Wednesday, July 31, 2013

Waasi DRC wapewa saa 48 kusalimisha silaha

Wanajeshi wa Brigedi Maalum wakiwa katika mazoezi makali yaliyofanyika  hivi karibuni huko Goma Mashariki ya Demokrasia ya Kongo
Mmoja wa walinda amani kupitia Brigedi Maalum inayoundwa na wanajeshi kutoka Tanzania, Afrika ya Kusini na Malawi akiwa katika moja ya mazoezi yaliyofanyika hivi karibu huko Goma. Kamanda Mkuu wa Misheni ya Kulinda Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ( MONUSCO ) Luteni Jenerali Carlos Albeto dos Santos Cruz ametakanza jana jumanne akiwa Goma kwamba MONUSCO itaanza rasmi kuitumia Brigedi Maalum na ametoa saa 48 kuanzia saa kumi jioni kwa saa za Goma jana siku ya Jumanne waasi wote kusalimisha silaha zao, na kwamba ifikapo saa kumi jioni kwa saa za Goma siku ya Alhamisi Agosti Mosi wale wote ambao watakuwa hawajasalimisha silaha zao watachukuliwa kama tishio la usalama kwa wananchi na MONUSCO italazimika kuwapokonya ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu kwa mujibu wa Mamlaka iliyopewa na Sheria zinazowaruhusu kufanya hivyo.

Na Mwandishi Maalum

Misheni ya Kutuliza Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( MONUSCO) imetangaza kwamba kwa mara ya kwanza itaanza kuitumia Brigedi Maalum ( Force Intervention Brigade) katika kudhibiti eneo maalum la usalama ( security zone ) kuzunguka mji wa Goma ulioko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na imewapa saa 48 waasi kusalimisha silaha zao.

Taarifa iliyotolewa na MONUSCO na kusambazwa na Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa jana jumanne, inaeleza kwamba watu binafsi katika eneo la Kivu ya Magharibi ambalo linajumisha Goma na Sake na ambao hawahusiki na vyombo vya usalama watapewa saa 48 kuanzia saa kumi jana kwa saa za Goma ( Jumanne ) kuzisalimisha silaha zao katika Misheni hiyo na kujiunga na mchakato wa DDR/RR unaoratibu upokonyaji, usambaratishaji, urejeshwaji makwao, kuwaunganisha na jamii na kuwapatia makazi.

Baada ya saa kumi jioni ya Alhamisi, Agosti Mosi. Taarifa hiyo inasema. Wale wote ambao watakuwa hawajasalimisha silaha zao watachukuliwa kama tishio kwa usalama wa wananchi na MONUSCO itachukua hatua zote muhimu kuwapokonya silaha hizo ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu kama ilivyoainishwa katika Mamlaka na sheria za ushiriki za MONOSCO.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo zaidi ya wananchi milioni moja wanaishi katika eneo dogo la Goma na Sake na kando kando ya barabara ambayo inawaunganisha na kambi ya wakimbizi ya Mugungu ambayo ni makazi ya muda ya watu karibu 70, 000 ambao wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano.

Kwa mujibu wa MONUSCO, tangu kati kati ya mwezi Mei eneo hilo limeshuhudia mapigano ya mara kwa mara kutoka kwa kundi la M23 dhidi ya majeshi ya Serikali ya FARDC ikiwa ni jaribio la wazi la kutaka kusonga mbele kuelekea Goma na Sake.

“ Katika mashambulizi hayo, likiwamo la hivi karibuni la Julai 14, M23 walitumia kiholela silaha zao za moto zikiwamo silaha nzito ambazo zimesababisha wananchi kujeruhiwa” .

Taarifa hiyo imeongeza kwamba kundi hilo la M23 katika mashambulizi hayo limelenga pia Vituo vya Umoja wa Mataifa.

Aidha taarifa hiyo inabainisha kwamba eneo hilo maalum la usalama ( security zone) litasaidia kudhibiti tishio la moja kwa moja mbali na eneo la nje ya Goma na pengine eneo hilo linaweza kupanuliwa na kurudiwa sehemu nyingine kutakako hitajika.

Tamko hilo la kutoa saa 48 kwa waasi kusalimisha silaha zao linafuatia kuwasili katika eneo la Goma kwa Kamanda Mkuu wa MONUSCO, Luteni Jenerali Carlos Alberto dos Santos Cruz, ambaye alitangaza kwamba Misheni ya MONUSCO itaunga mkono jeshi la Serikali ( FARDC) katika kuanzisha eneo la usalama kuzunguma eneo la Goma na vitongoji vyake.

Taarifa hiyo inamkariri Kamanda Mkuu wa MONUSCO akiyapongeza majeshi ya serikali kwa kazi nzuri iliyofanya wiki iliyopita ya kuwadhibiti M23. Ingawa anasema eneo la Goma na Sake bado limo katika mazingira magumu sana na kwamba ni wajibu wa wahusika wote kuhakikisha wahalifu wote hawaendelei kuhatarisha raia wa eneo hilo.

Kwa mwaka uliopitia , kundi la M23 pamoja na makundi mengine yenye silaha yamekuwa yakipambana mara kwa mara na majeshi ya serikali katika Mashariki ya Kongo, huku makundi hayo yenye silaha mwezi Novemba mwaka jana yakiikalia Goma kwa muda.

Aidha mapingano ya hivi karibuni ambayo safari hii yalihusisha pia kundi jingine la wanagambo wenye silaha lenye asili yake nchini Uganda, yamesababisha zaidi ya wananchi 100,000 kuyakimbia makazi yao na hivyo kuongeza mgogoro wa kibinadamu katika eneo hilo linalohusisha watu wengine 2.6 milioni ambao wameyakimbia makazi yao huku wengine 6.4 milioni wakihitaji chakula na huduma za dharura.

Wakati huo huo, Kaimu Mkuu wa MONUSCO Bw. Moustapha Soumare katika taarifa yake ametoa wito kwa pande zote kutafuta suluhu ya kisiasa kwa matatizo ya DRC kupitia Mpango Mpana wa Kisiasa wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani, usalama na ushirikiano wa maendeleo katika DRC na eneo la Maziwa Makuu uliopitisha mwezi wa Februari na viongozi 11 wa Afrika na Taasisi nne za Kikanda na Kimataifa.

Aidha akasema katika kipindi hiki ambacho suluhu la kisiasa linatafutwa MONUSCO itatumia nguvu iliyonayo kuwalinda wananchi dhidi ya hatari zitokanazo na makundi ya waasi.

ndoa za utotoni ni moja ya sababu zinazowafanya watoto wa kike kukatisha masomo yao

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea ua mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama jijini Gaberone nchini Botswana kutoka kwa binti Jessica Kissasi, anayesoma darasa la pili, Baobab International School t arehe 29.7.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Bwana Christopher Castle,Mkuu wa Idara ya HIV and Health Education kutoka Makao Makuu ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yaliyoko Paris nchini Ufaransa wakati Mama Salma alipowasiri kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama huko Botswana tarehe 29.7.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipewa maelezo mafupi na Dr. Patricia Machawira, Mshauri Mkuu wa HIV and AIDS wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika muda mfipi kabla ya kuanza kwa mkutano wa “High Level Group-Action on comprehensive sexuality education and health services for adolescents and young people in Eastern and Southern Africa “ unaofanyika Gaberone nchini Botswana tarehe 30-31.7.2013.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa High Level Group wakisikiliza hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Mama Salma Kikwete
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia wajumbe wa mkutano wa sikuk mbili wa “High Level Group” kutoka Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika unaofanyika katika hoteli ya Lansmore Masa Square jijini Gaberone nchini Botswana.
Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania ( kulia kwenda kushoto) Dr. Kadija Mwamtemi, Mwanahamisi Kitogo, Mshauri wa Rais kuhusu masuala ya huduma za jamii, Ndugu Daud Nassib, Katibu wa WAMA foundation na Balozi wa Tanzania nchini Botswana mwenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini Mheshimiwa Radhia Msuya Mtengeti wakisikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Mama Salma tarehe 30.7.2013.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipongezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki Mheshimiwa Jesca Eriyo baada ya kufungua mkutano wa “High Level Group” huko Gaberone nchini Botswana terehe 30.7.2013.

Na Anna Nkinda- Gaborone, Botswana

Imeelezwa kwamba ndoa za utotoni ni moja ya sababu inayowafanya watoto wa kike kukatiza masomo yao huku asilimia 24 ya watoto hao wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 18 wakiolewa katika nchi zilizopo kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Kutokana na umri wao watoto hao walitakiwa kuwa wanafunzi wa shule za Sekondari na siyo kuishi na wanaume hivyo basi jitihada za pamoja zinatakiwa ili kuhakikisha kuwa sheria na sera za kumlinda mtoto wa kike na kumjengea mazingira salama ya kuishi zinatungwa.

Hayo yamesemwa leo na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wajumbe waliohudhulia mkutano wa kamati maalum ya viongozi wanaoshughulikia huduma na elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka nchi za Jumuia ya Afrika ya Mashariki (EAC) na Jumuia ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kikanda kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika katika Hoteli ya Lansmore Masa Square iliyopo mjini Gabarone nchini Botswana.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa mkutano huo unafanyika kipindi ambacho jitihada kubwa zinafanywa na nchi wanachama wa EAC na SADC ili kuhakikisha kuwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na mimba za utotoni zinapungua.

“Taarifa ya Kanda inaonyesha kuwa Ugonjwa wa Ukimwi ni changamoto kwa vijana wetu kwani kati ya maaambukizi mapya 620,000 yanatokea kila mwaka kuna vijana wadogo wenye umri wa miaka 15hadi 24 kati ya hao asilimia 60% ni wasichana hii inamaana kuwa kwa saa moja wasichana 31 na wavulana 21 wanapata maambukizi”, alisema Mama Kikwete.

Alisema ili kukabiliana na tatizo hilo jamii inatakiwa kuhakikisha kuwa kuwa mtoto wa kike anapata elimu ingawa idadi ya watoto wa kike ni kubwa katika elimu ya msingi lakini wakifika elimu ya sekondari idadi yao inapungua.

Mama Kikwete alisema, “Ingawa kuna jamii zingine ni mwiko kwa wazazi kuongea na watoto wao kuhusu afya ya uzazi lakini watoto hawa wanatakiwa kufahamu afya ya uzazi na mabadiliko ya miili yao ili waweze kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi na mimba za utotoni”.

Alisema nchini Tanzania kupitia Taasisi ya WAMA kuna kampeni isemayo mtoto wa mwenzio ni wako mkinge dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi ambayo inaihamasisha jamii kuwalinda watoto pia taasisi hiyo inafadhili elimu ya sekondari kwa watoto ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi.

WAMA imejenga mabweni ya wasichana katika shule za Sekondari, kutoa vifaa vya maabara,huduma ya maji safi na kuhamasisha watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi pia kupitia klabu mbalimbali za wanafunzi mashuleni wametoa elimu ya uzazi na jinsia ili vijana waweze kujilinda na maambukizi ya HIV na kujikinga na mimba za utotoni.

Akifungua mkutano huo Prof. Alaphia Wright kutoka UNESCO alisema mambo watakayoyajadili yatapelekwa katika Serikali za nchi husika ili ziweze kuongeza msukumo wa kisera na kibajeti na kuhakikisha kuwa wanatatua changamoto za afya na uzazi zinazowahusu vijana.

VIJANA WAASWA KUJITAMBUA NA KUTHUBUTU ILI KUJILETEA MAENDELEO

Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk Fenella Mukangara akizungumza na washiriki wa kambi ya vijana leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua rasmi kambi hiyo ambayo imeanza tarehe 29 na inatarajiwa kumalizika tarehe 2 Agosti.Kambi hiyo ya vijana ya Dunia imeandaliwa na taasisi isiyo ya Kiserikali International Youth Fellowship(IYF) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Baadhi ya washiriki wa kambi ya vijana wakisikiliza hotuba ya Mheshimiwa Waziri Fenella Mukangara hayupo pichani alipokuwa akifungua rasmi kambi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha sanaa kutoka IYF wakicheza muziki wa kitamaduni kutoka Korea mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk Fenella Mukangara wakati wa hafla ya ufunguzi kambi ya vijana leo jijini Dar es Salaam.
Waimbaji wa Kwaya ya kimataifa kutoka Korea Gracias wakiimba wakati wa hafla ya ufunguzi wa kambi ya vijana l;eo jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha sanaa kutoka Tanzania wakionyesha mchezo wa Tai Kondo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk Fenella Mukangara akiteta jambo na Mkurugenzi wa IYF Tanzania Pastor Joen Hee Yong (katika) kushoto ni mwanzilishi wa IYF Duniani Pastor Park Ock Soo.
Waziri wa Habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk Fenella Mukangara akifurahia kwaya ya Gracias ilipokuwa inaimba wimbo wa Taifa wa Tanzania kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Tanzania Profesa Elisante Ole Gabriel. PICHA ZOTE NA Frank Shija - Maelezo

Tuesday, July 30, 2013

WAZIRI MKUU WA THAILAND Yingluck Shinawatra AWASILI NCHINI KWA ZIARA RASMI YA SIKU TATU

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mgeni wake Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya kikazi ya siku tatu nchini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mgeni wake Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra wakipokea heshima.
Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra akikagua gwaride.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra kwa viongozi mbali mbali Serikali waliofika kumlaki mgeni huyo. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mgeni wake Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra wakiangalia burudani ya ngoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mgeni wake Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra.
Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra akisalimiana na baadhi ya raia wa Thailkand wanaoishi nchini alipowasili katika hoteli ya Kilimanjaro Regency Hyatt jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuonesha mandhari ya bandari ya salama Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra alipowasili jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia Ikulu nwa mgeni wake Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra alipowasili leo Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinawatra alipowasili na ujumbe wake jijini Dar es salaam leo Julai 30, 2013 kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini.PICHA NA IKULU

Monday, July 29, 2013

UWAKILISHI WA KUDUMU NEW YORK ULIVYO MUAGA BALOZI MERO

Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, mwishoni mwa wiki uliandaa hafla fupi ya kumuaga Afisa mwenza Bw. Modest Mero na Familia yake, Bw. Mero aliteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais Jakaya Kikwete kuwa Balozi wa Tanzania Geneva, hafla hiyo ilifanyika katika Makazi ya Balozi Tuvako Manongi yaliyoko 86 Jadison. zifuatato ni baadhi tu ya picha ya hafla hiyo iliyoambatana na nyama choma na chakula cha jioni.
Moja ya Zawadi ambazo wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa waliyomizawadia Bw. Mero kama kumbukumbu, kutoka kushoto ni Balozi Tuvako Manongi na mkewe Upendo, Balozi Modest Mero na mkewe Rose.
Balozi Modest Mero akitoa shukrani zake kwa niaba ya familia yake nyumayake ni watoto wake na aliyekaa kushoto ni Bw. Ken Kanda Balozi wa Ghana katika Umoja wa Mataifa.
Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, akizungumza machache wakati wa hafla hiyo ambapo alimuelezea Balozi Mero kama mchapa kazi , anayejituma na wakati wowote alipohitaji au kuulizwa chochote alilkuwa tayari kukifanya au kujibu.
Balozi Modest Jonadhan Mero akiwa na Mke wake, Bibi Rose Mero.
Sehemu ya wageni waalikiwa waliojumuika katika hafla hiyo.
Balozi Mero akiwa na Afisa kutoka Ubalozi wa Uganda pamoja na mkewe wake.
Balozi Mero akiwa na Muwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi, Bw. Perfait Onanga-Anyanga akiwa na mkewe Annett.
Picha ya pamoja na maafisa na wafanyakazi wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

JK AHITMISHA ZIARA YAKE YA MKOA WA KAGERA LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na viongozi wa kitaifa na wa mkoa wa Kagera katika kikao cha majumuisho mchana huu katika Ikulu ndogo ya Bukoba. Chini ni taswira za wahudhuriaji