Thursday, March 31, 2016

Tanzanian Health Care Gets Boost from AKU’s New Nursing/Midwifery Training Facility

Aga Khan University opened the new home of its School of Nursing and Midwifery in Dar es Salaam today at Salama House. This state-of-the-art facility will educate nursing and midwifery leaders dedicated to saving lives and improving health care for the people of Tanzania. Since 2004, AKU has graduated more than 2,100 nurses in East Africa of which 600 are in Tanzania. Notable alumni of AKU include the country’s top nursing official – the Director of the Division of Nursing and Midwifery Services in the Ministry of Health – and the Chair of the Tanzania Nursing and Midwifery Council.

The €1.2 million (TSh 2.95 billion) Salama House project was funded as part of a €17.2 million (TSh 42 billion) grant to AKU from the Federal Republic of Germany to improve health in East Africa by providing nurses and midwives with high-quality education and training.

In addition to funding the renovation and expansion of Salama House, the grant includes funding to enable more students to attend AKU and has helped the University to develop the curriculum for its planned post-RM Bachelor of Science in Midwifery. The East African Community played an important role in making it possible for AKU to receive the funding.
Dr. Gerd Müller, German Federal Minister for Economic Cooperation and Development and Mr. AlKarim Haji, AKU Vice President, Finance and Chief Financial Officer unveiling the plaque to mark the official opening of the Aga Khan University Salama house
The opening was presided over by Dr. Gerd Müller, German Federal Minister for Economic Cooperation and Development; Dr. Helmut Schön, KfW Country Director for Tanzania; Dr. Richard Sezibera, Secretary General of the East African Community; Dr. Hamisi Kigwangalla, Tanzanian Deputy Minister of Health, Community Development, Gender, Elderly, and Children representing Minister Ms. Ummy Ally Mwalimu; and Mr. Al-Karim Haji, AKU Vice President, Finance and Chief Financial Officer.

“Despite all efforts maternal and newborn mortality are still unacceptably high in East Africa. Reducing them requires well-functioning health systems, including a skilled workforce. I am glad we found such able partners in the Aga Khan University and the EAC who will help achieve Sustainable Development Goal No. 3 – “Good health and wellbeing for all” – for all citizens of the East African Community and of Tanzania in particular,” stated Dr. Gerd Müller, German Federal Minister for Economic Cooperation and Development.
Dr. Richard Sezibera, Secretary General of the East African Community addressing the invited guests during the official opening of the Aga Khan University Salama house
“Tanzania has a fraction of the highly skilled nurses and midwives it needs. More modern facilities for nursing and midwifery education are needed,” said Mr. Al-Karim Haji, AKU Vice President, Finance and Chief Financial Officer. “With the opening of the new home of our School of Nursing and Midwifery, we are helping to change that. The partnership between AKU, the Federal Republic of Germany and the East African Community, plus the support of the Republic of Tanzania, will give more nurses and midwives an opportunity to improve their clinical and leadership capacities.”

“Aga Khan University is playing a leading role in the EAC’s effort to harmonize and modernize nursing curricula and standards across member states,” said Dr. Richard Sezibera, Secretary General of the East African Community. “This facility is another example of AKU’s longstanding commitment to educating much-needed nurses and midwives to improve the quality of health care for East Africans, and of the Aga Khan Development Network’s broader contribution to improving the lives of East Africans.”
Hon. Dr. Hamisi Kigwangalla, Deputy Minister of Health, Community Development, Gender, Elderly, and Children during his speech at the official open of the Salama house at the Aga Khan University
“The opening of this facility is a significant event in the development of nursing and midwifery in Tanzania,” said Hon. Dr. Hamisi Kigwangalla, Deputy Minister of Health, Community Development, Gender, Elderly, and Children on behalf of Ms. Ummy Mwalimu, the Minister of Health, Community Development, Gender, Elderly, and Children. “It will help Tanzania educate the kinds of nurses and midwives we need: those who can tackle complex problems and ensure that all Tanzanians get the health care they deserve. Aga Khan University, the Federal Republic of Germany, and the East African Community have our appreciation.”

AKU’s School of Nursing and Midwifery’s new home at Salama House on Urambo Street includes the resources needed to educate nursing and midwifery leaders using the latest methods: a library with new digital resources, a computer lab, modern classrooms, and a high-quality science lab and skills lab. In addition to enhancing the quality of the School’s existing nursing programmes, additional space has been added that will allow AKU to launch a new post-RM Bachelor of Science in Midwifery programme and to train more working nurses through its professional development programmes.

About AKU’s School of Nursing and Midwifery and Aga Khan Development Network

In Tanzania, AKU trains educators, specialist doctors, nurses and midwives. AKU has educated more than 600 nurses, including 311 who hold a Post-RN Bachelor of Science in Nursing; a degree that prepares graduates for leadership and that is held by relatively few Tanzanians. Its alumni include the country’s top nursing official – the Director of the Division of Nursing and Midwifery Services in the Ministry of Health – and the Chair of the Tanzania Nursing and Midwifery Council.

Aga Khan University is a not-for-profit institution that serves Tanzanians without regard to race, gender, or religion. All of its nursing students in Dar es Salaam are Tanzanian and 80 percent come from publicsector institutions. As a nonprofit organization, it strives to make its programmes affordable and accessible. On average, nursing students pay just one-fifth of what it costs the University to educate them. To date, the University has invested US$ 60 million in Tanzania, with significant additional investment planned.

AKU is a university of and for the developing world, focused on preparing men and women to improve the quality of life in their societies. Its work reflects the vision and continuing generosity of its founder and Chancellor, His Highness the Aga Khan. The University is part of the Aga Khan Development Network (AKDN), whose presence in Tanzania dates back to the establishment of the first Aga Khan Girls School in 1905. AKDN has been contributing to the health of Tanzanians for over 85 years.

In 2015, AKDN’s health services treated more than 430,000 inpatients and outpatients across Tanzania. AKDN is a private, international, non-denominational development organisation. It employs over 80,000 people in over 30 countries. Its agencies address complex development issues, including the provision of quality health care and education services, cultural and economic revitalisation, micro-enterprise, entrepreneurship and economic development, the advancement of civil society, and the protection of the environment.

About the East African Community

The East African Community (EAC) is a regional intergovernmental organisation of 5 Partner States: the Republics of Burundi, Kenya, Rwanda, the United Republic of Tanzania, and the Republic of Uganda, with its headquarters in Arusha, Tanzania.

The work of the EAC is guided by its Treaty which established the Community. It was signed on 30 November 1999 and entered into force on 7 July 2000 following its ratification by the original three Partner States - Kenya, Tanzania and Uganda. The Republic of Rwanda and the Republic of Burundi acceded to the EAC Treaty on 18 June 2007 and became full Members of the Community with effect from 1 July 2007.

SERIKALI KUIWEZESHA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI KUHAKIKI RASILIMALI NA MADENI YA VIONGOZI WA UMMA

Na Mwandishi wetu.
SERIKALI imesema kuwa italipa kipaumbele suala la uhakiki wa mali za viongozi wa umma  kwa kuiwezesha Sekretarieti ya Maadili ya viongozi kufanya kazi zake  kwa ukamilifu kwa mujibu wa Sheria ya  Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa imetembelea ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma kujua majukumu, mafanikio na changamoto zinazoikabili Taasisi hiyo  ili wakifika bungeni waweze kuisemea.

“Suala la uhakiki wa rasilimali na madeni ya viongozi tutahakikisha linapewa kipaumbele katika Awamu hii ya tano ya  uongozi,” amesema.
Kwa mujibu wa Waziri Kairuki, Serikali itajitahidi kuongeza jitihada ili uhakiki  wa rasilimali na madeni ya viongozi wa Umma ufanyike,  pamoja na kuiongezea Taasisi hiyo bajeti ya kutosha.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukum u ya ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Mhe  Salome Kaganda amesema viongozi wengi wanarejesha fomu za raslimali na madeni, ila wapo wachache wanaoshindwa kurejesha fomu hizo.
Amesema, “Tangu mwaka 2005/06 hadi mwaka 2014/15 tumesambaza  fomu 78,786, lakini fomu zilizorejeshwa ni 60,948 ambazo ni sawa na asilimia 77 ya fomu zote zilizosambazwa.”

Aidha Kamishna huyo amewaambia  wajumbe wa kamati hiyo ya Bunge kuwa tangu mwaka 2013 hadi 2015 Sekretarieti yake haikufanya uhakiki wa rasilimali na madeni kwa viongozi wa umma kutokana na  ufinyu wa bajeti.
Kwa upande wao baadhi ya Wajumbe wa kamati wamesema kuwa wataishauri serikali kuiongezea Sekretarieti bajeti ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sharia.

Pia wamependekeza kufanyiwa maboresho Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995 ili iwe na nguvu zaidi na kuwaruhusu kuwafikisha mahakamani viongozi wanaokiuka sharia hiyo.

Sekretarieti ya Maadil  ilianza kufanya kazi rasmi mwezi Julai, 1996 ikiwa na jukumu la msingi la kujenga na kukuza uadilifu miongoni mwa Viongozi wa Umma kwa kusimamia utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Maadili ya viongozi wa umma Na 13 ya mwaka 1995.

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya jamii yatembelea mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya TBC-Kisarawe.

 Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya jamii wakipitia taarifa ya shirika la utangazaji Tanzania (TBC) kuhusiana na upanuzi wa masafa ya usikivu kisarawe pwani na maendeleo yake.
Mkurugenzi wa shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw.Ayoub Ryoba akiwasilisha  taarifa ya shirika hilo  kwa wajumbe wa wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii kuhusiana na upanuzi wa masafa ya usikivu kisarawe Pwani.Wengine pichani ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye,Naibu Waziri wa wizara hiyo Bi.Anastazia Wambura na mwenyekiti wa kamati hiyo Bw.Peter Serukamba.Picha na Daudi Manongi-Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye (wa pili kulia) akiwasilisha jambo kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii walipotembelea mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.
   Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii Bw.Peter Serukamba akieleza jambo wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kuangalia mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisalimiana na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii Bw.Peter Serukamba katika viwanja vya urushaji wa matangazo ya shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Kisarawe

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA SERIKALI KWA UJENZI TB III


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA



Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeipongezaSerikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa kujenga jengo zuri la tatu la abiria (TB III)  litakaloboresha zaidi huduma za usafiri wa anga.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Norman Sigalla (Makete) wakati Wajumbe wa Kamati hiyo walipotembelea jengo hilo katika ziara yao ya kukagua miradi ya Serikali mwanzoni mwa wiki.

Jengo hilo linajengwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kwa Euro milioni 254 (sh. Bilioni 560) za mkopo kutoka Benki ya HSBC ya Uingereza na CRDB kwa dhamana ya Serikali ya Tanzania na Uholanzi.

Tayari TAA imeshamlipa Mkandarasi wake, Bam International ya Uholanzi, Euro milioni 96 baada ya kukamilisha asilimia 60 ya kazi. Jengo hilo linajengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ipo katika hatua za mwisho.

Mwenyekiti Sigalla na Wajumbe wengine wa Kamati hiyo walieleza kuridhishwa na kazi nzuri iliyofanywa na Serikali kujenga jengo hilo linalotarajiwa kukamilika Desemba 2017.

Baada ya kufurahishwa na kazi hiyo nzuri na kushauri uboreshaji zaidi wa utendaji, wabunge waliahidi kuisukuma Serikali iiwezeshe zaidi TAA kifedha ikamilishe miradi yake kwa wakati.

 Walisema hayo baada ya kupokea taarifa za utendaji na miradi ya TAA kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi George Sambali na Mkurugenzi anayesimamia Mradi wa TB III, Mhandisi Mohammed Millanga.
Pia walipokea taarifa ya  Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha aliyeeleza uhaba wa fedha wanazopewa unavyowaathiri katika kuendesha shughuli nyingi za kiwanja hicho ambacho ni kitovu cha mapato ya TAA.

TAA inayosimamia viwanja 58 vya ndege vya Serikali Tanzania Bara, hukusanya zaidi ya sh. Bilioni 67 lakini hupewa sh. Bilioni 17 tu kwa ajili ya kujiendesha huku JNIA ikipata sh. Milioni 700 tu kwa mwezi ukitoa za mishahara.

Taarifa  za watendaji TAA zilionesha maendeleo ya miradi ya ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege inayoendeshwa na kusimamiwa na TAA, jengo la TB III, ukarabati JNIA, changamoto zake kubwa na mipango ya Serikali kuzitatua.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi Sambali alieleza dhamira ya TAA kuwa na kiwanja kipya cha ndege nje ya Dar es Salaam au kupanua JNIA kwa kuongeza njia zaidi za kurukia ndege ifikapo 2030.

Hata hivyo, aliwaeleza wabunge changamoto ya TAA kutekeleza dhamira hiyo kuwa ni ulipaji fidia kwa wananchi na reli ya TAZARA kupanua eneo la sasa la JNIA au kupata zaidi ya dola milioni 500 kuanzisha kiwanja kipya nje ya Dar es Salaam.

Wabunge waliitaka TAA kufanya tathmini ya gharama za upanuzi wa JNIA kwa kulipa fidia wananchi na kuhamisha reli ya Tazara au  kujenga kiwanja kipya nje ya Dar es Salaam ili kuangalia uwiano kwa lengo la kuishauri Serikali mapema zaidi kabla ya 2030.

Wabunge walilalamikia ukosefu wa ndege za kutoa huduma na zilizopo kutoza nauli kubwa wakati Serikali inaboresha zaidi miundombinu.

Mhandisi Sambali alieleza ukosefu wa ndege unatokana na ushindani wa kibiashara wa mashirika ya ndege ambapo mengine hayaji kwa kukosa abiria wanaounganisha safari za  nje.

Pia alieleza Serikali kutokuwa na shirika imara la ndege kufuatia ATCL kuwa na ndege moja tu kumefanya asilimia 90 ya abiriawatumie nchi za jirani  kuunganisha safari za nje.

Kufuatia maelezo hayo, wabunge waliitaka Serikali inunue ndege nne ili ATCL  irudi hewani kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani alisema wamepokea rai ya wabunge akisisitiza dhamira ya Serikali ni kununua ndege.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA SHERIA NA UHUSIANO
MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA)
MACHI 30, 2016

Vodacom yadhamini michezo shule ya sekondari Nganza

 Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Domician Mkama akigawa Fulana za Vodacom kwa wanafunzi wa Nganza Sekondari katika Tamasha la michezo la shule hiyo waalilolidhamini jijini Mwanza jana. 
 Kanda: Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Domician Mkama akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza jana katika tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom. Picha na Lordrick Ngowi
  Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza wakishndana kukimbia na magunia jana katika tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom.
 Halima Juma na Jesca Balakekenwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza wakishindana kula keki na soda jana katika tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom. 
 Muntancy Rashidi na Rosemery Yohana wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza wakishindana kula chakula jana katika tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom
 Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza, Dativa Anold  akicheza jana kwenye tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom lililofanyika katika uwanja wa shule hiyo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza, Christopher Gachuma akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo jana kwenye tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom lililofanyika katika uwanja wa shule hiyo.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza wakifatilia michezo iliyokuwa ikiendelea jana kwenye tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom lililofanyika katika uwanja wa shule hiyo. Picha na Lordrick Ngowi.

