Sunday, December 24, 2017

WAZIRI JAFO AHAIDI KULIVALIA NJUGA SUALA LA WAKANDARASI NCHINI AMBAO NI WAZEMBE KATIKA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Selemani Jafo akikagua daraja la Gologombe ambalo limejengwa katika kata ya mafizi wakati alipofanya ziara yake ya kikazi ya siku moja Wilayani Kisarawe kwa ajili ya kuweza kutembelea miradi mbali mbali ya maenedeleo na kujione a changamoto zilizopo.
Waziri Jafo baada ya kutembelea mradi wa shule ya msingi Mtengwe ambayo kwa sasa inafanyiwa ukarabati wa baadhi ya madarasa ambayo yalikuwa yapo katika hali mbaya kutokana na uchakavu wa miundombinu yake.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Seleman Jafo wa kulia akitoka kukagua mradi wa bwawa kubwa la kuhifadhia maji lililopo kata ya Chole ambalo litaweza kuwanufaisha wakazi wa eneo hilo na maeneo mengine ya jirani kuweza kupata huduma ya maji.PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU


NA VICTOR MASANGU, KISARAWE 

WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ameahidi kulivalia njuga suala la baadhi ya wakandarasi hapa nchini ambao ni wazembe na wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati waliopangiwa ikiwemo sambamba na watendaji wavivu ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha juhudi za seriklali ya awamu ya tano katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi na badala yake watachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani.


Jafo ametoa kaui hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja katika Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, miundombinu ya barabaraba, afya pamoja na sekya sambamba na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi ii kuweza kusisikiliza na kizitafutia ufumbufu wa kudumu.


Alisema kwamba alibaini kuna wakandarasi wengine wanapewa kazi lakini cha kushangaza wanakamilisha mradi ambao unajengwa chini ya kiwango kinachotakiwa hivyo amesema kamwe hawezi kulifumbia macho suala hilo na kuongeza kuwa atakayebainika amehusika kuhujumu miradi hiyo atafikishwa mahakamani pamoja na kufukuzwa kazi ii iwe fundisho kwa wengine.


Hata hivyo katika hatua nyingine Jafo aliwatoa wasi wasi wananchi wa Kisarawe, Mkoani Pwani kuimaliza changamoto sugu ya iliyodumu kwa kipindi cha muda mrefu cha ukosefu wa upatikanaji wa huduma ya maji ambapo amebainisha serikali ya awamu ya tano imetenga kiasi cha shilingi bilioni 10 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji ambao chanzo chake kitaanzia mto Ruvu na kusambazwa katika maeneo mbali mbali ya Kisarawe.


“Kuhusiana na changamoto hii ya wananchi wa kisarawe juu ya tatizo la ukosefu wa maji kwa kipindi kirefu nadhani sasa linakwenda kufikia mwisho kwani serikali imeshatenga bilioni 10 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi wa maji ambao utaanzia kutokea mto Ruvu hivyo nipende kuwahakikishia kuwa tatizo hilo linakwenda kufikia mwisho na wananchi wataweza kupata maji ya uhakika,”alisema Jafo.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Hamis Dikupatile amesema kwamba kukamilika kwa baadhi ya miradi mbali mbali hususan wa kivuko cha daraja la Gologombe kutakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi ambao hapo awali walikuwa wanapata adha kubwa ya kuvuka hasa katika kipindi cha masika na kushindwa kufanya shughuli zao za kimaendeleo.


“Kwa kweli hapo awali wananchi wetu walikuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa sana ya usafiri, maana kuvuta ilikuwa wanapata tabu sana hasa katika kipindi cha mvua hivyo daraja hii litakuwa ni msaada mkubwa sana na wataweza kupata fursa za kuendelea kufanya shughuli zao mbali mbali za maendeleo, “alisema Mwenyekiti huyo.


Pia aliongeza kuwa ujenzi huo wa kivuko cha darala imegharimu kiasi cha shilingi milioni 127, ambapo kwa sasa limeshafikia hatua za mwisho, ambapo aliwaomba wananchi hasa wanatumia njia hiyo kuhakikisha kwamba wanaitunza miundombinu ya barabaraba ili iweze kudumu kwa kipindi cha muda mrefu bila ya kiharibika.


Akiwa katika ziara yake ya Kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Kisarawe Jafo ameweza kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo, ikiwemo miundombinu ya barabara, kukagua madaraja, shule za msingi, na sekondari ,vituo vya afya, pamoja na ujenzi wa bwawa la kutunzia maji lililopo katika kata ya chole.

No comments: