Saturday, November 10, 2018

TAKUKURU WATAJA WAFANYABIASHARA WANAOFANYA UDANGANYIFU KATIKA BIASHARA.

 Na.Khadija Seiif,Globu ya jamii.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wametaja makosa  ya baadhi ya wafanyabiashara nchini ambao wanajihusisha na udanganyifu kupitia matumizi ya mashine za Kieletroniki (EFD).

Naibu Mkurugenzi wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo akizungumza na wanahabari amesema Kodi ndio chanzo cha mapato kwa taifa lolote na Kodi hiyo inayotumika kuboresha huduma za kijamii na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Mbungo amefafanua zaidi kuwa TAKUKURU imeendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla waliojitokeza maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa wafanyabiashara kupitia magari ya matangazo maeneo ya Kariakoo,Buguruni,Gongo la Mboto,Tabata,Ilala,Mwenge,Tegeta na Tandika.

Vilevile wachunguzi kutoka taasisi hiyo waliendelea katembea maeneo tajwa na kufanya uchunguzi kujua iwapo bado kuna wafanyabiashara wanaokaidi maelezo hayo ya matumizi sahihi ya kisiti zinazotolewa na mas8hine za EFD na kuendelea kufanya udanganyifu.

Aidha,Mbungo ameeleza katika zoezi hilo wamebaini makosa ya udanganyifu ikiwemo wafanyabiashara wanaotoa risiti zenye kiasi tofauti na kiasi cha pesa halisi kilichotolewa ili kununua bidhaa husika, baadhi ya wafanyabiashara hawatoi kabisa risiti za kielekroniki baada ya kufanya mauzo. 

Na kwa upande mwingine Taasisi ya kuzuia na kupamabana na Rushwa(TAKUKURU) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) watawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kuendelea na tabia hiyo ya udanganyifu wenye lengo la kuikosesha serikali yetu mapato.

 Na kwa wanunuzi kuepuka udanganyifu huo kupita baadhi ya Wafanyabiashara ambao bidhaa na stakabadhi havilandani hivyo waepuke kupokea stakabadhi hizo na kwa sasa baadhi ya wafanyabiashara wameanza mahojiano kama vile Masai Shop,Malya Shop,Kanda Trading Company,Kiwanso builders corner,Kipata cafeteria, Mchapa kazi home appliance .


Naibu Mkurugenzi waTaasisi ya kuzuia na kupamabana na Rushwa (TAKUKURU)  Brigedia Jenerali John Mbungo amewataja baadhi ya wafanyabiashara nchini ambao wanajihusisha na udanganyifu kupitia matumizi ya mashine za Kieletroniki (EFD). 

No comments:

Post a Comment