Wednesday, August 14, 2013

TANROAD YAPANIA KUONDOA KERO YA MSONGAMANO WA MAGARI JIJINI MWANZA

Meneja wa TANROAD mkoa wa Mwanza Mhandisi Leonard Kadashi akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujenzi unaoendelea wa moja ya madaraja na hapa ilikuwa ni katika eneo la daraja la Mabatini jijini Mwanza, ambalo linajengwa sambamba na utanuzi wa barabara njia tatu kuondoa kadhia ya msongamano.
  
WAKALA wa Barabara Mkoa wa Mwanza(TANROAD) hatimaye imeanza utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete na serikali kwa kuanza mradi wa ujenzi wa barabara ya Lami ya Usagara hadi Kisesa yenye urefu wa kilomita 17.8 ili kupunguza msongamano wa magari makubwa na madogo kuingia Jijini Mwanza.

Meneja wa TANROAD Mkoa wa Mwanza Mhandisi Leonarld Kadashi alisema serikali baada ya kupata fedha ilitangaza kazi na kupatikana Mkandarasi aliyeshinda ambaye ni Kampuni ya kizalendo ya Nyanza Road Works Ltd ya Jijini Mwanza ambapo kwa sasa Mkandarasi huyo yupo kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa barabara hiyo ya Usagara-Kisesa ya kiwango cha lami.
 “Kazi imeanza tangu mwezi Julai mwaka huu na inaendelea kwa kasi na tayari Mkandarasi aliyopo kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa barabara hiyo  anaendelea na kazi ya kusafisha barabara ambapo kilomita 5 tayari na ujenzi wa madaraja sanjari na ujenzi wa nyumba za kambi ya Mhandisi mushauri na msimamizi na wafanyakazi wake kisha kuendelea na ujenzi wa kuweka lami”alisema
Mhandisi Kadashi alisema kwamba Rais Kikwete aliomba kufanyika mchakato wa kuanza ujenzi wa barabara hiyo ya Usagara-Kisesa wakati alipokuwa akifungua barabara ya Usagara-Kigongo kupitia Mjini Sengerema, Geita, Bukoba hadi Kigoma ya Lami mwaka 2011 na hivyo kuahidi kwa wananchi wa Wilaya za Misungwi na Magu ujenzi huo kwa kueleza kuwa ni lazima barabara hiyo ijengwe kwa kiwango cha lami.

 “Ujenzi wa barabara hii umeanza mwezi Julai mwaka huu na unaendelea na utasaidia magari yanayotoka barabara ya Usagara – Geita yenye urefu wa kilomita 90 na yale ya Kutoka njia ya Shinyanga-Mwanza yakielekea Mkoani Mara hadi nchi jirani ya Kenya kutolazimika kupitia katikati ya Jiji la Mwanza kwanza kabla ya kuendelea na safari zao,pia  kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi wa maeneo hayo. alisema Meneja.

Meneja, Kadashi alieleza kwamba mradi huo ulibuniwa na serikali, awali ulikuwa utekelezwe na Jumuiya ya Ulaya (EU) lakini walijitoa kuufadhili na kusababisha mradi kuchelewa kuanza kutokana na kukosa fedha na sasa mradi huu umepata fedha na unatekelezwa na Serikali kwa asilimia mia moja kupitia Wizara ya Ujenzi ambayo mbali na kugaramia ujenzi pia itawalipa fidia wananchi kwa kutumia taratibu za ndani wale watakaopitiwa na barabara hiyo.
“Wananchi wa maeneo hayo wasiwe na wasiwasi, serikali itawalipa fidia wananchi wote walio nje ya hifadhi ya barabara watakaoguswa na kupitiwa na mradi huo na uthamini unaendelea kwenye maeneo mengine yaliyobaki, lakini wale waliovamia na kufanya ujenzi ndani ya maeneo ya hifadhi ya barabara hiyo ya Usagara-Kisesa serikali haita walipa fidia na waanze kubomoa nyumba na vibanda vyao kwa mujibu wa sheria ili kuruhusu ujenzi wa mradi huo”alisisitiza
Mhandisi Kadashi alisema kwamba ujenzi wa mradi huo utagarimu shilingi bilioni 17.8 na unataraji kukamilika kwa kipindi cha miezi 15 kuanzia mwezi Julai mwaka huu ambapo tayari wananchi wameupokea na baadhi yao wameanza kuvunja nyumba na vibanda vyao baada ya kuwaelimisha kwenye mikutano ya hadhara na kuitambua sheria inavyoelekeza na viongozi wa vijiji wamekuwa wakitusaidia kuwaelimisha.
Uchimbaji udongo.
“Tuwashukuru wananchi kwa kukubali kuupokea mradi huo na kutuelewa, viongozi wa serikali za vijiji wamekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wao na kwa serikali pia hili ni jambo zuri na tuliwasihii sana wananchi kuacha kuwasikiliza wanasiasa waliokuwa wakiwahamasisha kukataa bila kujua faida ya kuwa na barabara ya kiwango cha lami sasa wajiandai kuitunza itakapo kamilika na kukabidhiwa”alisema.

Aidha Kadashi alisema kwamba mradi huo utakuwa na manufaa sana kwa Jiji la Mwanza kutokana na changamoto iliyopo ya musongamano wa magari makubwa ya mizigo na abiria kufika katikati ya Jiji na yale yanayopita kwenda maeneo mengine, barabara hiyo ikikamilika utakuwa umepunguza kwa kiasi kikubwa msongamano uliopo kwa sasa na kuwa njia ya mkato kwa kuelekea Magu na Misungwi na Kigongo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Fera kinachopitiwa na barabara hiyo Leonarld Mongo alisema kwamba wanaipongeza serikali ya awamu ya nne ya Rais Dkt. Kwa kutekeleza ahadi kwa vitendo ya ujenzi wa barabara hiyo kama ilivyowaahidi wananchi wa Wilaya hizo mbili na kutambua umuhimu wa kuwa kuwapatia maendeleo wananchi wake ikiwa na lengo la kuwarahisishia usafiri.
Ndani ya sehemu ambapo kumezungushiwa mabati pembezoni mwa barabara kwenye eneo linapo jengwa daraja la kivuko cha juu kwa waendao kwa miguu shughuli za ujenzi zinaendelea kusimika nguzo kuu shikizi za daraja.
Sehemu ambapo kunajengwa daraja la kivuko cha juu kwa waendao kwa miguu shughuli za ujenzi zinaendelea ndani, nao ujenzi ukitarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwaka 2014.

Sehemu ambapo kunajengwa daraja la kivuko cha juu kwa waendao kwa miguu shughuli za ujenzi zinaendelea ndani ya maeneo yaliyozungushiwa mabati, nao ujenzi ukitarajiwa kukamilika mwezi wa tatu mwaka 2014.
Upanuzi wa barabara ya Nyerere inayounganisha njia kuelekea Musoma mkoani Mara, unakwenda sambamba na utanuzi wa madaraja yote ya njia hiyo ili  kuendana na vipimo vya upana wa barabara.
Bango la mkandarasi ambapo juu linaloonyesha mchoro wa jinsi daraja la Mabatini litakavyokuwa.

No comments: