Tuesday, September 30, 2014

MKUTANO WA SIKU MBILI JUU YA MABADILIKO YA TABIANCHI, UHAKIKA WA CHAKULA NA HAKI ZA ARDHI WAANZA LEO JIJINI DAR

 Jenerali Ulimwengu ambaye ndiye mwezeshaji  akiendelea kutoa Mwongozo katika mkutano wa siku mbili juu ya mabadiliko ya Tabianchi, uhakika wa Chakula na haki za Ardhi mkutano ulioandaliwa na Oxfam pamoja na Forum CC


Robert Muthami Program Support Officer kutoka Pan African Climate Justice Alliance (PACJA) akitoa ufafanuzi juu ya baadhi ya mambo yanayohusu mabadiliko ya Tabianchi.

 Meza  ya Majaji wakiwa wanasikiliza kwa makini malalamiko ya walalamikaji kutoka Loliondo juu ya kuchukuliwa ardhi pamoja na Malalamiko kutoka Wilaya ya Kishapu.
Kushoto ni mmoja wa walalamikaji kutoka Loliondo akielezea kwa uchungu jinsi Muwekezaji alivyo wanyang'anya Ardhi yao na mpaka sasa hakuna kitu ambacho kinaendelea na wanahitaji kupata Msaada wa kisheria ili wapate rudishiwa Ardhi yao.
 Kushoto ni Mama kutoka Loliondo akitoa malalamiko yake Mbele ya Mahakama ya wazi Jinsi mwekezaji alivyochukua Ardhi, kusababisha uharibifu na akina mama kuteseka pamoja na wengine kuharibu Mimba zao pia kupoteza watoto ambapo mpaka sasa kuna mtoto hajaonekana.
 Mlalamikaji Mwengine kutoka Loliondo akielezea Mbele ya Mahakama ya wazi  jinsi ya eneo lao lilivyochukulia na mwekezaji, na kutaka agizo la Mh. Waziri Mkuu lifanyiwe kazi la kwamba ardhi ile ni ya wafugaji na wanatakiwa warudishiwe
Mmoja wa walalamikaji kutoka Wilaya ya Kishapu akitoa malalamiko yake mbele ya Mahakama ya wazi juu ya walivyo chukuliwa maeneo kwa ahadi ya kuyaendeleza na kuto fanya hivyo, na kuomba eneo hilo ambalo ni mashamba warudishiwe ili waendelee na kilimo kwa kuwa eneo hilo kuna shida ya njaa.
Mchangiaji kutoka Oxfam Bwana Marc akizungumza juu ya haki za binadamu na moja ya haki hizo ni haki ya kila mwanadamu kuwa na Chakula, na kuongezea kuwa hata Umoja wa Mataifa unafahamu hilo Pia amesisitiza kuwa ni jukumu la kila mtu kujua sheria za umiliki wa Ardhi
Mjumbe wa Bodi kutoka Forum CC akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo

 Mmoja wa wachangiaji akizungumza Jambo
Mh. Jaji Richard Mzilay Akitoa Maelezo ya kina juu ya Walalamikaji kutoka Loliondo ambao walikuwa wana malalamiko ya Ardhi na Kishapu ambapo walikuwa wanataka Eneo lao lirudishwe, Ametoa maelekezo ya yale ambayo wanatakiwa wayafuate.

 

Washiriki wa Mkutano huo
 Mama Shujaa wa Chakula 2014 akichangia maada
 Burudani Elimisha ikiendelea
 Wadau wameguswa na kujumuika kucheza
 Picha ya pamoja

Azam yadhamini maonesho makubwa ya Keki Dar

Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo. Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo.Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo. Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo.Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias. Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias.Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo na kulia ni Meneja Bidhaa za Azam, Abubakar Suleiman. Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan wazamini wa maonesho hayo na kulia ni Meneja Bidhaa za Azam, Abubakar Suleiman.

KAMPUNI ya Insights Productions Limited kwa udhamini wa Kampuni ya Azam Tanzania imeandaa maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa uandaaji na utayarishaji wa keki. 

Maonesho hayo yatajulikana kama 'Azam World of Cakes Exhibition'. Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias alisema maonesho hayo yanatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali binafsi, makampuni na taasisi waandaaji wa keki nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya kubadilishana uzoefu na kujifunza ubunifu zaidi wa shughuli hizo. 

