Friday, November 9, 2018

TAASISI YA SADAKA NETWORK,HOSPITALI YA MUHIMBILI,AGA GHAN NA WOMEN TO WOMEN FOUNDATION KURUDISHA TABASAMU USONI KWA WATU WALIOHARIBIKA MAUMBILE YAO.

Watanzania wameombwa kwa pamoja kushirikiana na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya SADAKA NETWORK , Hospitali ya Muhimbili na Aga Ghan kwa kushirikiana na Women to women foundation kuchangia kurudisha tabasamu usoni  kwa wakina mama na watoto waliopata matatizo hayo kwa  bahati mbaya, kupata ajali,kwa ukatili wa kijinsia, kupigwa au matatizo yoyote yaliyopelekea wao kuharibika maumbile yao ikiwa ni usoni ama sehemu nyengine ya mwili. 

Mwanzilishi wa taasisi hiyo Dkt. Ibrahim Msengi akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa gharama za kuwatibu watoto na akina mama ni kubwa na haziwezi kubebwa na Muhimbili au Aga Ghan peke yake wala Women to women foundation,bali ghalama hizi zitafanikiwa endapo wananchi wataungana kwa pamoja ili kutoa michango yao ili kufanikisha zoezi hilo.

"Upasuaji huu utafanyika katika Hospitali ya Muhimbili na Aga Ghan na tunatarajia kuwafanyia upasuaji watu 40 kutoka sehemu zote Tanzania,hivyo pesa inayohitajika ni Tsh Milioni 268" alisema Dkt. Msengi.
Dkt. Ibrahim Msengi(wa kwanza kulia) Muasisi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya SADAKA Network, alisema lengo la kuwaita waandishi wa Habari ni kutaka  kusaidiana katika kutoa huduma kwa jamii "SADAKA Network ikishirikiana na Aga Khan, Muhimbili wakishirikiana na Women to women Foundation ambao kazi yao kubwa ni kuwasaidia akina mama na watoto katika afya, wanakuja kuona akina mama na watoto pamoja na akina baba na watoto ambao wameharibiwa maumbile yao kwa sababu mbalimbali ambayo inaweza ikawa ni kwa bahati mbaya, kupata ajali,kwa ukatili wa kijinsia kwa kupigwa, kwa hiyo hawa ndugu wakishirikiana na sisi watakuja kurudisha kile kilichoharibika kirudi katika hali yake" alisema Dkt. Msengi. Alimalizia kwa kusema kuwa wataalam hao wanauwezo mkubwa wa kufanya upasuaji na kumrudisha mtu katika hali yake hata  kama atakuwa aliharibika kwa kiasi gani.
 Baba Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosis ya Dar es Salaam  Jackson Sostenes Jackson, alisema kuwa SADAKA Network ni jukwaa ambalo linaunganisha watu kwa umoja wao kama watanzania,kuacha itikadi na tofauti tulizonazo, amewashukuru Women to Women Foundation kutoka Marekani kuja kuungana na watanzania katika hali na majanga ambayo yamewakumba ndugu ambao wameathirika kutokana na unyanyasaji wa kijinsia. alimalizia kwa kusema kuwa "Mtu yeyote anaweza kuchangia kwa M-Pesa ama Tigo Pesa piga namba *150*92# kisha ingiza Code number yangu  ambayo ni P0002  kisha utachangia kile unachoweza kuchangia"
Sheikh Alhad Mussa Salum Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mwenyekiti wa kamati ya Amani wa viongozi Dini,alisema kuwa anaungana na watanzania wote kusapoti mradi huu unaoratibiwa na SADAKA Network  wa kurudisha tabasamu usoni muhimu wenye lengo la kuwasaidia wale wote wanaoathirika kwa njia moja au nyengine majumbani, alisema ili kuwachangia kwa kadili ya mtu na uwezo alionao, "Ukiwa na M-Pesa ama Tigo Pesa piga namba *150*92# kisha ingiza Code number yangu  ambayo ni A0002 kisha utachangia kile unachoweza kuchangia" alisema
Alhad Mussa Salum Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Balozi wa Rudisha Tabasamu lao  Msanii Maarufu wa kuigiza Filamu za Kitanzania Yvone Cherry maarufu kwa jina la Monalisa,alisema kwamba kuna changamoto nyingi ambazo wanapitia wazazi katika kulea watoto ambapo watoto hawa hukumbwa na majanga mengi hasa wakiwa majumbani ikiwa ni pamoja na kuungua kwa maji,chai, chakula ama moto hii inapelekea watoto kuharibika kwa moto. 
aliongeza kuwa kuwa wanaume wanawanyanyasa wakezao kijinsia kwa kuwapiga na hata pengine kuwachoma na moto na baadhi ya watu kumwagia wenzao tindikali jambo linalopelekea watu kuharibika miili yao. Hali hii inapelekea watu kukosa amani,furaha na kuishi vizuri kutokana na majeraha waliyoyapata. Ameishukuru taasisi ya kiraia ya SADAKA Network kwa kushirikiana na Women to Women Foundation kwa kuamua kurudisha tabasamu usoni kwa wote waliopatwa na majanga hayo. 
Mwisho aliwaomba watanzania kuungana pamoja kuwachangia watu hao .  "Ukiwa na M-Pesa ama Tigo Pesa piga namba *150*92# kisha ingiza Code number yangu  ambayo ni Y0002 kisha utachangia kile unachoweza kuchangia" alisema
Alhad Mussa Salum Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Olai Stephen Ndota Mkuu wa idala ya masoko na mawasiliano  akiwakilisha  Hospitali ya Aga Khan, alisema kuwa shirika la Women to Women Foundation linaundwa na madaktari bingwa wa upasuaji wanawake wanaotoka katika nchi za Canada, Uingereza pamoja na Marekani, "Zoezi hili la upasuaji lilianza mwaka 2016 na hii itakuwa ni awamu ya nne, katika awamu ya kwanza 2016  tuliweza kuwahudumia watu 37, awamu ya pili 2016 tuliwahudumia watu 35 na mwaka 2017 Novemba tuliwahudumia watu 30" Alisema Ndota.
 Viola Massawe Meneja Miradi kutoka taasisi ya SADAKA Network, alisema kuwa SADAKA Network ni mtandao unaopatikana 'Online' na 'Offline' "Jukumu letu kubwa ni kuweza kuwa karibu na jamii na kuwaweka viongozi wa kijamii karibu na jamii ili kuweza kutatua matatizo ya kijamii kwa kutumia miradi" alisema Viola. aliongeza "Tunawaomba watanzania sote kwa pamoja tuungane kuchangia ili tuweze kurudisha tabasamu usoni mwa akina mama hawa." alimalizia kuwa unaweza kuchangia kile ulichonacho kwa kuingia katika Tovuti ya SADAKA Network ambayo ni www.sadakanetwork.com kisha bonyeza miradi ya kijamii
Wanahabari na wadau na wadau wakiwa katika katika mkutano huo.
(PICHA NA FREDY NJEJE)

No comments: