Friday, January 26, 2018

Wizara ya Maliasili na Utalii kuikarabati nyumba ya Nyerere Magomeni-Dk Kigwangalla

Wizara ya Maliasili na Utalii kuikarabati nyumba ya Nyerere Magomeni-Dk Kigwangalla Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla (MB) mapema leo Januari 26,2018,amefanya ziara maalum katika Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda Namba 62, ambayo aliishi hapo miaka ya 1950's Dk. Kigwangalla ameweza kujionea mambo mbalimbali ndani ya makumbusho hayo huku pia akipokea maoni ya namna ya kufanyiwa maboresho ya kituo hicho ikiwemo ufinyu wa eneo la ofisi na maegesho ya wageni wanaotembelea hapo.

"Nimefika hapa leo kujionea Kituo hichi ambacho ni kielelezo kikubwa cha Mwasisi wa Taifa letu. Hapa pana hazina kubwa na kituo hiki kina mambo mengi sana ya kumuenzi Baba wa Taifa. Kwa hali tuliookuta kwa kweli tutakaa na timu yangu kuona tunafanya maboresho makubwa kabisa ili kiwe kama maeneo mengine yenye Wahasisi wa Mataifa yao, tumeona kama eneo alilozaliwa Mzee Mandela kule Afrika Kusini, nyumba yake imehifadhiwa vizuri na imekuwa na wageni wengi. Kwa hapa kwetu na sisi tutakaa na wenzetu kutatua changamoto hizi. 

Hapa tutajenga Maktaba ambapo watu watakuja kusoma vitabu vya Mwasisi wetu na kuona mambo aliyokuwa akifanya. Lakini pia tutaonana na Viongozi wa Halmashau ri ya Kinondoni kuona namna ya kupaboresha mahala hapa ikiwemo miundombinu ya Barabara ya kuingia na kutoka eneo ili" alieleza Dk. Kigwangalla.

Pia aliongeza kuwa, kituo hicho kipo katika hali mbaya kikikabiriwa na changamoto licha ya kuwa ni kituo muhimu sana hapa nchini. hivyo amewahakikishia wahifadhi wa Makumbusho hayo mipango iliyopo ni pamoja na kukifanyia marekebisho kutengeneza choo, kupaka rangi pamoja na kufanyia ukarabati mkubwa vionyeshi vya kumbukumbu nzima ya Baba wa Taifa.

Aidha, amesema kuwa, lengo kwa sasa ni kuifanya nyumba hiyo iwe kama nyumba halisi ailivyokuwa akiishi mwenyewe Baba wa Taifa kwani ndani bado kuna vitu halisi alivyokuwa akivitumia Mwasisi mwenyewe huku pia mikakati ni pamoja na kununua hata nyumba za jirani ili kuongeza eneo na kuongezwa baadhi ya ofisi na pawe na hadhi kama Mwasisi mwenyewe" alieleza Dk.Kigwangalla. 

  "Kiukweli nimefika hapa kushuhudia makumbusho haya ambayo kiuhalisia hapa ni hazina kubwa sana ya kumbukumbu ya Taifa letu hasa katika harakati za kupigania Uhuru pia zilianzia hapa katika nyumba hii. Pia tutaboresha zaidi kwa kuweka studio maalumu ambayo pia tutaboresha CD zote za Baba wa Taifa zitakuwa zikioneshwa humo ikiwemo zile za Hotuba.Awali Muhifadhi Mkuu wa Makumbusho hayo, Bi. Neema Mbwana alieleza changamoto zinazoikabili kituo hicho pamoja na kuomba kuboreshwa kwa vitu muhimu ikiwemo Ukarabati wa nyumba nzima, ikiwemo, paa na kupaka rangi. 

  Aidha, waliomba kuboreshewa vionyeshwa ikiwemo kujengea vioo katika kuta za vionyeshwa, kuzitengeneza picha katika fremu kitalaamu. Mhifadhi huyo aliendelea kusema kuwa, kwa umuhimu wa vitabu ambavyo hakuna nakala zake halisi ambavyo ni mali za Baba wa Taifa, walimuomba Waziri awachapishie tena nakaza zaidi ili ziweze kutumika kwa miaka mingi zaidi kwani vilivyopo vimezidi kuchakaa. 

  Mbali na kutembelea Makumbusho hayo ya Nyumba ya Baba wa Taifa hiyo ya Magomeni, Dk. Kigwangalla pia aliweza kutembelea soko kubwa la Vinyago lililopo Mwenge na kujionea wachngaji vinyago hao ambao ni kiungo muhimu cha Utalii hapa nchini hata hivyo alikutana na kero juu ya Watalii kusumbuliwa Viwanja vya ndege kwa bidhaa zao hizo za vinyago.
Muhifadhi Mkuu wa Makumbusho nyumba ya Nyerere iliyopo Magomeni Jijini Dar es Salaam,Bi. Neema Mbwana akisoma taarifa za kituo hicho kwa Waziri Dk Kigwangalla alipotembelea kituoni hapo mapema leo Januari 26,2018.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Kigwangalla akisaini kitabu cha Wageni alipowasili kituoni hapo
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Kigwangalla akitambulishwa wafanyakazi wa kituo hicho
Dk. Kigwangalla akitazama baadhi ya vitabu vya Mwalimu Nyerere ambavyo vimehifadhiwa nyumbani hapo
Dk. Kigwangalla akitazama baadhi ya picha mbalimbali za Baba wa Taifa ambazo zipo nyumbani hapo
Mhifadhi Mkuu Neema Mbwana akimuonesha Dk. Kigwangalla moja ya makochi aliyokuwa akiyatumia Baba wa Taifa wakati akiishi hapo
Dk. Kigwanglla akiangalia moja ya chungu cha shaba alichokuwa akitumia Mwalimu Nyerere katika nyumba yake hiyo ya Magomeni
Dk. kigwangalla akiangalia moja ya pasi ya mkaa aliyokuwa akitumia Baba wa Taifa wakati akiishi nyumbani hapo
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya vitanda vilivyokuwa vikitumiwa na watoto wa Baba wa Taifa wakati akikaa hapo. (Chumba cha watoto wa Baba wa Taifa walitumia)
Dk. Kigwangalla akiangalia kitanda alichokuwa akikitumia Baba wa Taifa wakati akiishi kwenye nyumba hiyo
Mhifadhi Neema Mbwana akimuonesha Waziri Dk. Kigwangalla nyuma ya nyumba hiyo na eneo lilivyo
Eneo la nyuma ya nyumba hiyo kama linavyoonekana
Akiwa katika Eneo la Vinyago Mwenge, Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kushuhudia baadhi ya bidhaa hizo ambazo pia zimekuwa ni kielelezo kikubwa cha watalii
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya kinyago cha Umoja abacho kinaelezea taswira mbalimbali ikiwemo hali ya uhifadhi wa hifhadhi za Taifa katika nyanja za Ulinzi wa wanyama
 
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya vinyao vyenye umbo tofauti ambavyo vimekuwa vikitumika sana katika maofisi za Serikali na mashirika ikiwemo Balozi
Dk.Kigwangalla akiwa anatembelea baadhi ya mabanda ya wachongaji vinyago hao
Dk.Kigwangalla akiangalia moja ya kinyago kikubwa chenye taswira ya Kimbunga
 
Mkurugenzi wa Mipango na matumizi endelevu ya misitu na nyuki nchini, Mohamed Kilongo (kulia) akimwelezea jambo Waziri Dk.Kigwangalla namna wanavyoshughulikia suala la Wachongaji vinyago hao haswa katika vibali vya miti
Dk.Kigwangalla akimsikiliza kwa makini mmoja wa wachonga vinyago ambao walilalamikia hali ya kutozwa kwa gharama kubwa katika viwanja vya ndege hasa kwa wageni ambao asilimia kubwa ni watalii
 
Dk.Kigwangalla akitoa maelekezo kwa viongozi wa Wachonga Vinyago Mwenge kukaa pamoja ili kuona watakavyoelewana namna ya kumiliki eneo hilo huku akiahidi kushughulikia suala la bidhaa zao zinazotozwa ushuru mkubwa viwanja vya ndege vya hapa nchini
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya michoro ya picha katika eneo la Tingatinga lililopo Oyster bay Jijini Dar es Salaam.
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya michoro ya picha katika eneo la Tingatinga lililopo Oyster bay Jijini Dar es Salaam.
 
Dk. Kigwangalla akiangalia moja wachoraji wakongwe wa Umoja wa michoro ya Tingatinga alipotembelea kujionea michoro hiyo eneo la Oyster bay Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE

No comments: