Thursday, August 29, 2013

Ziara ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein nchini Uholanzi


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamo wa Rais pia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya Rotterdam, Rene Van Der Plas,alipotembelea katika bandari hiyo  akiwa katika Ziara ya siku tano na ujumbe wake, nchini Uholanzi, {Picha na Ramadhan Othman Uholanzi].
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na ujumbe wake waliokaa wakipata maelezo kutoka kwa Makamo wa Rais pia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya Rotterdam, Rene Van Der Plas,walipotembelea katika Ofisi za Bandari hiyo  akiwa katika Ziara ya siku tano nchini Uholanzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) na ujumbe wake wakipata maelezo ya ramani ya Ujenzi wa Bandari na Mpango mzima wa utendaji kazi kutoka kwa Makamo wa Rais pia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya Rotterdam, Rene Van Der Plas,  alipotembelea katika Ofisi za Bandari hiyo  akiwa katika Ziara ya siku tano  nchini Uholanzi na ujumbe aliofuatana nao.
Baadhi ya Meli za Mizigo kutoka Nchi mbali mbali ikiwemo China,ni miongoni mwa Meli zinazotia nanga katika Bandari ya Rotterdam, Nchini Uholanzi kama inavyoonekana pichani ikiwa imesheheni makontena yenye Bidhaa mbali mbali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akiwa na wawakilishi wa Makampuni yanayotaka kuwekeza Zanzibar wakiwa katika mazungumzo ya kujadili nanama ya kufikia hatua za kuwekeza  Nchini,wakati alipokuwa katika ziara Nchini Uholanzi itakayochukua siku tano,ambapo atatembelea sehemu kadhaa za kimaendeleo katika nchi hiyo.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mitambo ya usambazji wa Gesi inayotumika katika nchi za ulaya,(GATE TERMINAL) Dick Meurs,alipokuwa akitoa maelezo kwa Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,ukioongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ziara nchini Uholanzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wawakilishi wa Makampuni wakati alipowasilim katika Chakula cha jioni kilichoandaliwa na Famili ya Mfalme panoja na makampuni nchini Uholanzi akiwa katika ziara ya siku tano nchini humo.

No comments: