Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel
kushoto akimkabidhi mabati 229 Katibu wa UWT Mkoani Tanga Sophia Nkupe
kwa ajili ya ujenzi wa wodi wakina mama hospitali ya wilaya ya Muheza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza
Mhandisi Mwanasha Tumbo
Katibu wa UWT Mkoani Tanga Sophia Nkupe kulia akimkabidhi 229
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo mabati 229 kwa ajili
ya ujenzi wa wodi wakina mama hospitali ya wilaya ya Muheza kushoto ni
Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto
akimkabidhi mabati 229 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza
kwa ajili ya
ujenzi wa wodi wakina mama hospitali ya wilaya ya Muheza kushoto ni
Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel
Katibu wa UWT Mkoani Tanga Sophia Nkupe akizungumza katika
halfa hiyo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel
akizungumza katika halfa hiyo
Meneja wa NMB Tawi la Muheza akizungumza katika halfa hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza akizungumza katika Halfa
hiyo kushoto ni Kaimu Meneja wa Benki
ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel
Sehemu ya watumishi wa benki ya NMB wilaya Muheza wakiwa kwenye
halfa hiyo
Sehemu ya wananchi wilaya Muheza wakishuhudia makabidhiano hayo
NA MWANDISHI WETU, MUHEZA.
BENKI
ya NMB nchini imetoa mabati 229 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wakima
mama katika hospitali ya wilaya ya Muheza ikiwa ni kuunga mkono juhudi
za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli
kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto za afya kwenye maeneo
yao.
Halfa ya makabidhiano hayo yalifanyika mjini Muheza
na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo akiwemo Katibu wa UWT
Mkoani Tanga Sophia Nkupe na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi
Mwanasha Tumbo.
Akizungumza baada ya kupokea mabati hayo
Katibu wa UWT huyo aliishukuru na kuwapongeza benki ya NMB kwa
kuwakubalia ombi lao la kuwasaidia mabati kwa sababu wamekuiwa mstari
wa mbele kusaidia lakini wanafanya hivyo kuunga mkono juhudui za Rais
katika dhamirta yake ya kuhakikisha huduma za afya zinakuwa bora,.
Nkupe alisema pia wana mpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa
juhudi kubwa anazofanya kuhakikisha wananchi wanaondokana na
changamoto mbalimbali ikiwemo za huduma ya afya na nyenginevyo
“Lakini pia nikushukuru Mh DC Mhandisi Mwanasha Tumbo kwa
juhudi zako unazozifanya kuhakikisha wilaya ya Muheza inapata
maendeleo makubwa pia niwaombe NMB mtusaidie wakina mama kwa sababu
tunateseka sana wanachombezwa na taasisi mbalimbali za mikopo yenye
riba kubwa”Alisema Katibu huyo wa UWT.
Awali akizungumza
wakati akikabidhi msaada huo wa mabati Kaimu Meneja ya NMB Kanda ya
Kaskazini Cosmas Gabriel Sadat alisema wameona watoe msaada huo
kutokana na ushirikiano mkubwa ambao wamekuwa wakiupata hauna kifani
huku wakiupongeza uongozi wa wilaya na Mganga Mkuu wa wilaya hiyo.
Alisema kwa sababu wakati DMO alipoona uwepo wa changamoto
hiyo ya jengo la wakima mama hawakuwaza mbali nao na walijua kwamba
mkombozi wao ni NMB na hivyo kupeleka maombi yao ambayo yalifanyiwa
kazi kwa uhakika hatua iliyowawezesha kunufaika na msaada huo ambao
utakuwa chachu kwao .
“Asanteni sana kwa kutupa dhamana
hii,mliona mnawadau wa uhakika wa kupeleka kilio chenu,tunatambua
juhudi kubwa za serikali hasa ya awamu ya tano zimekuwa na nguvu
kuhakikisha watanzania wa kawaida wanaishi maisha ya neema”Alisema
Kaimu Meneja huyo
Aidha alisema kwamba benki hiyo haiwezi
kuiacha serikali bila kuisaidia wao wapo nao bega kwa bega na jamii
popote pale nchini kuhakikisha inapata afya iliyo bora na elimu
iliyobora ili neema ya watanzania wote tuweze kuionja.
Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha
Tumbo alisifu juhudi kubwa zinazofanywa na benki hiyo kwa kuwapatia
msaada huo na kuwaomba wasiwachoke waendelee kushirikiana nao ili
kuhakikisha huduma za afya wilaya humo zinaweza kupatikana kwa urahisi
ili kila mmoja anapotaka kupata aweze kufika kwa urahisi na kuweza
kuendelea shghuli zao kwa wakati na kuchochea kasi ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment