WAKAZI wa Kisiwa cha Kerebe wilayani Muleba mkoani Kagera wameomba Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais,Dk. John Maguli kuwapelekea rasilimali watu hasa upande wa afya na elimu.
Wamesema kwa sasa wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali za kijamii kutokana na uhaba uliopo wa watumishi wa umma. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Michuzi blog juzi na jana, wakazi hao wamesema huduma za kijamii ni changamoto kwao.
" Zimekuwa zinawaumiza hivyo wamezitaka Wizara husika kusikia kilio chao na tunaomba tujengewa hospitali na shule ili watoto na wakina mama wajazito wapate hudumu muhimu,"wamesema wakazi hao.
Pia wameomba Serikali kuwatengenezea huduma bora katika usafiri wa majini kwa kuwapatia boti kwani wamekuwa wakitumia boti za mtu binafsi ambazo si salama kwao.Hivyo wanaomba upatikane usafiri ulio bora na wa uhakika katika kulinda maisha yao.
Hata hivyo Wakazi hao Kisiwa hicho asilimia 93 wanatengemea uvuvi wa Samaki na asilimia 7 wanajishughulisha na kilimo na ufungaji, hivyo basi wameitaka Serikali kuboresha katika sekta ya uvuvi pamoja na ufungaji ili waweze kuendana na mabadiliko ya nchi kwa kupata kipato kikubwa zaidi.
Kisiwa cha Kerebe kwa sensa ya 2012 kina jumla ya wakazi 3100 lakini idadi hiyo hupungua na kuongezeka kulingana na kilimo na upatikanaji wa samaki kwa wingi ziwani humo.
Hivyo basi kutokana na Serikali ya awamu ya tano inayosema 'Hapa kazi to' itasikiliza kilio chao na kuwapelekea huduma muhimu kwani kila Wizara itakuwa ipo tayari kushirikiana na wanakijiji hao kwa kupitia Wilaya ya Muleba
Na kuongeza viongozi mbalimbali waliochaguliwa wataimarisha ushirikiano wao kwa Serikali
No comments:
Post a Comment