Thursday, June 30, 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU, MELINDA GATES WAYAPONGEZA MASHINDANO YA MAMA SHUJAA WA CHAKULA YANAYO ENDESHWA NA OXFAM TANZANIA


Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani Bi. Melinda Gates akiongea na wadau mbalimbali na kulipongeza shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kwa kuendesha Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo lengo kubwa ni kuwawezesha wakulima wadogo wadogo wanawake kufanikiwa katika Kilimo cha chakula na umiliki wa ardhi.
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akitoa neno la utangulizi wakati wa sherehe hiyo.
Waziri wa Afya,Jinsia,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akilipongeza Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kwa kuendesha Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo linaonesha changamoto za wazalishaji wa chakula wadogo ikiwemo umiliki wa ardhi.
Mshereheshaji katika Hafla hiyo Maria Sarungi Tsehai akiendelea kutoa muongozo


Dkt. Eve Marie akizungumza kwa kina ni jinsi gani Serikali na Sekta binafsi zinaweza kuwekeza katika wakulima wadogo wadogo hasa wanawake ili kuongeza uzalishaji wa Chakula

Muwezeshaji kutoka Forum CC Faizal Issa akielezea namna wakulima ambavyo wanaweza kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi ambayo kwa sasa yanaathiri kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji katika kilimo.

Mwanamuziki maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva Mwasiti akitumbuiza wakati wa Sherehe hizo

Mama Shujaa wa Chakula Anna Oloishuro akizungumzia jinsi mabadiliko ya tabianchi yanavyo athiri katika kilimo pia kuomba Benki mbalimbali nchini zisaidie wakulima kwa kuwakopesha na kuwapa riba ndogo.

Profesa Marjorie Mbilinyi akizungumzia swala zima za wazalishaji wa chakula wadogo kukosa masoko alisisitiza Sheria mbalimbali zifuatwe ili kukabilina na hali hiyo.


Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Msichana Initiative Rebeca Gyumi akizungumzia tatizo la ajira kwa vijana Tanzania na kusisitiza ikiwa watawezeshwa katika mambo mbalimbali ikiwemo na umiliki wa Ardhi basi wataweza kufikia malengo yao.

Baadhi ya wageni wakiwa katika sherehe hizo wakifuatilia kwa makini mjadala uliokuwa ukiendelea fuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea
Mwigizaji Maarufu wa Bongo Movie na Balozi wa Oxfam Tanzania Jacob Stephen JB akitaja majina washiriki 19 katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2016 msimu wa tano
Aliyekuwa Mshiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa nne na Rais wa wakulima wadogo wadogo wanawake Afrika Bi. Eva Daud Mageni akitoa neno la Shukurani kwa Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani na kumpa zawadi maalum ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika kuendeleza jitihada za maendeleo Tanzania ikiwemo swala la Kilimo.
Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani akipokea zawadi maalumu kutoka kwa waliokuwa washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Misimu iliyopita
Picha ya Pamoja ya Waziri wa Afya,Jinsia,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu,Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani, Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster,Mabalozi wa Oxfam Tanzania pamoja na Baadhi ya Akina mama watakao Shiriki Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2016


Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwa katika Sherehe hiyo
Mkutano Maalum na waandishi wa Habari ukiendelea

Picha na Fredy Njeje


Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na mke wa tajiri namba moja duniani na mwenyekiti mwenza wa Bill and Melinda Gates Foundation, Melinda Gates kwa pamoja wamelipongeza Shirika la Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow kwa kufanya Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kama moja ya mbinu za kumkomboa mwanamke mnyonge kiuchumi.

Wawili hao waliyasema hayo kwenye mdahalo uliofanyika Juni 29 mwaka huu katika bustani ya Hoteli ya Serena jijini Dar ambapo walikuwa wageni waalikwa waliopata fursa ya kuzungumzia jinsi ya kumuwezesha kiuchumi mwanamke mzalishaji na namna ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Akizungumza kwenye mdahalo huo, Melinda Gates alisema kuwa yeye kupitia Bill and Melinda Gates Foundation wamelenga kusaidia nchi nyingi hasa za ukanda wa Afrika Mashariki kama Tanzania katika kubadilisha maisha yao kwa kutengeneza fursa za ajira na kuwasaidia vitendea kazi.

