Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu gawiwo la bilioni 1.8 la robo ya mwaka kwa wateja wa Airtel Money. katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda na Meneja wa Airtel Money, Ibrahim Marando.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda, akitangaza gawiwo la bilioni 1.8 la robo ya mwaka kwa wateja wa Airtel Money wakati kizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kulia ni Meneja wa Airtel Money, Ibrahim Marando.
Airtel Tanzania imetoa gawio linalofikia shilingi bilioni 14.8 hadi sasa kwa wateja wake na mawakala nchi nzima ikiwa ni sehemu ya faida waliyoipata tangu mwaka 2015.
Hili limebainishwa na Mkurugenzi wa masoko wa Airtel Tanzania, Isack Nchunda kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Airtel wakati akitangaza gawio la robo hii ambalo ni shilingi bilioni 1.8.
“Tangu tuanze kugawa sehemu ya faida yetu kwa wateja mwaka 2015, tumeshatoa jumla ya shilingi bilioni 14.8 na huwa tunagawa kila robo ya mwaka na kuhakikisha wateja na mawakala wanapokea fedha hizi kupitia akaunti zao za Airtel Money na wana uhuru wa kutumia fedha hizi wanavyotaka,” alisema.
Kwa mujibu wa Nchunda, hii ni mara ya sita mfulululizo kwa Airtel Tanzania kugawa sehemu ya faida kwa wateja wake tangu mwaka 2015. “Bwana Pesa hutoa gawio hili kwa wateja wa Airtel Money na mawakala kulingana na salio la mteja kila siku,” aliongeza.
Aliwashukuru wateja wa Airtel kwa kuendelea kutumia Airtel Money na kuifanya iwe huduma yenye tija na maarufu zaidi na kuongeza kuwa hadi sasa wana zaidi ya maduka 100 maalum kwa kutoa huduma ya Airtel Money ambayo yanafanya huduma hii iwe ya kuaminika zaidi na rahisi kupatikana.
“Maduka haya ya Airtel Money huhakikisha mawakala wana salio la kutosha muda wote ili wateja wasipate usumbufu wanapohitaji huduma hiyo,” alisema.
Kwa upande wake, Meneja wa Airtel Money, alisema kuanzia leo, wateja wa Airtel Money na mawakala watapata gawio linalofikia shilingi bilioni 1.8 kupitia akaunti zao za Airtel Money na wanaweza kutumia gedha hizo wanavyotaka ikiwemo kulipia huduma mbalimbali kama vifurushi vya mtandao, muda wa maongezi na LUKU.
Alitoa wito kwa mawakala wa Airtel Money kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa wateja ili kampuni hiyo iendelee kutoa gawio kwa wateja wake kila robo ya mwaka.
“Airtel Money imejizatiti kuendelea kutoa huduma bora na nafuu ambayo ni suluhisho kwa biashara za aina yoyote,” alisema na kuongeza kuwa Airtel inashirikiana na biashara zaidi ya 400 na ziadi na benki 30 katika kutoa huduma za kifedha.
Airtel ina zaidi ya mawakala 50,000 nchi nzima na inaendelea kutanua wigowake ili kuhakikisha huduma za kifedha zinapatikana katika miji na vijijini.
No comments:
Post a Comment