Thursday, July 31, 2014

MH. MAKALLA AKAGUA MIRADI YA VISIMA VYA MAJI MKURANGA

 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia), akipata maerlezo kutoka kwa kiongozi wa Mafundi wa Kampuni ya CDM Smith, John Donoherth, kuhusu ujenzi wa kisima kilichopo Mkwalia Mkuranga ambacho ni moja kati ya visima 8 vinavyofanyiwa utafiti maji wilayani humo. Makalla alifanya ziara ya kukagua miradi ya maji wilayani Mkuranga mkoani Pwani leo. Pia alikagua mradi wa  kisima cha maji cha Nyamato chenye uwezo wa kutoa maji lita 26,000 kwa saa kitakachohudumia wakazi wa vijiji vya  Mvuleni, Nyamato na Kilimahewa. 
 Waziri Makalla akiangalia mradi wa kisima cha Mkwalia ambacho kinafanyiwa utafiti
 Maji yakitiririka kwenye kisima hicho
 Makalaa akijadiliana jambo na Mkandarasi wa kisima hicho,John Donoherth
 Naibu Waziri Makalla akielezea namna Kisima kipya cha Nyamato kikianza kufanya kazi kuwa kitakuwa kinatoa lita 26,000 za maji kwa saa na kuhudumia sehemu kubwa ya wananchi wilayani Mkuranga, Pwani. Atakizindua kisima hicho mwanzoni mwezi ujao kitakapowekwa pampu iliyoagizwa Afrika Kusini. Kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyamage, Abdallah Kiyewehe ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya maji kijijini hapo.
 Mama mkazi wa Kijiji cha Mvuleni, wilayani Mkuranga akielezea mbele ya waziri jinsi wanawake wa eneo wanavyopata taabu ya kuata maji karibu umbali wa Km 5, na kuonesha furaha ya kupata kisima hicho kitakachowaondolea adha waliyokuwa wanaipata.
 Eneo la Kisima cha Nyamato kilichogauliwa. Kisimamhicho kinasubiri pampu tu ili kianze kufanya kazi.
 Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mvuleni baada ya kukagua kisima cha maji cha Nyamato, wakati wa ziara yake wilayani Mkuranga leo.
 Sehemu ya umati mkubwa wa wananchi ukimsikiliza Makalla akihutubia kwa kuwaeleza mikakati ya Serikali ya kuwaboreshea wananchi sekta ya maji., ambapo  zimetengwa zaidi ya Bilioni moja kwa ajili ya wilaya hiyo.
 Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Makalla
 Katibu wa Kamati ya Maji ya Mradi wa Nyamato, Ali Salum akielezea jinsi mradi wa Nyamato unavyosuasua kuzinduliwa, akidai anayesababisha hivyo ni Mkandarasi wa mradi huyo ambaye hatoi taarifa yoyote juu ya ucheleweshwaji huo.
 Mkandarasi wa mradi wa maji wa Nyamato, Jamila Chibwana wa Kampuni ya Mac Consultant  akitoa majibu ya ucheleweshwaji wa mradi huo, ambapo alisema moja ya sababu zilizosababishwa ni kutopewa fedga za ujenzi kwa wakati na uagizaji wa pampu kutoka Afrika Kusini.
Makalla akiagana na wananchi baada ya mkutano kumalizika.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

USIKU WA MNYAMA NA WANYAMA WATIKISA DAR LIVE SIKUKUU YA IDD PILI

Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Khalid Mohammed 'TID Mnyama' akizikonga nyoyo za mashabiki wa Dar Live katika Usiku wa Mnyama na Wanyama.

Mnyama TID akijiachia kwa mashabiki wake wa Dar Live.
Mwanamuziki Jafarai akipagawisha mashabiki waliofurika katika Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.
Jay Moe akifanya makamuzi katika steji ya kupanda na kushuka ya Dar Live.
Inspector Haroun akiwapa hi mashabiki wake ndani ya Dar Live.

Mwanadada Naaziz kutoka Kenya akilishambulia jukwaa la Dar Live.

Masai Sharo akifanya vitu vyake stejini.

Mashabiki wakijiachia kijanja ndani ya Dar Live.

TID akitunzwa Cheni na shabiki wake.

TID akifanya manjonjo yake mbele ya Naaziz.

