Friday, January 26, 2018

Waziri Ummy Mwalimu afungua CT-Scan hospitali ya Bugando

Na WAMJWW.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB)  ameahidi kuwaletea mashine ya uchunguzi ya MRI katika hospitali ya rufaa ya kanda ya ziwa Bugando mwaka huu.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati akifungua mashine ya  CT-scan ambayo itakua inapima magonjwa mbalimbali iliyogharimu shilingi za kitanzania bilioni 1.6 ambazo zinetokana na vyanzo mbalimbali vya mapato vya hospitali hiyo.

Aidha,Waziri Ummy ameahidi ndani ya miaka mitatu kuanzisha taasisi ya moyo ili kuweza kupunguza gharama kwa wananchi wa kanda ya ziwa na magharibi wanaopata matatizo ya moyo kwenda kupata vipimo na matibabu kwenye taasisi ya moyo ya  JKCI ya jijini Dar es Salaam.

 Waziri Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria ufunguzi wa  CT-Scan kwenye hospitali ya Bugando,kulia ni Baba Askofu wa Kanisa katoriki jimbo la Geita Flavian Kasala na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.
 Waziri Ummy mwalimu akiongea na watumishinwa hospitali ya rufaa ya kanda ya ziwa ya bugando wakati wa uzinduzi wa mashine ya CT-scan.
 Mkurugenzi wa hospitali ya rufaa ya bugando dkt.Abel Makubi akitoa shukrani mara baada ya uzinduzi wa mashine hiyo.
 Mtaalamu wa Mionzi wa hospitali ya Bugando akimpatia maelezo Waziri wa Afya mara baada ya ufunguzi wa mashine hiyo
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB) akiwajulia hali wagonjwa waliofika hospitalini hapo kupata matibabu.
 Waziri Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa Hospitali hiyo kwenye kitengo cha Saratani hospitalini hapo.
 Waziri Ummy Mwalimu akiongea na Mzee Juma Salumu kutoka tabora aliyefika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu ya masikio.Waziri amewahakikishia serikali ipo mbioni kuboresha huduma za kibingwa katika hospitali ya mkoa ya Tabora ili kupunguza gharama kwa wananchi.

Mashine ya CT-scan iliyogharimu shilingi za kitanzania bilioni 1.6

No comments: