Gavana wa Nampula, Mheshimiwa Victor Borges akiwa na Mheshimiwa Balozi Rajabu Luhwavi kushoto kwake wakikata utepe wakati wa kufungua Maonyesho ya Biashara Nampula tarehe 20 Agosti 2018. Maonesho hayo yalihusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na wenyeji wa Msumbiji.
Mheshimiwa Balozi Rajabu Luhwavi akitoa maelezo mafupi wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Biashara Nampula yaliyohusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania. Kwa upande wake Balozi Luhwavi, alieleza kuwa maonesho haya ni ya kimkakati kwa ajili ya kukuza na kuimarisha umoja, mshikamano na mahusiano ya kiuchumi yaliyojengwa na waasisi wetu hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; hayati Sheikh Abeid Amani Karume, aliyekuwa rais wa kwanza wa Zanzibar na hayati Samora Moises Machel, aliyekuwa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Msumbiji. Maonesho haya yalifungua fursa za masoko kwa bidhaa za viwanda vya Tanzania pamoja na kuendeleza juhudi za utekelezaji wa diplomasia ya uchumi kwa vitendo na kukuza uchumi, hususan uchumi wa viwanda.
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa kilele cha maonesho ya bidhaa za Tanzania mjini Nampula akiwa pamoja na Balozi Rajabu Luhwavi na Katibu Mkuu wa Jimbo la Nampula, Bi. Veronica Langa wakipata maelezo kuhusu teknolojia ya kisasa ya ufugaji samaki kutoka kampuni ya Dokaman ya nchini Tanzania. |
Kutoka kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mheshimiwa Rajabu Luhwavi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ndugu Juma Ali Juma, Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara TanTrade, Bi. Anna Bulondo wakipata maelezo kutoka kwa wawakilishi wa kampuni ya A- Z Textile Mills inayojishughulisha na utengenezaji nguo, vifaa vya plastiki, mifuko ya kuhifadhia mazao na bidhaa nyingine. |
Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mheshimiwa Rajabu Luhwavi akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi |
No comments:
Post a Comment