Mkurugenzi
mtendaji wa BancABC Dana Botha akizungumza na waandishi wa habali
katika ofisi zao Leo Jijini Dar es Salaam,kuhusu punguzo la tozo ya
mikopo mbali mbali kwa wateja wao.
Mkurugenzi
Mtendaji wa BancABC Dana Botha kulia,kushoto ni Mkuu wa kitengo cha
Hazina BancABC Barton Mwasamengo pamoja na Mkurugenzi wa kitengo cha
wateja binafsi na wafanyabiashara wa BancABC Joyce Malai katikati
wakishika bango linaloonyesha punguzo la tozo za Mikopo.
BENKI
ya BancABC imesema imetekeleza Sera ya fedha ya Benki Kuu ya
Tanzania(BoT) kwa kutangaza kutoa punguzo kwa wateja wake wapya
kuwezesha kukopa kuanzia Aprili 1 mwaka huu.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji was BancABC Dana Botha
amesema benki hiyo ni sehemu ya Atlasi Mara iliyosajiliwa katika soko
la hisa la Londan ikiwa na lengo la kujitanua ili kuwa kinara katika
masuala ya kifedha katika ukanda wa Sahara kwa kutumia uzoefu wake na
uwezo wa kukuza mitaji.
Hivyo
Botha amesema watapungunza riba kwa wateja wao katika mikopo ya
masharti ambayo itakuwa ni huduma ya Over draft pamoja na ya nyumba na
kufafanua mwaka jana benki nyingi zilipita katika wakati mgumu wa
ukwasi.
"Hivyo
kufanya uwezo wa kukopesha kuwa mdogo.Kwa miezi kadhaa sasa,Serikali
kupitia BoT imekuwa ikisisitiza kuhusu punguzo la riba hiyo kwa
kupunguza masharti kama vile kiwango cha chini cha fedha kwa
mabenki,"amesema Botha.
Ameongezea viwango vya punguzo,hati fungani za hazina na kukopesha
mabenki
kwa viwango vya chini na hiyo imewezesha ukopeshaji kwa watu binafsi na
kampuni mbalimbali ili kuimarisha biashara zao na hatimaye kuboresha
uchumi. "Na tunajivunia kuwa kati ya benki za kwanza kutangaza wazi
kuhusu punguzo hili."
Aidha
Mkuu wa kitengo cha Hazina BancABC Barton Mwasamengo amesema kuwa benki
hiyo inahudumia wateja zaidi ya 60,000 ambao wanamiliki bidhaa tofauti
za kibenki
Mwasomengo
amesema fursa hiyo itawawezesha kuwashawishi wateja kupata mikopo ya
Nyumba ambayo ilikuwa changamoto kubwa hasa kwa wananchi wa Daraja la
kati na chini.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara
wa BancABC Joyce Mlai amemalizia kwa kusema katika kujenga nyumba
wanaungana na Serikali kuwapa fursa ya kuwapatia mikopo ya Nyumba
wafanyakazi wa aina zote sekta binafsi,serikalini pmoja na wafanya
biashara.
No comments:
Post a Comment