Friday, February 28, 2014

THE AMERICAN PEOPLE’S COMMITMENT TO COMBATING WILDLIFE TRAFFICKING IN TANZANIA

By Virginia Blaser

I would like to take the opportunity of  this year’s World Wildlife Day to highlight the American people’s commitment to combatting the global scourge of wildlife trafficking and to draw attention to how and where the American and Tanzanian peoples and governments can work together to save the world’s precious wildlife.  

I know that everyday Tanzanians share these goals, and I note that President Mwalimu Julius K. Nyerere once said that "…the survival of our wildlife is a matter of grave concern to all of us in Africa. 

These wild creatures amid the wild places they inhabit are not only important as a source of wonder and inspiration, but are an integral part of our natural resources and our future livelihood and well being."  

During his trip to Tanzania last summer, President Barack Obama underscored the American commitment by signing an Executive Order on combating wildlife trafficking.  This order defined wildlife trafficking as “the poaching of protected species and the illegal trade in wildlife and their derivative parts and products.”  

Just a few weeks ago, President Obama added to our U.S. policy directions by signing the U.S. National Strategy for Combating Wildlife Trafficking.  This Strategy established the guiding principles and policy priorities for U.S. efforts to stem this illicit and highly destructive trade.

Combating wildlife trafficking is a global concern of particular significance to Tanzania.  Wildlife trafficking has become a lucrative trade in Tanzania, taking a serious toll on target species, driving poaching activities, and robbing Tanzania of precious resources, including elephants and rhinoceros. 

 Profits from this illicit trade also fund criminal enterprises and activities that endanger national security.  Furthermore, wildlife trafficking threatens a thriving tourism industry that provides employment to tens of thousands of Tanzanians and generates millions of dollars in revenue every year.  

Particularly frightening is the situation in the Selous Game Reserve, which demonstrates the dire need for action.  The Selous is the largest protected area on the African continent, covering 48,000 square kilometers; indeed it is so special that the Selous Game Reserve is one of only three UNESCO World Heritage Sites in Tanzania.  

Three years ago, Selous boasted 40,000 elephants.  Today you have barely 13,000.  If this trend continues unchecked, this unique and globally-recognized element of Tanzania’s natural heritage will disappear forever.

The Government of Tanzania has taken some significant, positive steps to combat wildlife trafficking and is deeply engaged in a process to ensure wildlife security issues are approached strategically and through an appropriate regulatory framework which also respects human rights.  

We support these ongoing efforts and encourage robust engagement across all ministries, including law enforcement and the judiciary.  The wildlife sector earns significant revenue for Tanzania and we encourage the government to dedicate an increased portion of this revenue to protect wildlife and the important jobs and industry that depend on this resource. 

  The American people are committed to working hand-in-hand with the Tanzanian people to build the capacity of local and national government agencies to address this critical issue and we encourage continued progress on these efforts.  To that end, the U.S. Government has offered technical assistance on both the economic and legislative aspects of the wildlife issue in Tanzania.

Through the United States Agency for International Development (USAID), the United States has contributed over $100 million to conservation in Tanzania since 1990 and we will continue our strong support of the biodiversity sector in Tanzania.  

We intend to continue our support of Wildlife Management Areas, landscape conservation and climate resiliency approaches to help conserve wildlife habitats and foster sustainable tourism for generations.  We are also developing a five-year program to assist the government of Tanzania and communities to improve the management and conservation of Tanzania's biodiversity.

Since 1990, conservation partners in Tanzania have received $4.1 million from the U.S. Government, through our Fish and Wildlife Service, for the conservation of elephants, rhinos, chimpanzees, and marine turtles.  We have also provided funds for Tanzanians to be trained in “wildlife investigations” at the International Law Enforcement Academy in Botswana and we recently funded 25 Tanzanian law enforcement personnel from TANAPA and the Wildlife Division to attend Regional Rural Border Patrol training. 

These courses offer Tanzania the opportunity to work with Uganda and Kenya to improve cross border cooperation to combat wildlife trafficking.  

Tanzania has some of the most important and largest wildlife populations and network of protected areas in the world, and these precious resources and treasured national legacy are under immediate threat due to poaching and the illegal wildlife trade. 

 I urge the Tanzanian people to robustly support anti-poaching initiatives at the local, regional and national level. Together we – members of government, international donor community, civil society, law enforcement, and environmentalists – can effectively put an end to this illicit trade and help protect the future of Tanzania’s natural resources for generations to come.

Wanafunzi wa Tanzania Thailand Waizungumzia sekta ya Madini

Kamishna Msaidizi wa Madini Mhandisi,Hamis Komba (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma masomo ya Geomolojia katika Chuo cha ‘Asian Institute of Geological Science’ (AIGS) nchini Thailand. Wa kwanza kulia ni Agatha Mwinuka, anayefuata ni Emmanuel Minja na wa kwanza kushoto ni Doricas Moshi.
Wanafunzi wa Kitanzania nchini Thailand, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wenzao kutoka mataifa mbalimbali , ambao wamelitembelea banda la Tanzania.
Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini katika picha ya pamoja na wanafunzi hao katika banda la Tanzania.

Na Asteria Muhozya, Bangkok

Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma masomo ya Geomolojia katika Chuo cha ‘Asian Institute of Geological Science’ (AIGS) nchini Thailand, wamewataka wadau wa tasnia ya madini ya vito na usonara nchini Tanzania kuichukua sekta hiyo kwa umakini mkubwa kutokana na mchango wake kiuchumi.

Aidha, wameeleza kuwa, nchi ya Thailand imepiga hatua kubwa katika sekta ya madini ukilinganisha na Tanzania lakini bado Tanzania inaweza kufaidika zaidi katika sekta hiyo ikiwa kila mdau atatimiza wajibu wake kikamilifu ili madini ya vito yaongeze mchango katika pato la taifa.

Wameongeza kuwa, Tanzania bado ina nafasi ya kujipanga upya kuhusu kuboresha zaidi sekta hiyo kama ilivyo kwa nchi nyingine endapo mipango mikakati ya maboresho itatekelezwa na kusimamiwa kikamilifu.

Wanafunzi hao wameyasema hayo, wakati walipolitembelea banda la Tanzania katika maonesho ya 53 ya Vito vya Usonara na Madini yanayoendelea katika jiji la Bangkok ambapo nchi zaidi ya 150 zinashiriki maonesho hayo.

“Thailand wamejipanga vizuri katika sekta ya madini. Wafanyabiashara wa madini wana umoja. Wadau wa madini wanatakiwa kuelewa kuwa madini yanawakilisha utajiri wetu tulionao”. Amesema Agatha Mwinuka.

Aidha, wameitaka serikali na wadau wa Tanzania wanaoshiriki maonesho hayo kujifunza kutokana na changamoto wanazozipata kutoka kwa nchi nyingine, jambo ambalo litasaidia kuboresha sekta ya madini na vito, ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanafuata sheria na taratibu zilizopo.

“Tunaiomba serikali iendelee kuendeleza viwanda vya kukata madini. Ni jambo zuri kama shughuli hizi za kukata madini zitafanyika ndani ya nchi badala ya nje. Jambo hili linasaidia sana kuongeza thamani ya madini. Ameongeza, Emmanuel Minja.

Akiongelea kuhusu umuhimu wa kuendeleza na kuboresha kituo cha Tanzania Geomological Center, Doricas Moshi, ameeleza kuwa, kituo hicho kinaweza kutoa mchango mkubwa katika tasnia hii hasa katika nyanja ya ukataji madini na uthamini wa madini hivyo, ameitaka Serikali kukiongezea nguvu kituo hicho kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo ya Tanzania.

“Chuotunachosoma hapa kinatumia sana mifano ya madini ya Tanzania katika kufundisha. Mengi yametoka nyumbani, hii ni ishara nzuri. Serikali iliangalie hili. Ameongeza Doricas.

Aidha, wameeleza kuwa, soko la kimataifa kwa madini ya Tanzania lipo, hivyo, wamewataka wadau wote kuhakikisha wanashirikiana vizuri na serikali kuendeleza sekta hiyo kutokana na umuhimu na mchango wake kwa taifa.

Akizungumzia mipango iliyopo ya kuboresha sekta hiyo, Kamishna Msaidizi wa Madini, Mhandisi Hamis Komba, amesema kuwa, Serikali kupitia Shirika la Madini Tanzania (STAMICO), inatekeleza mikakati ya kuwasaidia wachimbaji wadogo na wa kati ili waweze kuendana na mahitaji ya soko la kimataifa kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali yakiwemo ya kukata madini, kuyaongezea thamani na kuwapatia mikopo kupitia Benki ya TIB.

“STAMICO imepewa jukumu la kuwaendeleza wachimbaji wadogo katika sekta ya madini hususani katika masuala ya uchimbaji, uongezaji thamani madini na biashara ya madini. Serikali imejipanga vizuri katika hilo”. Ameongeza Kamishana.

Ameongeza kuwa, Serikali inatambua kwamba wachimbaji wengi wapo katika sekta ya madini ya vito na usonara hivyo, jitihada za kuwaendeleza zitasaidia kufikia kiwango bora cha utendaji wao wa kazi.

Vilevile, ameongeza kuwa, kutokana na kuboreshwa kwa Sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo inaiwezesha STAMICO kumiliki asilimia 50 ya hisa katika mgodi wa Tanzanite One, jambo ambalo linaifanya Serikali kuwa mmiliki katika mgodi huo.

Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga.

Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Godfrey William Mgimwa akibebwa Juu na Wanachama/wapenzi wa CCM mara baada ya Kuwasili Viwanja Vya Stendi-kata ya Ifunda.
Mapokezi Mazito yakiendelea ya Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara na Kijana Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa kwenye uwanja wa Stedi-Kata ya Ifakara hii leo wakati wa Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga.
 
Mh:Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara akisaini Kitabu akiwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa mara baada ya kuwasili Viwanja Vya Stendi Kata ya Ifunda.Chief Wa Wahehe,Chief Mkwawa ambaye pia ni Kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi akishikana Mikono ya Baraka na Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Godfrey William Mgimwa,Pia akisalimana na Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba hii leo kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni kata ya Ifunda-Kalenga.Kubwa zaidi CHIEF MKWAWA ambaye ni 
Mtoto wa Marehemu Mkwawa alikuwa anakanusha taarifa kuhusu Yeye Kuunga Mkono Chadema,Amesema hawezi kuunga Mkono chama ambacho hakieleweki kuanzia muundo wake na hata maamuzi yake ndani ya Chama.Yeye ni MwanaCCM damu damu,na ameapa atafia CCM.
 Msanii Dokii ambaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi akitumbuiza kwenye ufunguzi wa kampeni wa Jimbo la Kalenga kwa Chama Cha Mapinduzi.Dokii ametunga wimbo rasmi kwaajili ya Kalenga na Umuhimu wa Kijana Godfrey William Mgimwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo,
 Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini Ndugu Mtatulu akionesha baadhi ya Mitego inayodaiwa kuwekwa na Vijana wa CHADEMA kwenye njia ili Magari ya CCM yanayozunguka kwenye Kampeni yapate matatizo.  Ndugu Mtatulu alitaja majina ya Wahusika na ameshayapeleka Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.
Naibu katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba akiteta Jambo na Kijana Godfrey William Mgimwa ambaye ni Mgombe Ubunge Jimbo la Kalenga.
Wabunge wa Iringa(Wilaya+majimbo) wakitoa neno la kuomba Kura kwa Wananchi Wa Ifunda ili wamchague Mgombe wa CCM Kijana Godfrey William Mgimwa.
 Ni Naibu Katibu Mkuu CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na mamia ya Wananchi waliofurika Viwanja Vya Stendi Kata ya Ifunda hii leo kuhudhuria Mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga(CCM).Mh:Mwigulu Nchemba amewaomba Wananchi wa Kalenga kumchagua Kijana Godfrey William Mgimwa kwa sababu anakila sifa za kuwatumikia Wananchi wa Kelenga,Lakini pia  ni Kijana aliyependekezwa na Chama kuanzia ngazi ya Chini hadi Taifa kwa mtindo wa Kura za maoni na amewashinda wenzake 9.
Mh:Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa Kwa namna Marehemu Mgimwa alivyolitumikia Jimbo lake na kuiletea Heshima Nchi yetu na Jimbo la Kalenga,kuna kila sababu ya Kuipa nafasi CCM iendelee kutekeleza Ilani yake ndani ya Jimbo hilo.Mh:Mgimwa tangu kufariki kwake Vyama vya siasa vimekuwa mstari wa mbele kumsifia kutokana na Utendaji wake Kuanzia Wizara ya Fedha hadi Jimboni kwake hasa upande wa Miundombinu,Maendeleo yote yaliyofanyika ndani ya Jimbo la Kalenga ni Matunda ya sera nzuri za CCM na Ilani ya CCM ndani ya Jimbo hilo.
Pia Mwigulu amezungumzia kuhusu Amani na Mshikamano ulipo kwa Wananchi wa Kalenga ni lazima uendelee kudumishwa,Kitendo cha kukaribisha wapinzani kwenye jimbo hili ni sawa na kukaribisha Vurugu kwasababu Wapinzani hasa Chadema katika Taifa hili hawana rekodi nzuri ya kudumisha amani kwenye maneo wanayoongoza. 
Kubwa zaidi Mh:Mwigulu Nchemba ameendelea kuwaomba Wanakalenga kufanya Kampeni za  Ustaarabu,Kampeni za Amani na Utulivu.Kwa MwanaCCM kufanya Vurugu sio Jambo jema,bali tutumie Amani tuliyonayo kuwaelimisha hata wenzetu wa Upinzani kufanya siasa za kistaarabu,Waache michezo ya Kusababisha Vifo kwa Wananchi wasio na hatia yoyote ile.Siasa safi ni zile za Kupambanisha Sera na Uwezo wa Kujenga hoja majukwaani.
Hivyo tar.16/03/2014 Wanakalenga Wote wanajitokeze Kupiga Kura na Kumchagua Mgombea wa CCM Kijana Godfrey William Mgimwa kwa maendeleo ya Wote Wanakalenga.

Kijana huyu ameamua kurudisha Kadi ya Chadema baada ya Somo zuri Kutoka kwa Mh:Mwigulu Nchemba kwenye Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni Jimbo la Kalenga.
Naibu Katibu Mkuu CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey Mgimwa hii leo kwenye Ufunguzi wa Kampeni Jimbo la kalenga. Uchaguzi unategemewa Kufanyika  Machi 16, 2014.

 ...............................................................................................
WAKATI  kampeni za  uchaguzi  mdogo  jimbo la kalenga  Iringa  zikiendelea  kuchukua  kasi naibu katibu mkuu wa  chama  cha mapinduzi (CCM) Taifa Mwigulu Nchemba  amepiga kambi kwa  muda Kalenga  huku akiibua siri  nzito  ya Chadema kuanza  kununua shahada za  wapiga  kura.

Mwigulu  alisema  kuwa  kumekuwepo na mbinu  chafu  inayofanywa na  Chadema kwa kuanza kununua  shahada za  kupigia kura  kwa  wananchi wa jimbo la Kalenga .

Alisema  kuwa  Chadema  wameanza  mbinu  hiyo  chafu  baada ya  kubaini  wazi kuwa  mgombea  wa CCM Godfrey Mgimwa  tayari  amekwisha  shida  katika  uchaguzi  huo  kutokana na imani  kubwa ya  wana kalenga  kwa CCM.
 Hivyo  aliwataka  wananchi  kutodanganyika na pesa   zinazotolewa na Chadema kwa kununua haki  yao  na badala  yake  kutunza  shahada  hizo  ili kuzitumia kupiga  kura kama  sehemu ya haki yao ya Msingi.
"CCM imefanya mambo  mengi  katika jimbo la Kalenga  kama  kuboresha  miundo  mbinu   na mambo  mbali mbali  yakiwemo afya , elimu  ....jambo ambalo  wananchi  bado  wana imani  kubwa na  CCM".
Wakati  huo  huo   Chifu Mkwawa  Bw  Abdu Mkwawa amekigeuka  Chadema kuwa  kimedanganya  umma kuwa Chifu Mkwawa anakiunga mkono  chama  hicho.
Mkwawa  alisema  kuwa Dr Slaa amedangaya umma kuwa yeye anaunga mkono Chadema. Amesema hawezi kuunga Mkono chama ambacho hakieleweki kuanzia muundo wake na hata maamuzi yake ndani ya Chama.Yeye ni MwanaCCM damu damu,na ameapa atafia CCM. 

Kaya zaidi ya 5000 za manispaa ya Iringa kufikiwa na maji safi na salama

Katika kukamilisha ahadi na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011 – 2016), Serikali imejidhatiti kuwafikishia maji safi na salama wakazi wa zaidi ya kaya 5000 za Manispaa ya Iringa kufikia katikati ya mwaka huu wa fedha.

Hayo yalibainishwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayodhaminiwa na serikali na wafadhili.

Bibi Mwanri alisema kuwa katika kutimiza Mpango wa huo wa Maendeleo Serikali inawekea mkazo katika Kuendeleza adhma yake ya utekelezaji wa miradi ya maji iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) hasa katika maeneo sugu yenye upungufu wa maji hasa maeneo ya vijijini ili kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuuendelea kuimarisha usimamizi vyanzo vya maji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William alisema kuwa kupitia Mpango huo wa Maendeleo wa Miaka Mitano zaidi ya vijiji 10 vya mkoa wa Iringa vitanufaika na miradi hiyo ya maji ambayo inagharimu zaidi ya milioni 600.

Maji ni eneo mojawapo la kipaumbele la kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano unaoratibiwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Maeneo mengine.

ya vipaumbele yaliyoainishwa katika mpango ni pamoja na: miundombinu ya usafiri, nishati; kilimo; viwanda; maendeleo ya rasilimali watu; na huduma za jamii.
Mhandisi wa maji wa Manispaa ya Iringa, Taphali Ngwada (Kulia) akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa hiyo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Wataalam hao waliongozwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Watatu Kulia mwenye koti jeusi) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla, Prof. Longinus Rutasitara (Wapili Kulia).
Viongozi wa msafara wa wataalam wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Kushoto) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla, Prof. Longinus Rutasitara (Kulia) wakitaka ufafanuzi juu ya maendeleo ya mradi.
Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William (Kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa hiyo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William (aliyenyanyua mkono) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya tanki la kuhifadhia maji kwa ajili ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ya Iringa.
Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto wa Uwanja wa Ndege wa Iringa (Nduli) ambao ni wanufaika wa mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ya Iringa , Bw. Ranier Nyimbo (Mwenye Fulana nyeusi) akitoa maelekezo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwenye uwanja huo.
Baadhi ya wanavijiji wa Nduli na Kigonzile kutoka manispaa ya Iringa wakichota maji katika bomba pekee linalopatikana katika mpaka wa vijiji hivyo. Adha hii itaisha mwezi Juni mwaka huu mara baada ya kukamilika kwa mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ikiwemo wanavijiji hawa.
Mhandisi wa maji wa Manispaa ya Iringa, Taphali Ngwada (Watatu Kulia) akiwaonesha wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango moja ya mabomba yatakayotumika kusambaza maji. PICHA NA SAIDI A. MKABAKULI

MWIGULU ALIVYOZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA CCM KALENGA

 Abdul Adam, Mtoto wa Spika wa Bunge wa zamani Chifu Adamu Sapi Mkwawa, akimpongeza mgombea wa CCM katika Uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Godfrey Mgimwa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 Wananchi wakinyoosha mikono kuunga mkono kuwa mgombea wa CCM anafaa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba akionyesha makada wa CCM,  Alphonce John (kushoto) na Musa Tesha, walionusurika kuuawa na watu wanaodaiwa kutumwa na Chadema kwa mmoja kumwagiwa tindikali na mwingine kutobolewa jicho kwenye kampeni zinazohusu udiwani na Ubunge, katika maeneo ya Igunga na Kahama, alipokuwa akieleza fuji za Chadema, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
  Alfonce aliyetobolewa jicho Kahama akizungumza jukwaani.
  Mwigulu akihutubia, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 Mwigulu (4th) na mgombea wakitroti na Green Guard, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.
 Katibu wa CCM, wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu, alionyesha mbao zenye misumari inayodaiwa kutegwa njiani na Chadema, kwa nia ya kudhuru msafara wa mgombea wa CCM ktk jimbo la Kalenga.
 Katibu wa CCM  mkoa wa Iringa, akishauriana jambo na Mwenyekiti wake Joyce Msavatavangu
 Mjumbe Kamati Kuu ya CCM, Pindi Chana,  akitema cheche jukwaani, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.

Godfrey Mgimwa-Mgombea wa CCM uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa.
Imetayarishwa na theNkoromo Blog