Sunday, December 2, 2018

MSD YATAKIWA KUKAMILISHA VIFAA VYOTE VINAVYOHITAJIKA KATIKA VITUO VYA AFYA VILIYOBORESHWA



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akifunua kitambaa, ishara ya kuweka jiwe la msingi la ukarabati wa kituo cha Afya Koromije, ikiwa in sehemu ya majukumu katika ziara yake ya kukagua hali ya ubora wa huduma za Afya Mkoani Mwanza.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiendelea na ukaguzi wa miundombinu katika kituo cha Afya Koromije, ikiwa in mwendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya ubora wa huduma za Afya Mkoani Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe.Charles Kitwanga akisema jambo mbele ya wapiga kura wake (hawapo kwenye picha) katika kijiji cha Koromije Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya Waziri wa Afya ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya kijijini hapo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akihutubia wanakijiji wa Koromije (hawapo kwenye picha) pindi alipofanya ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya Mkoani Mwanza.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiongea na watoto wa kike baada ya kutoa burudani ya ngonjera, wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya Mkoani Mwanza.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiitazama chupa iliyo na Wine iliyotengenezwa na kikundi cha wanawake kijijini hapo kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiangalia gharama za matibabu kwenye mbao ya matangazo katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto aliyefika na mama yake katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi ili kupata huduma za Afya.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akikagua hali ya Dawa katika stoo yakuhifadhia Dawa katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (wakatikati) akikagua chumba cha kupima makohozi katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akikagua jengo linaloendelea kujengwa la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi.

………………………….

Na WAMJW – MISUNGWI, MWANZA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeitaka Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) kuhakikisha wanakamilisha kuleta vifaa vyote vinavyohitajika katika vituo vya Afya vinavyoboreshwa nchini kabla ya Januari 15, 2019 ili wananchi waweze kupata huduma.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy wakati akiweka jiwe la msingi la ukarabati wa kituo cha Afya Koromije na kukagua hali ya utoaji Huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.

“Haina maana ya kuwa na majengo makubwa na mazuri ya Vituo vya Afya kama hakuna vifaa vinavyohitajika, huku Wananchi wanaendelea kupata tabu”, alisema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewahasa Wazazi na Wananchi wote kwa ujumla kutodharau huduma za Chanjo, hivyo kuwahimiza Wananchi wote kuwapeleka katika vituo vyakutolea chanjo watoto waliofika umri wa kupata chanjo

“Kifafa, Kifaduro,Donda koo, Surua, hayapo siku hizi kwasababu ya Chanjo, kwahiyo tusije tukadharau chanjo, tuhakikishe kila mtoto mwenye umri wakupata chanjo , akapate chanjo” alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Aidha, Waziri Ummy amewataka Wananchi wa Misungwi kuhakikisha wanasafisha mazingira, na kutumia vyandarua vyenye dawa ili kuepuka kupata ugonjwa wa Malaria ambao umeendelea kuwa hatari nchini hasa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 na Wanawake Wajawazito.

“Ugonjwa wa Malaria umepungua kutoka Asilimia 37 hadi Asilimia 27, kwahiyo niendelee kuwahimiza Wananchi wa Misungwi, kwanza kuhakikisha wanafukia vidimbwi vya maji, kusafisha mazingira na kulala kwenye vyandarua vyenye dawa” Alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy aliendelea kusisitiza kuwa sio kila homa ni Malaria, hivyo kuwataka Wananchi kutotumia dawa bila kwenda kupata vipimo katika Kituo cha kutolea Huduma za Afya na kuthibitishwa kuwa una Malaria.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Rutha Thomas alisema kuwa Mkoa wa Mwanza unaishukuru Serikali kwa kuwapatia jumla ya shilingi Bilioni 2 zitakazotumika katika ujenzi wa Hospitali 2 za Hamashauri za Ilemela na Bushosa.

No comments: