Afisa
Utalii wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga
Samiji Mlemba (katikati) akitoa maelezo kwa wanafunzi wa Sekondari ya
Zanaki jijini Dar es Salaam waliopata ufadhili wa kutembelea hifadhi
hiyo waliopewa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) na Bodi ya
Utalii Tanzania (TTB) kupitia mradi wa Uwezo Award uliendeshwa na
Shirika lisilo la kiserikali la Great Hope Foundation. Picha zote na
Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG - Lushoto.
Afisa
Utalii wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga
Samiji Mlemba akiwa ameongozana na kuwapa maelezo wanafunzi na
wanahabari waliokuwa katika ziara hiyo.
Moja
ya bango linalowakaribisha wageni katika hifadhi ya Mazingira Asili ya
Magamba iliyopo Lushoto, Tanga na kuwapa maelezo machache.
Wanafunzi wakiendelea na safari ambayo iliwachukua saa 3 kufika katika kilele kwa km 2.2.
Wanafunzi wakifurahia katika kituo cha kwanza ambacho kilikuwa ni Chanzo cha Maji.
Pichani
ni wanahabari wa vyombo mbali mbali Msungu wa ITV (kwanza kulia) na
Said Makala (wa pili toka kulia) wakifurahia pamoja na maofisa wa GHF
Noela na Maria wa TTB... Juu ni Mwanahabari Cathbert Kajuna
-Kajunason/MMG akiwa na wanafunzi wakifurahia katika kituo cha pili
ambacho ni Mshai.
Afisa
Utalii wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga
Samiji Mlemba akitoa maelezo machache wakati wanafunzi hao walipofika
kituo cha Mshai wakielekea katika kilele cha mlima Kigulu Hakwewa.
Safari ya kuelekea katika kilele cha mlima wa Kigulu Hakwewa.
Safari ilikuwa ni ndefu ambapo wengine waliamua kupumzika ili kuweza kuvuta pumzi katika miti yenye umri wa miaka 40.
Muonekano wa miti mikubwa yenye kuvutia iliyoishi umri wa miaka 40 mpaka sasa.
Kila
mmoja alikuwa na furaha kufika katika kituo cha tatu cha Kwesimu ambapo
historia ya sehemu hiyo ilikuwa ni kupatikana kwa huduma za simu. Hapo
ndipo mawasiliano ya simu yakipatikana yani namaanisha kila mtu mwenye
simu alikuwa akifika hapo ili aweze kupata nawasiliamo (Network ilikuwa
ikipatikana eneo hilo).
Eneo hilo la Kwesimu ndipo mkondo wa maji ulikuwa ukipita.
Wanafunzi
wakifurahia katika mlango wa pango la Wajerumani walilolitumia katika
vita vya kwanza vya dunia vilivyotokea mwaka 1914 - 1918.
Wanafunzi
wakifurahia na mwalimu wao walieambatana nae katika mlango wa pango la
Wajerumani walilolitumia katika vita vya kwanza vya dunia vilivyotokea
mwaka 1914 - 1918.
Meneja
Uhusiano wa Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) nae aliweza
kupata wasaa katika lango la pango la Wajerumani lililotumika katika
Vita vya kwanza vya Dunia 1914-1918.
Ndani ya pango la Wajerumani walilolitumia katika vita vya kwanza vya dunia vilivyotokea mwaka 1914 - 1918.
Wanafunzi wakifurahia na Afisa Utalii, Samiji Mlemba (katikati) wakiwa kwenye geti la kuingia kilele cha mlima Kigulu Hakwewa.
Kilele cha Mlima Kigulu Hakwewa ambapo ni (1840 A.M.S.L) Usawa wa Juu wa Kiwango cha Bahari.
Kila mmoja akifurahia...
Makulaji kidogo!
Kila mmoja akiwa na uso wa furaha baada ya kutoka kilele cha Mlima Mgulu Hakwewa.
Baada
ya wanafunzi kutembelea kilele cha mlima Kigulu Hakwewa waliweza kufika
katika Msitu wa Asili wa Mkusu unaolimilikiwa na Wakala wa huduma za
misitu Tanzania (TFS) ili kujionea maporomoko ya maji ya Mvueni.
Wanafunzi wakifurahia katika maporomoko ya maji ya Mvueni yaliyopo katika Msitu wa Asili wa Mkusu uliopo Lushoto, Tanga.
Maporomoko ya maji ya Mvueni yaliyopo katika Msitu wa Asili wa Mkusu uliopo Lushoto, Tanga.
Wanafunzi wakifurahia katika Maporomoko ya maji ya Mvueni.
Hifadhi
ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga ni moja ya vivutio
vya hifadhi 12 za mazingira asilia vinavyosimamiwa na Wakala wa Huduma
za Misitu Tanzania (TFS).
Watu wengi wamekuwa wakisahau kuwa utalii wa ikolojia nao unafaida kwa
jamii yetu ili iweze kujifunza mambo mbali mbali kuhusu misitu na viumbe
hai.
Wakizungumza
kwa wakati tofauti mara baada ya kutembelea hifadhi ya mazingira ya
Magamba, Mfaume Salehe Msasa amesema “Kuwa Coordinator wa ni bahati
kwangu na furaha pia kwa kuwa nimejifunza vitu vingi sana tangia nimeaza
kuvolunteer @greathopetz pia naendelea kujifunza kwamaana kuwa
kujifunza hakunaga mwisho,"
Kwa kwaida kila mwaka @greathopetz hua tunatoa zawadi mbalimbali kwa
wanafunzi pamoja na shule zinazofanya miradi bora zaidi. Mwaka huu
tulikua na shule 100 ambazo zimefanya mradi na shule ambayo imefanya
mradi bora zaidi nakuweza kuwa mshindi wa kwanza ni Shule ya Sekondari
Zanaki.
“Miradi
ya mwaka huu imekua ni ya tofauti kubwa kwa mshindi wa mradi wa Uwezo
Award kupata zawadi nyingi na wamepewa safari ya kitalii ya kwenda msitu
wa Magamba kwa kudhaminiwa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania na
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Nae Meneja wa Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ameshukuru jinsi
wanafunzi walikuwa na moyo wa kujifunza kuhusu mazingira na kuomba
shule pamoja na wazazi waweze kujitokeza kuwapeleka watoto wao katika
vivutio mbali mbali vya utalii wa ikolojia ambao watu wengi wamekuwa
wakiusahau.
"Unajua
watu wengi wamekuwa wakikimbiali kuangalia wanyama ila huku napo ni
zaidi ya kule maana wale wanaopenda kuona mazingira yanavyotunzwa basi
hawana budi kufika bila kukosa, tunawakaribisha watanzania wote hasa
kipindi hiki cha likizo kwa wawalete watoto wao wajionee vivutio mbali
mbali mbali," amesema Tulizo Kilaga
Great Hope Foundation - GHF ni shirika lisilo la kiserikali
lililojikita katika kuwasaidia vijana kutambua na Kuendelea uwezo wao
katika maeneo mbalimbali. Shirika hubuni na kuendesha miradi katika
muktaadha wa kuwajengea uwezo Vijana.
No comments:
Post a Comment