Wednesday, February 28, 2018

WATAALAM WA AFYA MOJA KUANDAA MPANGO MKAKATI WA ULINZI NA USALAMA WA VIMELEA HATARISHI

Wataalam wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameanza kuandaa Mpango Mkakati wa ulinzi na usalama wa  vimelea hatarishi utakaosaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo hatarishi kutoweza kueeneza  magonjwa  kwa binadamu.

Mpango huo utatoa mwongozo wa namna sekta za Afya nchini ambazo ni sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira kushirikiana katika kuvichukua  vimelea kwa wanyama, binadamu na mimea  au  wakati wa kuvisafirisha na  kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.

Akiongea wakati wa Mkutano wa wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, leo tarehe 28 Februari,2018 mjini Morogoro, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu  alibainisha kuwa serikali imedhamiria kuijenga jamii yenye Afya bora kwa kuikinga na majanga yatokanayo na magonjwa ya mlipuko  hivyo imeamua kuandaa mpango huo ili kuboresha uratibu.  

Naye mratibu wa Mkutano huo anayeshughulikia masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya Afya, Jacob Lusekelo, alibainisha mpango huo ambao utatoa mwongozo wa sekta za Afya kushirikiana utasaidia kupunguza maabukizi ya vimelea hivyo kwa wanyama na binadamu.

Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughui za Afya moja nchini, ikiwemo wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, ambao unawajumuisha wataalamu wa kutoka katika sekta zote za afya katika masuala ya maabara.

Afya Moja ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na  mazingira katika kujiandaa , kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja  kwa kushirikiana na Shirika la Maabra  SANDIA na DTRA  wameandaa mkutano wataalam hao.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu akieleza  jambo wakati  wa Mkutano wa wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.
 Mtaalamu Masuala ya Mpango Mkakati  wa Maabara  kutoka Shirika la Maabara –SANDIA, Laura Jones, akifafanua umuhimu wa Mpango huo wakati  wa Mkutano wa wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini, uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.
 Baadhi ya Wataalamu wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini,  wakijadiliana namna ya kuandaa  Mpango Mkakati wa ulinzi  na usalama wa  vimelea hatarishi,  leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.
 Wataalamu wa Afya moja wanaounda  Mtandao wa Huduma za Maabara nchini  wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya   mkutano wa kuandaa  Mpango Mkakati wa ulinzi na usalama wa  vimelea hatarishi,  leo tarehe 28 Februari, 2018 mjini Morogoro.

VIONGOZI MTWARA FUATILIENI WATU WANAOTAKA KUHARIBU MASOKO YA KOROSHO-MAJALIWA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Mary Majaliwa (kulia) wakimsikiliza Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, Abdulrahman Sinani, wakati alipotembelea kiwanda hicho, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Gasper Byakanwa, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na mkewe Mary Majaliwa (katikati) wakiangalia mashine ya kubangulia korosho katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Abdulrahman Sinani, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mbanguaji korosho Zuhura Abdallah, katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, katikati ni Mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Gasper, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa mashine ya kuchambua korosho na Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Abdulrahman Sinani  katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mary, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akioneshwa mashine ya kukaushia korosho na Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Abdulrahman Sinani  katika Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mary, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia ubora wa korosho, iliyo teyari kuliwa, wakati alipotembelea Kiwanda cha Korosho cha Tandahimba Cashew, kilichopo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mary, Februari 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa mkoa wa Mtwara kupambana na makundi ya watu yanayotaka kuharibu masoko ya korosho.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa mnunuzi aliyekataa kununua korosho kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha ubora wa korosho alichokikuta ghalani.Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Februari 28, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba.

“Tandahimba korosho zote ni daraja la kwanza sasa korosho chafu zinatoka wapi? Kuna kundi linataka kuharibu soko lazima tupambane nalo.”Waziri Mkuu ameongeza kuwa “lazima mshirikiane kuwabaini walioleta korosho chafu Tandahimba na wakipatikana wachukuliwe hatua kali za kisheria.”

Amesema haiwezekani mnunuzi amenunua korosho daraja la kwanza alafu anakuja anakuta korosho nyingine tena chafu, lazima waliozibadilisha wasakwe. Awali, Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kubangua korosho cha Amama Farms, ambapo ametoa wito kwa walionunua viwanda vya korosho wafunge mashine mpya na kuanza uzalishaji.

Hata hivyo amewataka wamiliki wa viwanda vyote vya kubangulia korosho washirikiane na Serikali katika kufuata utaratibu wa kununua korosho.Pia Waziri Mkuu amezindua barabara yenye urefu kilomita tatu iliyojengwa kwa kiwango cha lami ambayo imegharimu sh. bilioni 1.38 zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba.

Kwa upande wake Meneja wa Kiwanda hicho Kwa Mahmoud Sinani alisema korosho zinazobanguliwa kiwandani hapo zinauzwa ndani na nje ya nchi.Amesema katika awamu ya kwanza ya uwekezaji huo umegharimu sh. bilioni 12 na wanatarajia kuendelea na awamu ya pili ambapo watawekeza dola milioni 20.

Amesema kwa sasa kiwanda hicho kimeajiri watumishi 250 na wanatarajia kuajiri watumishi 1,500 mara baada ya kumaliza awamu ya pili ya upanuzi wa kiwanda.Pia Waziri Mkuu amewapongeza watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba kwa kuweka kipaumbele katika ujenzi wa miundombini ya barabara kwa kiwango cha lami.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 28, 2018.

NEWS ALERT: TAARIFA KUTOKA NEC KUHUSU SHUTUMA ZA MBOWE

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
nembo%20ya%20NEC

                     Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesikia malalamiko yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambayo aliyawasilisha jana kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Malalamiko yaliyotolewa na Mhe. Mbowe yametusikitisha kwa sababu mbali na kumjibu kwa barua, Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani aliongea na Mhe. Mbowe kwa njia ya simu. Madai kwamba tume haikuwajibu malalamiko yao sio kweli. Ni upotoshaji wa hali ya juu ambao haupaswi kufanywa na kiongozi kama yeye.
Tume ya taifa ya uchaguzi haijibu malalamiko kwa matakwa ya mtu anavyotaka kujibiwa, bali inajibu hoja kwa mujibu matakwa ya katiba, sheria, kanuni na maadili ya uchaguzi na maelekezo yote ambayo yapo kwa mujibu wa sheria. Kama majibu ya tume hayakuwafurahisha CHADEMA, tume inasisitiza kuwa walijibiwa  kwa matakwa ya sheria na katiba na sio matakwa ya mkurugenzi wa uchaguzi, Tume, Chadema au chama chochote cha siasa.
Kanuni, sheria, maelekezo na maadili ya uchaguzi yameweka utararatibu wa kushughulikia malalamiko na changamoto zinazojitokeza wakati wa uchaguzi.  Utaratibu uko wazi kwa changamoto zinazotokea wakati wa uteuzi, wakati wa kampeni ambako kuna kamati za maadili na jinsi ya kukata rufaa.
Kwa masikitiko CHADEMA walitekeleza hatua moja tu katika vipengele hivyo wakati wa uchaguzi, kipengele walichotekeleza ni pale baadhi ya wagombea wao walipoenguliwa kugombea, walifuata utaratibu kwa kuwasilisha rufaa tume ya uchaguzi na Tume ilipitia na ikawarudisha wagombea wao kwenda kugombea.
CHADEMA walitaka wakati wa kampeni, Tume ifanye maamuzi kinyume cha maadili waliyoyasaini. Wakati wa kampeni kuna kamati za maadili ngazi ya jimbo ambayo mwenyekiti ni msimamizi wa uchaguzi na wajumbe ni kutoka vyama vyote vilivyosimamaisha wagombea na ndio wanaofanya uamuzi. Chadema waliwasilisha malalamiko kwa Tume badala ya kuwasilsiha malalamiko kwenye kamati hizo za maadili zinazosimamia malalamiko yote.
Sio sahihi kusema Tume hatukujibu malalamiko yao. Mfano tarehe 15 Chadema waliwasilsiha barua mbili Tume ya Uchaguzi, waliwasilisha barua moja asubuhi na saa 1.30 jioni waliwasilisha barua nyingine, jumla barua hizo zikiwa na hoja tano na Tume ikawaandikia barua zenye ufafanuzi wa hoja hizo.
Hoja ya kwanza, CHADEMA walitaka kuapishwa mawakala wao mbadala asilimia 15. Tuliwajibu kwamba hakuna kifungu cha sheria kinachokipa fursa chama chochote cha siasa kuapishiwa mawakala mbadala asilimia 15. Kifungu 57 (3) kinafafanua vizuri namna ya mawakala wanavyotakiwa kuwepo na kuapishwa
Lakini pia hata kama kifungu hicho kingekuwa kinatoa fursa hiyo, Chadema walileta malalamiko yao  tarehe 15 Februari 2018 wakati uteuzi wa mawakala ulikuwa tarehe 10 Februari 2018, hivyo hakukuwa na muda wa kuwaapisha mawakala wengine kwa mujibu wa sheria kwa kuwa hawakuwemo kwenye orodha.

Hoja nyingine ya CHADEMA ni msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni alikataa kuwapa mawakala barua na fomu za viapo. Tulifanya hesabu tukaona kwamba msimamizi alitakiwa kusaini barua 22,000 na fomu za viapo 14,000. Tukasema kwamba kutakuwa na utaratibu wa mawakala kupewa fomu na viapo vyao kupitia kwa wawakilishi wao na walipewa kwa njia hiyo. Hili tuliwajibu hivyo katika barua yetu.
Hoja nyingine mawakala wa CHADEMA waliambiwa kwenda na vitambulisho kwenye vituo vya kupigia kura. Katika hoja hii tuliwajibu kwamba wakala chama cha siasa ni mpiga kura kama walivyo wapiga kura wengine. Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia sheria ya uchaguzi kifungu namba 61 na namba  62 cha sheria za Serikali za mitaa, Tume ilitoa ridhaa kwa wapiga kura kutumia vitambulisho mbadala ili nao waweze kupiga kura ndio maana wakaelekezwa kwenda navyo.

Hoja nyingine ni kwamba msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni, hajatoa maelekzo ni wapi pa kuhesabia kura. Tukawajibu kwamba Tume ina barua kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi akiwajulisha vyama vya siasa kwamba sehemu ya kujumlishia kura itakuwa ni sehemu ya Biafra. Kanuni inasema wangejulishwa eneo hilo la kujumlishia baada ya kura kupokelewa, lakini msimamizi wa uchaguzi alijiongeza akawajulisha mapema eneo la kujumlishia kura.
Hoja nyingine ni wasimamizi wa vituo hawakuteuliwa kwa utaratibu. Majibu ya hoja hii ni kwamba sheria ya uchaguzi imeweka utaratiibu wa namna wasimamizi hao wanavyopatikana. Lakini kanuni za uchaguzi wa Rais namba 15 na kanuni 11 za Serikali za Mitaa zinaeleza namna msimamizi wa kituo anavyopatikana.

Kanuni hiyo inasisitiza kuwa msimamizi wa uchaguzi atatoa tangazo, Kwa jimbo la Kinondoni msimizi alitoa tangazo, watu waliomba, walifanya usahili na kabla ya uteuzi mkurugenzi wa uchaguzi alitoa matangazo ya majina katika mbao zote za kata 10 za jimbo la Kinondoni.
Msimamizi wa uchaguzi aliwaandikia barua vyama vyote kama vina pingamizi vijitokeze. Kama kulikuwa na tatizo vyama vilikuwa na fursa ya kuweka pingamizi, lakini hawakufanya hivyo na Tume tuliwajibu hivyo. Unaposema tume haikuwajibu sio kweli, labda CHADEMA waseme tuliwajibu nje ya matakwa yao waliyotaka na sio kwa mujibu wa sheria.

Hoja nyingine ni kwamba kuna wizi wa kura. Katika kituo cha kupigia kura kuna msimamizi wa kituo, msimamizi msaidizi na wakala wa chama cha siasa na kuna waandishi wa habari. Utaratibu ulikuwa wazi. Pia kuna utaratibu wa kisheria wa kuwasilisha malalamiko kama mtu haridhiki kabla wakati na baada ya kupiga kura, wakati wa kuhesabu na baada ya kuhesabu kura.
Mtu au chama kisipofuata uratibu huo, lazima utalalamika tu na utaona tume ni korofi. Hii ni kwa sababu mtu akija Tume kulalamika, ataelekezwa kufuata utaratibu huo. Mgombea akikataa kufuata utaratibu huo hata akija Tume kulalamika,ataelekezwa na Tume atumie wakala wake kujaza fomu zote namba 14 na 16 zinazohusika kisheria kuwasilisha malalamiko.

Tunamsihi Mbowe na chama chake, wasome sheria za uchaguzi na kuzielewa. Tume iko tayari kumpa elimu ya mpiga kura kuzifahamu sheria hizi kwa mapana yake.
Pia tunamwomba Mhe. Mbowe kama hakuridhika na taratibu za uchaguzi, ana fursa ndani ya siku 30 za kuwasilisha malalamiko yake mahakamani ndicho chombo pekee cha kutoa haki. Aende mahakamani kwa kutumia ushahidi ambao mawakala wake walijaza kwenye fomu namba 14 na 16 kwa sababu Tume ya Uchaguzi haina tena fursa ya kupokea malalamiko kisheria baada ya uchaguzi kupita.
Kailima, R.K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI

BALOZI SEIF AHAIRISHA MKUTANO WA TISA WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar katika Majengo ya Baraza hilo yaliopo Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi ya Mawaziri wa SMZ na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotuba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipotoa Hoja ya Kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar .
Baadhi ya Manaibu Mawaziri wa SMZ na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakimsikiliza Balozi Seif alipokuwa akisoma Hotuba ya Kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar M,h. Zubeir Ali Maulid akiongozwa na Askari wa Baraza hilo wakitoa nje ya Ukumbi baada kufungwa kwa Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi huko Chukwani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Jimbo la Dimani Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini baada ya kufungwa kwa Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi.

Picha na – OMPR – ZNZ.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mapambano yake dhidi ya vitendo vya udhalilishaji wa Kijinsia vilivyokithiri katika maeneo mbali mbali Nchini, kamwe haitamvumilia, kumuonea aibu, wala muhali Mtu yeyote wa cheo chochote na ngazi yeyote pindi atakapobainika kuhusika na vitendo hivyo.

Akitoa Hoja ya kuahirisha Mkutano wa Tisa wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar uliokuwa ukifanyika katika Majengo ya Baraza hilo Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alionya na kutahadharisha wazi kwamba Viongozi na Wananchi wanapaswa kutambua kuwa Sheria ni Msumeno.

Balozi Seif alisema Serikali itaendelea kuchukuwa hatua kali za kisheria dhidi ya wote watakaobainika kushiriki katika kadhia hiyo ikiwemo wafanyaji na wale wote wanaoshiriki katika kuwalinda na kuwakingia kifua wahalifu wote wa masuala ya udhalilishaji wa kijinsia.

Alivinasihi vyombo vya ulinzi na usalama kupambana zaidi dhidi ya vitendo hivyo vinavyolitia aibu Taifa sambamba na kuharibu maisha ya Wananchi, huku Jamii ikipaswa kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo hivyo katika Mkakati wa kukabiliana na tatizo hilo baya Kijamii na hata Kidini.

Balozi Seif alisema tabia ya baadhi ya Watu hasa Familia kuzimaliza kesi za Udhalilishaji Majumbani itakupunguza kasi ya Serikali kuwashughulikia wahalifu hao na kuwanasihi Wananchi wahusika kufika Mahakamani kwa kutoa ushahidi utakaotoa nguvu ya sheria kuchukuwa mkondo wake na haki kupatikana ili hatimae kuvimaliza vitendo hivyo katika Taifa hili.

Alieleza kwamba Baraza la Wawakilishi tayari limeshapitisha Sheria ya adhabu kwa wahusika wa vitendo vya udhalilishaji, ambapo imeweka bayana kuwa Mtuhumiwa ye yote wa kosa la udhalilishaji hatopaswa kupewa dhamana.

Balozi Seif alifahamisha kwamba Sheria hiyo sasa inangojea kuwekwa saini na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ili iwe Sheria ambapo Mheshimiwa Rais anatarajiwa kuifanya kazi hiyo muda sio mrefu kuanzia hivi sasa.

Akizungumzia suala la ulipaji umeme kwa Deni ya Shirika la Umeme Tanzania {TANESCO} kwa upande wa Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali ililiamuru Shirika la Umeme Zanzibar {ZECO}kulilipa deni hilo kwa Tanesco kwa kiwango cha Shilingi Bilioni Mbili kwa Mwezi.

Alisema malipo hayo yamepangwa kwenda sambamba na Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar pia kuagizwa kupunguza Deni hilo kwa kiwango cha Shilingi Bilioni Moja kwa Mwezi malipo ambayo yalianza utekelezaji wake.

Hata hivyo Balozi Seif alieleza kwamba utekelezaji huo ulikumbwa na changamoto zilizojitokeza kwa upande wa Shirika la Umeme Zanzibar {ZECO} kwa kutoendelea kulipa kwa ukamilifu kiwango kilichowekwa na Serikali na badala yake Shirika lililipa kwa Miezi Minne tu kuanzia Mwezi Juni, 2017 hadi Oktoba, 2017.

Alisema Miezi iliyofuata ZECO ililipa Deni hilo chini ya kiwango kilichoagizwa kutokana na ukusanyaji mdogo wa mapato yanayotokana na ankara za matumizi ya umeme kutoka kwa baadhi ya Taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na zile za Muungano wa Tanzania zilizopo Zanzibar.

Balozi Seif alisema hali hiyo imepelekea Shirika la Umeme Zanzibar kutokuwa na mapato ya kutosha kulipa deni hilo kila Mwezi badala ya kukidhi mahitaji mengine ya msingi na ya lazima ya kuliendesha Shirika hilo.

Kuhusu suala la upatikanaji wa huduma za Maji safi ya salama Mjini na Vijijini, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Serikali Kuu kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo imejipanga kutekeleza miradi Minne mikubwa ya huduma hiyo Nchini.

Aliutaja ule Mradi wa Uimarishaji wa Miundombinu katika kubadilisha Mabomba yaliyochakaa wenye urefu wa Kilomita 68 katika Maeneo ya Bumbwisudi, Kinumoshi, Kianga, Welezo, Muembe Mchomeke, Amani pamoja na Kiponda Mji Mkongwe.

Alisema utekelezaji wa Mradi huu unaofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Afrika wa Awamu ya 12 {ADF 12} unatarajiwa kugharimu jumla ya shilingi za Kitanzania Bilioni 48 hadi kukamilika kwake.

Balozi Seif aliutaja mradi mwengine wa Uimarishaji wa miundombinu ya Maji Mjini unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) kwa gharama ya Shilingi Bilioni 225 za Kitanzania utahusisha ujenzi wa Matangi ya kuhifadhia Maji katika maeneo ya Welezo juu pamoja na Welezo Magharibi.

Alieleza Mradi huo utakwenda sambamba na ulazaji wa Mabomba yenye urefu wa Kilomita 120 katika Zoni ya Migombani pamoja na uwekaji wa huduma za Umeme katika maeneo husika.

Balozi Seif alisema upo mradi mpya wa uimarishaji miundombinu ya Maji Mjini utakaofadhiliwa na Serikali ya India kwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni Mia 207 utakaohusisha ulazaji wa Mabomba katika maeneo ya Zoni ya Mfenesini, Kizimbani, Tunguu na Fumba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China imekubali kufadhili mradi wa uchimbaji Visima 11 pamoja na ulazaji wa Mabomba ndani ya Mkoa Kaskazini Unguja na baadhi ya Wilaya ya Kati na Magharibi “A” unaotarajiwa kugharimu shilingi Bilioni 12 za Kitanzania.

Alisema ili miradi yote iendelee kudumu kwa kipindi kirefu katika utoaji wa huduma zake Wananchi watawajibika kuchangia gharama za uendeshaji wa huduma hiyo kwa wale watakaopata badala ya kubakia na dhana ya uchangiaji wa huduma ya Maji safi ni jukumu la Serikali pekee.

Mkutano wa Baraza la Wawakilishi ulipokea na kujadili Ripoti za Kamati za kudumu Saba za Baraza hilo ambapo pia Wajumbe wa Baraza hilo walijadili na kuipitisha Miswada Mitatu ya Sheria.

Miswada hiyo ni ule wa kufuta Sheria ya kusimamia mwenendo wa Biashara na kumlinda mtumiaji ya Zanzibar Nambari 2 ya Mwaka 1995 na kutunga Sheria Mpya ya Ushindani Halali wa Biashara na Kumlinda Mtumiaji, Kuweka Masharti Bora zaidi pamoja na Mambo Mengine yanayohusiana na hayo.

Mwengine ni Mswada wa Sheria ya kufuta Sheria ya Adhabu na kutunga Sheria Mpya ya Adhabu, Kuweka Masharti Bora zaidi pamoja na Mambo Mengine yanayohusiana na hayo.

Mswada wa Tatu ni ule wa Sheria ya kufuta Sgeria ya Mwenendo wa Jinai Nambari 7 ya Mwaka 2004 na kutunga Sheria Mpya ya Mwenendo wa Jinai na kujweka utaratibu Bora wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai na Usikilizaji wa Kesi za Jinai na Mambo Mengione yanayohusiana na hayo.

Baraza la Wawakilishi Zanzibar limeahirishwa hadi Jumatano ya Tarehe 9 Mwezi Mei Mwaka 2018.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

27/2/2018.

CCM IRINGA MJINI YATEKELEZA AHADI ILIYOMSHINDA MBUNGE MSIGWA KWA MIAKA 10

Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya kushoto akiwakabidhi wafanyabiashara soko kuu TV na king'amuzi ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyomshinda mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (chadema) miaka 10 toka ahahidi 
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati ,katibu wa CCM Iringa mjini Marko Mbanga na mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Said Rubeya wakiwa na wafanyabiashara baada ya kutekeleza ahadi iliyomshinda mbunge Msigwa 

Na MatukiodaimaBlog 

CHAMA cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa mjini kimetekeleza ahadi ya TV iliyoahidiwa wakati wa kampeni za ubunge mwaka 2015 na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) katika soko kuu la Manispaa ya Iringa .

Akizungumza leo mara baada ya kukabidhi TV hiyo na king'amuzi chake kwa uongozi wa soko kuu mjini Iringa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Said Rubeya alisema kuwa CCM imelazimika kutekeleza ahadi hiyo ya TV nchi 58 baada ya wafanyabiashara wa soko hilo kuomba kusaidiwa TV hiyo kwa ajili ya kufuatilia habari mbali mbali zinazojiri nchini wakiwa katika sokoni hapo .

Alisema pamoja na kuwanunulia TV hiyo aina ya Sumsung wamepata kuwanunulia king'amuzi pamoja na kuwalipia malipo ya mwezi mmoja kuwa lengo la CCM kufanya hivyo ni kuendelea kuwahudumia wananchi na kutatua kero mbali mbali za wananchi bila kujali itikadi za vyama vyao .

" CCM tumeendelea kutekeleza ahadi mbali mbali ila kama mtakumbuka kata ya Kihesa kulikuwa na jengo ambalo lilikwama kwa zaidi ya miaka 10 ila baada ya CCM kushinda katika uchaguzi mdogo wa kata ya Kihesa mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Salim Abri aliahidi na tayari ametekeleza hivyo CCM tukiahidi tunatekeleza wenzetu wakiahidi wanatelekeza ahadi zao "

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) alisema kuwa mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt John Magufuli aliwaagiza viongozi wa CCM kwenda kutatua kero za wananchi na ndivyo ambavyo CCM Iringa mjini imekuwa ikifanya hasa ukizingatia kuwa chama kinachotawala ni CCM hivyo lazima CCM kutatua kero za wananchi bila kujali zilitolewa na upinzani ama CCM .

" Hatupendi kuona wananchi wanasikitika ama wanapoteza haki zao hivyo tutawasikiliza na kutatua kero zao wenzetu wanaahidi bila kutekeleza ila sisi kama CCM tutahakikisha ilani yetu inatekelezwa kwa nguvu zote na tutakwenda tena kuwasikiliza wanahitaji nini "

Katibu wa CCM Iringa mjini Marko Mbanga alisema kuwa kuwa pamoja na CCM kutekeleza ahadi ya mbunge Msigwa wa Chadema ila imeendelea kusaidia jamii katika shughuli za maendeleo kama kutoa bati 300 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa na kutoa elimu kwa wanawake juu ya ujasiliamali .

Alisema kuwa kutoka na wapinzani kufanya kazi ya kwenye mitandao ya kutukana na kubeza CCM ila wao CCM kazi yao ni kuwakomboa wananchi na kuona wanatatuliwa kero walizo nazo na kudai kuwa kwa kazi zinazofanywa na CCM Iringa mjini ndizo zinapelekea madiwani zaidi ya Chadema kujiuzulu na kujiunga na CCM .

" Hadi hivi sasa CCM toka madiwani wa kata watatu sasa ina madiwani 9 waliohamia CCM hivyo ndio maana tunasema madiwani waliobaki nje ya CCM wajiunge na CCM timu ya maendeleo maana shabaha kubwa ni kuwatumikia wananchi "

Katibu huyo wa CCM Iringa mjini alisema kumekuwepo na maneno mengi yasiyo ya kweli juu ya CCM kununua madiwani wa Chadema na kuwa suala hilo halipo kwani CCM haina pesa za kununua diwani ina pesa za kuwaletea wananchi maendeleo .

Mwenyekiti wa soko kuu la Iringa Sturmi Fussy akishukuru kwa msaada huo alisema kuwa TV hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wafanyabiashara sokoni hapo kwani itawapunguzia muda wa kutoka katika eneo lao la kazi kwenda kutazama TV nje ya soko hilo hata hivyo aliomba CCM kusaidia daladala kufika eneo hilo la soko ili kuongeza wateja zaidi katika soko hilo 

TADB, NDC SIGN MoU FOR AGRI-INDUSTRIAL RESOURCE MOBILIZATION

Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) and National Development Corporation (NDC) signed a Memorandum of Understanding of cooperation in resource mobilization, lending, distribution, and servicing of tractors and farm implements to farmers in Tanzania.

Speaking on the objective of cooperation, the acting managing director of TADB, Mr. Augustino Matutu Chacha said that the signed MOU will facilitate establishment of country-wide demand for tractors and farm implements as well as to facilitate mobilization of sustainable financial resources for provision of loans, procurement, distribution and servicing of tractors and farm implements to farmers in Tanzania and to facilitate the application of sound lending principles in the provision of loans for purchase of tractors and farm implements, including loan monitoring and evaluation.

Other benefits will include facilitating establishment of more efficient means of procurement, distribution, and delivery of tractors and farm implements; and providing a framework for establishing effective and continuing collaboration between the Bank and the Corporation.

“This MoU between the Bank and the Corporation will draw mutual benefits from cooperation between the two organizations in resource mobilization, lending, distribution and servicing of tractors and farm implements to farmers in Tanzania,” he said.

Mr. Chacha added that the Bank and the Corporation are desirous to establish cooperation in resource mobilization, lending, distribution and servicing of tractors and farm implements to farmers.

Adding that based on the mandate of the Bank, TADB is ready to facilitate increased access to finance through provision of short, medium and long-term credit facilities at affordable rates and terms across agricultural value chains of focus, including provision of loans for purchase of tractors and farm implements.

According to the signed document TADB will be mandated among others to manage financial resources for financing procurement of tractors and implements through extension of loans to farmers in Tanzania and design innovative financing products and services with favorable conditions for financing agricultural mechanization by farmers in Tanzania.

Other activities include conduct credit appraisal of identified agricultural projects earmarked for tractor and farm implement loans as well as managing the overall lending activities related to financing purchase of tractors and farm implements by farmers including loan monitoring and evaluation; and provide trade finance services to the Corporation as it relates to procurement of tractors and farm implements from source manufacturers.

On his part, NDC’s Boss, Eng. Ramson Mwilangali said one of the major focuses of the Corporation includes promotion of agricultural mechanization in Tanzania; hence the signed cooperation will assist in improving agriculture production for both domestic consumption in Tanzania.

He added that through the proposed cooperation NDC and TADB will facilitate the industrial feedstock through establishment of Tractor Assembly Plant at Kibaha for assembling semi knocked down (SKD) and completely knocked down (CKD) tractors along with farm implements for selling to individuals/groups of farmers.

“This collaboration between the Bank and the Corporation among others may entail any of the subject matters covered by their mandates,” he said.

He mentioned specific areas of collaboration that will include, but will not be limited to establishing country-wide demand for tractors and farm implements and costs thereof, formulating resources mobilization strategies for financing procurement Semi Knocked Down (SKD) and Completely Knocked Down (CKD) tractors for assembly alongside associated implements, provision of loans, distribution and servicing of agricultural inputs to farmers for the second phase II of the NDC Tractor Assembly Project as well as designing innovative financing products and services for loan financing and adoption of appropriate technologies by farmers in the country.

Others according to Eng. Mwilangali will include identifying and appraising loan applications for tractors and farm implements by farmers; and conducting needs assessment, preparing and implementing capacity-building programs related to the application of modern technologies in agriculture in Tanzania.

In order to facilitate implementation of the signed MoU, NDC is required to ensure timely procurement of Semi Knocked Down (SKD) and Completely Knocked Down (CKD) tractors and farm implements from abroad for assembly in Tanzania, ensure availability of tractors ready for sale to farmers at Tractor Assembly Plant in Kibaha and other designated sales centres and ensure timely delivery of tractors to farmers for which the payment and release order have been received.

Other responsibilities include providing after sale technical service of tractors and farm implements lent to farmers at the designated service centers countrywide as well as ensure adequate stocks of tractor spares are available at the designated service centers at all times; and providing and manage two years warranty for the sold tractors.

TADB and NDC are public owned institutions that aim at facilitate development in the country where the former is mandated to promote and support transformation of agriculture from subsistence to commercial undertaking to effectively and sustainable contribute to economic growth and poverty reduction while the latter is bestowed with a broad mandate as a development and promotion institution to stimulate industrialization in partnership with private sector.
 Acting Managing Director of TADB, Mr. Augustino Matutu Chacha (left) speaks on the role of the Bank in implementing Government’s Industrialization Strategy during MoU signing in ceremony between TADB and NDC held at TADB’s Headquarter in Dar es Salaam. Centre is NDC’s Managing Director, Eng. Ramson Mwilangali who is flanked by NDC’s Director of Heavy Industry, Mr. Abdalllah Mandwanga.
 NDC’s Managing Director, Eng. Ramson Mwilangali (right) stresses on position of NDC in supporting Government’s Industrialization Strategy during MoU signing in ceremony between TADB and NDC held at TADB’s Headquarter in Dar es Salaam. Centre is TADB’s Acting Managing Director, Mr. Augustino Matutu Chacha and left is TADB’s Head of Legal Service, Ms. Neema Christina John.
 Acting Managing Director of TADB, Mr. Augustino Matutu Chacha (left) together with NDC’s Managing Director, Eng. Ramson Mwilangali (right) sign MoU that aims at Design resource mobilization strategies for procurement of tractors and farm implements and provision of loans to farmers in Tanzania. The signing in ceremony held at TADB’s Headquarter in Dar es Salaam.
 Acting Managing Director of TADB, Mr. Augustino Matutu Chacha (left) and his NDC’s counterpart, Eng. Ramson Mwilangali (right) display signed MoU that aims at Design resource mobilization strategies for procurement of tractors and farm implements and provision of loans to farmers in Tanzania.
TADB’s management together with NDC’s counterpart in the Memoir Group Photo after signing the MoU that aims at Design resource mobilization strategies for procurement of tractors and farm implements and provision of loans to farmers in Tanzania.

TAARIFA KUTOKA NEC KUHUSU SHUTUMA ZA MBOWE

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
nembo%20ya%20NEC

                           TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesikia malalamiko yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambayo aliyawasilisha jana kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Malalamiko yaliyotolewa na Mhe, Mbowe yametusikitisha kwa sababu mbali na kumjibu kwa barua, Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani aliongea na Mhe. Mbowe kwa njia ya simu. Madai kwamba tume haikuwaibu malalamiko yao sio kweli, ni upotoshaji wa hali ya juu ambao haupaswi kufanywa na kiongozi kama yeye.