa uchaguzi wa Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za mitaa na kusema kuwa upendo na mshikamano ni msingi wa ushindi na usiri na uadilifu ni nyenzo muhimu katika utendaji wao wa kazi.

“Katika semina hii mtafundishwa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kazi na wajibu wenu kwa Chama na Jamii inayowazunguka hivyo basi muwe wasikivu na kuyashika yale mtakayofundishwa na watoa mada”, alisisitiza Mama Kikwete.

Akiongea kwa niaba ya wajumbe walioshiriki semina hiyo Rashid Thabit kutoka kata ya Rahaleo alishukuru kwa mafunzo waliyoyapata na kusema kuwa yatawasaidia katika utendaji wao wa kazi.

“Tunakushukuru MNEC kwa ajili ya kuandaa mafunzo haya ambayo yametupa uelewa na wajibu na kazi zetu kama mabalozi. Uwepo wako wakati wa uchaguzi uliopita ulitufanya tukashinda kwani tulishiriki pamoja nawe katika kampeni za kuwanadi wagombea wetu”.

Nawaomba wajumbe wenzangu tusibweteke na ushindi huu bali tuongeze kasi na bidii na kuweza kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu utakaofanyika hapo mwakani ili tuweze kulikomboa jimbo la Lindi mjini kutoka mikononi mwa Chama Cha Wananchi (CUF)”, alisema Thabit.

Semina hiyo ya siku moja iliyohudhuriwa na wajumbe 993 kutoka kata zote 18 za wilaya hiyo iliandaliwa na Mama Kikwete ambaye aliwaahidi mabalozi kuwapa mafunzo hayo ili wajue majukumu yao ya kazi. Mada zilizojadiliwa ni kazi na wajibu wa mabalozi na katiba mpya iliyopendekezwa.

UNATAKA AU UMEFUNGUA KAMPUNI, JE WAJUA NAMNA YA KUNUNUA, KUUZA HISA


Na  Bashir  Yakub

Katika adhma ya  ya mwendelezo wa makala za namna ya kuendesha kampuni leo tena tuangalie  kuhusu hisa na hasa namna ya kuhamisha hisa.

HISA NININI.
Kwa maana ambayo inaweza kueleweka kwa wepesi zaidi  ni kusema kuwa hisa  ni aina ya maslahi ya mtu ya katika kampuni.Natumia neno aina kwakuwa maslahi katika kampuni ni mengi si hisa tu isipokuwa hisa ni mojawapo ya maslahi. Hivyo kile ambacho mtu anamiliki katika kampuni  ndio hisa zake. Hisa hutofautiana kutokana na uwezo wa mtu kwa maana wapo wenye hisa ndogo wapo wenye kubwa na kati.

KUUZA  NA  KUNUNUA  HISA.
Hisa ni mali inayohamishika. Ni mali sawa na mali nyingine zozote zinazohamishika. Kama ambavyo mali nyingine zinaweza kununuliwa au kuuzwa, kutolewa zawadi na kurithiwa ndivyo pia hata hisa zinavyoweza kuwa.Hii yote huitwa kuhama kwa hisa. Kuhama kwa hisa kwa lugha ya kitaalam  ambayo ndio hutumika katika katiba za makampuni ni ( Transfer of shares). Mara nyingi suala la  kuuziana hisa linawahusu wanahisa wenyewe na hivyo  wanahisa wanapokuwa wameuziana hisa au wamepeana zawadi   ni lazima nyaraka inayoonesha muamala huo wa mauziano au zawadi ambayo ina muhuli wa wakili  iwasilishwe kwenye uongozi wa kampuni kwa ajili ya kusajiliwa.  Kama hakuna nyaraka yoyote iliyowasilishwa mbele ya kampuni  kuthibitisha uhamisho  ni kosa kampuni kusajili uhamisho au mauziano hayo.

KAMPUNI KUKATAA MAUZIANO
Pamoja na hayo kampuni inao uwezo wa kukataa mauziano ya hisa. Sababu zinazoweza kuifanya kampuni ikatae uhamisho ni pamoja na  iwapo taratibu za uhamisho zimekiukwa kwa mfano  nyaraka ya mauziano haina muhuli wa wakili, pia kampuni yaweza isitambue uhamisho wa hisa iwapo  mtu anayepewa hisa ambaye sasa ndo anaingia katika kampuni  wanahisa wengine hawamtaki . Na hili zaidi  linawezekana katika makampuni binafsi  ambako mtu hawezi kuwa mmoja  wa wanakampuni bila ridhaa ya wenzake aliowakuta. Au kama  ni suala la kifo na hisa inabidi zihamishwe  kwenda kwa  msimamizi wa mirathi pia wanahisa wanaweza wakamkatalia.Haya yote ni mazingira ambamo uhamisho wa hisa unaweza kukataliwa na kampuni. Wakati kampuni itapokataa uhamisho wa hisa itatakiwa ndani ya siku sitini kutoa taarifa ya maandishi kwenda  kwa mtu aliyekuwa amewasilisha nyaraka ya kuuziwa,kuuza au kurithishwa kwenye kampuni.Taarifa ya maandishi itamtaarifu  kukataliwa kwake ikiwa ni pamoja na sababu za kukataliwa huko. Kukataa kwa kampuni  hapa inamaanisha kukataa kwa wakurugenzi. Sheria imewapa wakurugenzi mamlaka ya kumkatalia yoyote  na hata bila kutoa sababu za  kukataa.

KAMPUNI  KUKUBALI MAUZIANO.
Aidha kama  aliyepewa hisa atakuwa amekubaliwa basi moja kwa moja atapewa cheti cha umiliki wa hisa(certificate of share) kikieleza kiasi cha hisa anazomiliki ikiwa ni pamoja na tarehe ambayo ameanza umiliki. Aliyepewa hisa ataingizwa katika kumbukumbu za kampuni na atawajibka kwa masharti yaleyale  kama aliyokuwa akiwajibikia  yule aliyemuuzia, aliyempa zawadi au aliyemrithisha. Pamoja na hayo ikiwa ni suala la kuhamisha  hisa  kwa njia ya kutoka kwa marehemu  kwenda kwa msimamizi wa mirathi basi ni lazima kwa msimamizi wa mirathi kuleta hati ya usimamizi wa mirathi kutoka mahakamani ili kuthibitisha uhalali wa kuhamishiwa hisa na iwapo atafanikiwa kufanya hivyo na akakubaliwa na kampuni basi atakuwa na haki sawa na haki alizokuwa nazo marehemu  ikiwa ni pamoja na kuuza ikiwa atataka kufanya hivyo.

KUGUSHI  KATIKA  MAUZIANO
Lipo jambo jingine ambalo huwa linajitokeza sana katika kuuziana hisa ambalo ni kughushi. Mara nyingi muhuri sahihi au hata tarehe huwa vinaghushiwa ili kutimiza malengo fulanifulani. Juzijuzi  katika sakata la ya Escrow hili limejitokeza sana. Hata kipindi cha Richmond na  EPA kughushi katika kuuziana hisa kulijitokeza. Nje ya kuwa kosa la jinai katika Kanuni za Adhabu(Penal Code)  katika masuala ya kampuni pia lina athari zifuatazo ;Kwanza mauziano hayo yanakuwa haramu na aliyenunua hawezi kuhesabika kama mwanahisa katika kampuni. Pili, kama kuna uzembe kampuni  ilifanya mpaka mtu kuuziwa hisa ghushi kampuni itatakiwa kumlipa  mnunuzi fidia pamoja na gharama, na tatu  kama kampuni haikufanya uzembe isipokuwa ni mtumishi fulani au mwanahisa basi huyohuyo atalazimika  kurudisha hasara za kampuni ilizopata  katika kulipa fidia kwa muathirika. Wiki ijayo tena katika mwendelezo wa namna ya kuendesha kampuni.

MWANDISHI  WA   MAKALA   HAYA  NI  MWANASHERIA NA MSHAURI   WA   MASUALA  YA  SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI   LA   HABARI  LEO KILA  JUMANNE, GAZETI JAMHURI  JUMANNE  NA  NIPASHE  JUMATANO.
0784482959
0714047241
bashiryakub@ymail.com




Music Planet ilivyobamba jijini Dar

Twaba kwa Red Carpet
Wapenzi wa music planet wakipata picha kabla ya kuzama ndani ya Music Planet iliyofanyika Samaki Samaki mpya ya Masaki,jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyoisha.
Masai wakiimba nyimbo zao juu ya mangoma makali kutoka kwa DJ Gabi ikiwa ni mambo ya Music Planet iliyofanyika Samaki Samaki mpya ya Masaki,jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyoisha.
Wapenzi wa Music Planet.
Tequila girl never misses matukio kama haya,ukimsemesha tu anakudunga shot.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya,Mad Ice akiangusha bonge moja la show sambamba na bendi yake katika Music Planet iliyofanyika Samaki Samaki mpya ya Masaki,jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyoisha.
red carpet smile ndani ya Music Planet.
tabasamu mwanana kwa wadau wakati Music Planet iliyofanyika Samaki Samaki mpya ya Masaki,jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyoisha.
Dj Cartel the undisputed champion 4 rounds wins all by K.O akifanya yake ndani ya Music Planet iliyofanyika Samaki Samaki mpya ya Masaki,jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyoisha.
Mdau Twaba Akiicharaza tumba sambamba na magoma ya DJ Cartel.
Mdau Edward Lusala (kulia) na Mwanamuziki Mad Ice (pili shoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wadau walioika kwenye Music Planet iliyofanyika Samaki Samaki mpya ya Masaki,jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyoisha.
Mdau Carlos ambaye ni Mwanzilishi na C.E.O wa Samaki Samaki zote hapa mjini (kulia) akiwa na swaiba wake wa longtime wakienjoy Music Planet iliyofanyika Samaki Samaki mpya ya Masaki,jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyoisha. .
Dj Dully smart on the One n Two.
Tayana (kati) na Mashost zake wakienjoy Music Planet iliyofanyika Samaki Samaki mpya ya Masaki,jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyoisha.

Monday, December 29, 2014

MBUNGE WA MOROGORO MJINI AZIZ ABOOD AENDELEA KUTEKELEZA AHADI ZAKE KATIKA KATA MBALIMBALI

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akiwasikiliza Viongozi wa CCM wa Kata ya Konga wakati wa Ofisi ya kata hiyo Mara baada ya Mh Mbunge Kufanya Ukaguzi hiyo Na Kuahidi kutoa Msaada wa Bati 100 Kwajili ya Kumalizia Ujenzi wa Ofisi hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akitoa maagizo kwa Mtendaji wa Kata ya Konga Kutafuta Eneo la Ujenzi wa Shule Hiyo haraka Iwezekanavyo.Mh Abood amemuagiza Mtendaji huyo ndani ya mwezi
Mmmoja wa amepata Eneo la Ujenzi wa Shule na Ujenzi Uanze Mara Moja Ambapo Mh Mbunge Amechangia Shilingi Milion 5 za Kuanza Ujenzi Huo .
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akiongea na Wato wa Kata ya Kauzeni  mara baad ya Kuwasili katika Kata hiyo kwajili ya Kusikiliza Kero Zinazowakabili wakazi wa Kata Hiyo.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya kauzeni walioudhuria Mkutano ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini.


Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood Akisisitiza Jambo wakati akielezea Namna ya Kutatua Kero kubwa ya Maji Inayowakabili wakazi wa Kata ya Kauzeni Iliyopo Manispaa ya Morogoro Ambapo Mh Aziz Abood Ametoa Million 5 Kwajili ya Kutekeleza Mradi wa Maji wa Kata Hiyo Ili Kutatua Kero Hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akitoa Onyo wa Watendaji wa Kata za Jimbo la Morogoro Mjini Kutumia Fedha Zinazoletwa katika Kata Hiyo kwa Maendeleao ya wananchi lasivyo Watakiona kwa wale watakaofuja  Fedha za Wananchi.
Bi Asha Ally akieleza Kwa Uchungu Kero Kubwa ya maji Inayowakabili wakazi wa Kata ya Kuuzeni.


Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiandika Kero za wananchi wa kata ya Kauzeni Mara baada ya Kuwapa nafasi wa kata Hiyo kueleza Kero zao.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akikabidhi vifaa vya Michezo wa Timu ya kata ya Kauzeni kwajili ya Kuendeleza Michezo ndani ya kata hiyo
Wachezaji wa Timu ya Mzinga ya Morogoro wakimsikiliza  Kwa makini Mbunge wa Morogoro Mjini alipowatembelea Leo.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akikabidhi vifaa vya Michezo kwa Timu ya Mzinga ya Morogoro akiwa kama Mdau Mkubwa wa Michezo hasa Mpira wa Miguu
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea na wandesha bodaboda kutoka kata ya mzinga namna wanavyokabiliwa na changamoto zinazowakabilikatika biashara yao.