Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akizungumza katika kikao na wataalamu watakaofanya uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
Mthamini wa ardhi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Chiku Mkina (aliyevaa miwani) na wataalaamu wengine wakisikiliza kwa makini mada katika kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina M Lutambi akichangia mada katika kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
Mkurugenzi wa kampuni ya Dighy Welly Dkt Jan Perold akiwasilisha mada katika kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
Mwakilishi wa Serikali katika zoezi la Uthamini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Linus Kinyondo akizungumza na wataalamu wa mkoa wa Singida katika kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
Mhandisi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Simwela Nuru Martin akifuatilia kwa makini kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
…………………….
Wananchi Mkoani Singida wameondolewa wasiwasi kuhusu fidia ya mali au ardhi yao ambayo itapitiwa na mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga kwakuwa hawatapunjwa bali itazingatia vigezo vya kimataifa na kitaifa.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo amesema hayo mapema leo wakati wa kikao na wataalamu wanaofanya uthamini wa mali na ardhi ambayo itapitiwa na mradi huo.
Tarimo amesema wananchi na taasisi zote wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kutaja gharama kulingana na thamani halisi ya mali zao na sio kuongeza gharama za juu kwakuwa vigezo vya kitaifa na kimataifa vitazingatiwa.
“wananchi wengine wasio waaminifu wananweza wakataja pesa kubwa au hata kuvamia maeneo ambayo siyo yao ilimradi wapate tu pesa, nawasihi wasifanye hivyo kwakua watakuwa wanakwamisha mradi huu muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu na majirani zetu Uganda”, amesema na kuongeza kuwa
“ Tunampongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John P Magufuli kwa kuhakikisha nchi yetu inapata mradi huu, tutoe ushirikiano wa kutosha ili mradi ufanikiwe kw kiwango kikubwa hasa kwa maeneo yote utakapopita kwa Mkoa wa Singida”, amesisitiza.
Tarimo ameongeza kuwa serikali ya Mkoa, wilaya, taasisi na wananchi wote wa Singida wamekuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano kwa miradi yote ya kitaifana kimataifa na hivyo basi wataalamu wanaofanya uthamini na wale watakaokuja kujenga wasiwe na wasiwasi wowote.
Ameongeza kuwa wananchina taasisi ziko tayari kunufaika na mradi huo kupita Mkoani Singida kwa kupata ajira za muda mfupi na mrefu, kufanya biashara pamoja na kutoa huduma mbalimbali.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina M Lutambi amewataka wataalmau hao kushirikiana na wataalamau wa ngazi zote kuanzia mkoa hadi vijiji ili zoezi la uthamini liende vizuri.
Dkt Lutambi amesema lengo la uthamini ni kuhakikisha wananchi hawapati madhara makubwa kutokana na kupita kwa mradi huo katika maeneo hayo pamoja na kuhakikisha sheria, miongozo na taratibu zote zinafuatwa.
Ameongeza kuwa wataalamu wanapaswa kuwa wazi kwa kushirikisha taasisi na mashirika ambayo kwa namna moja au nyingine yataguswa na mradi huo pamoja na kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa wote wanaohusika.
Wakichangia mada katika kikao hicho wataalamu kutoka Mkoa wa Singida wamesema uthamini uangalie athari zote ambazo zinaweza kutokea kutokana na mradi huo mfano athari ya kisaikolojia ya usumbufu wa kumhamisha mtu kutoka katika makazi yake pamoja na thari za maeneo kama vyanzo vya maji ambapo bomba litapita.