Sunday, October 28, 2012

MASISTA WA MERYKNOLL WAADHIMISHA MIAKA 100 YA KUANZISHWA KWAO

 Nembo ya Miaka 100 ya kuanzishwa kwa Shirika la Masista la  MaryKnoll,  Shirika ambalo limekuwa likitoa huduma mbalimbali za kijamii  zikiwamo za Elimu, Afya na Kiroho katika nchi 25  Ikiwamo Tanzania. wale waliosoma,  Nganza/Roselin, au Rugambwa, Nyegezi, na shule nyinginezo katika Ukanda wa Ziwa watakuwa wanawakumbuka sana Masista hawa kwa kazi yao nzuri.  Bango hilo limetundikwa katika Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyo katika eneo la Ossining nje kidogo ya Jiji la New York Nchini Marekani.
 Maonesho na mauzo ya bidhaa mbalimbali,   hizi ni baadhi  bidhaa  zikiwamo za kutoka Tanzania,  Kenya, Nambia na  Zimbabwe
 Sister Rosalie Larorte amewahi kukaa  Tanzania kwa miaka zaidi ya 14 anazungumza kiswahili safi, anasema " Naipenda sana Tanzania,  nikakumbuka  ugali wa muhogo  kwa samaki,  mlenda na kashumbari, tena kwenye menu yetu  ya leo  kwenye  shughuli hizi msikose kwenda kula kuna Pilau nyama,  kachumbari na  sambusa"

 Sister  Claudette ambaye akimuuzia mteja  Khanga za Tanzania
 Sister Nunzia yeye alifika  Tanzania mwaka 1946 anazumgumza  kiswahili fasaha, amekaa sana  Musoma anasimulizi nzuri kuhusu  namna alivyokuwa wakifika kumtembelea  Mama Maria Nyerere na Familia yake," siku moja tulikuwa tumekwenda kumtembela  Mama Maria, basi tulipokuwa pale nyumbani, Mwalimu Nyerere akaja akatukuta pale alikuwa tu ndiyo amerudi kutoka safari ya nje sikumbuki ilikuwa  ni nchi gani. akatualika kwenye kumbukumbu  ya kuzaliwa  mtoto wake wa kwanza"
 Zilikuwapo pia bidhaa pia kutoka nchi za Asia kama inavyoonekana hapa
 Na Folk Dance ilikuwepo, Waswede wakilimwaga segere lao
 Sehemu ya wageni waalikwa wakiishangilia  Ntuya Mayenje 
 Watanzania  wakiwaongoza wenzao , kulimwaga  segere la Saida  Karoli  katika  nyimbo yake Ntuya Mayenje. kabla ya kuanza kulimwaga segere lililowaacha hoi wageni wengi, watanzania waliohudhuria hafla hiyo kama kawaida yao walianza kwa kuimba  . wimbo wa "Tanzania, Tanzania,  nakupenda kwa moyo wangu wote, nchi yangu    Tanzania  jina lako ni nzuri sana" wimbo ulioitikiwa  kwa shangwe na masista wanaojuka kiswahili na waliowahi kuishi Tanzania.
Wachina nao walikuwepo 
 Mayenu
 Mori unapopanda inakuwa balaa
 Taratiiiibu
 Hata Mimi  Nayaweza ndivyo anavyojaribu kusema mgeni huyu mwalikwa ambaye kama wengine alishindwa kabisa kujiuzuia akajiunga na watanzania kuicheza Ntuya Mayenje pembeni yake ni Sister Immaculata Tegete (Mtanzania)
ahaaa kumbe tunapinda mgongo hivi hahahaha ilikuwa burudani tosha
 Mdundo wa ngoma unaponoga, lazima ufumbe macho, ni Bw. Marcues akiongezea  maraha kwenye  nyimbo ya Ntuya Mayenje
 Palichimbika,  Bwana huyo alishindwa kabisa kujizuia, mmarekani mweusi, lakini wote asili yetu moja akaamua kujimwaya uwanjani kulisakata Ntuya Mayenje
Watanzania waliokuja kuwaunga mkono  Masista wa MaryKnoll katika kuadhimisha  miaka 100 ya kuanzishwa kwa shirika lao.

No comments: