Sunday, December 24, 2017

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, JAPHET HASUNGA AMEIAGIZA TFS KUANZA MCHAKATO WA KUUNDA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA MISITU TANZANIA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akizungumza na  Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) makao makuu jijini Dar es Salaam jana . Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos Silayo
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Dkt. Ezekiel Mwakalukwa (kulia) akizungumza na Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) kuzungumza na Watumishi wa TFS makao makuu jijini Dar es Salaam jana .
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Dos Santos Silayo akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga baada ya kuzungumza na Watumishi wa TFS makao makuu jijini Dar es Salaam jana .
Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam. (Picha na Lusungu Helela-MNRTBaadhi ya Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati akizungumza nao jana jijini Dar es Salaam.
Picha na Lusungu Helela-MNRT


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ianze mchakato wa kuandaa sheria ya kutoka Wakala kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Misitu Tanzania ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa vile ikiendelea kubaki kuwa Wakala kuna baadhi ya mambo itashindwa kuyashughulikia

Wakala ni Idara za Serikali zilizoondolewa kwenye serikali kuu na zina nusu mamlaka na hazina mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yake zenyewe.Amesema uanzishwaji wa Mamlaka hiyo itasaidia kupunguza migongano kati ya misitu iliyo chini ya Tamisemi pamoja na vijiji kwa vile kutakuwa na Mamlaka moja ya kusimamia misitu tofauti na ilivyo sasa.

Ameyasema hayo jana wakati akizungumza na Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzani (TFS) makao makuu jijini Dar es Salaam.Amesema TFS kwa hatua iliyofikia kwa sasa haistahili kuwa Wakala kutokana na kazi kubwa iliyonayo hivyo inahitaji kuwa Mamlaka ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa uhuru zaidi.

Wakati akizungumza na Watumishi, Naibu Waziri Hasunga amemtaka Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos Silayo ahakikishe katika mpango mkakati utakaoandaliwa hivi sasa suala la uanzishwaji wa Mamlaka lipewe kipaumbele.Katika hatua nyingine, Ameiagiza TFS iunde chombo cha kusimamia na kudhibiti ubora wa mazao ya misitu.

Amesema chombo hicho kitakuwa kikipanga mazao ya misitu kulingana na ubora wake na sio kama sasa inavyofanyika mbao zozote zile zimekuwa zikiuzwa sokoni pasipo kujali ubora wake.Amesema kuna changamoto ya bei za mbao sokoni na pia kuna changamoto ya ubora wa mbao zilizoko sokoni, Mbao nyingi zimetengenezwa kwa miti ambayo imevunwa ikiwa na miaka sita au kumi ni lazima ubora wake uwe hafifu.

‘’ Halafu unaenda kumshindanisha na mtu anayeuza mbao ambazo miti yake imevunwa ikiwa na miaka 18 haziwezi kushindanishwa ubora kati ya mbao hizo lazima kiwepo chombo cha kuthibiti kama vile kwenye chakula kuna TFDA na kwenye bidhaa kuna TBS’’ alisema

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Hasunga amemtaka kila mtumishi ahakikishe anapambana na rushwa kwa kumuagiza Mtendaji Mkuu wa TFS Prof. Silayo kuwahamisha watumishi pale inapotokea fununu kuwa mtumishi fulani anajihusisha na rushwa hata kama bado haijathibitika kwa vile fununu hizo haziwezi kuanza tu bila ya kuwa harufu ya mazingira ya kupokea rushwa yanayotengenezwa.

Amesema katika suala la ugawaji wa vitalu kuna vitendo vya rushwa vinafanyika kwani baadhi ya watu wanapewa vibali vya kuvuna kwa muda wa miezi minne lakini uvunaji ule unaendelea kwa muda wa mwaka mmoja wakati ilitakiwa kitalu hicho kivunwe kwa muda wa wiki mbili tu.’’ Alisema

‘’Mimi sikurupuki kwenye maamuzi yangu na sio kwamba nasema nimekuja kuwatumbua leo lakini nina taarifa nyingi kuhusiana na rushwa inavyotembea katika ugawaji wa vitalu’’‘’Mtendaji ifanyie kazi taarifa hii ya rushwa ila nikiona mambo hayaendi kama ninavyotarajia nitakuja kivingine. alisisitiza

Katika hatua nyingine , Naibu Waziri Hasunga ameiagiza TFS iongeze ukusanyaji wa mapato kwa vile mapato yalipo sasa bado hayatoshelezi na yaliyokusanywa yatumike vizuri.‘’Taarifa nilizonazo kuna maeneo manne mapato yanavuja paangalieni hapo mparekebishe ‘’ alisema

Wakati huo huo, Hasunga ameiagiza TFS ianze kuwekeza katika maeneo ambayo inaona inaweza kuzalisha zaidi kwa mfano kwenye maporomoko ya Kalambo ili iweze kuongeza mapato‘’Yale maporomoko ukikaa Zambia huwezi kuyaona vizuri ila ukikaa Tanzania unayaona vizuri’ tumieni fursa hiyo baada ya miaka miwili ijayo kinaweza kikawa kituo kikubwa cha utalii nchini.’’Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TFS, Dos Santos Silayo amemhakikishia Naibu Waziri Hasunga kuwa atatekeleza maagizo yake yote aliyoyatoa kwa maslahi mapana ya TFS.

No comments: