Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (wa pili kulia) na Meneja Masoko
wa mafuta ya Ndege Puma Tanzania, Illuminata Yateri (katikati)
wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino wa Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL) Josephat Kagirwa (kulia) alipokuwa akizungumza na
wanafunzi kutoka Shule za Msingi wilayani Kisarawe walipofanya ziara ya
mafunzo uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni adhimisho la
mradi ujulikanao kama Sky is the limit.
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (wa pili kulia) akizungumza na
wanafunzi wa shule za msingi kutoka wilaya yake wakati wa ziara ya
kimafunzo kutembelea karakana ya ndege jijini Dar es Salaam jana kwa
kushirikiana na Kampuni ya Puma Energy Tanzania katika kuhudumia utoaji
wa mafuta ya ndege chini ya mradi ujulikanao kama Sky is the limit.
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, Meneja Masoko wa mafuta ya Ndege
Puma Tanzania, Illuminata Yateri na wanafunzi wa Shule za Msingi
wilayani Kisarawe, wakiingia kwenye Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania
(ATCL), walipofanya ziara ya kimafunzo katika mradi wa Sky is the limit
kwenye uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam (JNIA) jana.
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akimfunga vifungo mmoja wa
wanafunzi wakati walipofanya ziara katika uwanja wa ndege wa JNIA katika
mradi mradi ujulikanao kama Sky is The Timit
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, Meneja Masoko wa mafuta ya Ndege
Puma Tanzania, Illuminata Yateri na wanafunzi wa Shule za Msingi
wilayani Kisarawe, wakimsikiliza Injinia wa Ndege kutoka Shirika la
Ndege Tanzania (ATC), Nkhambi Salanga walipofanya ziara ya kimafunzo
katika mradi wa Sky is the limit katika uwanja wa ndege jijini Dar es
Salaam jana.
KAMPUNI
ya Mafuta ya Puma Energy (T) LTD kwa kushirikiana na Kampuni ya Air
Tanzania Limited imezindua mradi unaojulikana kama “Sky is the Limit
Project”wenye lengo la kuwatambulisha na kuwapa uelewa wanafunzi wa
shule za msingi wasio na fursa au uwezo wa kuufikia kwa urahisi
ulimwengu wa anga ili kuwapa uelewa kuhusu sekta hiyo yenye kuvutia.
Imeelezwa
lengo la mradi huo ni kuwahamasisha watoto wanaotoka mazingira ya
kawaida sana ya vijijini kwa kuwatia moyo katika masomo yao ili wajue na
kuvutiwa na sekta ya anga na maeneo mengine ya fursa za kazi za nje ya
maeneo wanaoishi.
Katika
kufanikisha mradi huo zaidi ya wanafunzi 40 kutoka Shule za msingi za
wilayani Kisarawe wamepata fursa ya kutembelea Shirika la Ndege la Air
Tanzania pamoja na kushuhudia namna Kampuni ya mafuta ya Puma
inavyohifadhi mafuta ya ndege katika Uwanja wa Ndege Terminal One jijini
Dar es Salaam.
Meneja
Masoko wa Mafuta ya Ndege Tanzania kutoka kampuni ya Mafuta ya Puma
Illuminata Yateri amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa kama neon
linavyojieleza la Sky is the Limit , mradi huo unataka kuamsha moyo wa
ujasiri na kujiwekea malengo ya juu katika kufanikiwa.
Amefafanua
mradi huo wa Sky is the limit utawapa wototo kutoka shule za msingi
waliochaguliwa kutoka kwa jumuiya zisizo na fursa na uzoefu wa sekta ya
anga kwa ukaribu zaidi, kwa kufanya ziara ya elimu inayofanywa katika
miundombinu ya uwanja wa ndege kama ugavi wa mafuta ya ndege,huduma
zinazotolewa kwenye ndege ,udhibiti wa safari za ndege, kupata habari
mbalimbali za ndege kupitia watalaam wa sekta ya ana wanaohusika.
“Watoto
watajua shughuli za kampuni ya mafuta ya Puma kuhusu biashara ya mafuta
ya ndege jinsi yanavyouzwa kwenye ndege za ndani na za
kimataifa.Kampuni ya Puma Tanzania ambayo ndio inayoongoza katika soko
la kuuza mafuta ya ndege nchini imekuwa mshirika wa muda mrefu katika
sekta ya anga katika kuunga mkono maendeleo ya kiuchumi ya Serikali ya
Awamu ya Tano.
“Pia
watoto watapata fursa ya kujua biashara ya kampuni ya ndege Tanzania
–Air Tanzania “The wings of Kilimanjaro” kwa kutembelea kituo cha
matengenezo ,kupata habari na kufahamu vizuri kuhusu juhudi zake za
kuchangia uchumi wan chi kwa njia ya usafiri wa anga,”amesema Yateri na
kuongeza kuwa idadi ndogo ya wanafunzi watapata fursa ya kupanda ndege
kwa safari fupi ambayo inajumuisha majadiliano kutoka kwa rubani na
wafanyakazi wa ndege katika siku za mbele.
”Tunashukuru
mamlaka ya Kisarawe chini ya uongozi wa Mkuu wa Wilaya hiyo Jokate
Mwegelo,Ofisa elimu Wilaya ya Kisarawe pamoja na walimu husika kwa
msaada wa kupata wanafunzi hawa ambao leo hii wamejifunza kwa
vitendo.Puma tutaendelea kushirikiana na walimu wa shule mbalimbali
nchini katika kuhakikisha tunashiriki kuwahamsisha wanafunzi kupenda
masomo ya sayansi na mwisho wa siku kuongeza wataalam wa mafuta ya ndege
na mambo ya anga,”amesema.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema kuwa
anaishukuru Kampuni ya Puma kwa kushirikiana na Air Tanzania kwa kandaa
mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya wanafunzi hao na kwamba hatua hiyo
inaonesha namna ambavyo wamedhamiria kuunga mkono juhudi za Rais
Dk.Magufuli katika kubooresha sekta ya anga nchini.
“Tumeona
juhudi za Rais wetu mpendwa katika kuboresha sekta ya anga.Kitendo cha
kuleta wanafunzi kujifunza kwa vitendo kuhusu masuala ya anga na mafuta
ya ndege maana yake ni moja tu tunakwenda kuhamasisha vijana wa Tanzania
kupenda masomo yanayohusu mafuta na anga.Tumepata taarifa kutoka Puma
kwa mhandisi wa mafuta ya ndege nchini Tanzania yupo mmoja tu na
anakaribia kustaafu, hivyo ujio wanafunzi hawa ni fursa nyingine ya
kuwahamasisha na hatimaye kuwa na wahandisi wengi wa mafuta ya
ndege,”amesema Jokate Mwegelo.
No comments:
Post a Comment