Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom,Rene Meza |
· Wateja kupata taarifa kupitia SMS, Facebook na Twitter.
·Yatoa pongezi kwa vyombo vya habari na timu.
Mdhamini
Mkuu wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, kampuni ya mawasiliano ya
Vodacom Tanzania, imewekeza katika kuwawezesha mashabiki wa soka kupata
taarifa na matukio ya mechi zote za ligi hiyo kupitia njia ya simu za
kiganjani na intanet.
Kupitia
mifumo mbalimbali ya kiteknolojia wateja wa Vodacom wataweza kupata
matokeo ya mechi mbalimbali kupitia simu zao za kiganjani ukiwa na
ujumbe mfupi wa maneno na mitandao ya kijamii.
Akizungumzia hatua hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene
Meza, amesema, Mtandao wa Vodacom una miundombinu ya kutosha na
unaongoza katika masuala ya teknolojia.
Hivyo
itatumika katika kuwawezesha mashabiki wa soka walioko ndani na nje ya
nchi kujua matukio mbalimbali ya ligi kuu ya Vodacom.
“Licha ya ligi yetu kuonekana katika kituo cha Televisheni cha Super
Sport.
Tumejipanga
sasa kuhakikisha inakuwa katika mitandao mbalimbali muda wote kwa kila
mchezo na kila tukio katika soka, Mashabiki watapata taarifa za ligi
popote watakapokuwa,” alisema Meza na Kuongeza kuwa, “Kupitia intanet
matukio haya yatapatikana kupitia Facebook na Twitter na mitandao
mingine ya kijamii.”
“Ili
kupata matokeo na taarifa mbalimbali kupitia njia ya simu mteja wa
Vodacom atatakiwa kupiga *149*01# kisha atachagua VODACOM FLAVA na
akisha kujiunga na huduma hiyo itakayo muwezesha kupata taarifa na
matokeo ya mechi mbalimbali”
Aliongeza kuwa,
“
Kwa wateja wanaotumia facebook na twitter kwao ni rahisi zaidi kwani
huduma hizo zinatolewa bure na Vodacom, hivyo mashabiki wa soka
watatembelea Ukurasa wetu wa facebook na Twitter na kupata taarifa
mbalimbali kuhusu ligi na wengine kujishindia zawadi kwa kujibu maswali
mbalimbali zikiwemo tiketi za mechi za ligi,”
Aidha
Mkurugenzi huyo alitoa Pongezi kwa Vyombo vya habari kwa kazi kubwa
inayofanya katika kuwahabarisha watanzania kuhusu michezo mbalimbali
hususani ligi kuu ya Vodacom kupitia Televisheni, Radio, Magazeti na
Mitandao ya kijamii.
“Vyombo
vya habari ni wadau wakubwa na wanafanya kazi nzuri sana katika kutoa
taarifa hizi wanastahili pongezi, nasi tunaangalia namna ya kuwaunga
mkono kwa namna moja ama nyingine katika jitihada za kukuza soka la
Tanzania na tunaamini tutafika mbali.”
Mkurugenzi
huyo alihitimisha kwa kutoa pongezi kwa timu mbalimbali zinazoshiriki
katika ligi kwa kusema kuwa zimeonesha hamasa kubwa na kubainisha kuwa
ni ishara ya ukuaji wa soka katika soka la Tanzania ambalo ndio lengo
kuu la Vodacom.
“Ligi
sasa imekuwa na msisimko kila timu inajitahidi kushinda kila mechi,hadi
sasa timu zote zimeonesha kiwango kikubwa na soka la kuvutia
tunatarajia maendeleo haya yataleta tija hata kwa timu yetu ya Taifa
kufanya vizuri.
Vipaji
vingi vinaonekana na ajira kwa vijana imeongezeka kupitia michezo,”
alihitimisha Meza.
Kampuni ya Vodacom katika kuongeza msisimko kwa mashabiki wa ligi imetoa
ofa mbalimbali msimu huu kwa kuwawezesha wateja wake kupata SMS 50,
Muda wa maongezi wa dakika 30 na MB 50 kwa shilingi 400 Ili kuwasiliana
na ndugu jamaa na marafiki.
Pamoja
na mambo mengine kampuni hiyo inaangalia namna ya kutoa adha ya ukataji
tiketi kwa wateja wake kutumia huduma ya M - pesa kununua tiketi za
mechi mbalimbali.