Tuesday, April 5, 2016

Serikali yahidi kuboresha usikivu wa shirika la utangazaji la taifa Mikoa ya pembezoni

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Zelote Stephen (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Mathew Sedoyeka (kushoto) wakiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye baada ya kuwasili katika Mkoa wa Rukwa jana kuzungumza na wadau wa sekta anazosimamia. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa CCM Mkoa wa Rukwa jana wakati wa ziara yake mkoani humo kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia. Kushoto kwa Waziri ni Mwenyekiti wa CCM Rukwa Bw. Hypolitus Matete
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelekezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kanda TBC nyanda za juu kusini Bw. Hosea Cheyo baada ya kukagua minara ya digitali ya kupitishia matangazo jana Mkoani Rukwa. Watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Zelote Stephen na wakwanza kushoto ni Meneja wa TCRA Kanda ya nyanda za juu kusini Eng. Lilian Mwangoka.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizugumza na watendaji kutoka Mkoa wa Rukwa pamoja na wadau wa kada za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alipokutana nao jana Mkoani hapo kujadili mambo mbalimbali katika sekta hizo pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa mawasiliano.
 Baadhi ya watendaji kutoka Mkoa wa Rukwa pamoja na wadau wa kada za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) alipofanya ziara yake jana Mkoani Rukwa  kujadili mambo mbalimbali pamoja na kukagua ofisi za TBC na kutoa vitendea kazi kwa Maafisa Mawasiliano wa Mkoa wa Rukwa. 
 : Mwamuzi na Mkufunzi wa mchezo wa netibali Mkoa wa Rukwa Bibi. Louisa Monji akichangia wakati wa kikao na  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipofanya ziara katika mkoa huo jana kujadili mambo mbalimbali pamoja na kukagua ofisi za TBC na kutoa vitendea kazi kwa Maafisa Mawasiliano wa Mkoa wa Rukwa. 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiikagua iPad kabla ya kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Zelote Stephen (kushoto) kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi kwa maafisa mawasiliano waliopo Mkoani hapo. Mhe. Nnauye alikabidhi iPad tatu kwa Mkoa wa Rukwa jana baada ya kufanya ziara fupi na kuonana na wadau wa sekta anazozisimamia.
 : Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Kimanta akitoa taarifa fupi kuhusu sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  kwa Waziri wa sekta hizo Mhe. Nape Moses Nnauye alipofanya ziara Wilayani hapo jana Mkoani Rukwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza moja kwa moja kupitia radio ya Wilaya NKasi FM alipofanya ziara katika radio hiyo kuona mafanikio yaliyoletwa na Wilaya ya Nkasi kwa kuwa na radio ya Wilaya.
Picha na: Genofeva Matemu- Maelezo, Rukwa

No comments: