Muonekano wa ubavuni wa jengo la bweni la wanafunzi
moja ya chumba cha wanafunzi ndani ya bweni
korido la moja ya bweni litakalotumiwa na wanafunzi wa kidato cha tano
ujenzi wa jengo la utawala ukiendelea
moja ya jengo la maabara ya kisayansi
baadhi ya vifaa vya majaribio ka vitendo vilivyopo ndani ya maabara ya sayansi
baadhi ya vifaa kwaajili ya mafunzo kwa vitendo
Halmashauri
ya Manispaa ya Kigamboni inatarajia kufungua kidato cha tano na sita
Julai mwaka huu katika Shule ya Sekondari Nguva kwa kuwa na wanafunzi
160 wa kiume pekee ikiwa na michepuo ya PCM,PCB,HGE na EGM.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Kigamboni Bw.Stephen Katemba amesema kuwa katika kutatua
changamoto ya ukosefu wa Shule ya Sekondari yenye kidato cha tano na
sita kwenye Halmashauri, na kutimiza maelekezo ya Serikali kwa kila
Halmashauri kuwa na shule ya kidato cha tano na sita, Manispaa iliamua
kuboresha miundombinu ya Shule ya Nguva ili iweze kukidhi mahitaji
hayo.
Aidha
amesema kuwa mradi huu unatekelezwa kwa thamani ya shilingi 492,864,576
kwa kushirikiana na Serikali kuu, ambapo Serikali kuu imeweza kuchangia
kiasi cha shilingi 259,000,000 na vyanzo vya ndani vya Halmashauri ya
Manispaa ya Kigamboni ilichangia shilingi 233,864.576.
Mkurugenzi
amesema kwamba ili kuhakikisha Shule ina hadhi ya kidato cha tano na
sita kwa mujibu wa vigezo vya wizara, ujenzi wa mabweni mawili kwaajili
ya wanafunzi, vyoo, ujenzi wa daharia ambao bado unaendelea, ujenzi wa
madarasa manne na ununuzi wa madawati, ununuzi wa vitanda kwaajili ya
mabweni ya wanafunzi, ukarabati wa maabara ya sayansi na ujenzi wa jengo
la utawala linalojengwa kwa juhudi za Mkuu wa Mkoa Mh. Paul Makonda
vimefanyika .
Mkurugenzi
amesema kuwa lengo kuu ni kuhakikisha masomo ya kidato cha tano na sita
yanatolewa kwa watoto wanaomaliza kidato cha nne kwa shule za sekondari
za Kigamboni.
Kukamilika
kwa mradi kutawezesha kuongeza idadi ya wanafunzi watakaojiunga na
kidato cha tano na sita,kuchochea maendeleo ya elimu katika Halmashauri
ya Manispaa ya Kigamboni kwa kutoa fursa pana kwa wanafunzi kujiunga na
elimu ya juu.
Ameongeza
kuwa ujenzi wa bwalo la chakula litakalowawezesha wanafunzi kutumia
kwaajili ya chakula linaendelea kujengwa kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali.
Imeandaliwa na:
Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano
Halmshauri ya Manispaa ya Kigamboni
13/04/2018
No comments:
Post a Comment