WAZIRI
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wa pili kulia akitazama mifugo ya
ngombe aina ya Borani waliyopo kwenye ranchi ya mzeri wilayani Handeni
mkoani Tanga wakati wa ziara yake wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya
Handeni,Godwin Gondwe
Mkuu
wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe kushoto akimuleza jambo WAZIRI wa
Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kulia ambaye alifanya ziara ya kikazi
wilayani humo
WAZIRI
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akisisitiza jambo wakati akizungumza
na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza ziara yake kushoto ni Mkuu
wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe
WAZIRI
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wa pili kutoka kushoto akiwa na Mkuu
wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe wakati alipoitembelea ranchi ya mzeri
wilayani humo
NA MWANDISHI MAALUM, HANDENI
WAZIRI
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amechukizwa na tabia ya baadhi
watendaji wa Serikali katika Hifadhi za Misitu, Mapori ya Akiba na
Serikali za Mitaa kukamata mifugo kiholela na kutoza faini zisizo na
misingi ya kisheria huku akisifu utendaji kazi ya wa Mkuu wa Wilaya ya
Handeni mkoani Tanga, Godwin Gondwe katika usimamizi wenye weledi wa
sheria za mifugo nchini.
Mpina
ametoa kauli hiyo akiwa wilayani Handeni ambapo alitumia fursa hiyo
kupiga marufuku ukamataji mifugo kiholela huku akimtaja Mkuu wa Wilaya
ya Handeni, Gondwe kama kielelezo cha kuwa kiongozi wa kwanza kitaifa
anayezifahamu vizuri na kuzisimamia kikamilifu sheria za mifugo na
kuleta tija katika ukuaji wa sekta hiyo ikiwemo kuanzisha kijiji cha
wafugaji,kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji na watumiaji wengine
wa ardhi na utoaji huduma bora za mifugo wakati wote.
Akizungumzia
tatizo hilo la ukamataji holela wa mifugo nchini, Waziri Mpina amesema
kama sekta hiyo isingekuwa inazalisha mazao ya mifugo na Serikali kuamua
kuagiza kutoka nje ya nchi basi ingezilazimu kutumia kiasi cha sh.
Trilioni 17.8 huku kaya milioni 4.49 za kilimo nchini zinajishughulisha
na ufugaji mifugo aina mbalimbali.
“Watendaji
wa Serikali waliofanya hujuma na dhuluma kwa wafugaji hawatabaki
salama, tutawafuatilia na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa
sheria”alisema.
Amesema
Sheria ya misitu na. 14 ya mwaka 2002 kifungu cha 26 kinazuia mifugo
kuingia kwenye hifadhi za misitu ya kitaifa au iliyo chini ya Mamlaka za
Serikali za Mitaa ambapo pamoja na wafugaji kuvunja sheria hiyo bado
wanahitaji kutendewa inavyostahili kwa mujibu wa sheria za nchi ili
kuweka ulinganifu wa watanzania wote mbele ya sheria za nchi.
Waziri
Mpina amebainisha kuwa kumekuwa na mazoea mbalimbali ya ukamataji
holela wa mifugo yanayoendelea nchini ambayo yanatekelezwa bila
kuzingatia sheria ya ustawi wa Wanyama (Animal welfare Act No.19 of
2008) na Kanuni zake za mwaka 2010 kifungu cha 7 na 8 na Sheria ya
Magonjwa ya Wanyama Na 17 ya mwaka 2003 (Animal Disease Act No.17 of
2003) hivyo mifugo imekuwa ikishikiliwa kama kidhibiti kwa muda mrefu na
mingine kufa kutokana na magonjwa na ukosefu huduma ikiwemo
matibabu,chanjo na kuogeshwa ili kuepuka magonjwa ndorobo na kupe.
Mkuu
wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amesema wao kama Serikali ya wilaya
katika sheria ndogo yao ikiwa kundi la mifugo litaingia kwenye maeneo
yasiyoruhusiwa wameweka faini isiyozidi sh 300,000 kwa kundi la ng’ombe
ambapo alisema pamoja na pongezi za Waziri Mpina bado wataendelea kubuni
mbinu mbalimbali za kuboresha sekta ya ufugaji ikiwemo uimarishaji wa
majosho, malisho na uzuiaji uuzaji nyama kiholela barabarani.
No comments:
Post a Comment