Thursday, November 8, 2018

SADAKA NETWORK YAWAOMBA WATANZANIA KUCHANGIA FEDHA KUFANIKISHA UPASUAJI WA WANAWAKE NA WATOTO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

TAASISI isiyo ya kiserikali ya SADAKA Network imeunga mkono juhudi za Hospitali ya Aga Khan, Muhimbili na Taasisi ya Women to Women katika kufanikisha upasuaji wa urekebishaji (upasuaji wa urembo) kwa wanawake na watoto utakaofanyika 27 November mwaka huu. 

Hospitali ya Agha Khan, Muhimbili na Taaisis ya Women to Women ziko kwenye harakati za kuweka tabasamu kwenye nyuso za wahanga wa ukatili wa nymbani uliosababisha wahanga hao kuathirika. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi wa SADAKA Network Dkt Ibrahim Msengi amesema kuwa SADAKA Network umeamua kuunga mkono kwa kuchangisha fedha kupitia programu yake ili kufanikisha mpango huo, wameamua kutumia viongozi wa jamii na watu maarufu ndani ya Tanzania kuhabarisha wananchi wote ili waweze kuchangisha fedha ili kwa pamoja waweze kusaidia kurejesha tabasamu kwenye uso zao. 

Dkt Ibrahim amesema kuwa, ukatili wa nyumbani na ajali unaweza ukasababisha mauti au majeraha yanayoweza kubadilisha muelekeo wa maisha ya yao, watu wameshuhudia, kusikia au kuona kupitia luninga wanawake na watoto ambao muonekano wao umebadilika kisa ajali au ukatili wa nyumbani au watoto wenye maisha yaliybadilishwa kisa wazazi waliowakatili. 

Amesema kuwa, Kwa pamoja wanatumia kauli mbiu ya "Kurudisha tabasamu usoni mwao" ili kuweza kurejesha utu watu, wanawake na watoto wanakuwa wamejeruhiwa sana na imewapelekea kuwa na aibu hata wanashindwa kuendelea na shughuli zao na majeraha haya yanawabadilisha, yanawafanya wajihisi kuwa tahamani yao kama binadamu imeshuka. 

Meneja Masoko na Mahusiano wa Agha Khan Hospital Olayce Steven Lotha amesema, kwa mwaka huu wamepana kuwafanyia upasuaji wanawake na watoto 40 kutoka kwenye Mikoa tofauti nchini ila uhitajiw a watu katika upasuaji huo ni mkubwa sana. 

Lotha amesema, "katika awamu ya kwanza ya mwaka 2016 tuliwafanyia upasuaji watu 36 na awamu ya pili wakiwa 35, na kwa mwaka 2017 ulihusisha wanawake na watoto 30 ila kwa 2018 lengo letu kuu ni 40 na tayari tumeshawapata kutoka Bunda, Kagra, Mwanza, Iringa, Mbeya, Dodoma na Tanga," 

Upasuaji huo utahusisha Madaktari bingwa wa upasuaji 16, 10 wakitoka kwenye taasisi yaWomen to women, watatu wakitoka Agha Khan na watatu Muhimbili, na timu ya manesi 10 pamoja na wataalumu wa dawa za usingizi. 

Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Jackson Jackosn , Balozi wa Rejesha tabasamu usoni mwao Yvyone Cherry kwa pamoja wameungana kuwaomba watanzania wachangie na kuuna mkono juhudi za SADAKA Network ili kuweza kuanikisha upasuaji huo na kurejesha tabasamu usoni mwao na kila mmoja achangie kwa uwezo wake. 

Mtendaji Mkuu wa SADAKA Nwtwork Viola James, ili kufanikisha upasuaji huu kinahitajika kiasi cha Shiling Milion 268 kwa gharama zote na tunatambua kuwa Hospitali ya Muhimbili haiwezi kugharamikia peke yake na ndio maana SADAKA tukaamua kushirikiana kwa pamoja kuweza kuchangisha fedha itakayosaidia kurejesha tabasamu usoni mwao. 

Viola ametaja namba za kuchangia kwa kiasi chochote kwa Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum kupitia namba *150*92# halafu unaandika namba A0002, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Jackson Jackosn *150*92# halafu P0002 na kwa Balozi Yvyone Cherry ni *150*92# Y003. 
Mwanzilishi wa SADAKA Network Dkt Ibrahim Msengi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na taasisi yake kuunga mkono juhudi za Hospitali ya Aga Khan, Muhimbili na Taasisi ya Women to Women katika kufanikisha upasuaji wa urekebishaji (upasuaji wa urembo) kwa wanawake na watoto utakaofanyika 27 November mwaka huu, kushoto ni Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na Meneja Masoko na Mahusiano wa Agha Khan Hospital Olayce Steven Lotha .
Meneja Masoko na Mahusiano wa Agha Khan Hospital Olayce Steven Lotha akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na upasuaji wa urekebishaji (upasuaji wa urembo) kwa wanawake na watoto utakaofanyika 27 November mwaka huu. 
Balozi wa Rejesha tabasamu usoni mwao Yvyone Cherry akiwa anawahisi jamii kuchangia kwa kiasi chochote ili kufanikisha upasuaji wa wanawake na watoto waliofanyika ukatili majumbani. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Jackson Jackson, Mwanzilishi wa SADAKA Network Dkt Ibrahim Msengi na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum. 
Waandishi wa habari na wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.

No comments: