*Yaomba radhi wasafiri, yafafanua utaratibu kusafirisha mazao ya misitu
*Pia yamzungumzia Ofisa wake wa Misutu, kumchukulia hatua za kinidhamu
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAKALA Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umepokea taarifa kupitia mitandao ya kijamii na wadau mbalimbali zinazohusisha namna Ofisa Misitu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga ambavyo alikuwa akitekeleza majukumu ya kusimamia Sheria ya Misitu Na. 14 ya Mwaka 2002 pamoja na Kanuni
zake za mwaka 2004.
Ofisa huyo alikuwa akitekeleza majukumu hayo kwa mujibu wa kifungu cha 93 (Powers of officers with respect to offences) inayompa mamlaka Ofisa Misitu au Ofisa wa Jeshi la Polisi kukagua, kukamata na kuzuia mazao yanayodhaniwa kupatikana kinyume na sheria.
Kwa kukumbusha tu leo kwenye mitandao ya kijamii kulikuwa na video inayosambaa kwa kasi kubwa ikionesha namna ambavyo wananchi wanalalamikia kitendo cha Ofisa Misutu akilumbana na abiria baada ya kulisamamisha gari na kubaini kuna vitanda vimebebwa.Hivyo kukaibuka malumbano ambayo yamechangia TFS kuamua kutoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari.
Taarifa ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) iliyotolewa leo Desemba 30,2018 imesema uongozi wa TFS umefanya uchunguzi wa haraka na kubaini kuwa abiria mmoja alikuwa akisafirisha vitanda viwili vipya kwa basi. Vitanda hivyo vililipiwa ushuru wa Serikali kupitia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) na kupewa stakabadhi halali ya Desemba 26, 2018 katika kituo cha Mkata, Handeni Mkoani Tanga.
Imefafanua katika kutekeleza majukumu yake, Ofisa wao alimtaka abiria huyo kuonesha hati ya Kusafirishia bidhaa hizo kwa mujibu wa Kanuni za Misitu Kifungu cha 13, sehemu ndogo ya 4 ambayo inakataza mwenye chombo chochote cha usafiri kusafirisha mazao ya misitu ambayo hayana hati ya usafirishaji ambapo abiria huyo hakuwa nayo.
"Hata hivyo, Ofisa wetu alishindwa kutafsiri masharti ya kifungu hiki na mahitaji ya utoaji wa hati ya usafirishaji kwani kama msafirishaji binafsi kwa matumizi ya nyumbani asingeweza kukidhi vigezo vya kuwa na hati hiyo. Hati ya usafirishaji huhitaji msafirishaji kuonesha usajili, leseni ya biashara,
utambulisho wa mlipa kodi na namba ya usajili wa chombo kinachotumika kusafirisha mazao hayo pamoja na kuonesha vituo atakavyopaswa kukaguliwa,"imeeleza taarifa ya TFS ambayo imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano.
Imeeleza kutokana na tukio hilo Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unamwomba radhi abiria huyo na umma wa watanzania kwa tukio hilo na usumbufu uliojitokeza na kwamba wakala unaendelea kufuatilia suala hilo, na utahakikisha kuwa tukio kama hilo halijirudii tena. Aidha hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa Kanuni za utumishi wa umma dhidi ya mtumishi aliyehusika na utoaji wa lugha isiyo na staha wakati akitekeleza sheria ya misitu ambapo alitegemewa kutoa elimu stahiki kwa umma. Hata hivyo TFS imefafanua ikiwa mwananchi yeyote amenunua samani mpya kutoka kwa watengenezaji au wauzaji mahali popote kuhakikisha anapatiwa risiti halali kwa malipo aliyofanya.
"Hivyo, mmiliki wa samani mpya kwa matumizi binafsi halazimiki kuwa na Hati ya Usafirishaji anaposafirisha toka eneo moja kwenda jingine isipokuwa awe tayari kuonesha uthibitisho wa nyaraka za malipo halali ya samani hizo kwa ukaguzi pale itakapohitajika. Mwananchi yeyote anayesafirisha samani zilizotumika kutoka eneo moja hadi jingine halazimiki kuwa hati za malipo wala kuwa na hati ya kusafirishia samani hizo.

"Serikali itaendelea kufanya mapitio ya Sheria ya Misitu na Kanuni zake ili kuepuka mkanganyiko wowote wa tafsiri ya sheria unaoweza kujitokeza na kuondoa usumbufu kwa wananchi. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unapenda kutoa rai kwa wananchi wote kuendelea kuzingatia Sheria za
uhifadhi wa misitu. Aidha, Wakala hauna nia ya kuzuia utengenezaji, usafirishaji na matumizi ya samani za mbao mahali popote nchini ilimradi tu upatikanaji wa malighafi zake uwe umefuata utaratibu. Lengo ni kuhakikisha kuwa rasilimali za misitu zinatunzwa na kutumika kwa njia endelevu kwa maendeleo ya Taifa.
"Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania utaendelea kutoa elimu kwa umma pamoja na watumishi wake kuhusu taratibu za uvunaji, usafirishaji na biashara ya mazao ya misitu nchini kupitia njia mbalimbali na kuhakikisha huduma bora kwa wananchi,"imesema sehemu ya taarifa hiyo ya TFS
No comments:
Post a Comment