Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa tatu kulia) akiwa na
baadhi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),
kutoka makao makuu Dar es Salaam akiangalia vitalu vya miche ya miti
wakati alipowatembelea wanakijiji wa Maguruwe wanaopakana na msitu wa
Hifadhi wa Kazimzumbwi waliojitolea kuotesha miche ya miti kwa ajili ya
kupanda kwenye eneo la msitu huo uliokuwa umevamiwa takriban theluthi
tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa kwanza kulia) akipata
maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Misitu wa Wilaya ya Kisarawe, Mathew
Mwanuo ( wa kwanza kushoto) wakati alipofanya ziara mwishoni mwa wiki
ya kutembelea kilichokuwa Kiwanda cha Caoline, kilichopo katika msitu wa
hifadhi Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani .
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akiwa na
baadhi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),
kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam wakioneshwa ramani ya Msitu wa
Hifadhi Kazimzumbwi na Kaimu Meneja wa Misitu wa Wilaya ya Kisarawe,
Mathew Mwanuo ( wa tatu kushoto) kuhusiana na“eneo la msitu huo
lilivyokuwa limevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia
mwaka 1993 hadi 2014.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiwa kwenye picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Kisarawe, Viongozi wa Wakala
wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wakiwemo watumishi wakati Naibu
Waziri huyo alipofanya ziara mwishoni mwa wiki ya kutembelea msitu wa
Hifadhi wa Kazimzumbwi na Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na
wanakijiji wa Maguruwe wanaopakana na msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi
waliojitolea kuotesha miche ya miti kwa ajili ya kupanda kwenye eneo la
msitu huo uliokuwa umevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha
kuanzia mwaka 1993 hadi 2014 wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara
mwishoni mwa wiki katika msitu huo.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akisaini kitabu cha
wageni alipotembelea eneo kilichokuwa Kiwanda cha Caoline, kilichopo
katika msitu wa hifadhi Pugu wilayani Kisarawe mkoani Pwani wakati Naibu
Waziri huyo alipofanya ziara mwishoni mwa wiki katika msitu wa Hifadhi
wa Kazimzumbwi na Pugu.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (katikati) akipatiwa
maelezo na Mkurugenzi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki wa Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Zawadi Mbwambo ( wa kwanza kushoto)
wakati alipofanya ziara jana ya kutembelea kilichokuwa Kiwanda cha
Caoline, kilichopo katika msitu wa hifadhi Pugu wilayani Kisarawe mkoani
Pwani
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa kwanza kushoto)
akioneshwa eneo la msitu Kazimzumbwi na Kaimu Meneja wa Misitu wa Wilaya
ya Kisarawe, Mathew Mwanuo lilivyokuwa limevamiwa takriban theluthi
tatu kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1993 hadi 2014 wakati Naibu Waziri
huyo alipofanya ziara mwishoni mwa wiki katika msitu huo.
Picha na Lusungu Helela-MNRT
……………………
NAIBU
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amewataka wananchi
wanaozunguka hifadhi za misitu katika wilaya ya Kisarawe kuzingatia
mipaka iliyowekwa pamoja na matumizi ya ardhi ili kuepuka migogoro
inayoweza kujitokeza baina ya wananchi na serikali.
Hasunga alisema jana kwenye ziara aliyoifanya alipotembelea Kiwanda cha Caoline, pamoja na msitu wa hifadhi Kazimzumbwi na Pugu.Alisema serikali haitakubali kuona maeneo ya hifadhi yanavamiwa ovyo na wananchi ama mifugo kuachiliwa bila utaratibu maalum.
“Kuna umuhimu mkubwa wa kukuza sekta ya utalii. Wataalii wengi wanapenda kuona misitu. Hii ni sehemu ya utalii,” alisema.Aliwataka Kisarawe kuangalia vivutio walivyonavyo ili kuboresha katika maeneo hayo kwa ajili ya kuvutia utalii.
Kwa
upande wake Kaimu Meneja Misitu Kisarawe, Mathew Mwanuo alisema wilaya
hiyo ina misitu minne ya hifadhi ya serikali Kuu ambayo ni Ruvu Kusini,
Masanganya, Pugu na Kazimzumbwi.Alisema msitu wa Kazimzumbwi umekuwa ukivamiwa mara kwa mara na watu kutoka maeneo mbalimbali hasa jijini Dar es Salaam.
“Msitu
huu ulikuwa umevamiwa takriban theluthi tatu kwa kipindi cha kuanzia
mwaka 1993 hadi 2014. Hata hivyo wavamizi hao waliendelea kuvamia kwa
nyakati tofauti hadi mwaka huu,” alisema.
Alisema
walianza kuwaondoa mwishoni mwa Agosti mwaka huu, Kamati ya Ulinzi na
Usalam ya wilaya ya Kisarawe kwa kushirikiana na maofis wa Wakala wa
Huduma za misitu Tanzania walianza kutembelea eneo la msitu kuangalia
uvamizi na uharibifu uliofanyika katika Msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi
ikiwa ni pamoja na kuona ukubwa wa uharibifu na namna ya kutekeleza
zoezi.
No comments:
Post a Comment