Bi. Elias alisema dhumuni la maonesho hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika Desemba 6, 2014 jijini Dar es Salaam ni pamoja na kusherehekea taaluma ya uokaji keki kwa kuonesha ubunifu na utaalam wa utengenezaji na upambaji wa keki bidhaa inayopendwa na watu wengi na kutumika katika shughuli anuai za kijamii.

 Alisema washiriki wa tamasha hilo mbali na kushindanisha na kuonesha bidhaa zao za keki pia wanatarajia kupata semina ya mafunzo juu ya utengenezaji bora wa keki ikiwa na lengo la kuboresha zaidi taaluma zao. Alisema washiriki hao pia watafanya maonesho ya utayarishaji wa vyombo vya kutengenezea keki, utayarishaji wa unga wa ngano kwa ajili ya kupikia keki, kutambua unga bora wa keki, uchanganyaji wa unga na viungo vingine kwa ajili ya uboreshaji wa radha ya keki. 

 Alisema maonesho mengine yatakayofanywa na wadau hao wa keki ni pamoja na uhifadhi bora wa keki kwa muda mrefu bila kuharibika na washiriki kuonesha maumbo mbalimbali ya keki yenye mvuto kwa watumiaji wa keki na jamii nzima. Alisema maonesho hayo yanayodhaminiwa na Azam watengenezaji wa unga bora kwa ajili ya kutengenezea bidhaa hiyo, yatawashindanisha wadau wa uandaaji keki na pia washindi watakao tajwa na majaji wa maonesho watajipatia fedha taslimu na bidhaa mbalimbali. 

 "...Onesho hili litahusisha jamii yote inayojishughulisha na utengenezaji wa keki, upambaji wa keki, wauzaji wa keki na wanaojishughulisha na bidhaa mbalimbali zinazotumika kutengeneza keki kama vile unga wa ngano wa Azam," alisema Mkurugenzi wa Insights Productions Limited, Bi. Elias. 

Akifafanua zaidi Mkurugenzi huyo alisema onesho hilo litajumuisha bekari na hoteli mbalimbali, Vyuo vya taaluma ya hotelia toka Tanzania na majirani (Afrika Mashariki) pamoja na watengenezaji keki binafsi. Wananchi watakaotembelea maonesho hayo ambayo hayata kuwa na kiingilio watapata fursa ya kujionea aina na mitindo mbalimbali ya utengenezaji wa keki pamoja na kuonja bidhaa hiyo kwenye maonesho ambayo yatafanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam. 

 Akizungumzia maonesho hayo Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan alisema Azam ikiwa ni kampuni inayotengeneza unga bora wa kutengenezea keki imeamua kudhamini ikiwa ni ishara ya kutambua taaluma hiyo ya uokaji keki nje na ndani ya Tanzania.

TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA GIZ

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John akitoa tamko kuhusu Siku ya Soko la Afya iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la GIZ , itakayofanyika Oktoba 2 katika ukumbi wa Diammond Jubelee jijini Dar es salaam.
Naibu Meneja wa Miradi ya Afya wa GIZ Bw. Christian Ptleiderer akizungumza na waandishi wa habari kutoa wito kwa mashirika mengine yanayotoa huduma za afya nchini kuendelea kusaidia na kusambaza huduma zao katika maeneo yenye changamoto ya miundombinu na uhaba wa watumishi wa afya.Kulia ni Mtaalam na Mawasiliano wa shirika la GIZ nchini Bi. Vida Mwasalla. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Shirika la Ujerumani la GIZ katika uanzishaji na uendelezaji wa programu mbalimbali za utoaji wa huduma za afya zinazolenga kupunguza vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akitoa tamko kuhusu Siku ya Soko la Afya  nchini iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Ujerumani la GIZ  itakayofanyika Oktoba 2,  jijini Dar es salaam.

Amesema Tanzania na GIZ zimekuwa zikishirikiana katika uboreshaji wa miradi mbalimbali ya afya kwa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kuanzia ngazi ya taifa, mikoa na Halimashauri za wilaya.

Ameeleza kuwa mikoa ya Lindi, Mbeya, Mtwara na Tanga imeendelea kunufaika na miradi mbalimbali ya ushirikiano  chini ya shirika hilo inayolenga kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma za afya katika maeneo hayo, uimarishaji wa mifuko ya Afya ya Jamii na ushiriki wa moja kwa moja kusaidia upatikanaji na uendelezaji wa wataalam wa kutoa huduma za afya maeneo ya vijijini.

Ameongeza kuwa GIZ imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika kuhakikisha kuwa jamii inamudu huduma bora za afya kupitia Mifuko ya Hifadhi ya Afya ya Jamii iliyopo katika maeneo yao.

Aidha, amebainisha kuwa maonyesho ya siku ya Soko la Afya yatakayowahusisha wadau mbalimbali na mashirika yanayotoa huduma za afya nchini yanalenga kuwakutanisha wadau hao ili waweze  kujadili changamoto za utoaji wa huduma za afya nchni, kujifunza mafanikio yaliyopatikana katika baadhi ya maeneo na kuweka mikakati ya kuyafikia maeneo mengi zaidi.

Kwa upande wake Mtaalam na Mawasiliano wa shirika la GIZ nchini Bi. Vida Mwasalla ameeleza kuwa maonesho ya mwaka huu yazilenga Wizara, Taasisi , Washirika wa Maendeleo, Makampuni, Mashirika binafsi  na Wakala zinazojihusisha na utoaji na uendelezaji wa sekta ya afya nchini.

Amesema katika maonesho hayo GIZ kwa kushirikiana na Wizara ya Afya itaonyesha mikakati mbalimbali ya kuwaokoa watoto wadogo wenye matatizo ya afya, namna walivyofanikiwa kuwapata watumishi wa afya katika maeneo ya Lindi na Mtwara, maeneo  ambayo hapo awali walikuwa hawakai katika vituo vyao.

Ameongeza kuwa mbali na Siku ya Soko la Afya kuhusisha huduma za utoaji wa elimu, vipimo, machapisho mbalimbali inalenga kuwaweka pamoja wadau hao ili waweze kubadilishana uzoefu na kuweka  mikakati ya kuchangia maendeleo ya sekta ya afya hapa nchini.

Naye Naibu Meneja wa Miradi ya Afya wa GIZ Bw. Christian Ptleiderer ametoa wito kwa mashirika mengine yanayotoa huduma za afya nchini kuendelea kusaidia na kusambaza huduma zao katika maeneo ambayo bado yanakumbwa na changamoto mbalimbali za miundombinu na uhaba wa watumishi wa afya.


Amesema wao kama GIZ kwa kuanzia wameanza na mikoa 4, na wanaendelea kujenga uwezo wa kuyafikia maeneo mengi zaidi kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani na Tanzania.

NSSF YATOA FURSA KWA WAKAZI WA MBEYA NA SONGEA

Kupitia Semina za Fursa zinazoendelea kufanyika katika mikoa mbali mbali hapa nchini, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) imekuwa ikitoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi na kuwahamasisha kujiunga na mfuko huo ili waweze kunufaika na mafao ya NSSF hususani matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi wake pamoja na mikopo kupitia SACCOS.

Fursa nyingine kutoka NSSF ambazo mwanachama anaweza kunufaika nazo ni pamoja na Pensheni ya uzeeni, Pensheni ya Ulemavu, Pensheni ya Urithi, msaada wa Mazishi, Mafao ya Uzazi, mafao ya Kuumia Kazini.

Semina hizi zinatoa fursa kwa wajasiriamali, wakulima pamoja na watu mbalimbali waliojiajiri wenyewe na kuuliza maswali mbalimbali kuhusu huduma zinazotolewa na NSSF na wengi hujiuga na NSSF baada ya kuona faida zake.

"Katika semina za Fursa NSSF inafanya uandikishaji wa wanachama wapya na pia inatoa nafasi kwa wananchi kuuliza na kufahamu mambo mbali mbali yanayohusu mfuko huo" alisema Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba.

Mpaka sasa NSSF imeshiriki katika Semina ya Fursa  katika mikoa ya Geita, Ruvuma, Mbeya na Morogoro. 
 Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba akitoa mada katika semina ya Fursa kuhusu Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi na kuwahamasisha wajiunge na mfuko huo ili waweze kunufaika na mafao yanayotolewa na NSSF hususani Matibabu Bure kwa mwanachama na wategemezi wake pamoja na mikopo kwa wanachama kupitia Saccos. Semina hiyo ilifanyika mkoani Mbeya hivi karibuni.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi, Ruge Mutahaba (katikati), Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba (wa tatu kutoka kulia) wakiwa meza Kuu pamoja na wageni wengine wakati wa Semina ya Fursa iliyofanyika mkoani Mbeya.
 Baadhi ya umati wa wakazi wa Mbeya mjini wakifuatilia kwa makini Semina ya Fursa iliyofanyika katika Ukumbi wa Benjamini Mkapa mjini Mbeya.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi, Ruge Mutahaba akitoa mada katika semina ya Fursa Mbeya iliyodhaminiwa na NSSF kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi wakazi wa Mbeya.
Afisa Matekelezo wa NSSF, Ally Mkulemba akitoa mada kuhusu faida za kujiunga na NSSF kwa wakazi wa mjini Songea wakati wa Semina ya Fursa iliyofanyika mkoani Ruvuma.
Msanii wa Bongo Fleva Mwasiti Almasi akiwasihi wakazi wa Songea wajiunge na NSSF ili waweze kupata Fursa ya kujikwamua kimaisha kupitia mafao mbali mbali ya NSSF kama Mikopo kupitia Saccos, Matibabu Bure, Pensheni ya uzeeni, pensheni ya ulemavu, pensheni ya urithi, msaada wa mazishi, mafao ya uzazi, mafao ya kuumia kazini. 
Afisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ally Mkulemba (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi, Ruge Mutahaba (kushoto) wakifuatilia kwa makini semina ya Fursa iliyofanyika Songea mkoani Ruvuma.

WAKANDARASI UMEME WASIOWAJIBIKA KUNYANG’ANYWA TENDA

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Meza Kuu-Katikati), akizungumza na wawakilishi wa Kampuni mbalimbali zinazohusika kusambaza umeme vijijini kutoka India, China na Sri Lanka zinazofanya kazi katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuhusu utekelezaji wa miradi husika.
Wawakilishi wa Kampuni mbalimbali zinazohusika kusambaza umeme vijijini kutoka India, China na Sri Lanka zinazofanya kazi katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na baadhi ya Mameneja wa Tanesco wa Mikoa husika, wakitoa mrejesho kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Meza Kuu – Katikati), kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Miradi husika. Kulia kwa Waziri Muhongo ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga na kushoto kwa Waziri ni Kamishna Msaidizi wa Nishati sehemu ya Umeme, Mhandisi Innocent Luoga.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Dk. Lutengano Mwakahesya akizungumza katika mkutano baina ya Waziri wa Nishati na Madini na kampuni zinazosambaza umeme vijijini kwa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Mwakahesya aliahidi kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa.

Na Veronica Simba

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amezitaka Kampuni zilizopewa tenda kusambaza umeme vijijini kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa vinginevyo watanyang’anywa tenda hizo.

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki mjini Dodoma katika Mkutano baina yake na wawakilishi wa Kampuni husika kutoka India, China na Sri Lanka zinazofanya kazi katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi pamoja na Mameneja wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) wa mikoa hiyo na Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Profesa Muhongo aliitisha Mkutano huo kwa lengo la kupokea taarifa kutoka kwa Watendaji wa Kampuni hizo kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini kabla ya kutembelea miradi hiyo kwa mara nyingine kama ambavyo amekuwa akifanya mara kwa mara kujiridhisha na maendeleo yake.

Akizungumza katika Mkutano huo mara baada ya kupokea taarifa za utekelezaji kutoka pande zote, Waziri Muhongo alimwagiza Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya kuhakikisha utekelezaji wa miradi hiyo unafuatiliwa kwa ukaribu na kusitisha tenda mara moja kwa kampuni zitakazobainika kutotimiza makubaliano ya mkataba walioingia.

“Fuateni utaratibu wa kisheria kwa kutumia vifungu vilivyomo kwenye mkataba vinavyoelekeza kuchukua hatua stahiki kwa kampuni isiyotekeleza wajibu wake ipasavyo,” alisisitiza Muhongo.

Aliongeza kuwa Serikali imedhamiria kuhakikisha inatimiza ahadi yake ya kuwapatia Watanzania umeme ili wajikwamue katika lindi la umaskini kwa kukuza kipato chao na cha Taifa kwa ujumla hali itakayofanya Tanzania kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

“Yeyote atakayetukwamisha au kuturudisha nyuma katika kufikia malengo yetu ya kuwaondolea Watanzania umaskini, tutapambana naye na kamwe hatutampa nafasi,” alisema Muhongo.

Vilevile, aliwataka Mameneja na watendaji wengine wa Tanesco kuachana na utamaduni wa kukaa ofisini na kusubiri ripoti za utekelezaji wa miradi badala yake watembelee miradi wanayosimamia na kuhakikisha kazi inafanyika kama inavyotakiwa.

Aidha, Waziri Muhongo aliwataka wakandarasi waliopewa tenda husika kuwa wakweli na waaminifu na kuachana na tamaa hususan wanapopewa kazi ambayo wanajua hawana uwezo wa kuitekeleza ipasavyo ili kuwapa nafasi wengine wenye uwezo huo.

Alisema ni bora kwa Mkandarasi kukubali kazi anayoimudu ili aifanye kwa ubora unaotakiwa na hivyo kujiongezea sifa za kupewa kazi nyingine kuliko kuomba kazi kubwa asiyoweza kuitekeleza kikamilifu na matokeo yake anaharibu na kupoteza sifa ya kufikiriwa kupewa kazi nyingine.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga aliwataka wote wanaohusika na utekelezaji na usimamizi wa miradi hiyo ya kusambaza umeme vijijini kutimiza wajibu wao   kwa vitendo.

“Achaneni na maneno maneno, mimi nataka kuona vitendo, nataka kuona matokeo,” alisisitiza na kuongeza kwamba hakuna sababu ya Wakandarasi kusuasua katika utekelezaji wa miradi hiyo kwani walioomba wenyewe wakijinadi kuwa wanaweza.

Naye Kamishna Msaidizi wa Nishati Sehemu ya Umeme, Mhandisi Innocent Luoga aliwataka Wakandarasi hao kujituma na kufanya kazi inavyostahili pasipo kusubiri kufuatwa-fuatwa na kuhimizwa kwa suala ambalo ni wajibu wao.

Wakichangia mawazo katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Edmund Mkwawa na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala huo, Dk. Mwakahesya waliahidi kufanya kazi bega kwa bega na wadau mbalimbali wa sekta hiyo ili kuhakikisha Watanzania hususan walioko vijijini wanapatiwa nishati ya umeme kama Serikali ilivyodhamiria na kuahidi.

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTUMIA REDIO JAMII KUELIMISHA UMMA

DSC_0009
Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye, akiutambulisha ujumbe wa wageni kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini kwa Wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika kuboresha masoko kwenye vituo vyao iliyofadhiliwa na shirika la maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na UNESCO.

