Monday, April 30, 2012

Diamond atua Mbagala kwa chopa

 Diamond akikupa saluti kabla ya kupasua anga
 Huko chini mashabiki wanakanyagana kumsubiri Diamond
 mashabiki
 Diamond ni nouma
 Anaingia Dar Live
 Akielekea kwenye chopa
 Rubani akimpa maelekezo Diamond
 Dua kabla ya kupasua anga...
 Nyomi ya Dar Live ikimsubiri supa star wao Diamond

 Sio kampeni ni Diamond akitua Mbagala
 Akiaga rubani wa chopa iliyomleta
 Mbagala hapatoshi
 Diamond akielekea ukumbini baada ya kutua na chopa
 Salamu kwa mashabiki
 Pamoja na mvua na mafuriko mashabiki wamo tu

Mnyonge mnyongeni, ila haki yake mpeni. Diamond hakamatiki....
Ni nani kama Diamond?
Diamond akipagawisha
Hakuna cha kujali mvua wala nini
Diamond full mzuka. Picha zote na Global Publishers

Sunday, April 29, 2012

BIAFRA KIDS YASHINDA MECHI YAKE DHIDI YA AFRICAN TALENT

Kinyang'anyiro cha mashindano ya Copa Coca Cola chini ya miaka 17 wilaya ya Kinondoni kimeendelea tena leo katika uwanja wa Mwl. Nyerere, Magomeni Makurumla kwa kuzikutanisha timu za Biafra Kids dhid ya African Talent. Mechi hiyo iliyokuwa ichezwe majira ya saa 10 jioni ilichezwa saa 5 asubuhi kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo waandaaji.
Biafra Kids wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa klabu ya michezo ya Biafra muda mfupi kalba ya kuanza mechi

Mechi hii, wachezaji walipania sana kushinda baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Eleven Boys kwa magoli 4 - 1. Hivyo walifanya mazoezi ya nguvu na kujiongezea ari kubwa ya ushindi na hatimaye kuichabanga timu ya African Talent kwa mabao 3 - 1.


Biafra Kids katika picha ya pamoja na wanachama na mashabiki

 Hamasa ya ushindi pia ilichangiwa na mashabiki wengi waliofunga safari kuja kuishangilia timu hiyo. kama picha inavyojieleza hapo juu, wanachama na mashabiki hao hawakujali mvua iliyokuwa ikinyesha bali walichohitaji ni ushindi tu na si vinginevyo. Mashabiki hao wake kwa waume waliishangilia timu yao tangu mwanzo hadi mwisho wa mchezo.
Biafra Kids - kikosi kilichoanza (first eleven) katika picha ya pamoja


Wachezaji wakipasha misuli kabla ya kuingia uwanjani


 Mfungaji wa goli la kwanza Abu Selemani (wa kwanza kushoto) na mfungaji goli la tatu Khamis Ibrahim (wa katikati)


Mabeki Machachari wa Biafra Kids Fareed Massoud (kushoto), Ahmad Ibraheem (kulia) na Abdul Moshi (nyuma)


tayari kwa ukaguzi na kuanza kwa mechi


Timu mwenyeji wa mechi hiyo African Talent wakisalimiana na Biafra Kids


Manahodha wa timu zote mbili katika picha ya pamoja na refa wa mchezo huo


Biafra Kids wakilisakama lango la African Talent

Karamu ya magoli ilifunguliwa na Abuu Selemani dakika ya 18 baada ya kupokea krosi safi ambapo aliiunganisha nyavuni na kumwacha kipa wa African Talent akiruka bila kuupata mpira. Baada ya kufunga tu goli hilo, kasi ya mchezo ilingezeka maradufu na mnamo dakika ya 24 Babulu Hamad aliipatia Biafra Kids bao la pili. African talent walijipatia bao la kufutia machozi kwa njia ya penati baada ya mchezaji wao kujidondosha katika eneo la hatari na kumhadaa refa kuwa amechezewa rafu . Dakika ya 41 karamu ya magoli ilihitimishwa na Khamis Ibrahim ambaye aliutia mpira nyavuni kiufundi. 

Mara baada ya nusu ya kwanza ya mchezo kukamilika, Biafra Kids walitanza soka la ukweli na kusababisha kosa kosa kadhaa na magoli ambayo refa aliyakataa.

Biafra Kids inatarajia kujitupa tena uwanjani tarehe 1 Mei, 2012  kuchuana na Vijana Muslim pale pale kwenye uwanja wa Mwl. Nyerere.

MUNGU IBARIKI TIMU YETU!

WASANII WA BONGO FLEVA WALIVYOPAGAWISHA MASHABIKI KATIKA SHOW YA KILI MUSIC AWARDS MKOANI DODOMA JUMAMOSI

Mshindi wa Kilimanjaro Star Search Issa akiwa Jukwaani huku akishusha burudani kwa wapenzi wa Muziki wakiojitokeza kushuhudia Tamasha kubwa la Washindi Wa Tuzo za Kili Musics Awards 2012
Mshiriki wa Shindano la Kili Star Search Juma akitoa Burudani katika show ya Washindi Wa Kili Music Award 2012 katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma 

Mamia ya Wananchi wakiwa kwenye foleni tayari kuingia ndani kwaajili ya Show ya washindi wa Kili Music Awards inayofanyika katika uwanja wa jamhuri mkoani Dodoma Mida hii
Wakazi wa Mkoa wa Dodoma wakiwa Wamejitokeza katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma kwenye Show ya Washindi wa Tuzo za kilimanjaro musics awards 2012

 Diamond & Ommy Dimpoz

Mdada akicheza kiduku stejini baada ya kupagawa na Show ya AT jana Katika Uwanja wa JAmhuri Mkoani Dodoma
Umati wa Wakazi wa Dodoma Wakiwa Kwa Wingi Katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma Hapo Jana katika Show ya Washindi wa Kili Music Award 2012 
 Umati wa Wakazi wa Dodoma na Vitongoji Vyake wakiwa kwenye Show ya Washindi wa Tuzo za Kili Music Awards iliyofanyika Jana katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Haki Thomas K. Ngowi na Edna Newton Kyando wameremeta

 Sheria Ngowi (kati) na nduguze katika mnuso wa Haki Ngowi
 Mama Ngowi akikaribishwa kutoa zawadi kwa Haki
 Mama Ngowi akitoa zawadi ya Biblia Takatifu kwa 
 Mama mzaa chema akienda kumpongeza bintiye
 Wazazai na ndugu wa binti wakimpongeza mtoto wao
 Ndugu wa binti wakienda kutoa mkono wa pongezi kwa maharusi
 Ndugu wa Bi Harusi
 Ni furaha na vifijo
 Shangazi akitoa wosia
 Keki
 Haki Ngowi akiwa na mpambe wake John Mwansasu
 Maharusi na wapambe mezani pao
 Furaha ya Kumeremeta

MC Evans Bukuku Kazini
 Madada wakila pozi
 Bi Harusi
Wapendanao