Sunday, October 28, 2012

NAPE,MGEJA NA MAIGE WAFUNGA KAMPENI ZA CCM KATA YA BUGARAMA, KAHAMA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni za CCM za udiwani Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga, jana Oktoba 27.
Madiwani wa Kata za Kahama wakiwa na mgombea Udiwani wa CCM, Kata ya Bugarama katika wilaya hiyo Nixon Ikoko wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za udiwani katika kata hiyo, uliohutubiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige wakati akimuombea kura mgombea udiwani wa CCM Kata ya Bugarama, kwenye mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika mji mdogo wa Bugarama.
Wazee wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipohutubia mkutano wa kufunga kampeni za udiwani za CCM Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga.
Mzee wa miaka 98, Nickson Toma akifuatilia kwa makini mkutano wa kampeni za udiwani Kata ya Bugarama mkoani Shinyanga uliohutubiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa katika mapokezi ya wananchi alipowasili kwenye mkutano wa kufunga kampeni za CCM za udiwani kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga.
Wananchi katika kata ya Bugarama , Kahama mkoani Shinyanga, wakishangilia wakati wa kufunga kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hiyo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige wakishiriki kucheza ngoma ya Baswezi, katika kijiji cha Buyange, Kata ya Bugarama, Kahama mkoani Shinyanga wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za udiwani za CCM kata ya Bugarama.
Madiwani wa Kata za Kahama wakiwa na mgombea Udiwani wa CCM, Kata ya Bugarama katika wilaya hiyo Nixon Ikoko wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za udiwani katika kata hiyo, uliohutubiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.(Picha na Bashir Nkoromo).

No comments:

Post a Comment