Thursday, October 25, 2012

Mhe. Hamad Rashid ateuliwa kuwa mjumbe kamati ya ukaguzi wa Hesabu za ndani IPU

Mhe. Hamad  Rashid Mohamed akitoka katika mkutano na  Mwenyekiti wa kamati ya maswala ya Ulinzi na Usalama wa kimatifa Mhe. Saber Chowdury kutoka Bangladesh mara baada ya mjadala huo

======================= 
Picha na Habari na Owen Mwandumbya
 Mbunge wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani Mhe. Hamad Rashid Mohamed ameteuliwa na kamati tendaji ya chama cha Mabunge duniani (IPU) kuwa mjumbe wa kamati ndogo ya ukaguzi wa ndani kwa mahesabu ya mwaka 2013 ya chama hicho.
Uteuzi huo ulifuatia pendekezo la umoja wa Mabunge ya Afrika lililowasilishwa na katibu mkuu wake Koffi N’Zi tarehe 22 Oktoba, 2012 kufuatia kikao cha wajumbe wa umoja wa Mabunge ya Afrika kumchagua Mhe. Hamad kuwakilisha Afrika kuwania pendekezo hilo mbele ya kamati tendaji ya chama hicho.
Mhe. Hamad Rashid Mohamed, hii ni mara ya pili kuiwakilisha Tanzania na Afrika katika kamati mbalimbali za IPU ambapo mwaka jana katika Mkutano uliofanyika Mjini, Benn, Uswis, alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya IPU cheo ambacho anakitumikia hadi hivi sasa.
Katika kamati hiyo ya ukaguzi wa ndani, Mhe. Hamad Rashid atafanya kazi pamoja na mjumbe mwingine aliyeteuliwa Mhe. Duarte Pacheko kutoka Ureno, ambapo wanatarajia  kutoa taarifa ya kazi yao mwaka 2014 katika mkutano mkuu wa IPU.
Katika hatua nyingine, Wabunge vijana wametakiwa kuwa chachu ya maendelo katika nchi zao kwa kushawishi kutengeneza mazingira ya upatikanaji wa ajira kwa vijana katika kipindi hiki cha uchumi wa kitandawazi.
Hayo yamesemwa jana na Mtaalamu wa maswala ya ajira kutoka shirika la la kazi la umoja wa mataifa (ILO) alipo toa maada katika mjadala wa Wabunge Vijana kujadili na namna ya kupunguza ajira kwa vijana hususani katika kipindi hiki cha uchumi wa utandawazi.
Mtaalamu huyo amesema ni wajibu wa wabunge kuwa na ushawishi mkubwa kwa serikali zao na baadhi ya taaisisi zinazotoa ajira ili kuwa na sera madhubuti kwa ajira za vijana hususani wanaomaliza vyuo kwa lengo la kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Amesema hivi saa duniani, zaidi ya asilimia 60 ya watu wote duniani ni vijana, na wengi wao wanakabiliwa na tatizo la ajira swala ambalo ni hatari kwa maendelo ya nchi nyingi duniani.
Wakichangia mada hiyo wabunge wengi walikubaliana dunia kuwa na tatizo la ajira na hususani kwa kushawishi serikali zao kuwa na sera madhubuti zenye kutatua tatizo la ajira kwa vijana katika nchi zao.
Mmoja wa wabunge kutola Denmark akichangia maada hiyo, amesema yeye anatoka katika mojawapo ya nchi zenye tozo kubwa la kodi katika sekata mbalimbali duniani, lakini wao kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa kuweka sera mathubudi zenye kuhakikisha kuwa vijana wanapata ajira mara tu wamalizapo shule.
Anasema moja wapo ya sera hizo ni pamoja na kuwa na kodi kubwa sana kwa mashirika au kampuni ambayo hayatoi idadi kubwa ya ajira kwa vijana au ambayo hayazingatii ajiri kwa  vijana. Pamoja na hilo, serikali ya Denmark imeweka utaratibu wa kutoa punguzo la kodi kwa mashirika au Makampuni yenye sera ya kuajiri vijana kutoka vyuoni ambapo hivi sasa ni asilimia 6% tu ya watu kutoka Denmak hawana ajira.
Tatizo hili limejitokeza sana katika chi za afrika, Asia na Latini Amerika ambapo Mbunge  kutoka Namibia akichangia mada hii amesema nchini kwake tatizo la ajira ni zaidi ya asilimia 52 na mashirika mengi na makampuni yanayojishughulisha na biashara kwa lengo la kupata faida, huona ni hatari sana kuajiri vijana wanaotoka kazini kwa kuwa wengi wao hawana uzoefu hivyo kufanya swala la uzalishaji kupungua kutokana na mda mwingi kutumika kufanya mafunzo kazini, jambo ambalo limepingwa vikali na wajumbe kutoka Afrika kusini, Tanzania, Norway na Maldives.

Mbunge David Kafulila aliyeshiriki semina hiyo kutoka Tanzania, amesema sio kweli kwamba serikali zetu zitafanya kila kitu kutoa ajira kwa vijana,  akichangia mada hiyo, kafulila alisema “ swala hapa ni kutengeneza mazingira ya kuwa na soko la ajira kwa vijana mara tu wamalizapo shule, sasa ni jukumu letu kushawishi serikali zetu kuwa na sera rafiki zenye kuweka mpango wa kutengeneza ajira kwa vijana” .
Kafulila aliongeza kuwa, mfano ni serikali zetu kuanzisha mikakati mipya ya maendeleo yenye kulenga kutoa elimu kulingana na soko la ajira, pamoja na kuvutia wawekezaji katika sekta muhimu zenye kutoa ajira kwa vijana.
Akitoa mfano wa Tanzania, Kafulila anasema hivi sasa sekta ya gesi, mafuta na Kilimo Tanzania ndiko soko kubwa la ajira liliko na lengo lao kama wabunge vijana Tanzania watahakikisha kuwa wanaishawishi sana serikali kuwa na sera ya jira kwa vijana kwa wawekezaji wote wanowekeza katika sekta hizi pamoja na kuongeza idadi ya vyuo vyenye kutoa elimu kulingana na mahitaji ya sekta hizi kuliko kuwa na wataalam wengi kutoka nje wanaokuja kufanya kazi Tanzania kwa kuwa kuna uchache wa wataalam katika sekta hizi.
Tatizo lililopo sasa ni kwamba nchi zetu ziache utaratibu wa kuongeza idadi ya vyuo vinavyotoa elimu inayofanana bila kuangalia mahitaji ya soko, kwani kuwa na idadi kubwa ya wasomi kwa fani moja tu nchini ni tatizo kubwa katika maendeleo ya nchi. 

Mkutano wa 127 wa IPU unaendelea leo hapa mjini Quebec ambapo mojawapo ya warsha itakayofanyika ni pamoja na ile inayosema “Kinga za Wabunge, ni Mzigo au ni kwa manufaa? 

No comments:

Post a Comment