Wednesday, January 9, 2019

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU DAR ES SALAAM LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akumuapisha Mhe. Doto Biteko kuwa Waziri wa Madini kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Zainab Chaula kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Doroth Mwaluko kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhandisi Elius Mwakalinga kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Faustin Kamuzora kuwa Katibu Tawala mkoa wa Kagera  kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Dorothy Gwajima kuwa Naibu Katibu Mkuu (TAMISEMI (Afya)  kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akumuapisha  Dkt. Francis michael kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji (Mst.) James Bwana kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma  kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. George Yambesi kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Yahya Fadhili Mbila  kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma   kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha  Bw. Daniel Ole Njoolay kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma  kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha  Balozi John Michael Haule kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma   kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapishab Bi. Bi. Khadija Ali Mohamed kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bi. Immaculate Peter Ngwale kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma   kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019 
 Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma  Jaji (Mstaafu) Harold Nsekela akiwaapisha viongozi walikula kiapo

 Viongozi walioapishwa wakila kiapo cha maadili
 Viongozi wa dini wakitambulishwa ukumbini
 Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma akiongea baada ya Rais kuwaapisha viongozi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
 Spika Job Ndugai akiongea baada ya Rais kuwaapisha viongozi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiongea baada ya Rais kuwaapisha viongozi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
 Viongozi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
 Viongozi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Spika Job Ndugai  baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wanahabari baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2019











Tuesday, January 8, 2019

SIMBA KUTUMIA 'YES WE CAN' KUUJAZA UWANJA KATIKA MECHI YAO DHIDI YA JS SAOURA YA ALGERIA ,KUCHUKUA POINT 3

*Manara asema wametumwa na Rais, lazima wachukue ubingwa, wachezaji kutua kesho wakitokea Z'bar

*Asifu uwezo wa Kocha wao,agusia umuhimu wa kununua jezi kuichangia Klabu yao

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KLABU ya Soka ya Simba imesema maandalizi ya mchezo wao dhidi ya JS Saoura ya Algeria Jumamosi ya Januari 12 katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam yanakwenda vizuri ,hivyo imewataka mashabiki ,wanachama wao na wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi na uwanja utakuwa wazi kuanzia saa nne asubuhi.

Pia imesema kutokana na jukumu ambalo lipo mbele yao la kutumwa nchini kwenye mchezo huo la ligi hiyo ya mabingwa Afrika ,wameamua wachezaji wao waliopo kwenye Kombe la Mapinduzi Zanzibar watarudi kesho kwa ajili ya mechi iliyopo mbele yao.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Msemaji wa Klabu ya Simba Hajji Manara amesema wakati wakijiandaa na mchezo huo wa Jumamosi ,mchezaji wao Eras to Nyoni amepata majeraha wakati wa mchezo dhidi ya KMKM ya Zanzibar.

Amefafanua jopo la madaktari wa Simba pamoja na madaktari wataasisi nyingine wametoa ripoti kuwa Nyoni anahitaji tiba maalum na mapumziko ya kutosha,kimsingi ni kwamba atarudi uwanjani katikati ya Februari.Kuhusu mchezo wao dhidi ya JS Saoura amesema wanakwenda kucheza na timu kubwa na kwamba lengo lao la kwanza lilikuwa ni kuingia hatua ya makundi na baada ya hapo wanafikiria malengo makubwa zaidi.

Amesema katika mipango yao ni kuhakikisha wanapata alama tisa nyumbani na uozefu unaonesha wakiwa nyumbani watanapata alama za ushindi huku akizungumzia weledi wa Kocha wao ambaye anajua mechi za Afrika.

Pia amefafanua wanatambua Rais Dk.John Magufuli amewaagiza Simba kufanya vizuri kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabibgwa Afrika na wanauhakika watachukua ubingwa mwaka huu.Manara amewahimiza mashabiki wa Simba kuwahi kufika uwanjani mapema badala ya kwenda uwanjani saa nane au saa tisa mchana na kwamba siku hiyo kutakuwa na burudani ya muziki kutoka bendi ya African Stars'Twanga Pepeta'.

Amesema wamezindua kampeni maalum ya kuhamasisha Wana Simba kuujaza uwanja huo kwa kutumia kauli mbiu ya Yes We Can na wanaamini hakuna kitakachoshindikana kwani Simba ni nguvu moja.Wakati huo huo amewahimiza wana Simba wakaichangia Klabu yao kwa kununua jezi na kuingia uwanjani kwa wingi,wakifanya hivyo hakutakuwa na sababu ya kupitisha bakuli kuchangishana fedha.

"Tunahamasisha Wana-Simba kununua jezi za timu yao kwa kufanya hivyo watakuwa wamechangia Klabu yao na hilo ni jambo la heshima.

"Jezi zetu zinauzwa kwa utaratibu maalum na tumejipanga kuhakikisha hakuna wanaofanya hujuma katika uuzwaji wa jezi za Simba,akibainika tutawaambia Polisi wawakamate," amesema Manara.

NAIBU WAZIRI DK MABULA AKERWA MAKUSANYO MADOGO YA KODI YA ARDHI KATIKA HALMASHAURI

Na Munir Shemweta, WANMM Geita

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amekerwa na makusanyo madogo ya mapato katika halmashauri mbalimbali nchini kupitia kodi ya ardhi.

Akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi wa Halmashauri za Mji na Wilaya ya Geita jana mkoani Geita alipofanya ziara ya kushtukiza kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa katika halmashauri hizo, Dk Mabula alisema, mapato ya sekta ya ardhi katika halmashauri nyingi hayaridhishi na kueleza kuwa halmashauri nyingi mapato yake yako chini ya asilimia 30.

Alisema pamoja na halmashauri hizo kuwa na mapato kidogo kupitia sekta ya ardhi lakini watendaji wake hawaoneshi jitihada zozote kuhakikisha wanakusanya mapato ya kutosha kupitia sekta hiyo na hivyo aliwataka watendaji hao kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato kwa kuwa msisitizo wa serikali ya awamu ya tano ni kukusanya kodi.

‘’Kwa staili hii tutafika kweli? Mna bahati mbaya sasa watendaji wa sekta ya ardhi katika halmshauri mtakuwa chini ya wizara moja kwa moja na rais amepiga kelele kuhuisiana na kodi ninyi mnarelax’’ alisema Dk mabula.

Hata hivyo, Dk Mabula aliisifu halmashauri ya Mji wa Geita kwa kukusanya mapato kwa zaidi ya asilimia sitini. Kwa Mujibu wa taarifa ya Halmshauri ya Mji wa Geita, kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba 2018, halmashauri hiyo imekusanya jumla ya shilingi 389,699,937.28 kati ya milioni 600,000,000 ilizopanga kukusanya.

Kwa upande wake Halmashauri ya Wilaya ya Geita kupitia, Afisa Ardhi wake Faraja Kaluwa pamoja na halmashauri hiyo kupewa malengo ya kukusanya milioni 150 lakini kufikia desemba 2018 imefanikiwa kukusanya shilingi milioni 12,480,500 tu.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwataka wakuu wa idara za ardhi katika halmashauri za Mji na Wilaya ya Geita kutoa ahadi ya utekelezaji maagizo aliyoyatoa na hatua gani zichukuliwe kwao iwapo maagizo hayatatekelezwa kwa wakati.

Maagizo aliyoyatoa Dk Mabula ni kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya kodi ya ardhi, uingizaji viwanja na mashamba katika mfumo wa kielektronik, utoaji hati za ardhi pamoja na utoaji hati za Madai (demand notes) kwa wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi.

Aidha, Dk Mabula ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinaingiza viwanja na mashamba kwenye mfumo wa malipo kwa njia ya kielektronik na kutaka kasi ya utoaji hati kuongezeka ili kuwawezesha wananchi kiuchumi na wakati huo kuiingizia serikali mapato kupitia kodi ya ardhi.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amezitaka halmashauri nchini kuhakikisha zinatoa leseni za makazi katika maeneo yenye nyumba zilizojengwa nje ya urasimishaji na mipango Miji na kueleza kuwa zoezi hizo linatakiwa kukamilika mwezi machi mwaka huu.

Dk Mabula amezitaka Halmashauri kuanisha maeneo yote ya nyumba hizo na kupatiwa leseni za makazi kwa gharama ya shilingi 5000 sambamba na kuziingiza katika kumbukumbu za halmashauri na kubainisha kuwa leseni hizo ni hatua za kuelekea wamiliki wake kupatiwa hati.
Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akizungumza alipowasili ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita alipofanya ziara katika mkoa huo jana kufuatilia utekelezaji wa maagizo yake kuhusiana na sekta ya ardhi katika halmashauri za Mji na Wilaya ya Geita.

BENKI KUU YAFAFANUA KUHUSU USIMAMIZI KWA WATOA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imetoa tangazo kwa umma kupitia tovuti yake (www.bot.go.tz) likiwataka watu na taasisi zote zinazofanya biashara ya huduma ndogo za fedha zilizoko Tanzania Bara (isipokuwa vyama vya ushirika vya
akiba na mikopo – SACCOS) kutoa taarifa zitakazotumika katika utayarishaji wa Kanuni za Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha.

Hayo yamesemwa leo na Meneja Usimamizi wa Maduka ya Fedha na Huduma Ndogondogo za Fedha Victor Tarimu kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT).Tarimu amesema taarifa hizo zinatakiwa kutumwa Benki Kuu ya Tanzania hadi 31 Januari 2019 na kwamba inatoa ufafanuzi ufuatao kuhusu tangazo hilo kuwa lengo la siyo kuvifunga au kuvibana vikundi vya kijamii kama VICOBA, watu binafsi na taasisi zinazotoa huduma ndogo za fedha kama ambavyo inapotoshwa na baadhi ya watu na mitandao mbalimbali ya kijamii.

"Bali ni kukusanya taarifa za awali kuhusu huduma hizo, kama amnavyo ilivyoainishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kupitisha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, lengo la
sheria hiyo ni kuwalinda wadau wote wanaohusika na huduma hizi (watoaji na watumiaji) kwa kuziwekea utaratibu mzuri zaidi wa uwekaji kumbukumbu, uendeshaji na uongozi kwa ujumla," amesema

Pia kuwalinda wamiliki na watumiaji wa huduma hizo dhidi ya vitendo vinavyoweza kusababisha kupoteza fedha na mali zao, pamoja na
kuzuia watu binafsi, taasisi na vikundi vya kijamii kutumika kufanya uhalifu ikiwemo utakasishaji fedha haramu.

Ameongeza kuwa Benki Kuu inafahamu baadhi ya watu binafsi, taasisi na vikundi vinavyotoa huduma ndogo za fedha vikiwemo VICOBA, havina usajili rasmi na hivyo havitambuliki kisheria. "Kwa kutambua hilo, Sheria imeweka kipindi cha mpito cha mwaka mmoja (kuanzia sheria itakapoanza kutumika rasmi) kwa wote wanaojihusisha na utoaji huduma ndogo za fedha, kujipanga ili wawe tayari kusimamiwa pale kanuni zitakapokuwa zimetolewa rasmi.

"Hivyo, katika kipindi hiki cha mpito, si kosa kwa watu binafsi, taasisi na
vikundi vya kijamii kutokuwa na usajili rasmi. Aidha, Wadau wote watashirikishwa kikamilifu katikautayarishaji wa Kanuni hizo, na mara zitakapokuwa tayari na kutolewa na Benki Kuu ya Tanzania, maelezo
zaidi kuhusu usajili yatatolewa," amesema.

Amesisitiza Benki Kuu inawataka wananchi wote kutokuwa na taharuki na inasisitiza uamuzi wa kusimamia watoa huduma ndogo za fedha umechukuliwa kwa nia njema na kwa faida ya watumiaji na watoaji wa huduma hizi. Aidha, Benki Kuu inautahadharisha umma kujiepusha na taarifa na miongozo inayotolewa kiholela na watu, kampuni na mashirika ambayo yanajitangaza kufanya shughuli za uandikishaji wa watoa huduma ndogo za fedha kwa
wananchi kwa niaba ya Serikali au Benki Kuu.

"Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu, kampuni au shirika
lolote litakalojihusisha na vitendo vya kuwakanganya wananchi kwa lengo la kupotosha au/na kujipatia mapato haramu.

"Tunawahamasisha wananchi kufuatilia taarifa zaidi kuhusu tangazo hili zinazoendelea kutolewa na Benki Kuu katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu usimamizi wa watoa huduma ndogo za fedha Tanzania Bara," amesema Tarimu.

SERIKALI KUSAINI MIKATABA YA UBANGUAJI WA KOROSHO JANUARI 10

Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza mpango wa serikali kusaini mikataba ya ubanguaji wa korosho wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara, leo tarehe 8 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara, leo tarehe 8 Januari 2019.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Prof Siza Tumbo akifatilia mkutano wa Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara, leo tarehe 8 Januari 2019.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara

Serikali imesema kuwa tarehe 10 Januari 2019 itasaini mikataba na wamiliki wa viwanda vya ubanguaji wa korosho waliojitokeza kwa ajili ya kubangua korosho za serikali za msimu wa mwaka 2018/2019 zilizonunuliwa na serikali kwa bei ya Shilingi 3300 kwa kilo.

Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 8 Januari 2019 wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara.Alisema kuwa hivi karibuni serikali ilitangaza kuwa korosho ghafi zote zitabanguliwa nchini hivyo utekelezaji wa jambo hilo umeanza, ambapo Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko itaingia mikataba ya ubanguaji.

Pamoja na wamiliki wa viwanda kupewa kazi ya kubangua korosho lakini pia serikali imewakaribisha wananchi kujitokeza kubangua korosho za serikali kupitia vikundi au mtu mmoja mmoja. “Wananchi wenye uwezo wa kubangua tunawaomba waende Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo-SIDO) kwa ajili ya kujiandikisha ambapo mpaka sasa watu 126 kwa ajili ya ubanguaji na Tani 29 zimechukuliwa kwa ajili ya kuanza kubanguliwa” Alisisitiza Mhe Hasunga

Katika mkutano huo Waziri huyo wa kilimo Mhe Japhet Hasunga amempongeza Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kushuhudia utiaji wa saini mkataba wa mauziano ya mahindi kati ya Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) wa Bilioni 21 zitakazoiwezesha NFRA kunua mahindi kwa wakulima hivyo kuimarisha soko la nafaka nchini. 

Mhe Hasunga alisema kuwa pamoja na kuanza ubanguaji kupitia SIDO lakini serikali imeanza mchakato wa kukufua viwanda vya ubanguaji vya serikali na watu binafsi nchini ili kuongeza ajira kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuanzisha vituo vya wabanguaji wadogo wadogo.

Akizungumzia kuhusu swala la malipo ya korosho na uhakiki wa wakulima alisema kuwa tayari kiasi cha korosho ambayo imekusanywa kwenye maghala makuu ni Tani 203,938.3 wakati korosho iliyopo kwenye Vyama vikuu vya ushirika ni Tani 29,803.53 inayofanya jumla ya korosho yote iliyopokelewa kwenye vyama vya ushirika na maghala makuu kuwa Tani 233,741.83 sawa na asilimia 84.7 ya lengo lililowekwa la ukusanyaji katika Mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na Pwani.

Kuhusu malipo ya wakulima alisema kuwa miamala ya malipo ambayo imefanyika ni 261,458 yenye jumla ya watu 203,569. Aidha, vyama 490 vilimelipwa kati ya vyama 617, Alisema Mkoa wa Mtwara jumla ya vyama 39 bado havijalipwa, Mkoa wa Lindi vyama vitano na Ruvuma viwili hivyo serikali imejipanga ndani ya wiki mbili vyama hivyo kuwa vimelipwa.

Waziri Hasunga amesema kuwa mpaka kufikia jana tarehe 7 Januari 2019 fedha ambazo zimeingizwa kwenye Account za wakulima ni zaidi ya Bilioni 257 huku ambazo tayari zimeingia kwenye Account za wakulima ni Bilioni 226.2 ambapo Zaidi ya Bilioni 30.7 zilizohakikiwa bado hazijaingizwa kwenye Account za wakulima kutokana na taarifa za baadhi ya wakulima hao kutofautiana majina ama vinginevyo. “Tunawaomba sana wananchi kwenda Benki kujiridhisha kama Account zao zinafanya kazi kwani serikali ina fedha za kuwalipa wakulima wote wa korosho” Alisema

“Tena nisisitize kwa wale wanaofanya biashara ya korosho kinyume na utaratibu maarufu kama (Kangomba) wajisalimishe na kuomba radhi wenyewe kuliko kusubiri serikali iwabaini” Alisema.Vilevile, Mhe Hasunga alisema kuwa wizara yake imeweka mikakati mbalimbali ambapo hadi kufikia Januari 31 mwaka huu zoezi la uhakiki wa wakulima wanaostahili kulipwa liwe limekamilika ambapo zaidi ya asilimia 80 ya wakulima wawe wamelipwa.

Pia amewataka wananchi kupuuza taarifa mbalimbali zizotolewa na baadhi ya wananchi wasiolitakia mema Taifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa serikali hailipi wakulima badala yake amesisitiza kuwa serikali ina fedha za kutosha kulipa wakulima wa korosho isipokuwa kangomba wao hawatalipwa.

World Bank Group President Kim to Step Down February 1

World Bank Group President Jim Yong Kim today announced that he will be stepping down from his position after more than six years in which the institution’s shareholders provided strong support to multiple initiatives to ensure that the Bank Group retains strong leadership in the world of global development.

“It has been a great honor to serve as President of this remarkable institution, full of passionate individuals dedicated to the mission of ending extreme poverty in our lifetime,” said Kim. “The work of the World Bank Group is more important now than ever as the aspirations of the poor rise all over the world, and problems like climate change, pandemics, famine and refugees continue to grow in both their scale and complexity. Serving as President and helping position the institution squarely in the middle of all these challenges has been a great privilege.”

Under Kim’s leadership, and with the backing of the Bank Group’s 189 member countries, the institution in 2012 established two goals: to end extreme poverty by 2030; and to boost shared prosperity, focusing on the bottom 40 percent of the population in developing countries. These goals now guide and inform the institution in its daily work around the globe.

In addition, shareholders strongly supported measures to ensure that the Bank Group be even better positioned to respond to the development needs of clients:
· The Bank Group’s Fund for the Poorest, IDA, achieved two successive, record replenishments, which enabled the institution to increase its work in areas suffering from fragility, conflict, and violence.

· In April 2018, the Bank Group’s Governors overwhelmingly approved a historic USD$13 billion capital increase for IBRD and IFC that will allow the Bank Group to support countries in reaching their development goals while responding to crises such as climate change, pandemics, fragility, and underinvestment in human capital around the world.

Over the past 6+ years, the institutions of the World Bank Group have provided financing at levels never seen outside of a financial crisis.

Recognizing the power of capital markets to transform development finance, the Bank Group during Kim’s tenure also launched several new innovative financial instruments, including facilities to address infrastructure needs, prevent pandemics, and help the millions of people forcibly displaced from their homes by climate shocks, conflict, and violence. The Bank is also working with the United Nations and leading technology companies to implement the Famine Action Mechanism, to detect warning signs earlier and prevent famines before they begin.

During his term, President Kim emphasized that one of the greatest needs in the developing world is infrastructure finance, and he pushed the Bank Group to maximize finance for development by working with a new cadre of private sector partners committed to building sustainable, climate-smart infrastructure in developing countries.

To that end, Kim has announced that, immediately after his departure, he will join a firm and focus on increasing infrastructure investments in developing countries. The details of this new position will be announced shortly.In addition to working on infrastructure investments, Kim announced that he will also be re-joining the board of Partners In Health (PIH), an organization he co-founded more than 30 years ago.

“I look forward to working once again with my longtime friends and colleagues at PIH on a range of issues in global health and education. I will also continue my engagement with Brown University as a trustee of the Corporation and look forward to serving as a Senior Fellow at Brown’s Watson Institute for International and Public Affairs.”

Kristalina Georgieva, World Bank CEO, will assume the role of interim President effective February 1.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 8,2019