Monday, July 31, 2017

VIONGOZI TUMSAIDIE RAIS KUTATUA KERO - WARIOBA


Na Judith Mhina – MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, anahitaji kupata usaidizi wa kutosha kutoka kwa viongozi na hasa wasaidizi  kuanzia ngazi ya nyumba kumi hadi taifa.
Maneno hayo yametamkwa na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba alipofanya mahojiano na Idara ya Habari – MAELEZO - ofisini kwake Oysterbay Jijini Dar-es-Salaam.
Jaji Warioba ameona kuna udhaifu mkubwa wa kiutendaji ambapo wananchi hawatoi changamoto zinazowakabili mpaka wamuone Rais amefika katika eneo lao, au wanaeleza changamoto zinazowakabili kwa viongozi husika ila, viongozi hawazifanyii kazi, ambapo wananchi wanaamua kuziwasilisha kwa Rais mara wanapomuona.
 “Rais hawezi kufanya kazi peke yake naomba tuimarishe utendaji wetu wa kazi, kama utendaji ungekuwa mzuri suala la makontena kufika hadi bandarini lisingekuwepo, na hata kugundulika kwake kusingefanywa na Rais,” amesema Jaji Warioba.
“Nampongeza sana Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan na  Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa, kwa utendaji wao wa kazi. Viongozi hawa ni wasikivu na wanatekeleza kazi zao bila mihemko kwa kutoa maagizo na maelekezo kwa wahusika ili wayatekeleze”, aliongeza  Mhe. Warioba.
Hivi karibuni, Rais ameona tatizo hilo, la kuachiwa kila jambo ili afanye  wakati kuna uongozi wa serikali, kuanzia ngazi ya nyumba kumi hadi taifa.  Rais amelisema hilo, alipokuwa kwenye ziara katika Mkoa wa Tabora, ambapo mabango mengi yaliyoandikwa na wananchi yakiwa na changamoto mbalimbali na kugundua kuwa viongozi walio wengi hawatatui changamoto hizo. Matokeo yake, Rais anapofika eneo husika, kila mwananchi anataka atatuliwe changamoto yake kitu ambacho hakiwezekani na wala sio sahihi.
Tabia hii haikumpendeza Rais Magufuli, ambapo alipotoa kauli kuwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na watendaji wengine ambao hawatatui matatizo ya wananchi atawaondoa katika nafasi hizo mara moja.
“Endapo nitarudi na kuelezwa kero ambazo mnaweza kuzitatua lakini mkashindwa kufanya hivyo, nitajua kuwa mmeshindwa kufanya kazi yenu kwa ufanisi” alisema Rais Magufuli.
Warioba ameongeza kwa kusema; “Sisi wote tulikuwa viongozi lakini hatukuwahi kuachiwa tufanye kila kitu bila usaidizi wa viongozi katika ngazi zote.
Tanzania ni kati ya nchi zilizojizatiti kwa kuwa na uongozi kuanzia ngazi ya nyumba kumi, shina, kata, tarafa, Wilaya, Mkoa hadi taifa. Kama kweli uongozi wa kila ngazi utajituma kutatua changamoto za wananchi itamrahisishia Rais kufanya majukumu yake.  
Mtakumbuka kuwa enzi za awamu ya kwanza na ya pili, sio kweli kwamba hali ilivyo sasa ni mbaya kuliko awamu hizo. Lakini wakati ule kilichotusaidia ni umoja wetu na mshikamano wa kutatua matatizo yetu kwa pamoja, hatukuachiwa kama viongozi tutatue changamoto za wananchi sisi wenyewe. Amesema Warioba.
Akisisitiza, Warioba amesema; “Iweje leo tumuachie Rais afanye kila kitu mwenyewe naomba sana tumsaidie na kumuunga mkono, hakika ana nia njema na rasilimali za nchi hii. Ni vema kilichofanyika kikaangalia rasilimali zote za nchini na sio wawekezaji wa nje tu hata wa ndani”.
Aidha, kiongozi mwingine aliyeliona tatizo hili ni Waziri Mkuu Msataafu Dkt. Salim Ahmed Salim, ambaye amesema Vijana ni lazima wajue siasa za nchi yao na nini muelekeo wa uongozi wa nchi kwa ujumla. Uongozi ni dhamana unayopewa kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, hivyo ni lazima uwatumikie ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili.
 “Bila kujua historia na siasa ya nchi yako utashindwa kuwatumikia wananchi badala yake utafanya kazi kwa matakwa yako, ambapo itakuwa sio sahihi. Wito wangu viongozi wote msaidieni Rais katika kutimiza wajibu wa Watanzania, msimuache afanye kazi peke yake, sisi sote tumuunge mkono”Amesema Dkt. Salim.
Tangu Rais ateue viongozi mbalimbali ni zaidi ya mwaka mmoja na nusu sasa, kila kiongozi anajua utendaji wa Rais na nini anataka wafanye. Viongozi wameapa na kupewa miongozo ya utendaji wa kazi zao. Kutokana na Rais kuwa wazi katika hilo nadhani sasa kila mhusika atafanya ipasavyo ili kutatua changamoto kadhaa zinazowakabili wananchi.
Mfano mzuri ni ule uliotolewa na Kamati ya maridhiano ya viongozi wa madhehebu ya dini Tanzania ya kuomba viongozi wengine kuiga utendaji wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, ambaye walimpongeza kwa kutatua kero za ardhi kila mahala hapa nchini. Kiongozi huyo amejitahidi kupunguza kero za watumishi wa ardhi wasio waaminifu kwa kudai rushwa, katika suala zima la kupata viwanja, kupima na kupata hati miliki.   
Hivyo, kila mhusika katika Mkoa, Wilaya, Tarafa, Kata, shina na nyumba kumi anawajibu wa kutatua kero na changamoto zinazowakabili wananchi wa eneo lake. Iwapo kero ipo nje ya uwezo wa uongozi wako, utashirikiana na ngazi iliyokuzidi kuhakikisha unaipeleka mbele zaidi itatuliwe na kuchukuliwa hatua zinazofaa.
Kiongozi hutumia busara, badala ya kusubiri Rais afike katika eneo lake na wananchi waanze kulalamika, tafsiri yake ni kwamba  hufai kuwepo kwenye nafasi husika, hivyo ni vema ukatafuta kazi nyingine ya kufanya.
Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliliona tatizo hili la wananchi na viongozi wote kuwa ni sehemu ya kulalamika badala ya kutafuta jinsi ya kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili kwa wakati huo baada ya uhuru.
Mwalimu akaliona kama donda ndugu ambalo likiachwa litaambukiza kizazi na kizazi,  hivyo alitafuta dawa na kuja na waraka wa serikali wa kusema “Toa Hoja usipige kelele” akiwa na maana hoja yako itaangaliwa, litafanyiwa kazi na kutolewa majibu , lakini kwa kupiga kelele watu wanaweza kudhani wewe ni mwendawazimu tu na wakakupuuza na tatizo litabaki palepale.       

Mpaka sasa Waraka huu wa Mwalimu Nyerere alioutoa mwaka 1964 una umuhimu na mantiki ya hali ya juu. Watanzania tutoe hoja tusipige kelele.

VIJIJI VYOTE KUWA NA UMEME IFIKAPO 2021 –DKT. KALEMANI

Na Tiganya Vincent
Serikali imesema kuwa jumla ya vijiji 7873 na vitongoji vyake vyote hapa nchini vitakuwa vimeshaunganisha na umeme chini ya Mradi wa Umeme Vijijini Awamu wa Tatu ifikapo mwaka 2021.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora  na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri.
Dkt. Kalemani alisema REA III itasaidia kukamilisha vijiji vilivyobaki ambavyo havijaunganishwa na umeme ifikapo mwaka 2021 kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya uchumi kati kuelekea uchumi wa viwanda.
Alisema kuwa lengo la Serikali ni kutaka wananchi wote hata wale wanaoishi visiwani waweze kufikiwa na huduma ya umeme kwa ajili ya matumizi yao na kwa ajili ya uendeshaji wa viwanda.
Aidha kwa upande wa Mkoa wa Tabora alisema vijiji vipatavyo 510 na vitongoji vyake vinatarajiwa kuwa vimeshaunganishwa na umeme wa uhakika wa ifikapo mwaka 2021 kupitia mradi wa REA III.
Aliongeza kuwa ili kuhakikisha lengo hilo la kuunganisha vijiji vyote vinakuwa na umeme, Serikali imeamua kuweka Wakandarasi wengi katika kila mradi na kuwaagiza kugawa kazi kwa Wakandarasi wadogo ambao ni wazawa na wenye sifa ili kurahisisha kazi na kuifanya iwe na ufanisi.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri alisema kukamilika kwa mradi wa REA III utaufanya mkoa huo kukua kwa kasi zaidi na kutoa wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza katika viwanda vya sekta mbalimbali ikiwemo za usindikaji wa mazao ya kilimo na mifugo na uchimbaji madini.
Alisema kuwa hivi sasa Mkoa huo unazidi kuimarika katika miundombinu ya barabara , reli , anga na upatikanaji wa maji  na umeme wa uhakika na hivyo kutokuwepo na vikwazo katika uzalishaji.
Uzinduzi wa uunganishwaji mradi wa umeme vijijini kwa awamu ya tatu unatarajiwa kufanyika tarehe 1 Agosti 2017 katika Wilaya ya Sikonge kwa niaba ya Wilaya zote za Mkoa wa Tabora.

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAITAHADHARISHA CUF

Na Margareth Chambiri, NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekishauri Chama cha Wananchi (CUF) kumaliza mgogoro unaoendelea ndani ya Chama hicho kwani unaweza kusababisha kupoteza nafasi za Udiwani katika Uchaguzi Mdogo unaotarajiwa kufanyika wakato wowote kuanzia sasa.

Tahadhari hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Bw. Kailima Ramadhani katika mahojiano maalum Ofisini kwake kuhusu tuhuma  mbalimbali zilizoelekezwa Tume hiyo ikiwemo suala la Uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum kupitia CUF.
Bw. Kailima amesema mvutano unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) hauna tija, hivyo ameshauri pande mbili zinazovutana kukutana na kumaliza tofauti zao kwani hali hiyo itawanyima nafasi ya kutoa wagombea kwenye uchaguzi huo mdogo.

 ‘Mimi niwashauri, CUF wana mgogoro wao wamalize mgogoro wao. Ni vizuri wakutane wamalize mgogoro wao kwani hii inaweza kuwaletea matatizo wagombea wakati wa Uchaguzi.’ alisesema Kailima na kusisitiza kuwa mgogoro ndani ya chama hicho hauna tija na badala yake unakidhoofisha. 

Amesema Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, inakitaka Chama cha Siasa kumsimamisha Mgombea mmoja kwa nafasi moja, lakini pia mgombea wa nafasi ya Rais na Mbunge  lazima fomu yake isainiwe na Viongozi wa ngazi ya Taifa wanaotambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.

‘Lakini ukisoma Maelekezo ya Vyama vya Siasa na Wagombea yanasema iwapo chama cha Siasa kina mgogoro ni lazima fomu zake zisainiwa na kiongozi wa juu wa ngazi ya Mkoa, sasa kwa hali hii iwapo CUF wasipokutana watapoteza nafasi.’ Amesema Mkurugenzi huyo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.  

Bwana Kailima amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatambua taarifa za Vyama vya Siasa iliyowasilishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa na kwa Chama cha CUF viongozi wanaotambuliwa na Tume hadi hivi sasa ni Mwenyekiti Prof. Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu ni Maalim Seif Sharif Hamad. 

‘Tume inatambua kuwa Mwenyekiti wa CU ni Prof. Ibrahim Lipumba, Inatambua Katibu Mkuu wa CUF ni Maalim Seif Sharif Hamad na Naibu Katibu Mkuu upande wa Bara ni Magdalena Sakaya’ amesema.

Amesema Tume haijazuiliwa na Mahakama wala na Msajili wa Vyama vya Siasa kwamba isifanye mawasiliano na Viongozi hawa, na kubainisha kuwa Tume itaendelea kufanya mawasiliano na Viongozi mpaka hapo itakavyoelekezwa vinginevyo na Msajili wa Vyama au Mahakama.

Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi amesema Tume inafanya kazi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu na kwamba mawasiliano ya Tume na Chama cha Siasa ni kwa mujibu wa maelekezo ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye ndiye anayesajili Vyama vya Siasa nchini.  

Aidha katika hatua nyingine Bwana Kailima ameelezwa kusikitishwa na taarifa za upotoshaji zinazoihusisha Tume kwenye kikao cha Wanasheria kwa lengo la kumshauri Spika wa Bunge kuhusu Chama cha Wananchi CUF na kubainisha kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote.

 Akielezea hatua zinazoweza kuchukuliwa na Tume dhidi ya upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya Wanasiasa na Vyombo vya Habari kuhusu utendaji kazi wa Tume Kailima amesema Tume itatumia Mamlaka zinazohusika na usajili ingawa hata hivyo amesisitiza kuwa ni vyema Vyama vya Siasa vitumie Wanasheria wao kusoma Sheria na taratibu za Uchaguzi ili kupata habari sahihi.

‘Hatua ya kwanza tunayochukua ni hii ya kuelimisha Chama pengine ni bahati mbaya lakini hatua ya pili ni ya kuzitaarifu mamlaka Kwa upande wa Vyama ni Msajili wa Vyama kwa upande wa Vyombo vya Habari vya Magazeti tunamtaarifu Msajili wa Magazeti ili ashughulike nao’ lakini kubwa tunawashauri jamani someni au ulizeni Tume,’ amesema Kailima.  

TANZANIA EXCELS IN STATISTICAL CAPACITY AMONG SUB-SAHARAN AFRICAN NATIONS, WB REPORT SHOWS

A graph showing Tanzania as a second country among  Sub - Saharan countries in better statistical capacity. According to the World Bank report,  Tanzania scored 90 percent for periodicity, 80 percent for source data and 50 percent for methodology which contributed to an overall of 73.3 percent. 

Tanzania has been ranked second, behind South Africa in statistical capacity among Sub-Saharan African nations. 
This is according to the World Bank (WB) 2016 Statistical Capacity Indicator (SCI). 
WB has been assessing national statistical capacity in developing countries since 2004 and has produced overall SCI score as well as scores for three categories, Methodology, Source Data and Periodicity. Regional overall and specific category SCI are also produced to allow for comparison.

For every dimension, a country is scored against specific criteria, using information available from the WB, IMF, UN, UNESCO, and WHO. 

A composite score for each dimension and an overall score combining all three dimensions are derived for each country on a scale of 0 - 100. A score of 100 indicates that the country meets all the criteria. 

The statistical methodology aspect measures a country’s ability to adhere to internationally recommended standards and methods, by assessing guidelines and procedures used to compile macroeconomic statistics and social data reporting and estimation practices by looking at an updated national accounts base year, use of the latest Balance of payment, external debt reporting and IMF’s Special Data Dissemination Standard and enrolment data reporting to UNESCO.

On source data, this measures data collection activities in line with internationally recommended periodicity, and whether data from administrative systems are available and reliable for statistical estimation purposes and periodicity of population and agricultural censuses, the periodicity of poverty and health related surveys, and completeness of vital registration system coverage.

The third aspect concerned with the periodicity and timeliness looks at the availability and periodicity of key socio-economic indicators of which nine are MDG indicators.

Tanzania scored 90 percent for periodicity, 80 percent for source data and 50 percent for methodology which, contributed to an overall SCI of 73.3 percent. Although this overall score ranks Tanzania as second behind South Africa (82.2%) there is still room for improvements, especially in methodology.  

The National Bureau of Statistics (NBS) is committed to continuing strengthening of the National Statistical System.

BALOZI WA KUWAIT ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI JIJINI DAR ES SALAAM


Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, liko katika mkakati wa kuingia ushirikiano na Serikali ya Kuwait katika shughuli zake za kukabiliana na majanga ya moto ikiwa ni juhudi zake katika kuyafikia maeneo mengi nchini. 

Akizungumza alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es salaam, Balozi wa Kuwait Nchini, Jasem Al-Najem, alisema serikali ya Kuwait ipo tayari kubadilishana mafunzo na kutoa msaada wa vifaa kwa Jeshi hilo.

“Ni vema tukatengeneza mpango ambao wataalam wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutoka nchini Tanzania wataweza kubadilishana uzoefu na wataalamu kutoka nchini Kuwait kwa ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na majanga pindi yanapotokea, ’’ Alisema Balozi huyo.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye alimshukuru kwa kumtembelea na kusema kuwa ujio wa balozi huyo, umefungua ukurasa mpya kwa upande wa misaada na mafunzo kwa Askari wa Jeshi hilo, kwani watapata fursa ya kubadilishana uzoefu na kuongeza tija kwa Jeshi lake.

“Tutapata nafasi ya kubadilishana uzoefu na kupata mafunzo kutoka Nchi ya Kuwait na kuongeza ufanisi katika majukumu yetu ya kila siku, lengo ikiwa ni kukabiliana na majanga mbalimbali yakiwemo ya moto,’’ alisema Kamishna Jenerali.


Katika kikao hicho Balozi wa Kuwait, Nasem Al-Najem alipokea taarifa ya changamoto zinazolikabili jeshi hilo ikiwemo uhaba wa vitendea kazi huku akiahidi kuzifanyia kazi na akisisitiza mchakato wa kusaini makubaliano ya hiari ukamilike kwani utakuwa msaada wa kutekeleza kwa haraka program za mafunzo ya muda mfupi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimkabidhi zawadi Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (kushoto), baada ya mazungumzo na Balozi huyo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo, jjini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (Wakwanza kulia) alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem, akizungumza wakati wa kikao na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (katikati) na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo, alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi jijini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akiongozana na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (kulia) alipowasili  Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo kwa mazungumzo yaliyohusisha ushirikiano kati ya Majeshi ya nchi hizo kubadilishana Utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem, akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo kwa mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Thobias Andengenye(hayupo pichani). Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (katikati) baada ya kikao cha mazungumzo yaliyohusisha ushirikiano kati ya Majeshi ya nchi hizo katika kubadilishana Utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

WANANCHI MONDULI KUNUFAIKA NA MAJI



Mkurugenzi wa kampuni ya Smart Vision ya Korea, Seo Young Kim (kushoto) na Andrew Chung ambaye ni mbunifu wa mtambo wa kusafisha maji wakionyesha mtambo huo kwenye uzinduzi wake kwenye kitongoji cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani Arusha
Mkurugenzi wa kampuni ya Smart Vision ya Korea, Seo Young Kim (kushoto) na mchungaji wa kanisa la Enyora Daniel Vengei wakiwa kwenye uzinduzi wake katika kitongoji cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani Arusha.
Wananchi wa kitongoji cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani Arusha wakishuhudia uzinduzi wa mtambo wa kusafisha maji na kuyachuja uliofanywa na kampuni ya Korea ya Smart Vision.

………………………….
Zaidi ya kaya 700 za wananchi wa Kitongoji cha Irmorijo Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli Mkoani Arusha, waliokuwa wanatumia maji ya kwenye bwana wanatarajia kunufaika na mradi wa kusafisha maji na kuchuja maji kuwa safi uliozinduliwa Kijiji hapo.

Awali, wananchi hao walikuwa wanatumia kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kupika, kufua, kuoga na kunywa maji hayo ya bwawa ambayo pia yalikuwa yanatumiwa na mifugo ya eneo hilo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Smart Vision ya Korea, Seo Young Kim akizungumza jana kwenye uzinduzi wa mradi alisema lengo ni jamii ya eneo hilo kunufaika na maji safi na salama yanayochujwa kupitia ubunifu wao.

Kim alisema kwa kuanza kuwanufaisha wananchi wa eneo hilo, wanatarajia kugawa majiko rafiki ya mazingira 22 na mitambo ya kuchuja na kusafisha maji ya bwawa kuwa safi na salama 22 kwa kaya 22 zitakazowanufaisha zaidi ya watu 220.

Alisema Smart Vision kupitia uwekezaji wa Korea Trade-Investment Promotion Agency. (KOTRA) jamii ya eneo hilo itanufaika na na mradi huo wenye lengo la kuondokana na matumizi ya maji yasiyo safi wala salama ambayo yanasababisha magonjwa ya tumbo.

“Jamii ya eneo hili kupitia mchungaji wa kanisa la Enyorata Daniel Vengei, walileta maombi kwetu kuwa wanatatizo la maji, hospitali na shule, ndipo tukaona tuanze kutatua hili suala la maji ndipo tukaleta mitambo hii ya kuchuja na kusafisha maji,” alisema Kim.

She said goal of project, Smart Vision head about maasai water problem in Korea. Smart Vision developed water purifier to help maasai people overcome water problem.

Kim said now Smart Vision a Korean Environmental company launches water project ina Tanzania, hopes to expand project to other parts of Tanzania where there is lack of drinking water.

“This project was aided financially bya KOTRA (Korea Trade-Investiment Promotion Agency) who supports international business of Korean companies, specifically, the KOTRA branc in Dar es salaam gave Smart Vision immense support in order to help people suffering from lack of drinking water though the water purification project,” said Kim.

She said people who helped with project is Director of Smart Vision Seo-Young Kim, Manager of Smart Vision, Hyun-Jung Chung and Purifier developer and volunteer, Andrew Chung.

Mkazi wa Kitongoji cha Emairete Rose Lemomo alisema alisema awali walikuwa wanakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama lakini kupitia mradi huo wataondokana na maradhi ya tumbo yaliyokuwa yakiwakabili hasa watoto.

Lemomo aliwashukuru wote waliohusika na kufanikisha mradi huo, kwani hivi sasa watakuwa wanachota maji bwawani na kuyachuja na kuyasafisha kupitia mitambo hiyo.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Irmorijo, Mirishi Songoyo alishukuru shirika la Smart Vision kwa kufanikisha mradi huo wa maendeleo ambao utainufaisha jamii ya eneo hilo walioteseka kwa muda mrefu juu ya suala la maji.

“Tunawaomba wananchi watakaofikiwa na mradi huu kuhakikisha wanawasaidia na wale ambao bado wanasubiri kupatiwa majiko na mitambo ya kuchuja na kusafisha maji,” alisema Songoyo.

Mwalimu wa shule ya msingi Irmorijo, Stephen Laizer aliwataka wananchi wote waliofanikiwa kupatiwa mradi huo kuhakikisha wanautunza ili kunufaika nao kwa muda mrefu kwani wameteseka kwa miaka mingi kwenye tatizo la maji.

“Wageni wanapokuja kwenu inawabidi kuwashukuru hata kama hawajaacha chochote ila hawa wametuletea teknolojia ya maji, wanaweza kutufanyia mengine mazuri,” alisema Laizer.

Vijana washauriwa kujiunga na awamu ya tatu ya program ya Via Jiandalie Ajira

Meneja Malezi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC), Bw. Daniel Mghwira (katikati) akizungumza kuhusu kuanza kwa kwa awamu ya tatu ya program Via Jiandalie Ajira kwa halmashauri zote za Dar es Salaam, Mkindani Mtwara, Dodoma na Kibaha Pwani, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF),Bi. Haigath Kitala na kushoto Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wafanyabiashara na Kilimo Tanzania(TCCIA),Bi. Magdalene Mkocha.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 24 wameshauriwa kujiunga na awamu ya tatu ya program Via Jiandalie Ajira inayoendeshwa na Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC) ili kupata mafunzo ya ujasiriamali, stadi za maisha, malezi ya kibiashara na kuunganishwa na taasisi za kifedha kupata mitaji kukabiliana na tatizo la ajira. 

Meneja Malezi wa Taasisi hiyo, Bw. Daniel Mghwira alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuwa vijana wajiunge na program hiyo ambayo imeingia katika awamu ya tatu kupata mafunzo hayo ili kukabiliana na tatizo la ajira. 

“Via Jiandalie Ajira awamu ya tatu inawalenga vijana wa Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es Salaam, Mikindani Mtwara, Dodoma na Kibaha Pwani,” na fomu za kujiunga zinapatikana katika ofisi za kata, ofisi za maafisa vijana za manispaa za maeneo hayo, aliongeza kusema Bw. Mghwira ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa taasisi hiyo.

Pia fomu hizo zinapatikana katika ofisi za Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogovidogo (SIDO) na Chemba ya Wafanyabiashara na Kilimo Tanzania (TCCIA).

Alifafanua kwamba fomu hizo zinatolewa bila ya gharama ambapo vijana watakao chaguliwa watafundisha mafunzo ya ujasiriamali, stadi za maisha, malezi ya kibiashara na kuwaunganisha na taasisi za kifedha kupata mitaji kwa njia ya mikopo kwa masharti nafuu, hivyo ni fursa kwa vijana wa maeneo hayo.

Alisema kuanzia sasa hadi mwaka 2020 taasisi yao kupitia program hiyo itafundisha vijana ,3,000 katika mikoa hiyo na hiyo itafanya jumla ya vijana 4,000 wakijumlishwa na waliofundishwa katika program ya kijana jiajiri.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF),Bi. Haigath Kitala alisema serikali imetoa kipaumbele katika uchumi wa viwanda, vijana wanahitajika kutumia fursa hiyo ili wasije kuwa watazamaji katika uchumi huo.

“Vijana wanapokuwa wamepata mafunzo kama haya, ni rahisi kwa mfuko wao kuwapatia mikopo ya riba nafuu,” na mfuko huo unatoa mikopo kwa vijana waliohitimu mafunzo ya ufundi stadi na wanawake wazalishaji mali na wanahitajika kuwa katika vikundi, alisema. 

Alisema pia mfuko unatoa mkopo wa vifaa na wa dhabuni sababu vijana wengi wanashindwa kutekeleza dhabuni hizo kwa kukosa fedha.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wafanyabiashara na Kilimo Tanzania,Bi. Magdalene Mkocha alisema chemba inashirikiana na taasisi hiyo katika kuwaandaa vijana kuingia katika ujasiriamali husani katika kutoa malezi.

“Tunapotaka kujenga kada nzuri ya wajasiriamali ni lazima kwa pamoja tushiriki katika hili,” na alitoa ombi kwa serikali na wadau wote kusaidia kusukuma jambo hilo,alisema.

Naye kijana ambaye amenufaika na mafunzo ya taasisi hiyo, Jackson Mmbando alisema mafunzo yanayotolewa na TECC yamewezesha kuanza na kuendesha biashara yake kwa mafanikio makubwa na anawataka vijana wenzake kuwa na nidhamu ya fedha ili kuanza au kuendeleza biashara.

Program hiyo ya Via Jiandalie Ajira inatekelezwa na TECC kwa kushirikiana na wadau wake kama Taasisi ya Kuendeleza Vijana Kibiashara ya Marekani (IYF), Mfukoa wa Rais wa Kujitegemea (PTF), SIDO, TCCIA , Manispaa au Halamashauri za Miji na Wilaya na sasa imefikia awamu ya mwisho kwa mwaka 2017.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MPANGO MKAKATI WA WATER AID TANZANIA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa mwaka 2016-2021 wenye kauli mbiu "Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa kitovu cha Maendeleo"iliyofanyika  kwenye hotel ya HyattRegency jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa mwaka 2016-2021 wenye kauli mbiu "Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa kitovu cha Maendeleo"iliyofanyika  kwenye hotel ya HyattRegency jijini Dar es Salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mohamoud Thabit Kombo wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa mwaka 2016-2021 wenye kauli mbiu "Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa kitovu cha Maendeleo"iliyofanyika  kwenye hotel ya HyattRegency jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha kitabu maalumu chenye mpango mkakati wa Water Aid ​

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassana leo amezindua Mpango Mkakati wa Water AID Tanzania .
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge, Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Mkurugenzi wa Water Aid Kanda ya Afrika Mashariki Bi. Olutayo Bankole –Bolawole,Mkurugenzi WaterAid Tanzania Dkt. Ibrahim Kabole na wadau mbali mbali wa maji, afya na mazingira.
Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Water Aid Tanzania wenye lengo la “ Kuweka Maji Safi na Usafi wa Mazingira (WASH)” katika mipango ya Maendeleo ya Jamii.
Makamu wa Rais aliwapongeza  Water Aid Tanzania kwa mpango wake huo, alisema Maji ni rasilimali ambayo haijawahi kutosheleza  mahitaji ya dunia na hapa kwetu pia kwani kuna mahitaji makubwa ya maji kwa ajili ya shughuli za kijamii, kiuchumi na kuhuisha na kutunza mazingira.
Vilevile  vyanzo vya maji vinaathiriwa sana na Ukame,kufurika n, kuvuruga mtiririko asilia, mabadiliko ya hali ya hewa ongezeko la idadi ya watu na viumbe wengine (Wanyama).
Mpango wa Water Aid Tanzania wa miaka mitano  utawezesha kuiweka Tanzania kwenye ramani ya matumizi endelevu ya rasilimali ya maji na utachangia katika utekelezaji wa malengo tuliyojiweka ya kupeleka huduma ya maji safi na salama kwa wananchi kulingana na Sera yetu ya Maji na pia kutekeleza ahadi tulizozitoa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya 2015.
Makamu wa Rais alisema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbali mbali imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo ya vijijini ambapo utekelezaji huo umeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini ambapo kwa mwezi Juni 2017 jumla ya watu 22,952,371 sawa na asilimia 72.58 ya wananchi waishio vijijini wanapata maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kama sera ya maji ya mwaka 2002 inavyoelekeza huku katika Miji Mikuu  ya mikoa kutoka asilimia 86 hadi asilimia 95, katika miji mikuu ya Wilaya , miji midogo na miradi ya Kitaifa kutoka asilimia 60 hadi asilimia 75 na katika jiji la Dar es Salaam kutoka asilimia 72 hadi asilimia 95 ifikikapo 2020.
Makamu wa Rais alisisitiza suala la usafi wa mazingira na kuhakikisha tunalinda afya zetu tusishambuliwe na magonjwa ya milipuko kama  vile kipindu pindu na homa za matumbo.  “Sote tunajukumu kubwa kuhakikisha tunapata maji na kuzungukwa na Mazingira safi”.
Makamu wa Rais aliwaagiza wanaohusika na usimamizi wa miradi ya maji na usafi wa mazingira kuongeza jitihada zaidi ifikapo 2020 idadi ya wananchi wanaopata maji iwe imeongezeka kufikia malengo tuliyojiwekea.
Mwisho, Makamu wa Rais aliwashukuru wawakilishi wa mashirika yote ya Maendeleo, wafadhili binafsi na Watendaji wengine ikiwa pamoja na Sekta Binafsi na Taasisi za Kidini ambazo zimesaidia katika upatikanaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira na kuboresha mazingira.

BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA -AfDB KUSHIRIKI UJENZI WA RELI YA KATI YA KISASA TANZANIA



Afisa Mwandamizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Said Nyenge (kulia) akimuongoza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro, alipowasili Wizara ya Fedha na Mipango kukutana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), Jijini Dar es Salaam.




Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia) akisikiliza kwa makini maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (hayupo pichani) kuhusu ushirikiano mzuri na Benki hiyo katika Maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (hayupo pichani) alipokutana naye ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia), akiishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika, AfDB, kwa namna inavyoshirikiana na Tanzania kukuza uchumi wake, wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayesimamia Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, akizungumza namna Benki yake itakavyofadhili ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwando cha Kimataifa (Standard gauge) pamoja na kuhuisha Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania-TANESCO, alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani), Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, anayehudumia Kanda ya Afrika, Dkt. Nyamajeje Weggoro (katikati) akimwonesha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), zawadi ya picha, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao, Jijini, Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (kushoto) na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kushoto) na Afisa Mwandamizi toka AfDB na Idara ya Fedha za Nje, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia) akiwa ameongozana na mgeni wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao, Jijini Dar es Salaam.

……………………………………………………………………

Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeahidi kushirikiana na Tanzania kujenga mradi mkubwa wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) kwa kuipatia mkopo wenye masharti nafuu.

Ahadi hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayesimamia kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji.

Dkt. Weggoro amesema kuwa Benki yake imeridhika na utendajikazi wa Serikali ya Awamu ya Tano ikiongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na hivyo kuifanya Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo kukubali kufanikisha ujenzi wa Reli hiyo kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Amesema kuwa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa ni muhimu kwa uchumi wa Taifa lakini pia kwa uchumi wa nchi za Maziwa Makuu kwa kuunganisha nchi kama vile Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na baadae itaunganishwa na Reli ya Kaskazini upande wa Kenya.

“Benki iko tayari na inasubiri Tanzania ilete mapendekezo ama maombi ili yafanyiwekazi, tutakaa pamoja ili tuone Benki itasaidia kiasi gani na Benki pia inaweza kuwatafuta wadau wengine tunaosaidiana nao katika miradi mikubwa kama hii” Aliongeza Dkt. Weggoro

Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (Standard gauge), yenye urefu wa kilometa 2,561 umepangwa kugharimu kiasi cha Dola bilioni 7.6 za Marekani, sawa na shilingi za Kitanzania Trilioni 16, awamu ya kwanza imeanza kujengwa kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro na baadae awamu nyingine zitafuata.

Aidha, Dkt. Weggoro amesema Benki yake itashirikiana na Serikali kuboresha utendajikazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) hasa upande wa muundo wake na madeni makubwa yanayolikabili shirika hilo ili liweze kuchangia ipasavyo ukuaji wa uchumi wa viwanda.

“Benki itatoa fedha ili kulifanya shirika hilo lifanyekazi kwa ufanisi zaidi, tunajadiliana na tutawashirikisha pia wadau wengine zaidi ili uamuzi wa Serikali wa kuifanya nchi iwe ya viwanda uweze kufanikiwa” Alifafanua Dkt. Weggoro

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kujaji, ameishukuru AfDB kwakuwa mshirika mkubwa wa kimkakati wa maendeleo kwa kusaidia miradi mbalimbali ikiwemo barabara, nishati ya umeme, kilimo na huduma za jamii.

Dkt. Kijaji amesema kuwa uwekezaji wa AfDB hapa nchini umefikia Dola bilioni 1.8 huku asilimia 74.5 za uwekezaji huo iko kwenye sekta ya miundombinu, ambapo barabara imechukua asilimia 51.4, Nishati (10.1%), Maji na Usafi wa Mazingira (13%) na Sekta nyingine za huduma za jamii, kilimo na masuala ya fedha (25.5%).

Amesema kuwa uamuzi wa Benki hiyo kuamua kusaidia ujenzi wa mradi mkubwa wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) pamoja na kuihuisha TANESCO ni hatua muhimu itakayochochea ukuaji haraka wa uchumi wa nchi.

Ameitaja miradi mingine ya kimkakati iliyotekelezwa kupitia msaada na mkopo nafuu kutoka Benki hiyo kuwa ni ujenzi wa barabara ya lami inayoanzia Afrika Kusini-Cairo-Misri-Tanzania, kuanzia mkoani Iringa, Dodoma hadi Babati mkoani Manyara, inayotarajiwa kukamilika katika kipindi cha takriban miezi miwili ijayo.

KILA MTU KUWA NA BIMA YA AFYA-WAZIRI UMMY MWALIMU

Na chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa kiu yake katika sekta ya afya ni kuona kila mtu ana bima ya afya.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kadi ya Bima ya Afya kwa Mtoto ‘Toto Kadi’ , amesema kuwa taifa kuwa lina maendeleo linatokana na msingi wa afya  ambapo msingi huo unatokana  na kuwa watoto wanaopata huduma za afya kwa uhakika.

Amesema kuwa  gharama za kulipa matibabu katika ukuaji watoto na hali uchumi  ni kubwa lakini kuwepo kwa bima hiyo kutanya wazazi kuwa na  furaha wakati wote hata ikitokea ugonjwa bima ndio inamaliza matatizo.
Ummy amesema kuwa wakati  anaingia madarakani alikutana na Rais Dk. John Pombe  Magufuli  alichoendanacho ilikuwa ni kuongeza ghrarama lakini Rais alisema hakuna kuongeza ghrama yeyote cha msingi waangalie jinsi ya kusaidia watanzania kuwa na bima.

Aidha Waziri  Ummy amewaomba Mfuko wa  Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)  kuja na bima ya mama mjamzito itakayotumika wakati ujauzito na badaa ya kujifungua.

Ummy amesema kuwa kampeni hiyo iwe endelevu kwa nchi nzima ili watoto wote kuwa na bima ya afya hapo tutakuwa tunajenga taifa lenye msingi bora wa afya.Waziri  huyo ameitaka kuweka utaratibu wa kubandika mabango katika kila kumbi za starehe ili wanavyotumia vinywaji waweze kuangalia watoto kama wana kadi ya afya bima ya afya.

Nae Mwenyekiti wa Bodi NHIF, Anne Makinda amesema kuwa wanafanya kazi nguvu kuhakikisha watanzania wanapata huduma za afya  pamoja na kulipa watu wanaotoa huduma kwa bima ya afya.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa bima ya afya ya Mtoto 'Toto Kadi' leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiangalia muundo wa kadi ya bima ya afya ya Mtoto mara baada ya kuzindua leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akipeana Mkono na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda  mara baada ya kuzindua bima  kadi ya bima ya afya kwa watoto leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda akimpa kadi Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa NHIF, Bernad Konga ,mara baaya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuzindua kadi ya afya ya Mtoto leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza katika uzinduzi wa bima ya afya kwa mtoto katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga akizungumza juu ya mpango wa bima ya afya ya Mtoto katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza juu ya bima ya afya kwa mtoto katika jiji la Dar es Salaam wakati uzinduzi wa bima hiyo katika viwanja vya mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima akizungumza juu ya mkakati wa wizara katika utekelezaji wa bima ya afya.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  akipata maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga akimpa maelezo katika banda la NHIF.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  akingalia jinsi maafisa  wa NHIF wanavyofanya kazi katika usajili kadi ya bima ya afya kwa Mtoto.  
Sehemu ya wawakilishi mbalimbali wa Sekta ya Afya na Jamii pamoja na watendaji wa NHIF  katika uzinduzi wa bima ya Afya kwa Mtoto.
Baadhi ya wananchi wa watoto wakiwa katika uzinduzi wa bima ya afya ya Mtoto katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Watendaji mbalimbali katika uzinduzi wa bima ya afya ya mtoto.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi wa NHIF, Anne Makinda (Kulia) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernad Konga.

Balozi wa Toto Kadi, Mrisho Mpoto akitumbwiza wakati wa uzinduzi wa kadi hiyo.
Mrisho Mpoto akishukuru baada ya kupewa ubalozi.


Wakicheza katika uzinduzi  wa bima ambayo ni bima ya afya ya Mtoto katika viwanja vya  Mnazi mmoja 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa na Watoto waliopata Kadi ya Bima ya Afya ya Mtoto.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiangalia muundo wa kdi ya bima ya afya hya mtoto.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimpa kadi mtoto mara baada ya kuzindua bima ya afya ya Mtoto.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  akiwa katika picha ya pamoja watendaji wa NHIF.




Picha mbalimbali katika uzinduzi bima ya afya ya mtoto