Thursday, November 30, 2017

WATEULIWA KUUNDA KAMATI NDOGONDOGO AFCON U17

Ukiacha Kamati Kuu ya kuratibu michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON U17/2019) kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefanya uteuzi mwingine.

Uteuzi huo umeegemea zaidi kwa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Maandalizi (LOC) wakiwamo viongozi wakuu wa TFF na wanafamilia wengine ambao kwa pamoja watafanya kazi ya kuandaa michuano hiyo itakayofanyika Tanzania mwaka 2019.

Wakati jina namba moja ni Mwenyekiti wa kila kamati ndogo wajumbe wengine katika kamati hizo ni kama ifuatavyo:

Miundombinu (Infrastructure)
  1. 1. Paul Makonda (Mwenyekiti)
  2. 2. Yusuph Singo
  3. 3. Sunday Kayuni
  4. 4. Leslie Liunda
  5. 5. Nassoro Idrissa
  6. 6. Mohamed Kiganja
  7. 7. Mhandisi Davis Shemangale

Masoko na Habari (Marketing, Commercial and Media)
  1. 1. Kelvin Twissa (Mwenyekiti) 
  2. 2. Angetile Osiah
  3. 3. Dk. Hassan Abbas
  4. 4. Dk. Omari Swaleh (Chuo Kikuu cha Mzumbe)
  5. 5. Iman Kajula
  6. 6. Tido Mhando
  7. 7. Head of Marketing – NMB

Fedha na Mipango (Finance and Planning)
  1. 1. Doto James (Mwenyekiti)
  2. 2. Mohamed Dewji
  3. 3. Dk. Seif Muba
  4. 4. Bernard Lubogo
  5. 5. Paul Bilabaye
  6. 6. Jacquelline Woiso
  7. 7. Cornel Barnabas

Usafiri na Malazi (Transport and Accommodation)
  1. 1. Mhandisi Ladislaus Matindi (Mwenyekiti)
  2. 2. Abubakar Bakhresa
  3. 3. Aziz Abood
  4. 4. Alhaj. Ahmed Mgoyi
  5. 5.  Mhe. Ahmed Shabiby
  6. 6. Dk. Maige Mwakasege Mwasimba
  7. 7. Shebe Machumani

Uratibu Utalii
  1. 1. Dkt. Khamis Kigwangala (Mwenyekiti)
  2. 2. Allan Kijazi
  3. 3. Devotha Mdachi
  4. 4. Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke
  5. 5. Hoyce Temu
  6. 6. Leah Kihumbi (Mkurugenzi Sanaa)
  7. 7. Athuman Jumanne Nyamlani

Itifaki
  1. 1. Kamishna Mkuu wa Uhamiaji (Mwenyekiti)
  2. 2. Mndolwa Yusuph
  3. 3. Filbert Bayi
  4. 4. Mkurugenzi Uwanja wa Ndege JNIA
  5. 5. Happiness Luangisa
  6. 6. Alex Makoye Nkenyenge
  7. 7. Alhaji Idd Mshangama

Tiba na Udhibiti wa Dawa za Kusisimua Misuli (Medical and Doping Control)
  1. 1. Prof. Lawrence Museru (Mwenyekiti) 
  2. 2. Dkt. Paul Marealle 
  3. 3. Dkt. Edmund Ndalama
  4. 4. Dkt. Christina Luambano
  5. 5. Daktari Mkuu wa Hospitali ya Temeke
  6. 6. Hiiti Sillo

Sheria na Taratibu
  1. 1. William Erio (Mwenyekiti)
  2. 2. Dk. Damas Ndumbaro
  3. 3. Edwin Kidifu
  4. 4. Ally Mayai
  5. 5. Khalid Abeid

Ulinzi na Usalama (Safety and Security)
  1. 1. IGP. Simon Siro (Mwenyekiti)
  2. 2. Michael Wambura
  3. 3. CP. Andengenye – Zimamoto
  4. 4. CP. Lazaro Mambosasa – Polisi Kanda ya Dar-es-Salaam
  5. 5. Mkuu wa Askari wa Usalama Barabarani.
  6. 6. TISS
  7. 7. Jonas Mahanga
Rasilimali Watu (Human Resources)
  1. 1. Dk. Francis Michael (Mwenyekiti)
  2. 2. Allan Kijazi
  3. 3. Wane Mkisi
  4. 4. Juliana Yassoda
  5. 5. Gerald Mwanilwa

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI IDARA KUU MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.

 Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kikao kilichofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu kutoka Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. James Kibamba(kulia) akiwasilisha mapendekezo ya marekebisho ya Muundo wa Utumishi wa Idara ya Ustawi wa Jamii uliopitiwa na kujadiliwa na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto lililofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
 Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu kutoka Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Deodatha Makani (kushoto) akifafanua masuala ya Kiutawala kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara kuu ya Mendeleo ya Jamii, Jinisa, Wazee na Watoto lililofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
 Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi (kulia) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara kuu ya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto lililofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akisisitiza wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto kuhusu umuhimu wa uzingatiaji wa Kada zote za Ustawi wa Jamii katika rasimu ya muundo unaopendekezwa kwenye Baraza lililofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Bw. Atupile Mwambene akitoa ufafanuzi kuboresha rasimu ya marekebisho ya Muundo wa Utumishi wa Idara ya Ustawi wa Jamii kwa wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto lililofanyika  mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
 Mwanasheria kutoka  Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Vicness Mayao akifafanua masuala ya kisheria  kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii waliokutana mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bibi. Magreth Mussai akitoa maoni yake kuhusu maboresho ya Muundo wa Utumishi kwa Kada ya Ustawi wa Jamii kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii lililofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.
 Mkuu wa chuo cha Buhare Bw. Paschal Mahinyira akitoa hoja kwa Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto lililofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.


Baadhi ya wajumbe wawakilishi wa Watumishi wa Idara Kuu Maendeleo ya Jamii wakifuatilia mijadala mbalimbali iliyojiri katika Baraza la Wafanyakazi wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto lililofanyika mjini Morogoro Novemba 30, 2017.

Picha na Kitengocha Mawasiliano WAMJW

CHINA YAAHIDI KUFADHILI UJENZI WA RELI KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA (SGR)

Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
BALOZI wa China hapa nchini, Wang Ke amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na kuahidi kuwa nchi yake iko tayari kushawishi taasisi za fedha ikiwemo Benki ya EXIM ya nchini humo kushiriki ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa baada ya kufanyika kwa upembuzi yakinifu wa mradi huo.

Alisema kuwa kutokana na ukubwa wa mradi huo, unaokadiriwa utagharimu Dola za Marekani bilioni 7.6 hadi kukamilika kwake, utahitaji kufanyiwa upembuzi yakinifu ili kukidhi masharti ya kupata mkopo kupitia Benki ya Exim na taasisi nyingine zitakazotaka kujenga mradi huo muhimu. 

“Mradi huu ni muhimu na wa kihistoria kwa nchi hizi mbili, China ingependa kuona mradi huo unaboreshwa ili uweze kutoa huduma ya kusafirisha mizigo na abiria na kwamba kuimarika kwake kutaokoa miundombinu ya barabara kwa kuwa shehena kubwa ya mizigo itasafirishwa kupitia reli hiyo.

Aidha, Balozi Ke alisema kuwa nchi yake inasubiri pia kukamilika kwa taratibu za ndani kati yake na Tanzania ili mradi wa reli ya TAZARA uanze  ili kuboresha usafiri na usafirishaji wa mizigo na abiria kati ya Tanzania na Zambia pamoja na nchi za maziwa makuu.

Balozi Ke alitumia fursa hiyo kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kukusanya kodi, kusimamia matumizi adili ya fedha za umma, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kupambana na rushwa.

Akizungumza mara baada ya mazungumzo na mgeni wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alisema kuwa Serikali imeridhia uamuzi wa China wa kufanya upembuzi yakinifu wa mradi huo wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) ili China kupitia taasisi zake iweze kujenga sehemu ya mradi huo.

“Tayari mradi umeanza kujengwa kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, kwahiyo kujitokeza kwa China kutaka kufadhili ujenzi wa mradi huo kutasaidia kukamilisha mradi huo muhimu kwa haraka na kwa wakati” Alisema Dkt. Mpango.

Alisema pia kuwa China imeonesha nia ya kusaidia kuujenga na kuupanga mji wa Dodoma kutokana na nchi hiyo kuwa na uzoefu wa kupanga miji ambapo nchi hiyo imeonesha nia ya  kujenga miundombinu ya elimu, barabara, uwanja wa ndege wa kimataifa-Msalato, kujenga mfumo wa maji safi na maji taka pamoja na majengo ya kisasa.

Kuhusu biashara, Dkt. Mpango alisema wamekubaliana kuwa China itaisaidia Tanzania kukuza kiwango cha biashara ambapo takwimu zilizoko zinaonesha kuwa urari wa biashara kati ya nchi hizo unaonesha kuwa Tanzania imekuwa ikinunua bidhaa nyingi kutoka nchini humo kuliko inavyo uza bidhaa na huduma zake.

“Mwaka 2016 Tanzania iliuza China bidhaa na huduma zenye thamani ya Dola za marekani milioni 460 wakati China iliuza hapa nchini bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.2, kiwango ambacho ni kikubwa karibu mara 5 ya kile tulichowauzia” Alisema Dkt. Mpango.

Ili kuvutia Sekta ya utalii, Tanzania imeiomba China kuanzisha safari ya ndege wa moja kwa moja kutoka China hadi Tanzania ili kuvutia watalii wengi kutoka nchini humo na kwamba utaratibu utafanyika ili Mamlaka ya usafiri wa anga iweze iratibu na kusaini makubaliano ya ushirikiano na hivyo kufanikisha jambo hilo.

“China imeandaa maonesho makubwa ya uwekezaji na biashara ya bidhaa na huduma mbalimbali mwezi Novemba, 2018, hivyo wafanyabiashara wa Tanzania pamoja na  Bodi ya Utalii nchini wahakikishe wanashiriki kikamilifu kwenye maonesho hayo ili kutumia nafasi hiyo kujitangaza” Alisistiza Dkt. Mpango.

Aidha, Dkt. Mpango alieleza kuwa Balozi Wang Ke, amesema kuwa Nchi yake itashiriki katika ujenzi wa miradi ya bandari ili kukuza masuala ya usafiri kwa kuboresha bandari za Tanga, Bagamoyo, Kigoma, Bagamoyo, Dar es Salaam, Mtwara na katika Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika.

Waziri huyo wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alitoa wito kwa wawekezaji kutoka China na nchi nyingine kuja kuwekeza nchini katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaipeleka nchi katika uchumi wa viwanda.

Miradi mikubwa ambayo China imewekeza na kufadhili hadi sasa hapa nchini ni Reli ya TAZARA, Kiwanda cha Urafiki, ujenzi wa barabara, majengo, ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi dar es Salaam, Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dare Salaam, Ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na miradi mingine kadha wa kadha.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati),  Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke (wa pili kulia), Mwakilishi wa masuala ya Uchumi na Biashara wa Ubalozi wa China Bw. Lin Zhiyong (wa pili kushoto) pamoja na maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango  wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Mkutano kati ya pande hizo kuhusu Biashara, uwekezaji na ushirikiano, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) na mgeni wake Bi. Wang Ke, wakitoka nje ya Jengo la Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao uliohusu masuala mtambuka ya ushirikiano kati ya Tanzania na China.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) na Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke,  wakiagana   baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao ambapo balozi huyo aliahidi kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kati nchi hizo mbili, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akiagana na Mwakilishi wa masuala ya Uchumi na Biashara wa Ubalozi wa China  nchini Tanzania Bw. Lin Zhiyong baada ya kumalizika kwa Mkutano kati ya Waziri huyo na Balozi wa nchi hiyo Bi. Wang Ke (hayupo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Kamishina wa Fedha za Nje Bw. John Rubuga (kushoto) na Afisa anayeshughulikia masuala ya nje katika dawati la China Bw. Alfonce Mayala kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa makini majadiliano kati ya Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke,  na Waziri wa Fedha na Mipango (hawapo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), wa pili kulia akieleza kuhusu fursa zilizopo katika Sekta ya Utalii wakati wa  Mkutano kati yake na Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke, (hayupo pichani), Jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), wa tatu kulia akiwa katika mkutano na  Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke (wa pili kushoto) ambapo walikubaliana kuendeleza ushirikiano katika Biashara na uwekezaji kwa manufaa ya pande hizo mbili, mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akieleza kuhusu kuwa na uwiano wa kibiashara kati ya Tanzania na China kwa manufaa ya pande hizo mbili wakati wa mkutano kati yake na Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke, (hayupo pichani), Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa China hapa Nchini Bi. Wang Ke, (katikati) akiongoza maafisa wake wa ubalozi wa nchi hiyo hapa nchini wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China hapa nchini, Bi. Wang Ke, akisisitiza jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)

MTANDAO WA UTEPE MWEUPE (WHITE RIBBON) WAZUNGUMZA NA WAKAZI WA KIJIJI CHA MAORE JUUU YA VIFO VTOKANAVYO NA UZAZI KWA KINAMAMA NA WATOTO WACHANGA

Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe kitaifa  (The White Ribbon Alliance ) Rose Mlay akizungumza na wananchi katika kijiji cha Maore wilayani Same wakati wa mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Taasisi ya Utepe mweupe (White Ribbon)  kujadili vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga .
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Maore wilayani Same akifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kuhusu vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga .
Mganga Mkuu wa wilaya ya Same,Dkt Godfrey Andrew akizungumza wakati wa mkutano na wananchi ulioandaliwa na Mtandao wa Utepe Mweupe (White Ribbon) kujadili  vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga .
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Maore wilayani Same akifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kuhusu vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga .
Mkutano ukiendelea katika jengo la Mahakama lililopo katika kijiji cha Maore wilayani Same.
Baadhi ya kina mama wakiwa na watoto wao katika mktano huo.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Maore wilayani Same wakichangia wakati wa mkutano uliondaliwa na Mtandao wa White Ribbon kuhusu vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

WANANCHI katika kijiji cha Maore wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro,wamesema tatizo la vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi pamoja na watoto wachanga vinachangiwa na upungufu wa watumishi katika zahanati ya kijiji pamoja na ufinyu wa wodi ya wazazi iliyopo.

Wakitoa maoni yao katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Taasisi ya Utepe mweupe (White Ribbon)  kujadili vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga katika kijiji cha Maore wilayani Same wananchi hao wameiomba serikali kuangalia namna ya kutatua changamoto hizo.

Mbali na changamoto hizo wakazi wa Maore wameeleza pia changamoto kubwa inayowakabili wanafunzi wa kike kupata ujauzito pindi wawapo shuleni kuna changiwa na wazazi kushindwa kuwaeleza ukweli  watoto wao kuhusu kuanza mahusiano wawapo shuleni .

Mganga Mkuu wa wilaya ya Same ,Dkt Godfrey  Andrew amesema vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi pamoja na watoto wachanga vimepungua wilayani Same hadi kufikia 15 mwaka huu ukilinganisha na vifo 60 vilivyotokea katika miaka miwili iliyopita ya 2015 na 2016 huku akibainisha mikakati iliyopo ya kupambana na changamoto za upungufu wa watumishi.

Mratibu wa Mtandao wa Utepe Mweupe kitaifa  (The White Ribbon Alliance ) Rose Mlay amesema  kuwekeza kwa mama mjauzito kunachangia kuzaliwa kwa kijana mwenye afya njema atakayechangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi na kulea maendeleo.

Same ni mojawapo ya wilaya saba zilizoko katika mkoa wa Kilimanjaro zinazokabiliwa na changamoto ya vifo vya akina mama wajawazito vitokanavyo na uzazi huku sababu ya vifo hivyo kwa kina mama ikielezwa kuwa ni Kifafa cha Mimba,kupasuka kwa mji wa mimba na kutokwa na damu nyingi.

FINLAND YAIPATIA TANZANIA MSAADA WA BILIONI 75 KUENDELEZA MISITU, MAFUNZO YA UONGOZI NA UBUNIFU

Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

Serikali ya Tanzania na Finland zimetiliana saini mikataba mitatu yenye thamani ya Euro milioni 28.8 sawa na Shilingi bilioni 75 kwa ajili ya kuendeleza misitu, ubunifu na masuala ya uongozi.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mikataba hiyo, Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James amesema, msaada huo kutoka Finland umetolewa ili kuendeleza  uwezo wa viongozi na kufanya maamuzi sahihi yenye tija kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa, mradi ambao unasimamiwa na Taasisi ya Uongozi, ambapo kiasi cha Euro milioni 9.90 zimetolewa kuendeleza mradi huo.

Aidha Serikali ya Finland imetoa kiasi cha Euro milioni 8.95 kwa mradi wa  kuiimarisha mfumo wa ubunifu nchini kwa kutengeneza mazingira rafiki kwa wabunifu ili kuweza kubuni na kuendeleza ubunifu wao na kuchochea ukuaji wa viwanda. 

Bw. James alisema fedha hizo zitatumika kuwasaidia wabunifu kwa kuwapatia vifaa na msaada wa kitaalamu ili kuyaendeleza mawazo yao na kuyafanya yawe ya kibiashara na kuweza kusaidia kubadili mawazo hayo kuwa viwanda. 

“Fedha hizi zitasaidia kutatua changamoto katika viwanda vilivyopo nchini ili vifanye kazi kwa ufanisi kwa kuwaunganisha wanataaluma mbalimbali nchini, ikiwa ni pamoja na wabunifu wachanga, wataalamu kutoka vyuoni, wataalamu kutoka Serikalini na Sekta binafsi” Alisema Bw. Doto James

Eneo lingine lililonufaika na msaada huo ni programu ya misitu, ambayo imepatiwa Euro milioni 9.95 kwa lengo la utuzaji wa misitu na uongezaji thamani ya mazao yatokanayo na misitu ili kuongeza kipato kwa Wananchi, kupunguza umasikini na kulinda mazingira.

Katibu Mkuu amemshukuru balozi wa Finland Nchini, Mhe. Pekka Hukka kwa msaada walioutoa na kwa kuunga mkono shughuli za maendeleo za Serikali, na kuongeza kuwa Finland wamekuwa wakifadhili miradi mbalimbali nchini, ukiwemo mradi wa kilimo biashara Mkoani Lindi na Mtwara (LIMAS), uliogharimu Euro milioni 9, Mradi wa kuimarisha usambazaji na upatikanaji wa umeme wa uhakika Jijini Dar es Salaam, uliogharimu Euro milioni 25, na Programu ya maboresho ya Serikali za Mitaa, Euro milioni 10.5

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja aliiishukuru Serikali ya Finland kwa kuendelea kuisaidia Taasisi hiyo.
‘Hii ni mara ya tatu Finland wamekuwa wakitusaidia kuendeleza jitihada zilizoanzishwa na Serikali yetu ambapo awamu ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2012 ambapo walitupatia Euro milioni 7, mwaka 2014 Euro milioni 12 na sasa wametupatia Euro milioni 9.90 huu ni msaada mkubwa’ alisema Profesa Semboja.

Aidha kwa upande wake Balozi wa Finland Bw. Pekka Hukka, aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendeleza ushirikiano na Serikali yake, na kuongeza kuwa msaada huo ni muhimu sana katika kutimiza malengo ya maendeleo ya nchi.Amesema msaada huo ukitumika ipasavyo hasa katika kuendeleza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu utasadia kuongeza ajira na kuongeza pato la Taifa.

Ameitaka Serikali kupitia Wizara ya nishati,  kushirikiana na sekta binafsi na kuitumia fursa hiyo ya kuboresha misitu ili kuiongezea nchi mapato zaidi yatakayotokana na makusanyo ya kodi.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) akionesha kalamu aliyozawadiwa na Balozi wa Finland Bw. Pekka Hukka (kushoto) ambayo imetengenezwa kwa mbao, akionesha uzalendo wa matumizi ya misitu. Kutoka kulia ni Kamishna wa Bajeti Wizara ya Fedha na Mipango Bibi. Mary Maganga na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. John Rubuga.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James (kulia) akitia saini moja kati ya mikataba mitatu yenye jumla ya shilingi bilioni 75 kama msaada kwa Tanzania, Kushoto ni Balozi wa Finland Bw. Pekka Hukka kwa pamoja wakisaini mikataba hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) akibadilishana mkataba na Balozi wa Finland Bw.Pekka Hukka. Mkataba wa kwanza wa Euro milioni 9.9 ni kwa ajili ya kusaidia Taasisi ya Uongozi, wa pili wa Euro milioni 8.9 kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa ubunifu na watatu wa Euro milioni 9.5 ni kwa ajili ya program ya misitu.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) pamoja na Balozi wa Finland Bw. Pekka Hukka (kushoto) wakionesha moja ya mikataba mara baada ya kumaliza kutia saini mikataba hiyo.
Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja (Kulia) akiishukuru Serikali ya Finland kwa kuwapatia msaada wa Euro milioni 9.9 ambayo itawasaidia kuendesha shughuli mbalimbali za Taasisi hiyo. Kushoto ni Balozi wa Finland Bw. Pekka Hukka.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (katikati, waliosimama mbele) akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla ya utiaji saini mikataba mitatu ya jumla ya shilingi bilioni 75. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

MAGEREZA SACCOS YAFANYA MKUTANO MKUU WA TANO, 2017 MKOANI DODOMA

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS Nchini akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana(wa pili kulia) alipowasili kwenye katika Ukumbi wa  Chuo cha Mipango Dodoma tayari kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Mkutano huo unafanyika kwa siku moja leo 30 Novemba, 2017 hapa mjini Dodoma. 

Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (TPS SACCOS) kimefanya Mkutano wake Mkuu wa Tano wa Mwaka 2017 kwa ufanisi Mkoani Dodoma.
Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere uliopo katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini,  Miyuji Dodoma leo Novemba 30,  2017.

Akiongea katika Mkutano huo Kaimu Naibu  Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw.  Charles Malunde kwa niaba ya Naibu Mrajisi ametoa angalizo kwa Vyama vya ushirika nchini kutokufanya biashara za Kibenki nje ya lengo la kuanzishwa kwa SACCOS.

Amesema kuwa katika  vyama vingi vya ushirika uzoefu umeonesha kuwa wakishakuwa na mtaji mkubwa huwa na wazo la kuanzisha Benki, ametoa angalizo kuwa masharti ya uendeshaji wa Benki ni tofauti kabisa na masharti ya uendeshaji wa vyama vya ushirika hivyo ameziasa Saccos zote nchini kutafakari vyema kabla ya kubadili vyama hivyo na kuwa Benki.
“ Ukianzisha Benki huduma za Saccos zitafifia, kumbukeni wateja wa Saccos ni pamoja na wale wa hali ya chini kabisa ikiwa benki hawa huenda mkawaacha” alisisitiza  Kaimu Mrajis Malunde.

Aidha,  amewaasa Magereza SACCOS pamoja na Saccos zote nchini kufanya shughuli zake kwa kufuata sheria  lakini pia kuheshimu na kusikiliza sana wenye mali ambao ni wanachama wa vyama hivyo vya ushirika.
Aliongeza kuwa kwakuwa Mkutano huu utahusisha uchaguzi wa wajumbe wa Bodi Bw. Charles Malunde pia amewaasa Wajumbe wa Mkutano Mkuu kuwa makini katika uchaguzi huo kwa kuchagua watu wenye weledi na wenye mapenzi ya dhati na ushiriki wao ili waweze kutimiza majukumu yanayokusudiwa.

Pia amewataka wagombea wote wanaowania nafasi mbalimbali za chama hicho kujiuliza mambo manne kama ifuatavyo;- Je, watumishi wa Jeshi la Magereza wote ni wanachama? na mnaweka Mkakati gani?, Je wanachama wanaweka akiba za kila mwezi?, Mnajiendesha kisayansi? Mtu akitaka mkopo anapata baada ya muda gani? na swali la mwisho uhusiano na vyama vingine vya ushiriki, SCULT, nje ya nchi ukoje?.

Awali akitoa taarifa ya Chama cha Ushirikia wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara (TPS SACCOS), Mwenyeki wa Bodi ya Magereza Saccos, DCP. Gideon Nkana amesema kuwa Idadi ya wanachama imeongezeka hadi kufikia wanachama zaidi ya 13,000 ikiwa na mtaji wa zaidi ya bilioni 18.
Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana(katikati) akimuongoza Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) ambaye pia ni Mlezi wa Magereza SACCOS kuingia Ukumbini tayari kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara(kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza SACCOS, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara ulifanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma..
Kaimu Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Charles Malunde akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi kama inavyoonekana katika picha. 
Mjumbe wa Mkutano huo ambaye pia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Kagera, Naibu Kamishna wa Magereza, Jeremiah Nkondo akichangia mada katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tano wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara . 
Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga akitoa neno la shukrani mara baada ya ufunguzi wa Mkutano huo. 
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiteta jambo na Mgeni rasmi Kaimu Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Charles Malunde kama inavyoonekana katika picha.
Kaimu Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Bw. Charles Malunde(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Watumishi wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara(waliosimama). Walioketi(wa tatu toka kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Magereza Saccos anayemaliza muda wake, Naibu Kamishna wa Magereza, Gideon Nkana(wa pili toka kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tano unaofanyika kwa siku moja Mkoani Dodoma(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano – Jeshi la Magereza).