Sunday, January 31, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

SIMU.TV:  Mgeni njoo mwenyeji apone, ziara ya waziri mkuu Mh.Majaliwa Kilimanjaro yaleta matumaini makubwa kwa wananchi mkoani humo;https://youtu.be/_0bjAYbNvyE   
 SIMU.TV:  Wazazi wamtelekeza mtoto wao baada ya kuzaliwa bila mikono, mwalimu wa shule pamoja na madiwani walazimika kumtunza mtoto huyo;https://youtu.be/eeHEXqmRlV8  
 SIMU.TV:  Serikali imetakiwa kuwashirikisha watu wa ngazi ya chini ili kuepuka migogoro inayojitokeza mara kwa mara hasa migogoro ya ardhi;https://youtu.be/HKZGztDDU0M
 SIMU.TV:  Serikali ya mapinduzi Zanzibar imeombwa kuwachukulia hata baadhi ya watendaji wa serikali wanaonyanyasa wananchi hasa katika kujenga katika maeneo ya wazi; https://youtu.be/gUowBoSqwCo
 SIMU.TV:  Shirika la viwango nchini TBS limewataka wazalishaji wa bidhaa nchini kutoa ushirikiano katika kampeni yake ya ondoa bidhaa hafifu katika masoko nchini;https://youtu.be/SH3irZuzyps
 SIMU.TV:  Meya wa Ilala aitaka manispaa hiyo kuongeza idadi ya mabwana afya katika machinjio ya Vingukuti ili kuongeza ufanisi wa ukaguzi wa nyama;https://youtu.be/qsX2qC9T_gA
 SIMU.TV:  Nguli wa mchezo wa tenisi Novak Djokovic aibuka mshindi wa michuano ya Australia Open baada ya kumburuza mpinzani wake Murray;https://youtu.be/NQDPUW5CnKg
 SIMU.TV:  Waziri Majaliwa, Lowasa washuhudia kusimikwa kwa askofu Dr. Fredrick Shoo. Askofu awasisitiza wabunge kuwa na nidhamu bungeni;https://youtu.be/k2zhEBY6GRg   
 SIMU.TV:  Warundi 28 washikiliwa na idara ya uhamiaji Geita kwa kuingia nchini bila kibali na Watanzania 2 kwa kuhifadhi wahamiaji haramu;https://youtu.be/OYuAX_glIe4  
 SIMU.TV:  Wakazi wa Dar es Salaam wamepongeza hatua ya Serikali kuchukulia hatua mzozo wa ufukwe wa Coco; https://youtu.be/p779vwtOxFQ
 SIMU.TV:  Wakandarasi katika miradi mbalimbali ya ujenzi nchini wameagizwa kutoa mikataba ya ajira wafanyakazi; https://youtu.be/r6JrLD88TB8  
 SIMU.TV:  Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda amewataka Watanzania kutumia fursa ya uhusiano uliopo kati ya China na Tanzania kujiletea maendeleo;https://youtu.be/8nanVBqRrQM
 SIMU.TV:  Ndanda FC yatoka sare ya kufungana bao la moja kwa moja na timu ya Mgambo JKT katika mechi iliyochezwa mkoani Tanga;  https://youtu.be/ffsLIm22DDs
 SIMU.TV:  Serikali yawatoa wasi wasi wananchi juu ya kuwepo kwa ugonjwa wa Zika nchini  ulioenea zaidi katika bara la Amerika la kusini; https://youtu.be/_LII-V824eI
 SIMU.TV:  Kanisa la KKKT launga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kupambana na watu wanaotumia mali za umma kujinufaisha wao; https://youtu.be/nlsvxWYcstk
 SIMU.TV:  Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini washauriwa kuwasimamia waandishi wa habari ili watoe habari zenye ubora;https://youtu.be/eG3WlZhnwQA
 SIMU.TV:  Wafanyakazi wa idara ya Mahakama nchini washauriwa kutenda haki kwa raia ili kuleta usawa kila mtu; https://youtu.be/t3eYaW4mCSw
 SIMU.TV:  Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda atangaza zoezi la upimaji afya bure kwa wakazi wa kinondoni kuwa ni zoezi endelevu;https://youtu.be/3M3KkBAr77M
 SIMU.TV:  Inaelezwa kuwa mkoa wa kagera uko mbioni kuunganishwa na gridi ya taifa ya umeme katika kuhakikisha umeme unakuwa wa uhakika mkoani humo;https://youtu.be/jSMBOWCmc_c
 SIMU.TV:  Kamati ya muda ya soka visiwani Zanzibar yamjia juu Rais wa TTF, Jamal Malinz kwa kusema haitambui kamati hiyo; https://youtu.be/n1gfYVterWM
 SIMU.TV:  : Kocha wa timu ya taifa ya Ivory Cost inayoshiriki michuano ya CHAN ajivunia kikosi chake kuwa kina vijana wenye vipaji vya hali ya juu;https://youtu.be/Ggi_kDTNn_U

MTAA WA GONGO LA MBOTO MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM WAENDELEA KUUNGA MKONO KAULI YA RAIS DK.MAGUFULI YA KUFANYA USAFI

 Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na kufanya usafi katika Mtaa wa Gongo la Mboto Manispaa ya Ilala,  Ali Mwinyimkuu (kulia), akishiriki kufanya usafi na wananchi Dar es Salaam jana, ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya usafi kila baada ya wiki mbili ili kuunga mkono kauli Rais Dk. John Magufuli ya kufanya usafi katika maeneo tunayoishi na kufanyia shughuli zetu nchini.
 Kazi ya usafi ikiendelea.
 Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na kufanya usafi katika Mtaa wa Gongo la Mboto Manispaa ya Ilala,  Ali Mwinyimkuu Omari akiwaongoza wenzake kufanya usafi.
 Hapa ni kazi tu tunaukataa uchafu.
 Wanawake wakishiriki kufanya usafi eneo la relini.
 Mwenyekiti wa Mtaa huo, Bakari Shingo (Aliyevaa kaputura), akishiriki kufanya usafi na wananchi wake Dar es Salaam jana, ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya usafi kila baada ya wiki mbili ili kuunga mkono kauli Rais Dk. John Magufuli ya kufanya usafi katika maeneo tunayoishi na kufanyia shughuli zetu nchini.
 Usafi ukiendelea.
Wasanii wa Kikundi cha Rock Star wa Mtaa huo nao walishiriki kufanya usafi.

Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wa Mtaa wa Gongolamboto Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameendelea kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kufanya usafi katika eneo hilo kwa wiki mara mbili ili kuyaweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea mtaa huo Dar es Salaam jana kujionea shughuli za usafi katika eneo Mwenyekiti wa mtaa huo Bakari Shingo alisema lengo lao kubwa ni kuiunga mkono kauli ya Rais Magufuli ya kufanya usafi ambapo wao wameamua kufanya usafi kwa wiki mara mbili.
Alisema lakini wao walianza kufanya usafi katika eneo kabla ya rais kuanza kuhimiza lakini kauli ya Magufuli ilichochea zaidi moto wa kufanya usafi kwa wananchi wa eneo hilo.
Shingo alisema katika mtaa wao kunavikundi ambavyo vinasaidia kufanya usafi ambapo wamegawa maeneo  na utaratibu huo umesaidia kuyaweka mazingira katika hali ya usafi.
Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envorotec Group kinachojishughulisha na usafi katika mtaa huo Ali Mwinyimkuu  Omari alisema kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa katika suala zima la usafi katika eneo hilo kutokana na utaratibu waliojiwekea.
Alisema wanamshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Issaya Mngulumi kwa kujitoa kwake kuwapa gari la kusomba takataka kila wanapofanya usafi hali ambayo inawapa moyo wananchi wa kufanya usafi hivyo kumungana mkono Rais Dk. John Magufuli katika suala zima la usafi nchini.

TANROAD YABOMOA NYUMBA ZILIZOJENGWA KATIKA HIFADHI YA BARABARA MAENEO YA BUZA, LUMO TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM

 Maofisa wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) na Polisi , wakisimamia ubomoaji wa nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara maeneo ya Buza kwa Lulenge Temeke jijini Dar es Salaam jana. Imeelezwa kuwa wamiliki wa nyumba hizo walikwisha lipwa fidia na Tanroad lakiwa wakawa wameshindwa kuondoka huku wengine wakiendeleza ujenzi.
 Wakazi wa Buza Sigara wakiondoa mabaki ya mbao baada ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad), kubomoa nyumba hizo.
 Kijana akipita jirani na nyumba iliyobomolewa.
 Mkazi wa Buza akiondoa mabaki ya mbao baada ya nyumba yake kubomolewa.
 Moja ya nyumba iliyobomolewa.
 Wananchi wakiangalia moja ya Baa iliyobomolewa.
 Tingatinga likiwa kazini.
 Watoto wakiangalia zoezi la ubomoaji lilivyokuwa likiendelea.
 Ofisa wa Tanroad akisimamia ubomoaji huo.
 Wananchi wakiangalia zoezi la ubomoaji.
 Tingatinga likiisambaratisha moja ya nyumba iliyojengwa kwenye hifadhi ya barabara eneo la Buza kwa Lulenge.
 Wananchi wakiangalia  ubomoaji huo.
 Tingatinga likifanya vitu vyake bila huruma.
 Askari wa kutuliza ghasia wakiwa eneo la tukio kuimarisha ulinzi.

Wachina waishio nchini waadhimisha mwaka mpya 2016 wa "Ngedere"

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akifungua Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kushoto ni mshereheshaji ajiyejitambulisha kwa jina la “Sharobaro”.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Salim Ahmed Salim (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (kulia) akifuatilia michezo mbalimbali wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (katikati) akifuatilia michezo mbalimbali wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salim  Dkt. Ahmed Salim na kushoto ni Mshauri wa Mambo ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Gao Wei.
 Mawaziri Wakuu Wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia) na Mhe. Mizengo Pinda (kushoto) wakisalimiana wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam
 Mawaziri Wakuu Wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Salim Ahmed Salim (kulia) na Mhe. Mizengo Pinda (kushoto) wakisalimiana wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam
 Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya raia wa Kichina wakiendelea na kujipamba kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya raia wa Kichina wakiendelea na kujipamba kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya raia wa Kichina wakiendelea na kujipamba kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya michezo iliyooneshwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya michezo iliyooneshwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya michezo iliyooneshwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Waziri Mkuu Mtaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akichanganya tiketi za bahatinasibu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
  Fashifashi na fataki  zilizowashwa kuashiria kuzinduliwa kwa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
 Fashifashi na fataki zilizowashwa kuashiria kuzinduliwa kwa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Fashifashi na  fataki zilizowashwa kuashiria kuzinduliwa kwa Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO

MAJALIWA AHUDHURIA IBADA YA KUMUINGIZA KAZINI MKUU WA KKKT TANZANIA ASKOFU SHOO MJINI MOSHI.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea picha aliyopewa na Askofu Mkuu Mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli,Askofu Frederck Shoo katika ibada ya kumuingiza kazini askofu huyo ilyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
 Baadhi ya waalikwa walioshiriki katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizunguza katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askofu Frederick Shoo kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo (kulia) na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu Alex Malasusa baada ya ibada ya kumuingiza kazini Askofu Shoo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

JAJI MKUU MHE MOHAMED CHANDE .OTHMAN AFUNGUA RASMI MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI MWAKA 2016


Watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wadau mbalimbali wa wakiingia katika viwanja vya Mnazi mmoja kwa maandamano leo jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.


Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Askari wa Jeshi la Magereza na Watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakiwa wamebeba mabango ya Ofisi zao wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini leo jijini Dar es salaam.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (Mwenye T-shirt nyeupe kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki (wa Pili kulia) na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania wakishiriki mazoezi ya viungo ya pamoja na wadau mbalimbali wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini.


Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (katikati) akiongoza mazoezi ya pamoja ya Wadau wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria nchini.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  akizungumza na wadau mbalimbali wa Mahakama waliohudhuria Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria mwaka 2016 katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini Dar es salaam.


Baadhi ya Wanachi wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini leo jijini Dar es salaam. Wengine katika picha ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (wa tatu kutoka kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (wa pili kutoka kushoto).


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na Watendaji wa Mahakama, Viongozi na Askari wa Jeshi la Polisi wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria leo jijini Dar es salaam.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu (wa tatu kutoka kulia) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) leo katika viwanja vya Mnazi Mmmoja wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa tatu kutoka kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omary Othman Makungu ( wa tatu kutoka kulia) na Jaji Kiongozi Mhe. Shaban Lila ( wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya  Watendaji na Watumishi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Ofisi ya Msajili wa Mahakama, Wakuu wa Idara  na Vitengo wa Mahakama ya Tanzania leo wakati wa Ufunguzi wa Wiki ya Sheria. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki (wa tatu kutoka kushoto).


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na Askari wa Jeshi la Magereza leo wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini.

 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali vya Mahakama ya Tanzania wakati wa Ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na Watumishi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS).