Nembo ya Miaka 100 ya kuanzishwa kwa Shirika la Masista la MaryKnoll, Shirika ambalo limekuwa likitoa huduma mbalimbali za kijamii zikiwamo za Elimu, Afya na Kiroho katika nchi 25 Ikiwamo Tanzania. wale waliosoma, Nganza/Roselin, au Rugambwa, Nyegezi, na shule nyinginezo katika Ukanda wa Ziwa watakuwa wanawakumbuka sana Masista hawa kwa kazi yao nzuri. Bango hilo limetundikwa katika Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyo katika eneo la Ossining nje kidogo ya Jiji la New York Nchini Marekani.
Maonesho na mauzo ya bidhaa mbalimbali, hizi ni baadhi bidhaa zikiwamo za kutoka Tanzania, Kenya, Nambia na Zimbabwe
Sister Rosalie Larorte amewahi kukaa Tanzania kwa miaka zaidi ya 14 anazungumza kiswahili safi, anasema " Naipenda sana Tanzania, nikakumbuka ugali wa muhogo kwa samaki, mlenda na kashumbari, tena kwenye menu yetu ya leo kwenye shughuli hizi msikose kwenda kula kuna Pilau nyama, kachumbari na sambusa"
Sister Claudette ambaye akimuuzia mteja Khanga za Tanzania
Sister Nunzia yeye alifika Tanzania mwaka 1946 anazumgumza kiswahili fasaha, amekaa sana Musoma anasimulizi nzuri kuhusu namna alivyokuwa wakifika kumtembelea Mama Maria Nyerere na Familia yake," siku moja tulikuwa tumekwenda kumtembela Mama Maria, basi tulipokuwa pale nyumbani, Mwalimu Nyerere akaja akatukuta pale alikuwa tu ndiyo amerudi kutoka safari ya nje sikumbuki ilikuwa ni nchi gani. akatualika kwenye kumbukumbu ya kuzaliwa mtoto wake wa kwanza"
Zilikuwapo pia bidhaa pia kutoka nchi za Asia kama inavyoonekana hapa
Na Folk Dance ilikuwepo, Waswede wakilimwaga segere lao
Sehemu ya wageni waalikwa wakiishangilia Ntuya Mayenje
Watanzania wakiwaongoza wenzao , kulimwaga segere la Saida Karoli katika nyimbo yake Ntuya Mayenje. kabla ya kuanza kulimwaga segere lililowaacha hoi wageni wengi, watanzania waliohudhuria hafla hiyo kama kawaida yao walianza kwa kuimba . wimbo wa "Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wangu wote, nchi yangu Tanzania jina lako ni nzuri sana" wimbo ulioitikiwa kwa shangwe na masista wanaojuka kiswahili na waliowahi kuishi Tanzania.
Wachina nao walikuwepo
Mayenu
Mori unapopanda inakuwa balaa
Taratiiiibu
Hata Mimi Nayaweza ndivyo anavyojaribu kusema mgeni huyu mwalikwa ambaye kama wengine alishindwa kabisa kujiuzuia akajiunga na watanzania kuicheza Ntuya Mayenje pembeni yake ni Sister Immaculata Tegete (Mtanzania)
ahaaa kumbe tunapinda mgongo hivi hahahaha ilikuwa burudani tosha
Mdundo wa ngoma unaponoga, lazima ufumbe macho, ni Bw. Marcues akiongezea maraha kwenye nyimbo ya Ntuya Mayenje
Palichimbika, Bwana huyo alishindwa kabisa kujizuia, mmarekani mweusi, lakini wote asili yetu moja akaamua kujimwaya uwanjani kulisakata Ntuya Mayenje
Watanzania waliokuja kuwaunga mkono Masista wa MaryKnoll katika kuadhimisha miaka 100 ya kuanzishwa kwa shirika lao.
No comments:
Post a Comment