Aliongeza kuwa kwa nchi kama ya Tanzania ambayo asilimia 25 ya mapato yake yanatokana na kilimo, taasisi yao imejikita katika kuwawezesha wakulima wadogowadogo ambao hata hivyo huwezi kuwaacha wakina mama kwa kuwa ndiyo wanaotoa mchango mkubwa kwenye sekta hiyo.

Akizungumzia kuhusu Shindano la Mama Shujaa wa Chakula, Melinda Gates alitoa pongezi zake za dhati kwa shirika la Oxfam na kuongeza kuwa, ikiwa nchi za Kiafrika hususan Tanzania itataka kupiga hatua lazima iwawezeshe kiuchumi wanawake kwa kuwa wao ndiyo wenye uwezo wa kubadilisha maisha yao na hilo ndiyo jambo muhimu zaidi. 


Naye Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye mdahalo huo alisema kuwa; kwa kipindi kirefu amekuwa mfuatiliaji wa mashindano hayo na kuahidi kuwa sera ya serikali ya awamu ya tano ni kuongeza vipaumbele kwa mwanamke kwa kutoa mianya kwa taasisi zinazomsaidia mwanamke ikiwemo shirika la Oxfam kupitia shughuli zake hasas shindano la mama shujaa wa chakula. “Nikiri tu kuwa nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa shindano hili tangu zamani, naahidi kuwapa ushirikiano mkubwa kwenu kwa kila jambo kwa kuwa mnaisaidia sana serikali,” alisema Ummy.

Aidha mdahalo huo pia ulioongozwa na mwanaharakati, Maria Sarungi Tsehai ulihudhuriwa na wanaharakati wengine wa masuala ya jinsia akiwemo Mkurugenzi wa Msichana Initative, Rebecca Gyumi, Mwanaharakati wa Mtandao wa Masuala ya Kijinsia, Marjorie Mbilinyi, Mwezeshaji kutoka Forum CC, Faizal Issa na Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2011, Anna Oloishuro.

WANANCHI WAJITOKEZA KUPATA HUDUMA ZA 4G YA TTCL, KATIKA VIWANJA VYA SABASABA.

 Afisa kutoka TTCL, Fredrick Benard (kushoto) akitoa maelezo kwa mteja aliyetembelea banda la TTCL.



 TTCL wakitoa huduma kwa wateja katika maonesho ya Sabasaba 
 Wafanyakazi wa TTCL wakitoa huduma kwa wateja.
 Wafanyakazi wa TTCL wakiwakaribisha wateja katika Banda.
Wateja wakipata maelezo kuhusu huduma za TTCL, katika viwanja vya sabasaba

Wananchi waendelea kujitokeza kwa wingi katika Banda la Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) kununua bidhaa bora za  4G katika viwanja vya Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa ya Sabasaba. 

Akizungumza katika Maonesho hayo, Emerco Mashele Afisa kutoka TTCL amesema kuwa katika msimu huu wa Maonesho ya Kimataifa ya SabaSaba, kampuni imeendelea kuwaletea watanzania bidhaa nzuri za 4G – LTE, zenye kiwango kikubwa cha ubora, bei nafuu na uhakika. 

“Safari hii tumewaletea Wananchi bidhaa bora na nzuri katika matumizi ya mawasiliano ya simu. Kwa huduma zetu tunatoa fursa kwa wateja wetu kupata intaneti yenye kasi ya 4G ukiwa na Laini za 4G ambazo zinapatikana hapa katika Banda TTCL na ofisi za TTCL katika jiji la Dar es salaam” amesema Emerco. 

Aidha, Bw. Emerco aliongeza kuwa katika Maonesho haya ya SabaSaba, TTCL inatoa fursa ya wananchi kupata   laini ya 4G, Modemu ya 4G, Mi-Fi ya 4G na Routers ya 4G.

Katika maonesho haya tuna laini za 4G ambazo zinapatika hapa na katika ofisi zetu za TTCL, Mteja anaweza kifaa cha 4G Mi-Fi ambapo mteja anaweza kuunganisha watu wengine 10 na kupata intaneti katika ubora ule ule. 4G Routers inauwezo wa kuunganisha watu 32 na inauwezo kwenda katika ubora ule ule, Aidha pia Routers inatoa fursa kwa watumiaji kupata huduma simu ya Mezani. 

RC MAKALA AAGIZA KUKAMATWA KWA MKANDARASI WA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA SONGWE BAADA YA KUSHINDWA KULIPA MAFAO YA VIBARUA ZAIDI YA 50.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla,akitolea ufafanuzi na kujibu kero mbalimbali zilizotolewa na wananchi wa Mkoa wa Mbeya, katika kikao maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkapa, ambapo kubwa zaidi katika siku hii, Makala amesema serikali itahakikisha inamkamata mkandarasi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Songwe kutoka kampuni ya Kundan Sigh, baada ya kushindwa kulipa mafao ya vibarua zaidi ya 50. 

Na Emanuel Madafa, Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameagiza kukamatwa kwa mmiliki wa kampuni ya Kundan Singh, ambaye alipewa tenda ya kujenga uwanja wa ndege wa Songwe, baada ya kushindwa kulipa mafao ya vibarua zaidi ya 50.


Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa kauli hiyo , wakati akijibu na kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa kipindi kirefu, hali iliyochangia wananchi kuichukia serikali kwa madai ya kushindwa kuwatendea haki.

Awali, akitoa malalamiko hayo kwa Mkuu wa Mkoa, Joshua Mwasilonde kwa niaba ya vibarua wenzake, amesema wamekuwa wakidai mafao yao tangu mwaka 2012/2013 katika mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF na kwamba kila wanapofuatilia wamekuwa wakipigwa kalenda.

Akilizungumzia hilo, Makala amesema, kwakua serikali iliingia mkataba na kampuni hiyo na kumalizana nayo bila ya kuacha deni lolote hivyo mkandarasi huyo anapaswa kuwalipa vibarua hao na kuutaka uongozi wa NSSF, kuhakikisha unavishirikisha vyombo vya dola katika kumkamata mkandarasi huyo.

Meneja NSSF Kanda ya Nyanda za Juu kusini, Robert Kadege, akilitolea ufafanuzi suala hilo, amesema suala la vibarua hao linafanyiwa kazi na kwamba tayari mahakama imetoa hukumu na kuupa ushindi mfuko huo.
Katibu tawala Mkoa wa Mbeya Mariam Mtunguja, akitolea ufafanuzi baadhi ya masuala ya kiutendaji katika kikao hicho. 
Baadhi ya wananchi waliofika kutoa kero na malalamiko katika kikao hicho.
Baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali katika kikao maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkapa June 29 mwaka huu. 
Baadhi ya wananchi wakitoa malalamiko na kero zao katika kikao maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkapa June 29 -2016 ambapo MKuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ndiye aliyepokea kero hizo sanjali na watendaji wa serikali na taasisi mbalimbali za serikali.
Kikao kikiendelea.(Picha E.Madafa).

YALIYOJIRI BUNGENI LEO

TBC: Je, ni utaratibu gani EWURA inatumia kupanga bei ya umeme ncini ? Naibu waziri  nishati na madini Dkt.Medard Kalimani anafafanua ; https://youtu.be/9vfH0mLy4RM
 SIMU.tv: Naibu Waziri Mhe. Luhaga Mpina akiwasilisha taarifa ya mwaka wa fedha zilizo kakugulia za baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira  mwaka 2015; https://youtu.be/zPTV9k3FuBw
SIMU.tv: Je ni mfumo upi ulioweka na serikali kwa mishahara ya wafanyakazi wa viwandani na kampuni binafsi? Naibu waziri Athony Mavunde anafafanua; https://youtu.be/_RrQcgc4hu8
SIMU.tv: Mbunge wa viti maalumu Mhe. Mariam Kisangi aibana serikali kuhusu mama Ntilie na machinga wanaosumbulia na mgambo wa jiji; https://youtu.be/Xurkil5lGMo
SIMU.tv: Je,serikali ina mpango gani wa  kuendeleza bonde la mto Luhuhu kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji? Naibu waziri Mhandisi Kamwelwe anafafanua; https://youtu.be/ybsR61DQnMg
SIMU.tv: Sakata la kufunga na kuyaondoa machimbo ya madini ya ujenzi yaliyopo Kigamboni yanayotoa malighafi muhimu kwa ujenzi lachukua sura mpya bungeni. https://youtu.be/dh5QO971QKI
SIMU.tv: Ikiwa khanga ni vazi la asili kwa mwanamke wa kitanzania, je serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha uzalishaji bora wa Khanga nchini? https://youtu.be/7ef-O3ZderI
TBC: Mhe. Manyanda Masele aihoji serikali juu ya usanifishaji na upembuzi yakinifu wa miundombinu ya barabara wilayani Mbogwe mkoani Geita. https://youtu.be/_ofj2ooj8Y8
SIMU.tv: Eng. Masauni atoa tamko la serikali juu ya uwepo wa vifo vyenye utata vya kisiasa vya wapinzani visivyopewa kipaumbele katika upelelezi. https://youtu.be/rEJVuvvw0YY
SIMU.tv: Hotuba ya waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumzia  suala la upinzani nchini hususani wabunge kususia vikao  vya bunge; https://youtu.be/k7NXxYvAOp0
SIMU.tv: Fahamu alichokisema waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa kuhusu mpango wa pili wa maendeleo ya taifa wa miaka mitano ikiwemo suala la kodi; https://youtu.be/p2iefVT1g0M
SIMU.tv: Waziri mkuu Kassim Majaliwa  akizungumzia suala la maadili kwa viongozi na watumishi wa umma na suala la mahakama maalumu ya mafisadi nchini; https://youtu.be/xuSDxPKMEcc
SIMU.tv: Fahamu kauli ya serikali kuhusu hali ya chakula nchini pamoja na suala la kuongeza uzalishaji wa sukari katika kukabiliana na uhaba wa bidhaa hiyo; https://youtu.be/HvD_sRgR78A
SIMU.tv: Hotuba ya waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumzia suala la viwanda nchini  kwa lengo la kukuza uchumi wa taifa; https://youtu.be/eUnXAi5DdhA
SIMU.tv: Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumzia suala la serikali kuendeleza mpango wake wa umeme vijijini REA; https://youtu.be/LARzJSKK1pY
SIMU.tv: Sehemu ya hotuba ya Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumzia akizungumzia suala la mkopo wa wanafunzi waa elimu ya juu; https://youtu.be/oXk8wDjqNGE

DIASPORA WAHIMIZWA KUTII SHERIA BILA SHURUTI

TANGAZO KWA WATANZANIA WOTE NA WALE WANAOISHI NJE YA NCHI (DIASPORA)

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inaendelea na jitihada zake za kuhamasisha Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) katika kuchangia maendeleo ya nchi yao. Ili kufanikisha hilo, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo imekuwa ikizishawishi taasisi mbalimbali hapa nchini kutoa huduma na fursa za biashara na uwekezaji, ambazo zitasaidia Diaspora kuwekeza kiurahisi hapa nchini. Juhudi hizi ambazo zilianza tokea Serikali ya Awamu ya Nne zimeanza kutoa matunda makubwa ambapo thamani ya uwekezaji kutoka kwa Diaspora inaongezeka kila kukicha.

Kutokana na umuhimu wa Diaspora katika kuchangia maendeleo ya nchi na huduma nyingine za kijamii; Serikali inapenda kutumia nafasi hii kuwakumbusha Watanzania wote wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) umuhimu wa kuheshimu na kutii sheria na taratibu katika nchi wanazoishi. Aidha, Serikali pia inapenda kuwakumbusha tena Watanzania wote wenye nia ya kusafiri nje ya nchi kwa lengo la kupata ajira au kutafuta maisha bora (greenpastures), kuhakikisha kuwa mikataba ya ajira inatambulika na mamlaka za nchi husika. Sambamba na hilo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi za Balozi za Tanzania nje ya nchi zitaendelea kuwa mstari wa mbele kusaidia kutatua matatizo ya namna hiyo kwa Watanzania; pamoja na Taasisi za Serikali kama vile Wakala wa Ajira Tanzania (TAESA). 

Serikali pia inawakumbusha Watanzania wanaotaka kusafiri nje ya nchi kwa malengo mbalimbali kama vile masomo, biashara, makazi au masuala yoyote binafsi nao kuheshimu sheria na taratibu za nchi husika. Taratibu hizo ni pamoja na:

1) Kujitambulisha na kujiandikisha kwenye Ofisi za Balozi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nchi wanazoishi au kama katika nchi hizo hakuna Ofisi ya Ubalozi wanashauriwa kuwasiliana na Ofisi za Ubalozi zilizo karibu na nchi yao. Kufanya hivyo kutarahisisha maafisa wa Ubalozi kuweka kumbukumbu zao kwa ajili ya mawasiliano ili kama kuna taarifa muhimu ziwafikie kwa wakati; au endapo watapata majanga ya aina yoyote waweze kuhudumiwa mapema; 

2) Kuheshimu sheria, taratibu na kanuni za nchi wanazoishi na kuwa raia wenye uzalendo na hekima; 

3) Kutojihusisha na tabia chafu zitakazohatarisha maisha yao kama vile kufanya biashara za magendo na madawa ya kulevya ambazo zinaweza kuwa na madhara kwao binafsi na pia kuiletea nchi yetu sifa mbaya; 

4) Kutunza Hati za Kusafiria (pasipoti) kwa kuwa ni utambulisho muhimu kwao na pia ni nyaraka muhimu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

5) Kutumia fursa zilizopo katika nchi wanazoishi kwa madhumuni ya kujiletea maendeleo yao na bila kusahau kutumia ujuzi, elimu, na maarifa waliyoyapata kwa ajili ya kuchangia kukuza uchumi wa nchi yao; 

6) Kuendelea kuitangaza Tanzania na kuwa mabalozi wazuri wenye uelewa na upendo wa nchi yao ili kuvutia watalii na wawekezaji wengi kuja hapa nchini; 

7) Kuendeleza matumuzi ya Lugha ya Taifa ya Kiswahili popote walipo ikiwa kama sehemu ya kukuza diplomasia ya utamaduni wetu;

8) Kuwaelimisha na kuwahimiza ndugu zao na watoto wao popote walipo huko ughaibuni kutumia lugha ya Kiswahili na kueneza historia na tamaduni za Kitanzania ili wasisahau walikotoka. 

Tunapenda pia kutumia nafasi hii kuwakumbusha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na jitihada zake thabiti za kutengeneza mazingira wezeshi ya kuwatambua, kuwahamasisha na kuwashirikisha Diaspora katika kuleta maendeleo yenye matumaini na tija kwa Tanzania. Michango ya Diaspora katika maendeleo ya nchi kupitia sekta za kiuchumi, kibiashara, afya, elimu, miundombinu, na nyingine ni muhimu; na inazidi kukua na hatimaye itaipelekea Tanzania kuwa na uchumi wa kati katika miaka ya mbele. Hivyo, Diaspora popote mlipo mnahimizwa kuzidi kushiriki kikamilifu katika kujenga Taifa letu bora la leo na la kesho. 

IDARA YA DIASPORA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA 
USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
DAR ES SALAAM.
30 Juni, 2016

MFUKO WA PENSHENI WA PPF KUTOA HUDUMA ZOTE KWA WATEJA WAKE VIWANJA VYA SABASABA

Muonekano wa nje ya Jengo la PPF lililopo Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere jijini Dar esSalaam (Sabasaba).
Maandalizi.

Afisa Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Tulla Mwigune (kulia) Afisa Michango wa Mfuko huo, Saluna Aziz Ally (katikati) na Afisa Michango Glory Maboya, wakijiandaa kuhudumia wateja leo asubuhi katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
Afisa Utafiti Neema Mjema (nyuma) na Mwanasheria wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Nyambilila Ndoboka, pia wakijiandaa kuweka mambo sawa kabla ya kuanza kupokea wateja katika Bandao lao la Maonesho kwenye Viwanja vya Sabasaba leo.
Afisa Uwekezaji wa Mfuko huo, Jonas Mbwambo akiweka mambo sawa kabla ya kuanza kupokea wateja katika Banda lao namba 86 viwanja vya Saba saba.

Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Pauline Msanga, akitoa maelezo kwa wananchi kuhusu Huduma za uendeshaji Mfuko huo, wakati walipotembelea katika Banda lao lililopo kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam, leo.

Sehemu ya wananchi waliotembelea Banda la Mfuko wa Pensheni wa PPF wakipata elimu kuhusu Mafao yatolewayo na Mfuko huo na jinsi mwanachama anavyoweza kujiunga na kuchangia.

Afisa Michango wa Mfuko huo, Saluna Aziz Ally, akimfafanulia mwanachama wake kuhusu uchangiaji wa michango ya Wanachama,

Afisa Huduma kwa Wateja wa PPF, Mwajuma Msina, akizungumza na Mwananchi aliyefika kutembelea Banda hilo wakati akimwelezea kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko huo.

Afisa Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Tulla Mwigune (kulia) akifafanua jambo kwa mstaafu wa PPF.

Mtaalamu wa Mifumo ya Habari wa Mfuko wa PPF, Isabela Ngalawa, akimwelekeza mmoja kati ya Wanachama wa Mfuko huo kuhusu 'PPF Taarifa Mobile Apps' ili mwanachama aweze kupata taarifa za michango yake kupitia simu yake ya mkononi.

Afisa Huduma kwa Wateja, Mohamed Siaga, akizungumza na Mwananchi aliyefika katika Banda la PPF kuhusu jinsi ya kujiunga na Mfumo wa 'Wote scheme kutoka sekta isiyo rasmi.
Mmoja kati ya Wanasheria wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Nyambilila Ndoboka, akimwelekeza jambo mwanachama wa Mfuko huo kuhusu masuala ya Kisheria, wakati alipofika kutembelea Banda la Maonesho la PFF leo.
Afisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Temeke, Sostenes Lyimo (kushoto) akifafanua jambo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea Banda hilo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya Banda lao Namba 86 lililopo katika Viwanja vya Sabasaba.

Picha Zote na Mafoto Blog

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) LAANZA KUTOA HUDUMA KATIKA MAONESHO YA 40 YA KIMATAIFA YA SABASABA

Banda la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) likiwa katika Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara, yanayofanyika kila mwaka katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam tayari limeanza rasmi kutoa huduma zake katika viwanja hivyo.
Afisa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Bi Edith Nguruwe akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la (NHC) kuhusina na huduma zinazotolewa na Shirika hilo.
Afisa Mauzo Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Emmanuel Limo (kushoto), akimuelezea Wananchi Kuhusiana na mradi wa SAFARI CITY uliopo Arusha alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Sabasaba.
Afisa biashara (NHC), Clara Lubanga akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa Wananchi aliotembelea banda hilo kuhusiana uzwaji wa nyumba (katikati), Afisa Mauzo wa (NHC), Joseph Haule.
Afisa Mauzo (NHC), Jasson Ipyana akimuelezea mwananchi kuhusina na miradi ya nyumba ya bei nafuu ilioko nchini.
Bw: Klison Sanane (kushoto), akifafanua miradi mbalimbali ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Aika Swai (kushoto), akielezea kuhusiana na utaratibu wa unaoutumika katika ununuzi wa nyumba za (NHC) huku baadhi ya wadau kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakimsikiliza kwa umakini.PICHA NA PHILEMON SOLOMON.