Serikali imeiagiza Mamlaka ya Reli ya Tanzani na Zambia (TAZARA), Kampuni Hodhi
ya Rasilimali za Reli (RAHCO) na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), zianze
kubomoa nyumba zote zilizojengwa kwenye hifadhi ya reli na barabara kuu zote nchini
ili kuilinda miundombinu hiyo isiharibiwe.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa mkoani Mbeya mara baada ya kukagua Daraja la Reli ya Tazara lililopo
Mbalizi nje kidogo ya mji huo na kusisitiza umuhimu wa wananchi kulinda miundombinu
“Sheria iko wazi, lazima muisimamie msisubiri mpaka Waziri aseme. Mwananchi
yeyote aliyeifata miundombinu ya reli lazima mmvunjie nyumba yake ili miundombinu
iliyojengwa kwa kutumia fedha nyingi iweze kudumu”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Meneja wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Mkoa wa Mbeya Bw. Fuad Abdallah akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu uharibifu wa Daraja la Reli ya TAZARA eneo la Mbalizi Mkaoni Mbeya kutokana na shughuli za kibinadamu, alipotembelea daraja hilo leo.
Prof. Mbarawa amesema Serikali ipo katika hatua za kuboresha miundombinu ya reli ya
kati na reli ya Tazara ili kuhakikisha mizigo yote ya ndani na nje ya nchi inayopitia
kwenye bandari ya Dar es Salaam na kupita katika barabara inapita katika reli.
“Mizigo inayopita katika reli ni asilimia 4 tu kutoka bandarini hivyo lazima tujipange
kuanza kutafuta masoko na kuchukua mizigo hiyo ili kulinda miundombinu ya barabara
inayoharibiwa na uzito mkubwa”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na ukaguzi wa karakana ya Mbeya.
Aidha Waziri Prof. Mbarawa ameuhimiza uongozi wa TAZARA kuongeza juhudi katika
utoaji elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya uchimbaji mchanga, kokoto kwenye
hifadhi ya miundombinu ya reli hasa kwenye mito na chini ya madaraja ili kuzuia
uharibifu kuhatarisha usalama wa usafiri wa treni.
Naye Meneja wa TAZARA wa mkoa wa Tanzania Bw. Fuad Abdallah amemueleza
Waziri Mbarawa zoezi la kubomoa nyumba litatekelezwa kama sheria ya reli
inavyosema kwa wananchi kuacha ya mita 30 kwa vijijini na mita 15 kwa mjini.
Ameongeza kuwa mamlaka itaendelea kutoa elimu ya utunzaji wa miundombinu ili
wawe sehemu ya utunzaji kwa kuacha kufanya shughuli zao kwenye maeneo hayo.
Katia ziara hiyo, Waziri Prof. Mbarawa amekagua pia Karakana ya TAZARA ya Mbeya
ambayo inatoa huduma ya matengenezo ya vichwa vya treni 39 aina ya Diesel Electric
(DE) pekee na kubaini ukosefu wa baadhi ya mitambo, uchakavu wa mitambo iliyopo na
ukosefu wa vipuri.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua
mashine ya kichwa kimojawapo cha treni wakati alipokagua ukarabati wa vichwa hivyo
katika karakana ya Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na
mmoja wa abiria wakati alipokagua huduma za Mamlaka ya Reli ya Tanzania na
Zambia (TAZARA).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na
wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA), (hawapo pichani)
wakati alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani Mbeya.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA)
wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
(hayupo pichani), wakati alipozungumza nao, Mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisikiliza maoni
kutoka kwa wakazi wa Lyunga, Mbeya mara baada ya kumaliza kuongea na
wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) Mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisikiliza maoni
kutoka kwa wakazi wa Lyunga, Mbeya mara baada ya kumaliza kuongea na
wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) Mkoani Mbeya.
No comments:
Post a Comment