Meneja
Mkuu wa Pizza Hut Afrika Ewan Davenport (kushoto) akiwa na watoto
kutoka Shule ya Msingi ya Nzinga wakati wa uzinduzi wa mradi wa
kuhamasisha watoto kusoma na kuandika wa Kiafrika ambapo walipewa boksi
nyenkundu zenye vifaa mbalimbali vya kusoma na kuandika. Kampeni hii ni
mradi wa kijamii wa kampuni hiyo ulioanzishwa mwaka 2016. Mradi huu
uliundwa ili kuhamasisha elimu kupitia utoaji wa rasilimali na
kushirikisha wateja ili kuleta mabadiliko katika jamii.
Meneja
Mkuu wa Pizza Hut Afrika Ewan Davenport (kushoto) akionyesha vifaa
ambavyo vitakuwa kwenye mradi wao mpya uitwao "Red Reading Boxes" kwa
ajili ya kuhamasisha watoto kusoma na kuadika. Kampeni hii ni mradi wa
kijamii wa kampuni hiyo ulioanzishwa mwaka 2016. Mradi huu uliundwa ili
kuhamasisha elimu kupitia utoaji wa rasilimali na kushirikisha wateja
ili kuleta mabadiliko katika jamii.
Mpango wa Pizza Hut wa Elimu wa Afrika Kuletwa Tanzania
Chapa
kubwa ya Pizza duniani yabadili boksi zake kuwa boksi nyenkundu za
kujisomea kama mradi wake wa kuhamasisha watoto kusoma duniani
KAMPENI
mpya inayosafiri ya Pizza Hut Afrika inayohamasisha kusoma kwa watoto
imefika jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo inayoenda kwa jina la
‘Kipande cha Afrika (Slice of Africa)’ inaongozwa na Meneja Mkuu wa
Pizza Hut Afrika Ewan Davenport na timu yake ambayo wanasafiri katika
miji 14 na nchi 12 barani Afrika kufuatia mchoro wenye umbo la kipande
kikubwa cha chakula aina ya pizza.
“Badala
ya kusambaza pizza tunasambaza viboksi vya rangi nyekundu (Red Reading
Boxes) tukishirikiana na shirika lisilo la kiserikali ‘READ Educational
Trust’, katika kutafuta njia za kivumbuzi za kuendeleza elimu kwa ajili
ya watoto katika kila nchi,” alisema Davenport.
“Kutokana
tafiti zinazosema kwamba zaidi ya watoto milioni 280 barani Afrika
hawajui kusoma, kampeni hii ni muhimu sana. Elimu na kujisomea ni fursa
kubwa katika kuleta maendeleo na tumelenga kutumia ukuaji wa migahawa
yetu barani Afrika ili kuleta mabadiliko katika jamii tunazotumikia.”
Katika
safari yao timu hiyo ya ‘Slice of Africa’ ikiwa na wafanya biashara wa
kampuni hiyo ya Pizza Hut watazindua kampeni ya kujitolea kwa wateja
katika kila nchi ili kukusanya fedha zitakazojumuishwa na za kampuni
hiyo ili kuweza kusambaza maboksi mengi zaidi.
Katika
kila nchi Pizza Hut imechagua shirika lisilo la kiserikali ambalo
litafanya kazi ya kutambua walengwa kutoka katika mashirika au shule
watakaopatiwa boksi hizo nyekundu. Watoto kutoka shirika la Room to Read
wameambatana na timu ya Davenport nchini katika kampeni hii.
“Uwezo
wa kusoma katika darasa la nne ukiwa na miaka kumi ni muhimu sana
kwasababu kuanzia darasa la kwanza hadi la tatu unajifunza kusoma na
kuanzia darasa la nne hadi 12 ni wakati wa kujifunza,” aliongezea
Davenport. “Elimu inaenda nje ya darasa na kuweza kumsaidia mtoto kuwa
na ujuzi na kujiamini ili kuweza kushiriki kikamilifu katika jamii.
Tunapoona watoto wakifurahia boksi hizi nyekundu ni jambo ni furaha
kwetu. Watoto wanapata hamasa ya kusoma na hiyo inatupa matumaini.”
“Shirika
la READ linajivunia kuwa mshirika wa kampeni hii inayotupa nafasi ya
kuchangia katika lugha na elimu ya mtoto katika bara la Afrika kwa
kutengeneza yaliyomo katika boksi hizi nyekundu,” alisema Meneja
Mawasiliano wa READ Lizelle Langford.
“Tukitumia
vitu mbalimbali ikiwemo hadithi, michezo ya aina mbalimbali boksi hizi
nyekundu zinamhamasisha mtoto anayepokea pamoja na familia nzima na
hivyo kuwa njia bunifu ya kukuza lugha ya Kiingereza na ujuzi wa
kielimu. Kuwa na vifaa vya kujisomea ni hatua muhimu ya kuelimika
zaidi.”
Kampeni
hii pia inajenga daraja la kiutamaduni na kilugha kwa kukusanya hadithi
katika kila kituo ambazo zote zitaenda kwenye boksi nyekundu ambazo
zitasambazwa maeneo mengi Afrika wakati wa Siku ya Elimu duniani mwezi
Septemba mwaka huu.
“Tunaamini
kuwa kuweza kutoa vifaa vya kujisomea kutaisaidia watu kukua na
kutengeneza jamii zenye uwezo zaidi na ni matumaini yetu kila nchi
itashirikiana nasi katika hili,” alimalizia Davenport. “Kila senti
inayochangwa katika nchi inaenda kwenye kutengeneza boksi hizi nyekundu
kwa nchi hiyo. Ni wakati sasa kujiunga na kuwapatia fursa wale watoto
wanaohitaji.”
No comments:
Post a Comment