Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia akiwapungia wananchi
wa Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Septemba
30, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea ufunguo ikiwa ni ishara ya kukaribishwa
Dodoma na Meya wa Manispaa ya Dodoma Jafar Mwanyemba katika mapokezi
yaliyofanyika kwenye makazi yake , Mlimwa Septemba 30, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha ufunguo aliokabidhiwa na Meya wa
Manispaa ya Dodoma, Jafar Mwanyemba (kushoto) kuashiria kupokewa rasmi
kwenye manispaa hiyo. Makbidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi yake
eneo la Mlimwa Septemba 30, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa Dodoma
baada ya kukaribishwa kimira na wazee hao Septemba 30, 2016.
Mke
wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizawadiwa kimira na wanawake wa Dodoma
ikiwa ni ishara ya kumkaribisha karika Manispaa hiyo, Septemba 30, 2016.
Mke
wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizawadiwa kimira na wanawake wa Dodoma
ikiwa ni ishara ya kumkaribisha karika Manispaa hiyo, Septemba 30, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri
Mkuu, Kasim Majaliwa na mkewe Mary wakiagana na watuimishi wa Makazi ya
Waziri Mkuu ya Dar es salaam kabla ya kuondoka kuelekea Dodoma Septemba
30, 2016
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa
Manispaa ya Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma
Septemba 30, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na Madiwani wa
Manispaa ya Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma
Septemba 30, 2016.
Waziri
Mkuu, Kasim Majliwa akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye
makazi yake mjini Dodoma Septemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Wananchi
wa Dodoma wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
alipozungumza nao kwenye makazi yake eneo la Mlimwa Septemba 30, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia sasa mtu yeyote mwenye shida ya kuonana
naye itabidi amfuate Dodoma na kwamba atarudi Dar es Salaam pindi akiitwa na
Mheshimiwa Rais au Makamu wa Rais.
Ametoa kauli hiyo leo jioni (Ijumaa, Septemba 30, 2016) wakati akizungumza na
viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa Dodoma waliofika kumpokea mara baada ya
kuwasili mjini hapa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa Julai 25 kuwa
atahamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu.
“Tukio hili la
kuhamia Dodoma si la mzaha, hakuna siasa na wala si jaribio. Tumeshakeleza.
Kama kuna waliokuwa wanafiria kwamba halitekelezeki watambua kwamba tayari
tumeshafika. Na kuanzia sasa atakayetaka huduma ya Waziri Mkuu
Waziri
Mkuu amesema Dodoma si ndogo kama baadhi ya watu wanavyodai na kwamba
huduma zilizopo zinatosha kukidhi mahitaji ya sasa. "Mkakati uliopo wa
kupanua huduma za tiba, maji, umeme na masoko utawezesha watumishi wote kuishi
bila bugudha yoyote."
“Awamu ya kwanza inaanzia Septemba hadi Februari mwakani. Mimi nimeshatangulia
na wanaofuata ni mawaziri na manaibu wao wote, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu
Wakuu wote. Natambua kwamba wote wana nyumba za kuishi na kama wapo ambao
hawana hawazidi asilimia tano na nyumba zipo
Amewataka
watumishi wote wa Serikali watambue kwamba safari imeshaanza na kila mmoja ajipange,
na akarudia wito wa Mheshimiwa Rais kwamba atakayegoma kuhamia Dodoma atakuwa
amejifukuza kazi.
Waziri
Mkuu amewataka watendaji wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA)
wasifanye kazi kwa mazoea, bali wabadilike na kwa kuwa amehamia Dodoma ameahidi
kuafuatilia kwa karibu zaidi.
Mapema akizungumza katika hafla hiyo,
Waziri wa Nchi (OWM SUBKAV), Jenista Mhagama amesema kilichofanyika leo ni
uthibitisho kuwa yale ambayo Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi sasa hivi
imeanza kuyatekeleza.
"Tuliahidi kukusanya kodi, tuliahidi elimu bure, tuliahidi kupambana na
mafisadi, tuliahidi kuondoa watumishi hewa, tuliahidi kuifufua ATCL na kununua
ndege mpya na yote tumetekeleza,” amesema.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. George
Simbachawene amesema uamuzi wa kuhamia Dodoma ni uthibitisho kuwa
viongozi wetu kweli wamedhamiria kutekeleza ahadi ya Baba wa Taifa ya
kuhamishia makao makuu ya nchi hapa Dodoma.
"Dodoma imeanza kuchangamka na hii ni fursa tosha kwa mkoa wetu
kubadilika. Tushirikiane na CDA kuijenga Dodoma mpya. Kitendo cha Mheshimiwa
Waziri Mkuu kuingia Dodoma leo hii maana yake ni kwamba Serikali iko rasmi
Dodoma," amesema.
Hafla
hiyo ilihudhuriwa na Manaibu Waziri Anthony Mavunde na Dk. Ashatu Kijaji, Makatibu
Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais (Utumishi), Wakuu wa Wilaya za
Mkoa huo, wazee wa mkoa huo, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi zilizoko
mkoani na baadhi ya wananchi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA
WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA
IJUMAA,
SEPTEMBA 30, 2016.