WAZIRI WA AFYA AKAGUA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA KATIKA MAJIMBO YA MTWARA VIJIJINI, MASASI NA NDANDA

Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) akiwasili katika hospitali ya Rufaa Ndanda Mission.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari wametembelea Hospitali ya Mji wa Masasi (Mkomaindo), Hospitali ya Rufaa Ndanda Mission na Kituo cha Afya cha Nanguruwe kilichopo Jimbo la Mtwara Vijijini.
 
Katika ziara hiyo ya siku 2 Mh. Ummy alipata fursa ya kukagua shughuli mbalimbali za sekta ya afya ikiwemo kukagua wodi za wagonjwa, maabara pamoja na kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa watumishi wa idara ya afya na wananchi katika utoaji wa huduma za afya katika maeneo hayo.

Mh. Ummy alisema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe Dk. John Pombe Magufuli imejikita zaidi katika kuwahudumia wananchi hasa wa kipato cha chini kwa kuimarisha Nidhamu na Uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma. Pamoja na kusimamia Uwazi na matumizi bora ya rasilimali za Taifa.

Licha ya kukiri kuwa sekta ya Afya inakabiliwa na changamoto mbalimbali Mh. Ummy aliwapongeza na kuwashukuru madaktari na wauguzi kwa kazi na nzuri wanayoifanya ktk kutoa huduma kwa wananchi. Alieeleza kuwa Serikali inatambua na kuthamini kazi yao na imedhamiria kutatua changamoto zilizoko katika utoaji wa huduma ikiwemo kuongeza watumishi wa afya na kununua vifaa tiba na kuboresha mazingira ya kazi ya watumishi wa afya hasa walioko pembezoni.

Aliwaasa wananchi kuwathamini madaktari na waaguzi na iwapo kuna malalamiko dhidi ya watumishi hao basi wananchi wazingatie Sheria, Kanuni na Taratibu ktk kuonyesha malalamiko yao badala ya kujichukulia sheria mkononi.

Alisema, Hata hivyo wapo watumishi wachache ambao wanafanya kazi kwa kutozingatia maadili ya kazi na viapo vyao, hivyo aliwataka wabadilike kwani Serikali ya awamu ya 5 haitamvumilia mtumishi yeyote anaejihusisha na vitendo vya rushwa na uzembe kazini.
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wananchi Ndanda mission.

Pia aliwaasa watumishi hao kujiepusha na mambo ambao yanaweza kuleta mgongano na hisia mbaya kwa wananchi. Mfano tuhuma dhidi ya mfamasia wa Wilaya kumiliki maduka matatu ya 3 ambapo mhe Waziri ameelekeza uchunguzi wa TAKUKURU ufanyike.

Katika Hospitali ya Mkomaindo, Mhe Ummy ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Masasi kwa mafanikio waliyopata ktk ukusanyaji wa mapato ambapo baada ya kufunga mfumo wa kukusanya mapato wa kielektronik mapato yao yameongezeka kutoka shs 500,000 hadi 1,500,000 kwa siku. Amezitaka Halmashauri zote nchini kuiga mfano wa hospitali ya Mkomaindo kwa sababu hatua hii itachangia sana kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi ikiwemo uwezo wa Halmashauri wa kununua dawa na vifaa tiba.

Katika Kituo cha Afya cha Nanguruwe Mh. Ummy aliihimiza Halmashauri kukamilisha ujenzi wa wodi mbili ili Kituo hicho kiweze kupandishwa hadhi kuwa Hospitali ya Wilaya. Pia aliwataka kuongeza jitihada katika kuingiza wananchi/kaya nyingi katika Bima ya Afya kwani asilimia 5 wa waliojiunga ni ndogo sana.
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wananchi ili kujua kero zao katika ziara ya siku mbili mkoani humo.

Katika Hospitali ya Rufaa ya Mission Ndanda Mhe Ummy ameipongeza kwa kufanyia kazi agizo lake la wiki mbili zilizopita la kuzitaka hospitali za Taasisi za Dini zinazopokea ruzuku ya Serikali (Fedha na au Watumishi) kutekeleza kwa vitendo sera za Taifa za Serikali ikiwemo ya Matibabu Bure kwa Wajawazito, Watoto chini ya umri wa miaka 5 na Wazee. Hospitali ya Rufaa Ndanda imekubaliana na Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kuanza utekelezaji wa jambo hili kuanzia Julai 1, 2016.

Mh. Ummy pia amepongeza upatikanaji wa huduma za uchunguzi na matibabu bure ya Ugonjwa wa Kifua kikuu hospitalini hapo ambapo alisema ni asilimia 10 tu ya vituo vya afya/Hospitali binafsi nchini zinazotoa huduma hizo licha ya Serikali kuwa tayari kuvipatia vifaa vya uchunguzi na dawa bure. Mhe Ummy amezitaka hospitali nyingine binafsi kuunga mkono jitihada za Serikali za kutokomeza ugonjwa wa Kifuu kikuu kama sehemu ya mchango wao kwa jamii.Mhe Ummy pia ametembelea Chuo cha Maafisa Tabibu na Chuo cha uuguzi vilivyoko Masasi.
IMG-20160331-WA0025
Waziri Ummy akiongea na wagonjwa aliowakuta wakisubiri huduma katika hospitali ya Mkomaindo Masasi.
Mohammed Bakari
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari akizungumza na Watumishi wa Afya Ndanda Mission katika ziara aliyoambatana na Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu.
Mohammed Bakari
IMG-20160331-WA0023
Baadhi ya watumishi wa afya wakimsikiliza kwa makini Waziri wa afya Mh.Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati ziara yake tar 30 Machi.
Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wakinamama aliyelazwa kwenye wodi ya wazazi alipokua akikagua maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.
Mussa Rashid
Kaimu Mganga mkuu Halmashauri ya mji wa Masasi DK. Mussa Rashid akitoa taarifa kwa Waziri wa afya alipotembelea chumba cha vipimo katika hospitali hiyo. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammed Bakari.
Ummy Mwalimu
Waziri Mh. Ummy Mwalimu akibadilisha mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Bernard Nduta. Kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa Ndanda, Fr. Silvanus Kessy.

MWENYEKITI WA MTAA WA OYSTERBAY, LUBUVA ASAIDIA WATUNZA MAUA WA MBUYUNI JIJINI DAR.





WANAKIKUNDI cha Green Garden ambao wanafanya biashara uuzaji na utunzaji  maua  pembeni kidogo ya kituo cha mabasi cha Mbuyuni jijini Dar es Salaam wapewa mpira kumwagilia maua wa Mita 100 na Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva.

Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva amesema kuwa ameona vyema kutimiza ahadi alizoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mtaa kwa wanakikundi hicho kwani aliwaahidi kuwasaidi amesema Mwenyekiti huyo wakati wa kukabidhi mpira wa kumwagilia wa mita 100 leo pembeni ya kituo cha mabasi ya Mbuyuni jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wa kikundi cha Green Garden, Mohamed Mombo ameashukuru  Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva kwa kutimiza ahadi ahadi yake.

"Tulikua na mpira ambao ulikuwa umetoboka tulijitahidi kuziba na makaratasi ili usivuje sasa tumepata mpya tena wa mita 100 sasa tutakuwa kukijitahidi kutunzaji wa maua vizuri"

Mombo amesema kuwa kikundi hicho kimeanzishwa mwanzoni mwa mwaka 1985 mpaka sasa wapo tuu kwa sababu ya kujitafutia liziki ikiwa wanapata changamoto mbali mbali hasa za kukosa wateja kwa mda mwingine.
 Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), Zefrin Lubuva akimwagilia maua mara baada ya kuwakabidhi mpira wa Mita 100 kwa wanakikundi cha Green Garden jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa kikundi cha Green Garden, Mohamed Mombo akizungumza kwa mwandishi wetu mara baada ya kupewa msaada wa mpira wenye mita 100 utakao wawezesha kumwagilia maua kwa urahisi zaidi tofauti na mwanzo na 

 Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM), (kushoto) Zefrin Lubuva  akikabidhi Mpira wa Mita 100 kwa wanakikundi cha Green Garden kilichopo Mbuyuni jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM) (Mwenye kitambulisho), Zefrin Lubuva akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi mpira wa mita 100 jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Oysterbay(CCM) (mwenye kitambulisho), Zefrin Lubuva akipewa maelekezo na Mwenyekiti wa kikundi cha Green Garden, Mohamed Mombo mara baada ya kukabidhi mpira wa kumwagilia maua katika kikundi hicho kilichopo Mbuyuni jijini Dar es Salaam.
Wanakikundi wakiufungua mpira kwaajili ya kuanza kazi  mara baada ya kukabidhiwa mpira wa mita 100 leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

MSHINDI WA SHINDANO LA TEKNOLOJIA KUPATIKANA LEO.

Mshindi wa shindano la uvumbuzi wa Teknolojia mpya itakayo saidia jamii kupatikana leo na kuzawadiwa shilingi milioni tano (5,000,000) katika mkutano wa wadau wa teknologia unaofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo umeandaliwa na Bites&Bytes ukishirikiana na IBM, TWAWEZA, FSDT pamoja na CBA, mktano huo ambao utahamasisha uendelezaji wa mawazo mapya na uvumbuzi kwa waanzishaji wapya wa biashara na kuwapa mwanya wa kubadilisha mawazo na wadau wengine.



Mwanzilishi wa Bits&Bites, Lilian Madeje akiwakalibisha wageni na kufungua mkutano wa Uvumbuzi wa Teknologia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mwalimu Nyerere.
Mwakilishi wa IBM na mstakabali wa Innovation, Ben Mann akifafanua jinsi IBM ilivyofanya kazi kwenye Teknologia hapa nchini.
 Mwakilishi mwenza wa Bits&Bytes,Zuweina Farah akizungumza na wadau wa Teknologia waliokusanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya DTREE, Lucy Silas akizungumza na wadau wa teknolojia na uvumbuzi wa teknologia katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya wadau wa Teknologia wakimsikiliza  mtoa mada (Hayupo) pichani jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere.
  Mwakilishi mwenza wa Bits&Bytes,Zuweina Farah akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Teknologia na uvumbuzi wa teknologia mpya itakayo wasaidia wanachini kufanya kazi kwa urahisi zaidi, leo katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Amesema kuwa leo washiriki 16 walioshiriki kuvumbua teknoloia mpya wameshiriki katika mkutano huo na ndipo mshindi atakaye fanikiwa kushinda katika shindano hilo atazawadiwa shilingi Milioni 5 kwa kuwa na wazo zuri kuliko wengine ili aweze kuwa na mtaji kwaajili ya kuendeleza uvumbuzi wake.
Mwanafunzi mshiriki wa uvumbuzi wa Teknologia mpya itakayo wasaidia jamii, Gibson Kawago wa shule ya Sekondari ya huko Arusha akiwa amegundua taa za miale ya jua(Solar Power) zinazoweza kuchaji simu za Smati kwa zaidi ya masaa nane.
 Mwakilishi wa Fist Financial Sector Deeping(FSDT), Revis Mushi akizungumza na waaandishi wa habari katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa mkutano huo utasaidia jamii na wananchi kwa ujumla kusaidia kupata mfumo mwepesi wa Teknologia.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Atamizi (DTB) ambayo ipo tume ya Sayansi, George Mulamula akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere kuhusiana na amesema kuwa Tume ya Sayansi imeungana katika mkutano wa Teknologia ili kuwapa ujuzi zaidi Vijana. Pia amesema kuwa katika Tume ya Sayansi wameweza kuvumbua mfumo wa Max Malipo na wa mfumo wa kudahili wanafunzi wa TCU.
Mshiriki na Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani,  Necta Richard akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya mkutano wa Teknologia uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya washiriki katika mkutano wa Teknologia. 


 Washiriki.