Na Mwandishi Wetu, Sengerema
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kupitia Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) itaanza kutoa elimu inayohusu sheria ya vyama vya siasa na sheria ya gharama za uchaguzi kupitia redio za jamii ili kuwawezesha wananchi kutambua wajibu wao katika kulinda amani ya taifa kuelekea katika uchaguzi na wakati wa uchaguzi.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Beatrice Stephano wakati akizungumza na mameneja wa redio hizo katika warsha yao ya siku 5 iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Sengerema.
Beatrice alikuwa akizungumzia mradi anaousimamia ambao umedhaminiwa na UNDP kupitia UNESCO kwa ajili ya kuelimisha umma wa watanzania kupitia redio za jamii katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi 2015.
Alisema uamuzi wa kutumia redio za jamii unatokana na redio hizo kuwafikia wananchi wengi zaidi, hali ambayo wadau katika masuala ya demokrasia wameona kwamba inaweza kutumika kuboresha zaidi uelewa wananchi.
DSC_0013
Meza kuu: Kutoka kushoto ni Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa mkoani Mwanza, Bw. Isaya Makoko, Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano, Mwenyekiti wa Warsha hiyo kutoka Orkonerei Radio Service Simanjiro Manyara, Bw.Baraka Ole Maika (katikati), Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia) pamoja na Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia (kulia).
Uelewa huo upo katika sheria za uchaguzi, gharama na kuona wajibu wao wa kumsaidia Msajili wa Vyama vya Siasa kukabiliana na mazingira hatarishi ya amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
Alisema ni kazi ya Ofisi Msajili wa Vyama vya Siasa kusimamia sheria ya vyama namba tano ya mwaka 1992 ya kusajili vyama na kuviangalia na ile ya namba sita ya mnwaka 2010 ambayo inagusia gharama za uchaguzi.
Mratibu huiyo amesema kwamba timu kutoka Ofisi ya Msajili itafika kwenye redio hizo za jamii na kuzungumza na wananchi kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wao katika siasa na kuimariuka kwa demokrasia.
Aidha elimu hiyo inatarajiwa kuwasaidia wananchi kutambua kwamba wana wajibu katika kuhakikisha kwamba menejimenti za uchaguzi zinawajibika pamoja na muuingiliano wake ili kuwa na michakato salama ya cuhaguzi na uchaguzi wenyewe.
DSC_0081
Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano (wa pili kushoto) akizungumza na mameneja wa redio za jamii nchini wanaohudhuria warsha ya siku tano inayofanyika kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza kuhusiana na ofisi yake kufanya kazi kwa pamoja na redio za jamii nchini katika kutoa elimu kwa umma.
Naye Afisa mfawidhi ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa mkoani Mwanza, Ludovick Ringia akizungumzia sheria mbili za vyama vya siasa alisema kwamba ni wajibu wao kuwaeleza wananchi kuhusu maadili na kanuni katika sheria zinazogusa ukuzaji wa amani katika duru za siasa na demokrasia.
Alisema mradi huo wa kuelimisha wananchi ambao unafanyika kwa udhamini wa Unesco kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ni moja ya njia za kufanikisha amani katika kipindi chote kuanzia uchaguzi wa mwisho hadi mwingine.
Alisema wanatumia redio za jamii kwa kuwa redio za kibiashara zimekuwa kikwazo hasa bajeti inapouma kidogo.
Alisema mradi huo ambao unafanyika kwa mwaka mmoja ni sehemu ya juhudi za taasisi hiyo za kuliwezesha taifa kuendelea kuwa na utulivu.
DSC_0073
fisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph (wa pili kulia), akielezea uwezo wa redio za jamii zinavyoweza kufikia jamii kubwa zaidi nchini wakati ujumbe kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ulipofanya mazungumzo na Wenyeviti wa Bodi na Mameneja wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano iliyofadhiliwa na shirika maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na UNESCO iliyofanyika kwenye kituo cha habari na mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza.
Wenyeviti wa bodi na mameneja hao katika warsha hiyo walielemishwa uboreshaji wa masoko na umuhimu wa redio za jamii juu ya matumizi ya Tehama kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kazi na kushirikisha zaidi wananchi.
Aidha Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Al Amin Yusuph akizungumzia mafunzo hayo alisema kwamba mradi huo umekuja wakati muafaka ili kutoa elimu kwa umma, kwani kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa takribani asilimia 70 ya wananchi wanaoishi vijijini wanasikiliza redio huku asilimia 5 tu ndio wanaangalia runinga.
DSC_0119
Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia (kulia) akielezea ufanyaji kazi wa sheria mbili za vyama vya siasa kwa wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini wakati wa warsha ya siku tano iliyofadhiliwa na SIDA na kuratibu na UNESCO ambayo imefanyika kwenye kituo cha Redio Sengerema mkoani Mwanza.
DSC_0034
Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa mkoani Mwanza, Bw. Isaya Makoko akiwasilimia wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini (hawapo pichani).
DSC_0135
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo akihoji swali kwa ujumbe uliotoka kwenye ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini.
DSC_0126
Pichani juu na chini ni baadhi ya wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano iliyomalizika mwishoni mwa juma kwenye kituo cha Redio Sengerema mkoani Mwanza kwa ufadhili wa SIDA na uratibu wa UNESCO.
DSC_0085

Taswira za mnuso wa mkutano wa jumuiya ya Watanzania Sweden na kumkaribisha balozi dorah Msechu

 Mama Dora Msechu Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchi za kinordic na Baltic alipokelewa kwa shangwe.
 Muziki hadi lyamba
 Wadau wakiserebuka
DJ Richie akiwa engine room
  Dj Richie na Dr Erick Kalebi wakiwajibika
 Mama Dora Msechu Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchi za kinordic na Baltic alipokelewa kwa shangwe.
 Palipendeza...
 Mbili zatosha???
 Ukumbi ukiwa nyomi
 Ngoma na nyimbo za kwetu

 Nyomi
Ukumbi umenona