Nyomi ikifuatilia burudani za Idd Pili ndani ya Dar Live.
(PICHA NA RICHARD BUKOS NA GABRIEL NG'OSHA / GPL)

IPTL, Al-Madinah washerehekea sikukuu ya Eid na mayatima 500


Meneja rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune (mwenye suti ya kijivu) akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500 mayatima kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula iliyoandaliwa na taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL. Kulia ni meneja maswala ya kampuni ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta na wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa taasisi ya Al-Madinah Sheikh Ally Mubarak. 
 Meneja rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune (kulia) na Meneja maswakla ya kampuni wa IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta (katikati) wakikabidhi sehemu ya bidhaa zilizonunuliwa wakati wa karamu ya chakula kwa watoto yatima wapatao 500 kutoka vituo mbali mbali Dar es Salaam na Wilaya ya Kondoa, kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr. Kushoto ni Mkurugenzi wa taasisi ya Al-Madinah Sheikh Ally Mubarak, ambao waliandaa karamu hiyo baada ya kufadhiliwa na IPTL. 
 Meneja rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune (mwenye suti ya kijivu) akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500 mayatima kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula iliyoandaliwa na taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL. Kulia ni meneja maswala ya kampuni ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta.
Meneja maswala ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500 mayatima kutoka vituo mbalimbali Dar es Salaam na Wilaya ya Kondoa kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula iliyoandaliwa na taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL.

ZAIDI ya watoto 500 wasio katika mazingira magumu na mayatima jijini Dar es Salaam na Wilayani Kondoa wameungana na waislam wengine duniani siku ya Jumanne kusheherekea sikukuu ya Eid, sikukuu inayoashiria kuisha kwa mwezi wa mfungo wa Ramadhani.

Watoto hao kutoka katika vituo mbali mbali vya watoto yatima, walipata fursa ya kula na kufurahia pamoja na wengine wakati wa karamu ya chakula cha watoto yatima ililoandaliwa na taasisi ya Ai-Madinah Social Service Trust na kudhaminiwa na kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Bw. Aidan Kaude, Meneja Rasilimali Watu wa IPTL aliejumuika na watoto hao jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe hizo alisema kampuni yake imeona haja ya kuisaidia Al-Madinah katika kuhakikisha kuwa watoto hao wanaohitaji msaada pia wanapata haki ya kusheherekea wakati huu muhimu katika maisha ya waislam wote dunia mzima.

"Tulipopata maombi toka Al-Madinah ili kusaidia kufanikisa karamu hii, Mwenyekiti wetu mtendaji Bw. Harbinder Singh Sethi aliidhinisha haraka ombi hilo na kusema kuwa ni jambo la kheri sababu watoto hao walengwa ni mayatima na wanahitaji msaada toka kwa kila mtu ili waweze kuishi maisha ya kawaida kama wengine wanavyoishi licha ya kupoteza wazazi wao," alisema.

Mkurugenzi wa Al-Madinah Social Service Trust, Sheikh Ally Mubarakí aliyeandaa tukio hilo alisema kuwa baada ya kufanyakazi karibu na kwa muda mrefu na makundi mengi na taasisi mbali mbali za kiislam, taasisi yake imegundua kuwa mayatima wengi wanakumbwa na changamoto nyingi ambazo ni pamoja na ukosefu wa mahitaji ya msingi kama vile chakula, mavazi na malazi. 

Alisema taasisi yake iliomba msaada wa kifedha toka IPTL ili nao kuwapatia msaada wale watoto wenye maisha magumu, nafasi ya kusheherekea na waislam wenzao. Waislam walianza kusheherekea sikukuu ya Eid Jumatatu kwa dhehebu la Sunni na Jumanne kwa wengine, baada ya mwezi kuonekana na kuonesha mwanzo wa Shawwal, mwezi wa kumi wa Kalenda ya mwezi wa kiislama. 

Kuonyesha mwanzo wa Eid na kutoa Sunnah, kwa kuyafanya yake yaliyoganya na Mtume Muhammad, waislam wengi waliamka mapema kusali sala ya Asubuhi ya Sarat ul-Falr. 

Waslam wanasheherekea sikukuu kwa kukusanyika pamoja na marafiki na familia, na kuandaa vyakula vizuri , nguo nzuri kupeana zawadi na kupamba nyumba zao. Salaam ya kawaida wakati wa sikukuu hii ya Eid Madhubuti ya "Eid Mubarak" ikimaanisha "uwe na Eid iliyo na upendo."

Wednesday, July 30, 2014

MIEMBENI FC WATINGA FAINALI BAADA YA KUIFUNGA BAO 2-1 BILELE FC KWA DAKIKA 120!

Wachezaji wa timu zote mbili Miembeni Fc na Bilele Fc  wakisalimiana kabla ya Mtanange kuanza jioni hii.
Kikosi cha Timu ya Miembeni Fc
Kikosi cha Timu ya Bilele Fc

Mabingwa watetezi wa kombe la KAGASHEKI, Bilele Fc, wamefungwa leo na Timu ya Miembeni Fc bao 2-1 kwenye mtanange uliopigwa dakika 120, Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa  kutoshana nguvu kwa bao 1-1.
Timu ya Bilele Fc ndio walianza kupata bao la mkwaju wa penati katika dakika ya 62 kupitia kwa Fikiri David na Miembeni Fc wakasawazisha bao hilo ndani ya dakika moja na Rashid Mandawa kupita katika dakika 63 baada ya mpira kuanza kati na kufanya shambulizi.
Dakika 90 zilimalizika na kwenda katika dakika za ziada na katika dakika ya 105 Miembeni walifanikiwa kupata bao la ushindi na mtanange kumalizika. Mtanange huu pia haukuweza kumalizika vyema kwani wachezaji wawili wa Miembeni Fc wameoneshwa kadi nyekundu 2 na kucheza pungufu katika dakika za mwishoni kwa kufanya makosa tofauti tofauti.
Ushindi huu unawapeleka  Miembeni Fc  hatua ya Fainali wakisubiri mshindi wa kesho kati ya Kitendaguro Fc na Kagondo Fc.
Bilele Fc wao wanasubiri atakayefungwa kesho kati ya Kitendaguro na Kagondo ili waje wakutane kutafuta mshindi wa tatu.Fikiri David wa timu ya Bilele Fc akimfunga kipawa Miembeni Samwel Geofrey kwa Mkwaju wa penati katika kipindi cha pili dakika ya 62.Fikiri David akishangilia bao lake mbele ya Mashabiki wao Nao Miembeni hawakupoteza nafasi walisawazisha bao hilo  ndani ya dakika chache moja na kufanya 1-1 katika kipindi hicho cha pili, Bao likifungwa na Rashid Mandawa.Kipa wa Miembeni akipangua mpira uliopigwa kwa kona.Wachezaji wa Bilele fc wakimdhibiti mchezaji wa Miembeni.Jesse Johansen wa Miembeni Fc akimkimbiza mchezaji wa Bilele fc Mohamed Nunda Mchezaji wa Miembeni Babu Seif (kushoto) akimtoka mchezaji wa Bilele fcKipa wa Miembeni fc Samwel akiwapanga wachezaji wake Frii kiki kuelekea lango la Miembeni fcKipa wa Miembeni Samwel Geofrey aliumia katika kipindi cha pili na mpira kusimama kwa mudaKipa wa Miembeni Samwel Geofrey akisimama na kuendelea kulinda lango lakePatashika langoni mwa timu ya Bilele FcKipa wa Miembeni samweli Geofrey akiokoa mpira wa kona langoni mwake Kipindi cha dakika za ziada 120 wachezaji wa Miembeni waliboresha ngome yao ili kulinda bao lao na hatimaye kuibuka na ushindi.Mashabiki wa Miembeni Fc wakishangilia baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-1 na kwenda hatua ya Fainali jioni hii.
Mashabiki wa Miembeni wakiwa wanawapongeza wachezaji wao baada ya kuwafunga Bingwa Mtetezi Bilele Fc na Ushindi huu kuwapeleka hatua ya Fainali.
Tunaenda Fainali!!! Mashabiki na Wachezaji wa Miembeni wakifurahia Ushindi huo!

Taswira la Baraza la Eid Karimjee hall jijini Dar es salaam

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Kamilius Membe, akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, huku waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (kulia) akifuatilia mazungumzo hayo kwa pembeni, wakati wakiwa kwenye hafla ya Baraza la Idd El Fitr,  Julai 29, 2014, kwenye Viwanja vya Kariamjee, Jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi kwenye Baraza la Eid ElFitr, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiingia kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, akisindikizwa na  Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Kassim.
 Pinda akimsalimia Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi baada ya kuwasili ukumbini
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsalimia Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Shaaban Issa Simba baada ya kuwasili ukumbini.
 Pinda akimtazama kwa furaha wakati Mwinyi akizindua kitabu kwa furaha ambacho kimeandikwa na Sheikh Mkuu, Shaaba Issa Simba, kitabu hicho chenye jina la Al Muhtaswar ni makusanyo mbalimbali ambayo sheikh Mkuu huyo ameyakusanya na kisha kutengeneza kitabu kwa ajili ya kukisambaza nchini kote kusaidia waislam kuzingatia vyema dini hiyo. Pamoja na wadau kadhaa, Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe amechangia kuwezesha uchapishaji wa kitabu hicho.
 Mtoto  wa jijini Dar es Salaam, Arafat Msham akiduusu kitabu hicho
 Membe, Dk. Salim na Sumaye wakisoma kitabu cha Sheikh Mkuu Shaaban Issa Simba
Pinda akitoa hotuba yake kwenye Baraza hilo la Idd
 Kinamama kwenye Baraza hilo la Eid ElFitr
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (kulia) akiwa na Mama Shamim Khan kwenye Baraza hilo la Eid 
 Mwanazuoni akighani kaswida maalum kwenye Baraza hilo la Idd
Wanazuoni wakitumbuiza kaswida kwenye Baraza la Idd
 Ustaadhi Mroki Mroki wa Habari leo akifuatilia kwa makini shughuli za hafla hiyo ya Baraza la Eid
 Baadhi ya Wasanii maafurufu wa Bongo Movie akiwemo Steve Nyerere  nao walihudhuria Baraza hilo
Membe akiagana na wadau baada ya shughuli za Maulid. 
Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog