Mhe. Hamad Rashid Mohamed akitoka katika mkutano na Mwenyekiti wa kamati ya maswala ya Ulinzi na Usalama wa kimatifa Mhe. Saber Chowdury kutoka Bangladesh mara baada ya mjadala huo |
=======================
Picha na Habari na Owen Mwandumbya
Mbunge wa Tanzania ambaye pia ni
Mjumbe wa Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani Mhe. Hamad Rashid Mohamed
ameteuliwa na kamati tendaji ya chama cha Mabunge duniani (IPU) kuwa mjumbe wa
kamati ndogo ya ukaguzi wa ndani kwa mahesabu ya mwaka 2013 ya chama hicho.
Uteuzi huo ulifuatia pendekezo la
umoja wa Mabunge ya Afrika lililowasilishwa na katibu mkuu wake Koffi N’Zi
tarehe 22 Oktoba, 2012 kufuatia kikao cha wajumbe wa umoja wa Mabunge ya Afrika
kumchagua Mhe. Hamad kuwakilisha Afrika kuwania pendekezo hilo mbele ya kamati
tendaji ya chama hicho.
Mhe. Hamad Rashid Mohamed, hii ni
mara ya pili kuiwakilisha Tanzania na Afrika katika kamati mbalimbali za IPU
ambapo mwaka jana katika Mkutano uliofanyika Mjini, Benn, Uswis, alichaguliwa
kuwa mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya IPU cheo ambacho anakitumikia hadi
hivi sasa.
Katika kamati hiyo ya ukaguzi wa
ndani, Mhe. Hamad Rashid atafanya kazi pamoja na mjumbe mwingine aliyeteuliwa
Mhe. Duarte Pacheko kutoka Ureno, ambapo wanatarajia kutoa taarifa
ya kazi yao mwaka 2014 katika mkutano mkuu wa IPU.
Katika hatua nyingine, Wabunge vijana
wametakiwa kuwa chachu ya maendelo katika nchi zao kwa kushawishi kutengeneza
mazingira ya upatikanaji wa ajira kwa vijana katika kipindi hiki cha uchumi wa
kitandawazi.
Hayo yamesemwa jana na Mtaalamu wa
maswala ya ajira kutoka shirika la la kazi la umoja wa mataifa (ILO) alipo toa
maada katika mjadala wa Wabunge Vijana kujadili na namna ya kupunguza ajira kwa
vijana hususani katika kipindi hiki cha uchumi wa utandawazi.
Mtaalamu huyo amesema ni wajibu wa
wabunge kuwa na ushawishi mkubwa kwa serikali zao na baadhi ya taaisisi
zinazotoa ajira ili kuwa na sera madhubuti kwa ajira za vijana hususani
wanaomaliza vyuo kwa lengo la kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Amesema hivi saa duniani, zaidi ya
asilimia 60 ya watu wote duniani ni vijana, na wengi wao wanakabiliwa na tatizo
la ajira swala ambalo ni hatari kwa maendelo ya nchi nyingi duniani.
Wakichangia mada hiyo wabunge wengi
walikubaliana dunia kuwa na tatizo la ajira na hususani kwa kushawishi serikali
zao kuwa na sera madhubuti zenye kutatua tatizo la ajira kwa vijana katika nchi
zao.
Mmoja wa wabunge kutola Denmark
akichangia maada hiyo, amesema yeye anatoka katika mojawapo ya nchi zenye tozo
kubwa la kodi katika sekata mbalimbali duniani, lakini wao kwa kiasi kikubwa
wamefanikiwa kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa kuweka sera mathubudi
zenye kuhakikisha kuwa vijana wanapata ajira mara tu wamalizapo shule.
Anasema moja wapo ya sera hizo ni
pamoja na kuwa na kodi kubwa sana kwa mashirika au kampuni ambayo hayatoi idadi
kubwa ya ajira kwa vijana au ambayo hayazingatii ajiri kwa vijana.
Pamoja na hilo, serikali ya Denmark imeweka utaratibu wa kutoa punguzo la kodi
kwa mashirika au Makampuni yenye sera ya kuajiri vijana kutoka vyuoni ambapo
hivi sasa ni asilimia 6% tu ya watu kutoka Denmak hawana ajira.
Tatizo hili limejitokeza sana katika
chi za afrika, Asia na Latini Amerika ambapo Mbunge kutoka Namibia
akichangia mada hii amesema nchini kwake tatizo la ajira ni zaidi ya asilimia
52 na mashirika mengi na makampuni yanayojishughulisha na biashara kwa lengo la
kupata faida, huona ni hatari sana kuajiri vijana wanaotoka kazini kwa kuwa
wengi wao hawana uzoefu hivyo kufanya swala la uzalishaji kupungua kutokana na
mda mwingi kutumika kufanya mafunzo kazini, jambo ambalo limepingwa vikali na
wajumbe kutoka Afrika kusini, Tanzania, Norway na Maldives.
Mbunge David Kafulila aliyeshiriki
semina hiyo kutoka Tanzania, amesema sio kweli kwamba serikali zetu zitafanya
kila kitu kutoa ajira kwa vijana, akichangia mada hiyo, kafulila
alisema “ swala hapa ni kutengeneza mazingira ya kuwa na soko la ajira
kwa vijana mara tu wamalizapo shule, sasa ni jukumu letu kushawishi serikali
zetu kuwa na sera rafiki zenye kuweka mpango wa kutengeneza ajira kwa vijana” .
Kafulila aliongeza kuwa, mfano ni serikali
zetu kuanzisha mikakati mipya ya maendeleo yenye kulenga kutoa elimu kulingana
na soko la ajira, pamoja na kuvutia wawekezaji katika sekta muhimu zenye kutoa
ajira kwa vijana.
Akitoa mfano wa Tanzania, Kafulila
anasema hivi sasa sekta ya gesi, mafuta na Kilimo Tanzania ndiko soko kubwa la
ajira liliko na lengo lao kama wabunge vijana Tanzania watahakikisha kuwa
wanaishawishi sana serikali kuwa na sera ya jira kwa vijana kwa wawekezaji wote
wanowekeza katika sekta hizi pamoja na kuongeza idadi ya vyuo vyenye kutoa
elimu kulingana na mahitaji ya sekta hizi kuliko kuwa na wataalam wengi kutoka
nje wanaokuja kufanya kazi Tanzania kwa kuwa kuna uchache wa wataalam katika
sekta hizi.
Tatizo lililopo sasa ni kwamba nchi
zetu ziache utaratibu wa kuongeza idadi ya vyuo vinavyotoa elimu inayofanana
bila kuangalia mahitaji ya soko, kwani kuwa na idadi kubwa ya wasomi kwa fani
moja tu nchini ni tatizo kubwa katika maendeleo ya nchi.
Mkutano wa 127 wa IPU unaendelea leo
hapa mjini Quebec ambapo mojawapo ya warsha itakayofanyika ni pamoja na ile
inayosema “Kinga za Wabunge, ni Mzigo au ni kwa manufaa?
No comments:
Post a Comment