Balozi
wa Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja
wa Mataifa, Tuvako Manongi akizungumza wakati wa mjadala wa wazi
ulioandaliwana Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa na kufunguliwa
na Katibu Mkuu Ban Ki Moon. Mjadala huo ulihusu uhusiano kati ya Amani
na Haki na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC) miongoni mwa
mambo aliyosisitiza Balozi Manongi ni pamoja na kuishauri ICC kutenda
haki bila kuegemea upande wowote na kwamba ijitahidi kujiepusha na
ushawishi wa kisiasa kutoka nchi yoyote ile likiwamo Baraza Kuu la
Usalama.
Wajumbe
wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa katika mkutano wake wa
wazi uliokuwa ukijadili uhusiano kati ya Amani na Haki na Mahakama ya
Kimataifa ya Makosa ya Jinai.
Na Mwandishi Maalum
Mahakama
ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC) imeshauria kutekeleza majukumu
yake bila ya kushawishi wa kisiasa kutoka nchi yoyote ile likiwamo
Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Ushauri huo umetolewa na Tanzania kupitia Balozi wake wa Kudumu wa
Tanzania katika Umoja wa Matiafa, Tuvako Manongi, wakati wa mjadala wa
wazi uliohusu uhusiano kati ya Amani na Haki na Mahakama ya
Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC).
Mjadala
huo uliandaliwa na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Akizunguma katika mjadala huo uliofunguliwa na katibu Mkuu wa UM, Ban
Ki Moon, Balozi Manongi amesema, ili Mahakama hiyo iweze kutekeleza
majukumu yake ipasavyo inapashwa kujiepusha na ushawishi au
mashikinikizo ya kisiasa.
Akafafanua
kwamba, kwa Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine ambazo zimekwisha
kuitambua mahakama hiyo, inategemea na inaamini kwamba itatekeleza
majukumu yake bila ya upendeleo wa aina yoyote ile.
Akaeleza
wazi kwamba nchi nyingi hasa zile za Afrika zimekuwa zikionyesha wasi
wasi wao juu ya mwenendo wa Mahakama hiyo licha ya ukweli kuwa , nchini
nyingi za Afrika siyo tu zimeitambua lakini masuala mengi
yanayoshughulikiwa na makahama hiyo yanaihusu Afrika.
“ Uhuru wa kutoadhibiwa lazima uzingatiwe wakati wowote na mahali
popote”.
Anasema
Balozi na kuongeza. “ Usemi kwa kwamba haki ni lazima itendeke, lakini
vile vile lazima ionekane. Na huu ni ukweli kwa chombo chochote cha
kisheria kama inavyotakiwa kufanyika pia katika ICC”.
Akasisitiza.
Na
kuongeza kwamba ili haki hiyo itendeke na kuonekana ni lazima basi iwe
kwa wote bilaya kujali au kuzingatia ushawishi wa kisiasa.
Na kufafanua zaidi kwamba mataifa mengi ya Afrika yanaona kama vile
uwajibishwaji katika ICC unalenga upande mmoja. Na hili ni tatizo
ambalo linapelekea ICC kutopata ushirikiano wa kutosha.
Akaeleza
kwamba majukumu ya Baraza Kuu la Usalama la UM na yale ya ICC kwa
kiasi fulani yanashabihiana kutokana na kweli kwamba asilimia kubwa ya
majukumu yao yanaihusu Afrika.
“ Jukumu la kutafuta amani na haki ni jukumu la msingi kwa Baraza
kuu na hali kadharika kwa ICC. Na mara nyingi imeelezwa kuwa amani
haiwezi kuwapo bila haki.
Na
kwa hakika amani na haki ni kama pande mbili za sarafu zinazotegemeana,
kwa sababu upande mmoja hauwezi kustawi bila ya mwingine” akasisitiza
Balozi Manongi
Na kuongeza lakini katika mazingira Fulani Fulani, Jumuia ya
Kimataifa na Baraza kuu la Usalama zimejikuta zikilazimika kujaribu
kutafuta uwiano kati ya pande hizi mbili hasa pale upande mmoja
unapoonekana kuuelemea upande mwingine.
“ Ndio maana haishangazi kwamba kitendo cha kutafuta uwiano kati ya
haki na amani kumezua hofu kubwa.
Kutokana
na kwamba ni jambo lisiloingia akilini kwa mahakama kutafuta haki kwa
gharama ya mchakato wa kutafuta amani. Hata kama itamaanisha kutoa
unafuu wa muda kwa watuhumiwa kutochukuliwa hatua” akasema Balozi
Na kusisitiza kwamba, mchakato wa kutafuta amani kwa namna yoyote ile
usilinganishwe na uhuru wa kutoadhibiwa.
Aidha
amelitaka Baraza Kuu kuwa wazi zaidi kwa kutoa maelezo kwa nchi
ambazo zimeomba uahilishaji wa mashtaka na hii itasaidia kuboresha
ushirikiano na kuondoa hisia potofu dhidi ya ICC.
Halikadharika Mwakilishi huyo wa Tanzania katika UM, anasema ICC si
chombo pekee chenye jukumu la kutafuta haki kwa waathirika wa vitendo
vya jinai.
Kwakile
alichosema hata nchi moja moja zinawajibu na haki ya kutafutua haki
kwa waathirika kwakutumia taasisi zake za kisheria, kinachotakiwa ni
kuzijengea uwezo wa kutekeleza jukumu hilo hasa kwa nchi zile ambazo
zimetoka katika vita au machafuko.
Kwa
upande mwingine, Tanzania imelitaka Baraza Kuu kuisaidia ICC kwa
maana ya raslimali ili iweze kutekeleza majukumu yake ya msingi na vile
vile kuzishawishi nchi kutoa ushirikiano kwa mahakama hiyo.
No comments:
Post a Comment